Mjadala: Mume akitaka kuondoka nyumbani, ni lazima aombe ruhusa au kutoa taarifa kwa mkewe?

lolypop

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,430
1,681
Wapendwa wababa, wamama, vijana wa kike na wa kiume, mliyooa na kuolewa na wenye familia.

Naomba tujadili juu ya suala hili;
ya kwamba mwanaume akitaka kuondoka nyumbani anatakiwa kuomba Ruhusa kwa mkewe au kutoa taarifa?
Mfano:-KUOMBA RUHUSA-mume anamwambia mkewe "mama preta naomba niende dukani kwa kijwajuni one kununua vocha"
KUTOA TAARIFA- mume akiwa ameshajiandaa amevaa viatu, mkono mfukoni anampita mkewe aliyekua amekaa sebuleni huku akiwa ameukaribia mlango " mama preta nafika kwa kikwajuni one kuchukua vocha kwa hiyo badae"

Karibuni tujadili hili .wew unaona ipi ni sahihi
 
Wale waliokulia mboga saba na kusoma accademy labda ndio wanafanya hivyo,..ila kina iwe kama mimi NEVER,...maake makuzi tuliyokulia yanatusuta.

By the way_am proud of,.......!
 
Busara ni kutoa taarifa mapema sio muda wa kutoka, hii inasaidia kama mke anapingamizi aweze kulisema mapema ili muweze ku sort out. Ninaishi na mke wangu namna hii. Huwa siombi ruhusa ila huwa natoa taarifa mapema na mke wangu hupata fursa ya ku challenge ratiba yangu, imenisaidia kuwa na amani ktk familia yangu
 
YES !! ili kudumisha Ustaarabu na uungwana katika familiya ili hata watoto wakulie tabiya na hulka nzuri..Hilo jambo ni lazima lifanyike..Maana unajenga mazingira mazuri kwa zoezi la kuridhiana kati ya wazazi (mume /mke)!!

vingine huko maOfisini mbona hutoki ovyoovyo bila kuomba rukhsa au kutoa taarifa?!!
 
Hinikutokana na malezi utakuta mtu mfano jumamosi na jumapili ikifika saa8 akisha kula chakula anaoga anavaa huyoooo hata kusema tu baadae au naenda sehem ningumu yani tabia ka zambwa!lo minakerekaga sana
Ni tabia mbaya kabisaa hii. Umenena sawa, tabia ya kinyama si ya kibinadamu maana haina kujali utu. Hii mara nyingi hutokana na malezi ambayo mtu alilelewa. Hakuona baba yake akimuaga mama yake na pia hakufunzwa kuwa unavotoka lazima uage.
 
Hinikutokana na malezi utakuta mtu mfano jumamosi na jumapili ikifika saa8 akisha kula chakula anaoga anavaa huyoooo hata kusema tu baadae au naenda sehem ningumu yani tabia ka zambwa!lo minakerekaga sana

Inakera sana, unakuta mtu uko let say jikon au mahali pengine tofauti na chumbani. Mtu anajiandaa anakuja kukuaga na kuondoka hata bila kusema anaelekea wapi? Akipatwa na tatizo hujui unajibu nini kwa jamii, watoto na hata ndugu.

Kwamba aliondoka tu hata bila kuaga!!! Kweli??? Wanaume mjirekebishe hata kama mnaenda kwenye madeal yenu tajeni basi hata direction ili iwe rahisi kufuata nyayo pindi itokeapo dharura...

Mfano. Nitaanzia posta then Magomeni kisha Manzese hata mtu ukisikia tukio unakuwa na pa kuanzia.

Basi wewe mwanamke ufanye hivyo... weeeee utasemwa na wakati mwingine kipigo. Hata sisi tunapenda kuagwa jamani.....
 
Back
Top Bottom