Mimbo ya utotoni

aaah kumbe na wewe ni mtu wa tizi ? Poa ila wewe upo mwanza na mimi nipo mbali . Labda tuwe tunaamshana asubuhi kwa pm ili tusipitiwe na usingizi.

eti kuamshana kwa PM hehe,kwani wewe uko api?
 
Ukuti ukuti
Wameme Wameme
Wamwisho akamatwe
Atiwe gerezani.

-Halafu kuna ule wa
Kula mbakishie baba ukiangusha kijiti unakula kipigo hadi ukimbilie ushike mti ndipo uachwe
 
Watoto wa siku hizi waliozaliwa kipindi cha jakaya wenyewe wamejikita kwenye bongo fleva za akina diamond na ali kiba. Sidhani kama wanapata ladha tulioipata sisi
Nakumbuka mimbo tuliyokuwa tunaimba tukiwa watoto halafu natabasamu mwenyewe Kama huu
sandakalawe amina,mwenye kupata apate,kipapatio cha kuku,kuku gani?mweupe,analiaje?kwiii kwiii
wewe unakumbuka upi?either wa shuleni au mtaani?

Kabakabana! Kwa nini hukuifanyia editing title ya thread yako? Niliisoma kama Mimba za utotoni, halafu niliposoma maelezo yake nikagundua ni nyimbo za utotoni, ingawa hukuandika hivyo. Mimi hata moja sikumbuki. Wacheki hawa wafuatao wanakumbuka vizuri kwa sababu bado yankee sana.
1,Radhia Sweety
2.Golden Mpoleee
3.Smile
4.Kipipi
 
hehe mimi nilikulia huko nyamokisingo kanda za kati kusini na wewe je?
Watoto wa siku hizi wanaimba shakira shakira
hapo kwenye red nimekoma mwenyewe...usingezijua hivyo hizi nyimbo...anyways inawezekana nyimbo hizi ni common tanzania nzima
 
Ukuti ukuti
Wameme Wameme
Wamwisho akamatwe
Atiwe gerezani.

-Halafu kuna ule wa
Kula mbakishie baba ukiangusha kijiti unakula kipigo hadi ukimbilie ushike mti ndipo uachwe

kaka usinikumbushe bong'oa,..mtu anadondosha shilingi makusudi ukiinama kuiokota bonge la shuti mat*ko...
 
1.aamina,amina kadara,sinoowela,amina dumpepee,amina magerezaa,magereza,amina tush,tush,tush,tush,kama dada wanipenda, kaninunulie zeze,nikilala kitandani, zeze lanibembeleza..
2.by short i love you baby.....(huu wimbo hadi leo sijui kama unaimbwa wote kwa kiswahili au kidhungu maana tulivyokuwa tunaimba ni soo!!)
 
Ukuti ukuti
Wameme Wameme
Wamwisho akamatwe
Atiwe gerezani.

-Halafu kuna ule wa
Kula mbakishie baba ukiangusha kijiti unakula kipigo hadi ukimbilie ushike mti ndipo uachwe

mimi nilikuwa mjanja kwenye kula mbakishie baba ikikaribia kuisha nakuula kidoogo ili nisidondoshe kijiti.
 
Kabakabana! Kwa nini hukuifanyia editing title ya thread yako? Niliisoma kama Mimba za utotoni, halafu niliposoma maelezo yake nikagundua ni nyimbo za utotoni, ingawa hukuandika hivyo. Mimi hata moja sikumbuki. Wacheki hawa wafuatao wanakumbuka vizuri kwa sababu bado yankee sana.
1,Radhia Sweety
2.Golden Mpoleee
3.Smile
4.Kipipi

hawataki kuchangia ili tuwaone wakubwa eeti.
 
Nani anakumbuka hii ?
Maua mazuri yapendeza * 2
ukiyatazama yanameremeta hakuna limoja lisilo pendeza * 2 Nzu nzu nzu eeh mama nyukilia we .
 
1.aamina,amina kadara,sinoowela,amina dumpepee,amina magerezaa,magereza,amina tush,tush,tush,tush,kama dada wanipenda, kaninunulie zeze,nikilala kitandani, zeze lanibembeleza..
2.by short i love you baby.....(huu wimbo hadi leo sijui kama unaimbwa wote kwa kiswahili au kidhungu maana tulivyokuwa tunaimba ni soo!!)

ni by short au by shoo jamani? Mimi nakumbuka by shoo i love u baby the baby to the saa sijui nini na nini tena
 
Nani anakumbuka hii ?
Maua mazuri yapendeza * 2
ukiyatazama yanameremeta hakuna limoja lisilo pendeza * 2 Nzu nzu nzu eeh mama nyukilia we .

huu tuliuimba vidudu kwa marehemu babu kaiwanga
 
Masikini tunda langu ae, ae,
tunda lenye rangi yangu ae, ae, nilikwenda msituni ae, ae, mimi na rafiki yangu ae, ae, risasi ikaponyoka ae, ae, ikampiga rafiki ae, ae.
 
Back
Top Bottom