Mjadala: Ni ipi dawa ya kutibu maumivu ya jino bila kung'oa?

mkuu mzizimkavu mimi pia nina tatizo la meno ila yangu hayaumi ilianza kitobo katikati ya meno mawili ya juu baadae ikawa kama mwanya nikaenda hospital wakaziba baada ya muda pakaachia kuna mtu akaniambia pameachia sababu ya moshi maana navuta sana bange sasa ule uwazi unazidi kuongezeka nahofia miaka michache ijayo nitakuwa na mapengo tena reception nahisi kuna mdudu anakula meno yangu msaada mkuu.

DAWA YAKUTIBU MENO NA FIZI

1) Tangawizi ya unga unachanganya pamoja na chumvi kisha unapiga mswaki. Hii inaondosha maumivu ya kuumwa na meno na kuvimba na ufizi na pia kutoa meno harufu mbovu.

2) Maji ya moto na chumvi uwe unasukutuwa kwa mara 3 au 4 kwa siku. Hii inaondosha kuvimba na ufizi na maumivu makali ya meno.

3) Kutafuna karafuu pia inasaidia kuondosha maumivu na uvimbe na harufu.

4) weka unga wa karafuu kwenye sehemu iliyotoboka litatulia

Tumia mojawapo kati ya hizo Dawa hapo juu ukisha pona uje utupe feedback.

ukiwa na matatizo yako ya kibinafsi wasiliana na mimi kwa njia ya baruwa ya pepe email Address yangu hii

hapa fewgoodman@hotmail.com
 
Sijawah kuvumilia maumivu ya jino zaid ya masaa 12. ,jino linauma sana mimi huwa nayatoa, yaani huwa sihitaji ushauri wa dawa toyote ile, sijui dawa ya kutibu jino bila kung'oa. Nimeshatoa meno (magego,) matatu.

Kama linauma pole sana, nenda kwa dentist (daktari wa meno) akusaidie ushauri na tiba pia. Good luck
 
Daktari wa jino anayejua kazi yake hakung'oi jino unless liwe limeharibika sana. Unafanyiwa ROOT CANAL na unaendelea kua na jino lako. Wanachofanya ni kuua mishipa ya fahamu ya kwenye jino.
Ni kiji process and a bit expensive. Kung'olewa jino unatiwa ulemavu bila kujijua ambapo kama una uwezo ungeuzuia.
Nimefanyiwa root canal meno matano. Matatu ya mbele na huwezi kujua.
Kama una uwezo usitoe jino nenda kwa mtaalam wa meno akuelimishe kuhusu root canal.
 
Habari zenu wana jf,

Mimi ninasumbuliwa na maumivu ya jino kwa muda mrefu sasa,nimevulia kwa muda mrefu tatizo hili japo wengi wananishauri niende kwa doctor nikang'oe jino!

Je, kuna dawa yeyote ya kutibu jino bila kung'oa?Saidia mimi,nateseka sana hasa wakati huu wa baridi!

Mbarikiwe sana.

Nawasilisha.

Kwa lugha rahis tu nenda hosp dr atalichunguza jino lako, ataamua matibabu sahihi kwa jino lako. Kung'oa huwa ni final decision kwa lile jino ambalo kwanza limecheleweshwa pili hakuna namna yoyote ya kuliokoa au lina hatarisha maisha yako. Usiogope Dr's were frndly
 
Habari wana JF,

Kama mada inavyoxema hapo. Mimi ni mtoto wa miaka 15 nasumbuliwa na meno hasa ya nyuma upande wa chini yametoboka yakianza kuuma inakuwa ishu. Msaada kwa anayejua dawa/matibabu.

NATANGULIZA SHUKRANI KWENU.
 
Habari wana JF,

Kama mada inavyoxema hapo. Mimi ni mtoto wa miaka 15 nasumbuliwa na meno hasa ya nyuma upande wa chini yametoboka yakianza kuuma inakuwa ishu. Msaada kwa anayejua dawa/matibabu.

NATANGULIZA SHUKRANI KWENU.
Nenda hispital utapata ushauri murua kabisa. Na watajua ni njia gan ya kukusaidia. Kama meno yame oza kabisa wata ng'oa ila kama yameathirika kidogo. Watakusafisha na kuziba yaliyo toboka. Pesa yako tu
 
Habari wana JF,

Kama mada inavyoxema hapo. Mimi ni mtoto wa miaka 15 nasumbuliwa na meno hasa ya nyuma upande wa chini yametoboka yakianza kuuma inakuwa ishu. Msaada kwa anayejua dawa/matibabu.

NATANGULIZA SHUKRANI KWENU.

Take this very serious kwa faida yako na members wote humu JF na hata wale wasio members kuwa ukiwa na tatizo lolote lile la meno dawa kubwa ni kusukutua ule mkojo wako wa kwanza wa asubuhi pale tu unapoamka. amini usiamini mkuu mimi nilikuwa na tatizo kuzidi hilo lako na nilipoambiwa hiyo tiba nikawa siamini huku nikiwa na kinyaa lakini siku moja nikaamua kufumba macho na nikafanya kama nilivyoelekezwa huwezi amini matatizo ya meno sasa nayasikia kwako / kwenu na nimepona kila kitu cha kuhusu meno na kinywa. vile vile mkojo wako mwenyewe wa asubuhi unatibu vitu vingi sana ambavyo nikikuambia hapa hautaamini. kila la kheri na pole kwani najua jinsi gani meno yanavyouma.
 
Back
Top Bottom