Mjadala: Mume akitaka kuondoka nyumbani, ni lazima aombe ruhusa au kutoa taarifa kwa mkewe?

Busara ni kutoa taarifa mapema sio muda wa kutoka, hii inasaidia kama mke anapingamizi aweze kulisema mapema ili muweze ku sort out. Ninaishi na mke wangu namna hii. Huwa siombi ruhusa ila huwa natoa taarifa mapema na mke wangu hupata fursa ya ku challenge ratiba yangu, imenisaidia kuwa na amani ktk familia yangu
Ni ombi kidiplomasia Mkuu
 
MIE NIKITOKA HOME NINAMUAGA MKE WANGU ILA SWALI LINALO NICHUKIZA UNATEGEMEA KURUDI SAA NGAPI??HILO NDIO SILIPENDI NAONA KAMA KANIONA MTOTO VILEE SIJUI WAKATI MUAFAKA WA KURUDI
 
Ni ombi kidiplomasia Mkuu
Kwa upande mwingine ni kweli kwasababu mke wangu anaweza kunieleza kitu amacho kitanifanya nibaki. Hawezi kunizuia, ila wakati mwingine anaweza kuwa na jambo la msingi ambalo angependa tulifanye pamoja, na kutokana na uzito wa jambo lake naweza kubaki au kutokana na uzito wa jambo langu nitamweleza kuwa ni lazima niende. Usitumie nguvu, ni HEKIMA kidogo tu inatakiwa kuishi kwa wema na mkeo. Fanyeni hivi ili AMANI na UPENDO vistawi katika ndoa zenu.
 
Ni kumpa tu taarifa mwenzako naenda sehemu fulani basi.....hivi imagine unaulizwa mmeo yuko wapi unajibu sijui......inakuja kweli.....? Unapotoa taarifa inasaidia hata kuonyesha kuwa mna mawasiliano mazuri baina ya mke na mme........kwani ukisema unaenda mwenge lazma uende mwenge si unaweza kwenda hata morogoro ingawa umesema unaenda mwenge......
 
Unaweza kunipafaida utakayopata ukifahamu?
Kuna vitu ni nadharia katika ndoa hasa Kama hujajisajili. Mwanamke ni Nguzo ya ndoa Na ni boss. Akikataa usiondoke piga ua hata ukiondoka roho itakusuta urudi. Ila yeye haombi ruhusa bali anatoa taarifa. Umenipata?
 
Ujue kuna jambo lingine halina uzito kabisa.

Siwezi kujiandaa eti kwa ajili ya ruhusa ya kwenda dukani, tena wala si mbali.

Kuna mtoko unaweza aga kabla na kuna mtoko kama wa vocha mimi napotea wala sikuagi.

Watu wa kuaga aga hasa kwa Mwanamme wanakuwa wanatengeneza mazingira mazuri ili itakapotokea la kutokea, awe na sababu aliaga
 
Kwa upande mwingine ni kweli kwasababu mke wangu anaweza kunieleza kitu amacho kitanifanya nibaki. Hawezi kunizuia, ila wakati mwingine anaweza kuwa na jambo la msingi ambalo angependa tulifanye pamoja, na kutokana na uzito wa jambo lake naweza kubaki au kutokana na uzito wa jambo langu nitamweleza kuwa ni lazima niende. Usitumie nguvu, ni HEKIMA kidogo tu inatakiwa kuishi kwa wema na mkeo. Fanyeni hivi ili AMANI na UPENDO vistawi katika ndoa zenu.
Wewe inaonyesha upo katika game. Wengine ni nadharia tu
 
Back
Top Bottom