Mke kuomba ruhusa kwa mume ili kusafiri, hata safari za kikazi - imekaaje? Mama Salma Kikwete huwa anaomba ruhusa! Je, Boss Ladies wanaomba ruhusa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,640
Wanabodi,

Kwa mila na desturi za kiasili za Kiafrika, Traditional African tradition, kwenye ngazi ya familia, mume ndie mkuu wa familia, ndie anayechagua mchumba, ndiye anaya posa, adie anayelipa mahari, kununulia bidhaa ya mke!, ndie anaye oa, na kukabidhiwa bidhaa yake na kumhesabu mkewe ni mali yake!. Hivyo mume huwa yuko huru kutumia mali yake atakavyo!. Mke naye husubiri kuchaguliwa, kuposwa, kulipiwa mahari na kuolewa na kazi yake ni kutoa huduma, kumhudumia mume na familia.

Na ndani ya African families, role ya Mume ndie kichwa cha familia, ndie the bread winner, na role ya mke ni kutunza mume na familia, na traditional place ya mwanamke yaani nafasi ya mwanamke ni jikoni!, (woman's place is at the kitchen). Dini Pia zitatambua different roles and responsibilities kati ya mume na mke. Mume anawajibu wa wa kumpenda mkewe, kumtunza na kuwa the provider, na mke ana wajibu wa kumtii mumewe!, kutunzwa na kumuhudumia mume na kutunza familia.

Wenzetu waliiendelea marriage ni an institution yenye watu wawili equal, hakuna kuoa kwa mahari hivyo hakuna mkubwa na mdogo, hivyo ikitokea mume hana kazi, mke analisha familia bila manyanyaso.

Kutakana na mabadiliko ya kimaendele ya dunia, kumeanza kutokea changing roles, kwa baadhi ya wanawake ndio bread winners kwenye familia zoo, huku waume wakiwa idle, or jobless!, kuna baadhi ya wanawake ni mabosi makazini kwao, basi ubosi huo huuleta hadi nyumbani!.

Nikiwa jijini Bujumbura, Burundi, (Mimi ni miongoni mwa wale tulioitikia ule wito wa mmoja wa viongozi wetu kututaka tuhamie Burundi, hivyo nimehamia Burundi), Mama Salma Kikwete, amekuja hapa Bujumbura, kuhudhuria mkutano wa high level delegation ya viongozi wanawake Barani Afrika, tulipomuona, tumefarijika sana!, Tulioitika Wito Kuhamia Burundi, Tumefarijika Sana Kumuona Former First Lady, Mama Salma Kikwete. Kumbe Rais Akiwa Mwanamke, Nchi Haina First Lady!

Akihutubia mkutano huu Mama Salma anasema baada tu ya kuupokea mwaliko huo, aliomba ruhusa kwa mumewe JK, akamruhusu, ndipo akasafiri!.

Kauli hiyo ya Mama Kikwete, ya kuomba ruhusa kwa mumewe, imeshangiliwa ukumbi mzima na kumuonyeshea ni moja ya tabia njema za mke mwema

Swali ni jee ruhusa hii huombwa hata kwa safari za kikazi?. Jee ma Boss Ladies wengine wote akiwemo Boss la Boss, nao pia huwa wanaomba ruhusa kwa waume zao kabla ya kusafiri safari za kikazi? au hawa huwa wanawataarifu tuu wenzi wao kuhusu safari lakini sio kuomba ruhusa?

Baada ya kuipost hii video kwenye mitandao ya Jamii, imepata different reaction, hivyo kwa vile mimi sasa naishi hapa Bujumbura, Burundi, na Mama Salma Kikwete, bado yupo hapa Bujumbura, nitamtafuta atufafanulie hili la mke kuomba ruhusa kwa mume ndipo ya asafiri!, limekaaje!.

My Take
Kiukweli Kabisa, upendo, utii na unyenyekevu ni pillars muhimu sana za kudumisha ndoa!, kuna ndoa moja naifahamu ya jamaa mmoja fulani, al maarufu wa enzi hizo!, ndoa yao ilivunjika kwa kitu kidogo sana, mume toka familia masikini alioa mke toka familia tajiri, familia ya mke ikampatia binti yao scholarship ya miaka 4 Marekani, mume hakushirikishwa ila aliarifiwa tuu!, na kugharimiwa kwenda kuwa baby sitter wakati mke akiwa darasani and that was the end!, mpaka Leo mke yuko US, mume Bongo, ndoa chali!.

Kuna wanaume wengi wanapitia mateso na manyanyaso makubwa kutoka kwa wake zao ambao ni ma bosi, ila wanaume wameumbwa na kabah, hawasemi!.

Ombi
Enyi wanawake ma Boss Ladies na wenye vipato kuliko waume zenu, msiwanyanyase wanaume zenu kwa dharau mapuuza, mateso na manyanyaso, mkitaka kusafiri ambeni ruhusa kama mama Salma Kikwete, na mara moja moja when you are not too busy, muingie jikoni mpike!, mpikie mumeo mara moja moja na siku umeme ukikatika mpeleke maji ya kuoga bafuni!

Viva Salma Kikwete!
Viva!
Viva Wake Wema Wote!
Viva!
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Tungeweza kutofautisha mamlaka za kwenye Ndoa na zile za Kazini basi maisha yangekua poa sana. Nawasifu sana Askari wote, uaskari unaishia huko huko nasikia wakiwa home wanakua wadogo kama piritoni.

Mama Samia nadhani aliwahi kulisemea hili, kuwa akiwa nyumbani yeye ni Mke na mambo ya "Umakamu wa Raisi" (by then) yanaishia Kazini ila akatahadharisha kuwa wanaume tuna njia nyingi za kupoza kiu ukilinganisha na Wamama.....
 
Sidhani wanawake huomba ruhusa ya kusafiri kikazi kutoka kwa waume wao bali hutoa taarifa tu. Mume apende asipende mke atasafiri tu. Wake mabosi ndiyo kabisa atamtaarifu mumewe kuwa amesafiri kikazi akiwa tayari amefika kituoni.

Binafsi niliwahi kushuhudia mume wa mfanyakazi akienda kwa boss wa mke wake kwa kumfokea kuwa akome kabisa kumpangia mkewe kazi za nje ya kituo. Mume wa mfanyakazi alienda mbali zaidi kwa kumtishia boss huyo kuwa akiendelea kumpangia mkewe kazi za nje ya kituo kitampata cha kumpata na atajuta!

Lakini mke ambaye ni mtumishi alimpinga vikali mume wake na kumwambia boss wake asimsikilize mumewe kwa kuwa posho za safari anazopata zinamsaidia kutunza familia yake na kwamba mume hana uwezo wa kifedha kukidhi mahitaji ya msingi ya familia.

Kwa hiyo waume wengi hawana uwezo wa kuwazuia wake zao kusafiri kikazi na hupewa taarifa tu za safari. Waume ambao wake zao hawajaajiriwa ndiyo wana mamlaka juu ya wake zao kwa kila kitu na wanawafaidi vizuri sana wake zao.
 
Hahaaaa!!!!et wanawafaidii sana wake zao

Traditional Africans mila na desturi, kwenye ngazi ya familia, mume ndie bread winner, ndie anayechagua mchumba, ndiye anayelipa mahari, ndie anaye oa, na kumhesabu mkewe ni mali take!. Mke naye husubiri kuchaguliwa, kuposwa, kulipiwa mahari na kuolewa.

Na ndani ya African families, role ya Mume ndie kichwa cha familia, indie the bread winner, na role ya mke ni kutunza familia, na traditional place, Nafasi ya mwanamke ni jikoni!, (woman's place is at the kitchen). Dini Pia zitatambua different roles and responsibilities kati ya meme na mke. Mume anawajibu wa kumpenda mkewe, na mke ana wajibu wa kumtii mumewe.

Katakana na mabadiliko ya kimaendele ya dunia, kumeanza kutokea changing roles, kwa baadhi ya wanawake ndio bread winners kwenye familia zoo, huku waume wakiwa idle, or jobless!, kuna baadhi ya wanawake ni mabosi magazine kwao.

Nikiwa jijini Bujumbura, Burundi, (Mimi ni miongoni mwa wale tulioitikia ule wito wa mmoja walą viongozi wetu kututaka tuhamie Burundi), Mama Salma Kikwete, amekuja hapa Bujumbura, kuhudhuria mkotano wa viongozi wanawake Bara Afrika.
Akihutubia mkutano huu Mama Salma anasema baada too ya kuupokea mwaliko huo, aliomba ruhusa kwa mumewe JK, akamruhusu, ndipo akasafiri.

Kauli hiyo ya Mama Kikwete, ya kuomba ruhusa kwa mumewe, imeshangiliwa ukumbi mzima na kumuonyeshea ni moja ya tabia nema za mke mwema

Swali ni jee ruhusa hii huombwa hata kwa safari za kikazi?. Jee ma Boss Ladies wengine wote akiwemo Boss la Boss, nao pia hula wanaomba ruhusa kwa waume zao? au hawa wanawataarifu tuu wenzi wao?

Baada ya kuipost hii video kwenye mitandao ya Jamie, imepata different reaction, hivyo kwa vile mimi sasa naishi hapa Bujumbura, Burundi, na Mama Salma Kikwete, bado lupo lupo hapa Bujumbura, nitamtafuta atufafanulie hili la mke kuomba ruhuna ya kusafiri!

My Take
Kiukweli Kabila, upendo, util na unyenyekevu ni pillars kudumisha ndoa, kuna ndoa moja naifahamu ya jamaa fulani mmoja, al maarufu hapa nchini wa eni hizo!, ndoa yao ilivunjika kwa kitu kidogo sana, mume toka familia masikini alia mke toka familia tajiri, familia ya mke ikampatia binti Yao schollarship ya miaka 4 Marekani, mume hakushirikishwa ila aliarifiwa tuu!, and that was the end!, mpaka Leo mke yuko US, mume Bongo, ndoa chali!.

Kuna wanaume wengi wanapitia mateso na manyanyaso makubwa kutoka kwa wake zao amber ni ma bosi, ila wanaume wameumbwa na kabah, hawasemi!.

Ombi
Enyi wanawake ma Boss Ladies na wenye vipato kuliko waume zenu, msiwanyanyase wanaume zenu kwa dharau mapuuza, mateso na manyanyaso, mkitaka kusafiri ambeni ruhusa kama Salma Kikwete, na mara moja moja when not bussy, muingie jikoni mpike!, umeme ukikatika mpeleke maji ya kuoga bafuni!

Viva Salma Kikwete!
Viva!
Viva Wake Wema Wote!

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.

Sawa umeeleweka P.

Mito mingi mikubwa juu Huwa panaonekana kumetulia.

Bt chini maji Huwa yanaenda Kasi ya ajabu.
 
Najua hapo umemsema Mama
 
Kuna kuomba ruhusa; ambapo mwombwaji ataruhusu au atakataa.
Kuna kuomba ruhusa kwa kutoa taarifa; ambapo mwombwaji amefungwa mikono na jibu ni safiri salama.
Kuna kutoa taarifa ya safari (wanawake wengi wapo hapo) ambapo mwombaji halazimiki kufuata kauli ya mtolewa taarifa. Akubali au akatae safari lazima ifanyike (come what may!)
Na kuna kutotoa taarifa ya kuwasili alipokwenda (wanawake walio mabosi).
 
Nadhani kwa taratibu za kihandisi na mambo ya fluid mechanics and dynamics, ujue kabisa Hoja yako hii itazua mjadala mkubwa !!!
====
Usidhani sijaiona post ya kwanza ya uzi huu, la asha!! Nimeona kabisa, lakini bado naiona ya moto sana.
Post ya kwanza ya Uzi iliyo moto ni ipi Hy ndugu TUJITEGEMEE.

Ndugu Pasco Huwa anaanzia mbali Sana kulowesha ardhi iliyobeba mizizi,

Baada ya hapo, utashangaa mti mkubwaaaa Chali.

Burundi Pana mambo!!!!
 
Kauli hiyo ya Mama Kikwete, ya kuomba ruhusa kwa mumewe, imeshangiliwa ukumbi mzima na kumuonyeshea ni moja ya tabia nema za mke mwema
Nadhani hilo la kuomba ruhusa lipo katika misingi ya Uislamu, ambapo ukienda juu zaidi inabidi mume akusindikize hata sokoni au dukani. Kwa Wakristo unatoa taarifa na kuaga, inatosha.
 
Ni nadra sana kumuona Samia akiambatana na mwenza wake. Niliwahi kumuona "Mr" mara moja wakati wa mazishi ya hayati JPM.
Enzi za Mwinyi,Mkapa,Kikwete na Magufuli pale alipokosekana mwenza ubavuni mwa watajwa hao, ilikuwa ni nongwa na habari kubwa ya kuuza magazeti kwa wiki nzima. Najiuliza tu, Chief wetu Hangaya hana sababu ya kuambatana na mwenza wake popote anapokwenda.... Achilia mbali kuomba ruhusa kwa kichwa cha familia? 🤔 :oops:
 
Mke Akishaajiriwa Mnamshukuru Mungu Kwa Kipato Kuongezeka. Ila Fedheha Ni Kubwa na Ndo Sadaka ya Mume Kutunza Ndoa.

Kumbuka Mume akitaarifiwa na Mke wake kuhusu safari ya kikazi, hawezi kamwe kuuliza Kazini kwa Mke kama ni safari ya kweli au Magumashi.

Tunateseka Sana.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom