Mkakati wa Kuwafelisha Waislam Kidato Cha Sita Wabainika

Status
Not open for further replies.
Usiniambie hapo ulipo hujui hata ulipata matokeo gani ya kidato chako cha sita. Isije ikawa humu JF tunajibizana na MISUKULE wajemeni!

nimemaliza kidato cha sita miaka ishirini iliyopita nikaondoka Tz. kila siku mambo yanabadilika. nisije nikaweka mahesabu yangu ya enzi zile ikawa siyo hivyo. ndio maana nikauliza nasio kukurupuka na kuweka calculation zangu humu za miaka ishirini iliyopita. kwa mimi kama mtu angeuliza swali kama langu humu, ningejiuliza maswali mengi kwa nini huyu mtu ameuliza hivi. na I m sure ningekuwa na jibu zuri kuliko hilo ulilolitoa hapo juu. Mambo yanabadilika kila siku ndugu yangu.
 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limebadili kinyemela bila taarifa matokeo ya Kidato cha Sita ya wanafunzi Waislam. Hii inatokana na malalamiko yaliyotolewa kuhusu kufeli mno wanafunzi Waislam hasa somo la "Islamic Knowledge". Baraza limebadili matokeo yote ya "Islamic Knowledge" kwa kusema kuwa IT wao alikosea pale alipogawanya wastani kwa 4 badala ya 2 kwa kuwa mitihani ilikuwa miwili.

Ukiingia katika website ya NECTA hutapata "new" ya habari hiyo, hivyo kuonesha Baraza linajijua limefanya makosa, na kubadili kibyemela matokeo. MASWALI MUHIMU:-

1. Jee Waislam waliokwisha omba vyuo wakati wana matokeo tofauti na yaliyotolewa na Baraza inakuwaje?
2. Jee hii si dhulma Waislam waliyokuwa wanaitoa kwa Baraza kuwa linawaonea?
3. Kwa nini Baraza wasijiuzulu kwa kashfa hii kubwa?

NB: Naomba mods msiitoe hii, fuatilieni mtajua ni kweli, mdogo wangu alikuwa na Div III, sasa ana Div I.
source pliz... ucje kuwa umeckia kuna mwanafunzi ame-appeal na akabadilishiwa matokeo bac na wewe uka-genelalize
 
Kila jambo lina mwisho wake.
Kuna waliokuwa wanazijua dhulma hizi kwa miaka mingi sana na kutahadharisha serikali.

Dhulma kwa Waislam si agenda mpya hata kidogo.

Wengi tulioitahadharisha serikali tulipuuzwa na kupewa majina kadhaa si haba.
Siasa kali, mujahiduna nk.

Maneno haya hapo chini nimeandika miaka mingi sana iliyopita hebu yapitie kwa kujikumbusha ikiwa ulipata kuyasoma:

TUJIKUMBUSHE
“Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingeathirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali. Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam.

Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo. Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam.

Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo. Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri 8 waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo. Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika serikali na wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam 4 kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kumtaarifu udini alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais, Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM.”

Kutoka kitabu: “Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes…”
 
Nawashukuru wanaJF kwa kuona mbali, nadhani watu wengine wanahisi hii ni sehemu ya kuzusha mambo na watu wote waitikie NDIYO! Hapa ma-mbumbumbu hamna, wewe unataka kujaza watu hasira juu ya baraza eti udini umeanzia kwenye matokeo.

Na kesho wakifeli Waislam wengi useme nilisema baraza linapendelea wakristo, unasahau kwamba kwenye booklets hawaweki majina na dini wanazoamini. Somo moja utoke pts 13 mpaka 9!
Twende shule tusome, tuelewe na tuijenge nchi yetu kwa kuvumiliana kwenye imani zetu. Haipendezi kuangalia kila kosa kidini zaidi kuliko makosa ya kawaida ya kibinadamu au uwajibikaji mbovu wa mtu binafsi.

Naomba kuwasilisha.:crazy:
 
Kila jambo lina mwisho wake.
Kuna waliokuwa wanazijua dhulma hizi kwa miaka mingi sana na kutahadharisha serikali.

Dhulma kwa Waislam si agenda mpya hata kidogo.

Wengi tulioitahadharisha serikali tulipuuzwa na kupewa majina kadhaa si haba.
Siasa kali, mujahiduna nk.

Maneno haya hapo chini nimeandika miaka mingi sana iliyopita hebu yapitie kwa kujikumbusha ikiwa ulipata kuyasoma:

TUJIKUMBUSHE
"Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingeathirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali. Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam.

Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo. Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam.

Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo. Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri 8 waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo. Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika serikali na wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam 4 kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kumtaarifu udini alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais, Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM."

Kutoka kitabu: "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes…"

Sasa we kwa source hii ulitegemea kukuta jipya linalosema kuna usawa wa kidini Tanzania?
 
Dk.Ndalichako anapaswa kuachia ngazi,je katika masomo mengine hamna makosa ya kiufundi?kama anavyodai na kwa nini iwe islamic knowledge,sina imani na NECTA
 
me nikiulizwa umefaulufaulu vipi??ntajibu kuwa nimesoma ndo maana nimefaulu,wadogo zangu waislam wenzangu na wakubwa wenzangu nawaomba mjitahid kusoma,leo necta wamebadil matokeo SAWA kesho umejiajiri utamsingizia nani????duniani huku kunataka kompitensi bhana si miujiza,,,,,hakuna wa kumlaumu,,,,waliochezesha matokeo wana wajibu wa kuwajibila,maana wameharibu mipango ya watu,lakini msome wadau punguzeni umwinyi,punguzeni kulalama elimu ni vita,,,maana waislam weeengi wamepitia hapohapo necta,nami nilifanya ISLAMIC KNOWLEDGRE PIA,nashukuru nilifaulu,ila nilijiandaa kwa kuisoma
 
Kama ni kweli kuna kosa la kiufundi lililofanyika ktk kugawanya hayo matokeo kama mwanzisha thread anavyosema,huo ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa baraza ambao hufanyika kwa mwanafunzi yoyote yule na wala usionekane kuwa ni special kwa kuwa umewagusa waislam kama thread yenyewe inavyoonekana kuegemea.. Ingekuwa ni somo la Bible Knowledge kwa upande wa wakristo wala isingekuwa issue maana ni procedure ya kawaida na wahusika wasingepoteza muda kuleta uzi kama huu hapa jukwaani..... tusipende kila kitu kukipeleka kwenye udini....

changamoto ni pale somo la dini ilivyobadilisha matokeo kutoka Div III mpaka Div I
 
NB: Naomba mods msiitoe hii, fuatilieni mtajua ni kweli, mdogo wangu alikuwa na Div III, sasa ana Div I.

Mkuu Makelele, hii ya kwako ni ya mwaka.
Yaani mdogo wako katoka div.III hadi I kwa sababu ya somo moja tu la Islamic Knowledge?
 
Sijacheki website yao lakini kama hizi habari ni za kweli, ni lazima watu wanaohusika wawajibike...
 
Yo Yo mwepesi ka nape, kwamba nikigawa kwa 4 mwanafunzi anapata F, ninarekebisha na kugawa kwa 2 sasa huyu mwanafunzi anapata A, hebu tufikirie all possible scenerios, huyu dogo inawezekana alipata ngapi ambazo nikizigawa kwa nne zinampa F lakini nikizigawa kwa mbili zinampa A????

hahahaaaa Yo Yoooooooo!
ha! ha! ha! ha! arifu mie nilimueleza jamaa aliesema hawezekani mtu kutoka div 3 mpaka one.....basi.....mambo ya kugawa sifahamu waligawa vipi baraza..ndio maana nilisema baraza nao wamechemka kichizi arifu.....
 
Kwa hili ni babu kubwa mi nashindwa kuelewa nachojua kama mtu matokeo yake yana matatizo ana - appeal kinaeleweka lakini kubadili matokeo ya watu wote! hapa kuna tatizo tena kubwa hii ni agenda ya siri mtu atoke div III hadi div I? ''NB: Naomba mods msiitoe hii, fuatilieni mtajua ni kweli, mdogo wangu alikuwa na Div III, sasa ana Div I.''tunakoipeleka hii nchi sijui.
 
Kila jambo lina mwisho wake.
Kuna waliokuwa wanazijua dhulma hizi kwa miaka mingi sana na kutahadharisha serikali.

Dhulma kwa Waislam si agenda mpya hata kidogo.

Wengi tulioitahadharisha serikali tulipuuzwa na kupewa majina kadhaa si haba.
Siasa kali, mujahiduna nk.

Maneno haya hapo chini nimeandika miaka mingi sana iliyopita hebu yapitie kwa kujikumbusha ikiwa ulipata kuyasoma:

TUJIKUMBUSHE
“Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingeathirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali. Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam.

Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo. Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam.

Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo. Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri 8 waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo. Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika serikali na wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam 4 kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kumtaarifu udini alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais, Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM.”

Kutoka kitabu: “Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes…”
eeeeeeh aisee uwanja wako huu umefikishwa.......alafu hujasema kuhusu uamsho kuchoma makanisa....
 
Thread inahusu NECTA KUBADILISHA MATOKEO YA WAISLAM,sasa dr Slaa Anahusika vp?

WatapatA kazi ya Kuwa walimu Wa madrasa

We kilaza hujui kuna Bc of islamic studies, na lazima uwe umefaulu islamic knowledge?

hebu nikumbushe Dr. wenu slaa ni wa nini vile?

Hapa ndio utakapowajua wana CDM, juzi tu hapa walimsifia slaa kutoka diploma hadi udr wa dini, leo wanasema kufaulu dini sio kwa ajili ya uongozi.
hahahahahahahahahahaha

Aweza kuwa mshauri wa Rais JK wa mambo ya 'islamic telecomunications'. Halafu mahakama ya Kadhi itaanzishwa soon. Aweza pia kuwa judge wa mahakama kuu ya kiislam, ya rufani, au hata islamic telecomunications engineer wa mahakama ya kadhi:israel:

Slaa alipata hiyo div 1?

naomba nikujibu swali lako la kwanza..,kwenye kuapply vyuo masomo kama islamic knowledge, divinity hayahusiki..yatahusika endapo unaaply theology au usheikh (sipo sure kama usheikh unasomewa)..kwahyo hapo hamna kilicho badilika kwenye cutpoints za kuingia chuo.

Bible Knowledge ukipata A inakupeleka wp? hahahahahaha
Nime"qoute" hizo hapo juu kuonesha tu jinsi tulivyolewa na dini. Tumezama katika kusifia dini zetu na kudharau za wengine wakati hatujui kinachoendelea katika dini hizo, kama kwamba nje ya dini zetu hakuna chengine, halafu tunatoa hoja hizi kwenye ma"Great Thinkers".

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limebadili kinyemela bila taarifa matokeo ya Kidato cha Sita ya wanafunzi Waislam.
Baraza limebadili matokeo yote ya "Islamic Knowledge" kwa kusema kuwa IT wao alikosea pale alipogawanya wastani kwa 4 badala ya 2 kwa kuwa mitihani ilikuwa miwili.

NB: Naomba mods msiitoe hii, fuatilieni mtajua ni kweli, mdogo wangu alikuwa na Div III, sasa ana Div I.
RED: Masomo au mitihani ya dini si kwa ajili ya watu wa dini hiyo tu. Wapo Wakristo hufanya mtihani wa dini ya Kiislamu na Waislamu wanaofanya mtihani wa dini ya Kikristo. Kuhusisha moja kwa moja Islamic Knowledge na Uislamu ni "kutokujua" unalolisema.
KIJANI: Kumbe Baraza lilishatoa sababu za kubadili, sasa malalamiko ya nini, au unatafuta "sympathy" na "hatred" za kidini?
BLUE: Wengi wamekutaka uweke matokeo ya mdogo wako kuona yametoka vipi DIV.III kuwa DIV. I, au angalau ueleze mwanzo alikuwa na points ngapi, lakini unakwepa swali/hoja. Funguka uaminiwe badala ya kudhaniwa kuwa ama umdini au mdaku.
 
' Sikuamini! Lakini nimeona kwenye mtandao ni kweli! kwanini Baraza hawakutangaza officially, wamebadili kimya kimya? baada ya waislamu kulalamika. Kuna jambo kubwa limejificha hapa. Ninaanza kuwaelewa waislamu sasa! Sababu zilizotolewa na Baraza kama ni hizo ni rediculous, na ni kuficha ukweli halisi, why Bible knowledge haikugawanywa kwa 4 kama Islamic Knowledge. Naelewa pia kwa nini always shule za makanisa ' Hutesa(wanasema zimepasua)' Sina imani pia na masomo mengine lazima uchunguzi ufanywe wa kina otherwise inatoa picha kuwa wanayodai waislam kudhulumiwa kielimu miaka yote ni kweli. Sikutegemea kuwa dhulma hiyo ipo hadi Baraza?. Ni jambo la hatari hatari sana.

... Nilishangazwa na waislamu kukataa kuwepo kwenye mchakato wa TCU, sasa ninawaelwa, kama hali yenyewe ndio hii inabidi wajihami kwa mengi. Mwisho wake ni kudai Baraza lao LA Mitihani, kwani hili lililotokea halikubaliki.

Njoo polepole basi, A level wanasoma Divinity, si Bible Knowledge.
 
ha! ha! ha! ha! arifu mie nilimueleza jamaa aliesema hawezekani mtu kutoka div 3 mpaka one.....basi.....mambo ya kugawa sifahamu waligawa vipi baraza..ndio maana nilisema baraza nao wamechemka kichizi arifu.....

Kweli hesabu ngumu.
Hebu chukulia Scenerio hii.
Kwenye islamic knowledge, mwanafunzi alikuwa na jumla ya alama 160, kwa pepa 1&2.
Ikagawanywa kwa 4, anapata 40, ni E.
Ikigawanywa kwa 2, anapata 80, ni A kali tu.
Lets say alikuwa HGL, akawa na His D, Geo D, Eng S, islamic knw E.
Wakichukua masomo matatt aliyofaulu zaid(His, Geo, Isl), anakuwa na Div 3. 13.
Akiwekewa A ya Islamic baada ya kugawanya vema, anakuwa na Div 1. 9, yani His D, Geo D, Isl Knw A.
Sasa hapo mnachoshangaa na kushindwa kuelewa ni kipi?
 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limebadili kinyemela bila taarifa matokeo ya Kidato cha Sita ya wanafunzi Waislam. Hii inatokana na malalamiko yaliyotolewa kuhusu kufeli mno wanafunzi Waislam hasa somo la "Islamic Knowledge". Baraza limebadili matokeo yote ya "Islamic Knowledge" kwa kusema kuwa IT wao alikosea pale alipogawanya wastani kwa 4 badala ya 2 kwa kuwa mitihani ilikuwa miwili.

Ukiingia katika website ya NECTA hutapata "new" ya habari hiyo, hivyo kuonesha Baraza linajijua limefanya makosa, na kubadili kibyemela matokeo. MASWALI MUHIMU:-

1. Jee Waislam waliokwisha omba vyuo wakati wana matokeo tofauti na yaliyotolewa na Baraza inakuwaje?
2. Jee hii si dhulma Waislam waliyokuwa wanaitoa kwa Baraza kuwa linawaonea?
3. Kwa nini Baraza wasijiuzulu kwa kashfa hii kubwa?

NB: Naomba mods msiitoe hii, fuatilieni mtajua ni kweli, mdogo wangu alikuwa na Div III, sasa ana Div I.
Hapo kwenye red ulitaka wahanga wawe akina nani? Mbona muda wote mmnakuwa a fikra za kuonewa? then matokeo ya masomo ya dini hayaangaliwi katika udahili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom