Mrejesho baada ya kung'oa jino. Shikamoo Jino

grandMullah23m

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
235
312
Jamani nawaasa na kuwaomba chondechonde tuliheshimu jino. Jino limeniweka kwenye nusu kaput, umwamba wote, mafunzo yote ya kibabe niliyasahau

Nimeapa kuwa balozi mzuri kuhusu haya mambo:

Tuzingatie usafi wa kinywa siku zote maana haya mambo huwa yanaanza mdogomdogo kama mzaha.

Wenzangu mnaopiga zile bia mbili tatu(haswa zile za ofaa za kule kambini) tusisahau kusukutua hata kidogo na maji ya chumvi.

Kumbe sio bia tu...hata juisi tunazogida nyumbani...pamoja na akina energy...zoote hizo usisahau kusukutua na maji masafi mara baada ya kunywa.

HAKUNA DAWA YOYOTE MTAANI itakayotoa suluhu ya kuumwa jino...tofauti na kufika tu hospitalini na kupata matibabu (tuache kubeti na jino tafadhali, nilikuwa mbishi sana ila duh nimejikuta katikati ya uhai na kifo).

Tuache uoga kwenye kufwata matibabu...Kuna tofauti kati ya Dokta, Dakitari na Daktari....aheshimiwe sana huyu wa mwisho(Daktari).

Mwisho kabisa tujipende wenyewe na tuheshimu wake zetu nimepikiwa mtori na mke wangu na anapambania sana afya yangu...michepuko yote haisaidiagi ukifikia hapa....Mama chanja I promise..nimeacha hayo mambo

Viva
 
😂😂😂😂😂😂😂Hapo mwisho umenifurahisha sana, kwamba michepuko haisaidiagi.
 
Mkiambiwa mle vitamin c kama kinga mnasema watu wamezidi ukisasa ungetakiwa uoze mpaka fizi.
 
Dah umenikumbusha mbali mno mno niliumwaga na hio kitu usiku alafu mvua kubwa inapiga balaa niko geto alone sina hata kipande Cha paracetamol!
Nikicheki muda hauendi nizunguka kama kichaa mpaka nikaingia chini ya kitanda(sijui niliwaza Nini!)

Saa kumi na Moja kamili nilishafika zahanati ya levolosi arusha nikalichomoa tu
 
Pia yalinde na kuimarisha meno yako kwa kutafuna vitu vigumu kama mahindi ya kuchoma.

Ni mazoezi na inasaidia sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom