Mkasa!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Wakuu, nimepata message toka kwa jamaa yangu tunayeheshimiana sana akieleza mkasa uliompata jioni ya leo...
....baada ya kumpima huyo demu kwa kutumia kipimo cha mkojo, akaonyesha yuko positive(mjamzito)_ na kwa bahati mbaya nikakiweka kipimo kwenye suruwale yangu na kukisahau, na leo mke wang amekikuta...Anataka nimwambie nimempima nani, na kwanini nibaki na kitu kama hicho, na kwahiyo nina mwanamke mwengine nje!
.


Wonders will never end kwa kweli!
Jamani, nashindwa nianzie wapi kumshauri huyu broda cha kufanya!...ha ha haaa!
Hebu jameni pimeni situation hii, na kutoa ushauri kwa huyu raia!
 
Alivyotungisha mimba nje alikua anategemea nini?Wakati anatoka nje ya ndoa aliomba ushauri?Nashindwa kuelewa watu wengine wanaoa ili iweje?Kama hawajatosheka na mambo ya dunia si wahangaike mpaka watakapoona imetosha?Nwyz nakasirishwa sana na watu wanaingia kwenye ndoa wakijua fika utulivu hawana!Aseme ukweli tu maana kama mtoto atazaliwa hawezi kumficha milele.Alafu kwanzia sasa hivi muwe mnaomba ushauri kabla ya kucheat sio mpaka kigeuke ndo muanze kutoa machozi ya mamba!
 
Kama huyo jamaa yako kazi yake inahusiana na taaluma katika ngazi yoyote aseme tu kuwa ni matokeo ya mwanafunzi wake mengine yatajulikana baadaye.Tofauti na hapo mh......
 
Daahh
Eehh huyo
Kapatikana kweli

Mie naona atoke clean
hapo akidanganya itambidi
Awe anadanganya kila siku ku
cover it up..(plan A)

Au anaweza achukue
plan B ambayo ni kukana
mpka kifo duuuuhhh..
halafu hapondo ndo
Wajuku wakutan e kwenye mazishi lol

Both plans comes
With extra package
my opinion take
Plan A
 
jamaa inabidi akubali kosa halaf aombe razi tu. wanamama wameumbwa na mioyo laini atasamehe tu na hii itampa uhuru wa kuwa karib na mwanawe, sio anaonana na mwanawe kwa kunyatia nyatia.

halaf uzembe mwengine bana! hivi jamaa anatembea na mikojo hata halufu haskii? au jamaa anakoga weekend tu so pua lake halitafautishi mkojo na pafyum?
 
Dah, Ukweli utamweka huru!!!
Uongo utamgarimu zaidi!!!!

Wanaume tulieni na wake zenu!!!!
 
Mhh wake nao hawatulii :lol::lol::lol::lol:

Dah, maisha ni Sarakasi tu sasa hivi MR. Baba anapita kushoto mama kulia.........
Mmmmmh heri mwenye kumjua Mungu na kuheshimu mafundisho yake!!!!!!
 
Za mwizi ni arobaini IMETIMIA maana huyo hata mimi kumshauri nimeshindwa maana ni aibu halafu sijui hilo soo atalimalizaje kama mwanamke ngangari amepatikana
 
Mhhh! Hii kali! hata mtoa ushauri unaweza kupata kigugumizi kwa kutojua uanzie wapi!
 
Aseme ni mkojo wake yeye mwenyewe:lol::lol:, hivi ukiangalia mkojo kwa macho utajua huu ni wa mwanamke au huu ni wa mwanaume???
 
pakajimmy,

sio kila swala ukihusishwa NI LAZIMA USHAURI

kuna baadhi ya mambo NI BORA UKAACHANA NAYO!

WAACHE WAFU WAWAZIKE WAFU WENZAO
 
tunaipenda jf yetu ila kiukweli threads nyingine unakuwa huna cha kuchangia zaidi ya kuandika kmn hv.
 
Wakuu, nimepata message toka kwa jamaa yangu tunayeheshimiana sana akieleza mkasa uliompata jioni ya leo...
.

Wonders will never end kwa kweli!
Jamani, nashindwa nianzie wapi kumshauri huyu broda cha kufanya!...ha ha haaa!
Hebu jameni pimeni situation hii, na kutoa ushauri kwa huyu raia!

Ndo yale yale ya kutembea na ganda la condom iliyo tumika.

Jamaa ako mzembe aliweka mfukoni ili iweje? alitaka aje akutambie kuwa mwenzio tayari nimepiga kitu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom