Mke Msomi + Mume Msomi = Ndoa nzuri yenye mafanikio?

Tumeongelea sana elimu, pia kuna vyeo au madaraka hata kama wote ni wasomi. Mke akiwa na madaraka makubwa kumpita mume inaweza kuleta shida fulani aidha kwa mke kujiona yuko juu au mume akawa na complex inferiority!!

Hiyo ya mwanamke kuwa na madaraka makubwa kazini inaweza kuwa tatizo kubwa zaidi kuliko hata kama angekuwa na elimu. Mfano, mwanaume uwe msomi na mwajiriwa wa shirika fulani na una kipato kizuri. Mkeo aingie kwenye siasa, tena siku hizi kama mzaha mzaha tu anaukwaa Ubunge wa viti maalumu halafu Rais anamkandamizia na Unaibu Waziri.....Hapo msipokuwa makini ndoa lazima ilegelege aisee!
 
Michango mingi imenivutia.Napenda kuongezea kuwa ili ndoa isimame au ifanikiwe kuna bare minimums zinazotakikana bila kujali pesa au usomi ambao nao una nafasi/athari zake:
1. Mmekutana wapi - wengi hupuuza sana hii lakini ina nafasi yake maana itaamua huko mbele ya safari kutakuwa vipi. Mmekutana kwenye mazingira yenye kutoonyesha uhalisia kisha mkaamua kuoana basi ni tabu na shida tupu kwa vile mtakuja kugundua mengi ambayo hamkuyatarajia na ugomvi utakuwa hauishi
2. Mna interests za kufanana? k.m mmoja anapenda kujiendeleza mwingine hapendi anapenda starehe zaidi.Hata kama usomi upo ni tatizo maana matumizi ya rasilimali yatahitaji maamuzi magumu na assuming kuwa mama ndio ana pesa zaidi au msomi zaidi baba hatapenda kusikiliza ushauri au maamuzi ya mkewe maana anajiona yeye ndio kichwa lazima asikilizwe.
3. Heshima- Kama wanandoa hawaheshimiani au dharau imetawala, basi usomi unakuwa kama mwiba kwenye uhusiano.Haijalishi ni mwanamke au mwanaume.
4. Uelewa wa pamoja kuhusu kuingia katika ndoa - wengi husukumwa kuingia kwenye ndoa bila hata kujua wanajiingiza kwenye majukumu makubwa yenye kutaka commitment kubwa pia.Wengi ndoa ni fashion au ni tamaa zaidi ya kutaka kuwa pamoja bila kujua mapenzi kama mapenzi yana maisha mafupi kabla uhalisia haujaingia.Usomi huweza kujenga kiburi cha kukimbia majukumu au kutokutaka kusahihishwa pale mtu anapokosea. Ingetarajiwa usomi usaidie watu kupima kama kweli wanaingia kwenye ndoa wakiwa well informed au wanaingia tu kama fashion.Bahati mbaya sana wasomi wengi ndio wa kwanza kuingia kwenye ndoa wakiwa ignorant kuliko wasiosoma.Wasiosoma utakuta wanaingia kwenye ndoa wakijua hasa nini wanakifuata, heshima inakuwepo, nk. Usomi + pesa = jeuri, dharau, kujiamini kwa kipumbavu, kutokujali nk.

Cha msingi ili ndoa isimame wanandoa wanatakiwa wawe na yafuatayo:
Uvumilivu, unyenyekevu, staha, Heshima, kumcha Mungu,na kujua kuwa ndoa si lele mama - ni msalaba na siyo fungate!
 
Kutoka moyoni, nashukuru sana dada/mama/kaka/.. Kwa somo zuri namna hii. Mungu akubariki na akupe neema na nguvu yakuendelea kutuelimisha/kunielimisha zaidi na zaidi. Mungu Ibariki JF.
 
Ndoa ni maelewano, na mnapokutana regardless of your background kinachowakutanisha ni penzi, baada ya muda ndio mnaanza kujuana tabia,ndugu na kisomo

Kwa upande wangu mimi na mume wangu kielimu tuko sawa ila tunafanya kazi tofauti, mwaka huu Mungu akipenda tutatimiza miaka 7 bila kokoro wala kelele I thank God daily for meeting and calling this man my husband,

Mambo tunayobishania hapa home mara nyingi sana ni future plans kama kubadili kazi,ujasiriamali etc maana kila mtu ana maono yake but we compromise,

Hatujawahi kuhitlafiana kuhusu elimu kwa watoto or matumizi ya pesa zetu za mshahara, kila mmoja anakatwa kiasi sawa kwa mwezi kuingia ktk account za watoto

Hapo kwenye kubishana mara kwa mara ndipo sie wanaume tunakereka, tunapenda tubishiwe lakini isizidi, ukweli unabaki palepale, kwa sasa mwanamke msomi au mwenye mafanikio zaidi ya mme wake huwa wanakuwa na kauendawazimu fulani hivi, nadhani ni ulimbukeni kwani sababu hali haikuzoeleka miaka ya nyuma, baadaye wataona ni hali ya kawaida. Nilialikwa kwenda dinner kwa Proffessor wa kike(sheria) na mme wake polisi constable mstaafu ( hawa wote ni wazungu kwenye nchi iliyoendelea), nilichokiona pamoja na usomi wake nyumbani ni mke mwema kama walivyokuwa wake wa miaka ya 1850s. Huko kwa wenzetu kuna ambao ulimbukeni wa mafanikio umeshaanza kuwatoka wengine bado wehu na kuamua kuishi kwa upweke wanishia kupendana na mbwa wao maana wameshindwa kuenzi hisia za mwanume. Cha muhimu wanaume tuwapende wake zetu ili nao watuheshimu kama inavyosema Bibia- kwa wakristo.
 
Usomi ni muhimu lakini dimension za mapenzi hazipimwi kwa usomi wa mtu. Ndio maana kuna prof wangu anafanya research Nasa alioa ba maid wa pale vatican sinza.
 
Couples za wasiosoma kabisa huwa zimetulia sana! Refer enzi za ujima na zama za mawe ndoa zilikuwa zinadumu sana.

Nakubaliana na wewe kwa 100%. NI kweli couples ambazo hawajasoma sana huwa wanamafanikio sana na upendo mkunwa. Tatizo la kusoma sana ni kujua mengi na hivyo daima huwa kila mtu anataka kuonyesha kujua kwake dhidi ya mwingine.

Pia kusoma sana kunaambatana na kupenda mali na vitu. So daima wanandoa waliosoma huwa na upendo uliofungama na kupenda mali.

Mimi naona hakuna kitu chenye amani kama kuweka Elimu yako pembeni inapkuja masuala ya familia.

Usiombe kuoa mwanamke aliesoma Sheria. Nyumba inaweza ikageuka kizimba cha kujibu mashitaka na tuhuma kila kukicha...!
 
Usomi ni muhimu lakini dimension za mapenzi hazipimwi kwa usomi wa mtu. Ndio maana kuna prof wangu anafanya research Nasa alioa ba maid wa pale vatican sinza.

Ndoa A inaweza ikawa na tofauti kubwa sana na ndoa B pamoja na kuwa ndoa zote hizi zinaweza zikawa zimewahusisha wasomi au wale ambao si wasomi au mhusika mmoja ni msomi na mwingine si msomi. Tabia ya wahusika ndani ya ndoa ndiyo sababu kubwa ya ndoa moja kushamiri, kuendelea kuwepo kwa miaka mingi na huku ndoa nyingine zikififia au kufa. Tabia kama za uvumilivu, usikivu, usafi wa wahusika wote, kuonyesha mapenzi, tabia zozote mbaya ambazo zinaweza kumkwaza mume/mke n.k. Hivyo kwa maoni yangu sidhani kama kuna formula maalum ya kuhakikisha ndoa inafanikiwa.

Tabia za wahusika ndani ya ndoa ndiyo muamuzi mkubwa wa kushamiri na kudumu kwa ndoa na si usomi au kutokuwa msomi kwa mmoja wa wahusika au wote.

Kwa ushauri na uzoefu wangu, wanawake wasomi hawajishughulishi. Kwenye shughuli anaweza kuwa anasoma gazeti.
 
Couples za wasiosoma kabisa huwa zimetulia sana! Refer enzi za ujima na zama za mawe ndoa zilikuwa zinadumu sana.

Na hata ukichunguza utaona ndoa zao zilidumu hadi zaidi ya miaka 50 na kupata watoto wengi! Kazi kwetu wasomi!!!, ukifikisha miaka 10 inakuwa rekodi.
 
Hapo kwenye kubishana mara kwa mara ndipo sie wanaume tunakereka, tunapenda tubishiwe lakini isizidi, ukweli unabaki palepale, kwa sasa mwanamke msomi au mwenye mafanikio zaidi ya mme wake huwa wanakuwa na kauendawazimu fulani hivi, nadhani ni ulimbukeni kwani sababu hali haikuzoeleka miaka ya nyuma, baadaye wataona ni hali ya kawaida. Nilialikwa kwenda dinner kwa Proffessor wa kike(sheria) na mme wake polisi constable mstaafu ( hawa wote ni wazungu kwenye nchi iliyoendelea), nilichokiona pamoja na usomi wake nyumbani ni mke mwema kama walivyokuwa wake wa miaka ya 1850s. Huko kwa wenzetu kuna ambao ulimbukeni wa mafanikio umeshaanza kuwatoka wengine bado wehu na kuamua kuishi kwa upweke wanishia kupendana na mbwa wao maana wameshindwa kuenzi hisia za mwanume. Cha muhimu wanaume tuwapende wake zetu ili nao watuheshimu kama inavyosema Bibia- kwa wakristo.

Post yako ilianza vema sana na kunifanya kuwa vere siriaz kuisoma hadi nipofika hapo kwenye rangi nyeusi nikajikuta nachenchi gia bila kupenda kutoka namba 5 hadi namba 1!
1. Huyo mke mwema anayeonekana mwema kwa kipindi cha takriban masaa 2-3 ya dinner ni kiboko! Ina maana wewe ukikaa na mtu masaa 2 basi yanatosha kumjaji kuwa ni mwema au mwovu tena pale ambapo kakukaribisha kupata chakula wewe mwafirika naye mzungu? Kwanza nijuavyo wenzetu weupe hadi wakukirimu lazima kuna jambo siyo " matter of fact" kama wamatumbi tufanyavyo.Hivyo kuweka best behaviour si ajabu.

2. Mke mwema wa enzi za 1850s...tuko 2011 sasa lazima ubadilike na wakati.Enzi zile hata jino liling'olewa bila ganzi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom