Miraji Kikwete: Vurugu za Mbeya CHADEMA isizingiziwe

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Safi sanaa kijana (MIRAJI) kwa kuusema ukweli,kwani tumekuwa tukitupa lawama kwa chadema mda wote kwa kila jambo baya,

kama mtoto wa Raisi kauona ukweli basi hata Raisi nadhani atakuwa ameuona ukweli huo

Nakupongeza kwa kuwa mtu wa kwanza kwa upande wa ccm kuweza kusema na kuona ukweli huo
Chanzo ni Gazeti la Tanzania Daima,
Mtoto wa kikwete aitetea chadema
Asema ni chama cha watanzania kwa ajili ya watanzania.

Mtoto wa rais jk,Miraji jakaya kikwete,amekitetea chama cha CHADEMA akipinga chama hicho kuhusishwa na vurugu mbalimbali zinazotokea nchini,zikiwemo zile za wamachinga zilizotokea jijini mbeya hivi karibuni.

Mtoto huyo wa Rais alionyeshwa kukerwa na watu wenye mtazamo wa kukisingizia chama hicho kikuu cha upinzani kwa kuhusishwa na vurugu wakati hali halisi inaonyesha wazi kuwa wananchi wenyewe awalizishwi na hali ya mambo ilivyo na hivyo kuamua kuwa mstari wa mbele kupigania haki zao.

Miraji aliweka wazi msimamo wake huo kupitia mtandao wa facebook akichangia mjadala mzito uliohoji kwanini chadema kinazingiziwa kuanzisha vurugu.
 
Kikwete anawatoto wengi sana, aliyesema ni nani au ni kamchondo, kale kadogest?
 
Hakuna kitu pale labda kaambiwa aseme hivyo kichwa hakina kitu kile kimejaa picha za akina da.......tu
 
Hivi akisema mtoto yeyote wa Kikwete ndio tamko la Serikali? acheni kutuzingua bwana, aseme atakacho shauri yake, sisi tunataka majibu ya zile mali alizojilimbikizia chanzo chake ni nini?
 
Safi sanaa kijana (MIRAJI) kwa kuusema ukweli,kwani tumekuwa tukitupa lawama kwa chadema mda wote kwa kila jambo baya,

kama mtoto wa Raisi kauona ukweli basi hata Raisi nadhani atakuwa ameuona ukweli huo

Nakupongeza kwa kuwa mtu wa kwanza kwa upande wa ccm kuweza kusema na kuona ukweli huo

Mkuu tupe detailed infromation plz..thread yako haina mashiko...
 
Kasema hivyo lini na wapi??
Unapokua unapost thread,
Jivue uhusika wa M-post thread ujivike wa msomaji kisha ujiulize inaeleweka ama vipi kabla ya kui-submit.
 
Jamani,

Mimi sijaelewa vizuri heading na pongezi anazopewa huyu mnayemwita mtoto wa Rais. Heading inasomeka: "VURUGU ZA MBEYA CDM ISINGIZIWE" yaani ametaka CDM ibambikizwe. Unless mleta mada aseme alimaanisha "ISISINGIZIWE".

Naomba kutoa hoja.
 
Mkuu tupe detailed infromation plz..thread yako haina mashiko...

acha uvivu mkuu

ingia ktk face book,sikiliza magazeti,na hata igoogle utapata yote hayo,mimi nimekupa 20% yaliyobaki 80% tafuta

nilichokiweka kipo kama klivyo ktk mitandao mingine ya kijamii
 
Jamani,

Mimi sijaelewa vizuri heading na pongezi anazopewa huyu mnayemwita mtoto wa Rais. Heading inasomeka: "VURUGU ZA MBEYA CDM ISINGIZIWE" yaani ametaka CDM ibambikizwe. Unless mleta mada aseme alimaanisha "ISISINGIZIWE".

Naomba kutoa hoja.

soma tena,ni swala la uelewa hapo mkuu
 
Mbona hujaeleweka mkuu! mtoto yupi? aliongea wapi? au ulikuwa unapiga naye story2 akasema hivyo ukapagawa mwenyewe
 
Back
Top Bottom