engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
Safi sanaa kijana (MIRAJI) kwa kuusema ukweli,kwani tumekuwa tukitupa lawama kwa chadema mda wote kwa kila jambo baya,
kama mtoto wa Raisi kauona ukweli basi hata Raisi nadhani atakuwa ameuona ukweli huo
Nakupongeza kwa kuwa mtu wa kwanza kwa upande wa ccm kuweza kusema na kuona ukweli huo
kama mtoto wa Raisi kauona ukweli basi hata Raisi nadhani atakuwa ameuona ukweli huo
Nakupongeza kwa kuwa mtu wa kwanza kwa upande wa ccm kuweza kusema na kuona ukweli huo
Chanzo ni Gazeti la Tanzania Daima,
Mtoto wa kikwete aitetea chadema
Asema ni chama cha watanzania kwa ajili ya watanzania.
Mtoto wa rais jk,Miraji jakaya kikwete,amekitetea chama cha CHADEMA akipinga chama hicho kuhusishwa na vurugu mbalimbali zinazotokea nchini,zikiwemo zile za wamachinga zilizotokea jijini mbeya hivi karibuni.
Mtoto huyo wa Rais alionyeshwa kukerwa na watu wenye mtazamo wa kukisingizia chama hicho kikuu cha upinzani kwa kuhusishwa na vurugu wakati hali halisi inaonyesha wazi kuwa wananchi wenyewe awalizishwi na hali ya mambo ilivyo na hivyo kuamua kuwa mstari wa mbele kupigania haki zao.
Miraji aliweka wazi msimamo wake huo kupitia mtandao wa facebook akichangia mjadala mzito uliohoji kwanini chadema kinazingiziwa kuanzisha vurugu.