Mimbo ya utotoni

Maperaa X 2.. Mama kapika maperaa nakifaranga chakuku, tia hapa tia hapa( hapo unaonesha upande wa kushoto na kulia wa kiuno) kama utaki niambie, nikae chini nil.....
 
namsaka mke wangu namsaka mke wangu,hapa hayupo hapa hayupo,kaenda wapi kaenda wapi,kaenda kusuka kaenda kusuka,chanuo kampa nani, chanuo kampa nani,kampa msusi kampa msusi......

hadi leo sijui kama huu wimbo ulikuwa ni fumbo la mambo ya ndoa ama vipi?
 
Jua lile literemke mama haiya iya iya iya mama * 2
nyota nazo ziteremke mama haiya iya iya iya iya mama *2
hii tulikuwa tunakimbia mchaka mchaka shuleni ndio tunaimba.
 
Maperaa X 2.. Mama kapika maperaa nakifaranga chakuku, tia hapa tia hapa( hapo unaonesha upande wa kushoto na kulia wa kiuno) kama utaki niambie, nikae chini nil.....

hehehehe jamani mtalingolo umenifurahisha kweli enhe mwingine mtoto mzuri?
 
namsaka mke wangu namsaka mke wangu,hapa hayupo hapa hayupo,kaenda wapi kaenda wapi,kaenda kusuka kaenda kusuka,chanuo kampa nani, chanuo kampa nani,kampa msusi kampa msusi......

hadi leo sijui kama huu wimbo ulikuwa ni fumbo la mambo ya ndoa ama vipi?

nahisi ulikuwa una maana.Yaani baba labda alikuwa anamkataza mke wake kwenda saluni,mkewe akatoroka na kila kitu kinachohitajika kapewa na msusi lol mafuta kampa nani mafuta kampa nani?msusi msusi hehe
 
Jua lile literemke mama haiya iya iya iya mama * 2
nyota nazo ziteremke mama haiya iya iya iya iya mama *2
hii tulikuwa tunakimbia mchaka mchaka shuleni ndio tunaimba.

hivi leo ukikimbizwa utakimbia futi ngapi?
 
ukuti ukuti wa meme wa meme,mwenzetu mwenzetu,kagongwa kagongwa,na nini na nini,na gari na gari,tumpelele mnazi mmoja,asiende kusema kwa mama yake..
 
yesa yesa yesa yeeee

mbona kila wimbo/mchezo nilioucheza/imba unaujua?hivi hadi leo hizi nyimbo watoto wa siku hizi wanziimba?tulikuwa kitaa kimoja nini?inawezekana nilikuwa baba ulikuwa mama(kibaba/kimama)lol
 
mbona kila wimbo/mchezo nilioucheza/imba unaujua?hivi hadi leo hizi nyimbo watoto wa siku hizi wanziimba?tulikuwa kitaa kimoja nini?inawezekana nilikuwa baba ulikuwa mama(kibaba/kimama)lol

hehe mimi nilikulia huko nyamokisingo kanda za kati kusini na wewe je?
Watoto wa siku hizi wanaimba shakira shakira
 
upane wa kwanza: ''mwaanangu ee..''
upande wa pili: ''eee''
upane wa kwanza: ''mimi baba yenu''
upande wa pili: ''eee''
upane wa kwanza: ''sina nguvu tena''
upande wa pili: ''eee''

upane wa kwanza: ''..ya kuua simba...''

.............................................

sorry nimesahau, huu sio wimbo ni michezo ya utotoni.
 
simba ni mkali eeeh,aliua baba eeeh,akaua mama hehehe umenikumbusha huu wimbo jamani nilikuwa naupenda kweli
 
Tulinge bayooo x2
Tunamuomba kaba kabana aingie kati atuonyeshe maringo yake bingili bingili mpaka chini!
 
Back
Top Bottom