Miaka takribani 50 ya Uhuru Tanzania: Ni yapi ya kujivunia?

Viongozi wengi wana duniani hasa wa nchi ni wa koloni ila tofauti inakuja ni nani na kwa njia zipi wanatekeleza ukoloni wao. Tanzania kwa kuwa hatuna ushawishi hata kwa majirani zetu tumebaki kupigana pini sisi kwa sisi,mbuzi ale kulingana na urefu wake hata ndani ya familia. Yaani kiufupi Tz turipofika mfumo unaturazimisha kukamuana mpaka basi.
 
hivi Tanzania ina haja ya kusheherekea miaka hamsani ya uhuru wakati taifa liko katika msiba wa matatizo lukuki? nadhani hizo hela za kuandalia hizo sheree zingetumika kununulia majenereta ya kupunguza mgao wa hili giza!!!!!
 
Miaka hamsini ya uhuru na mfumo wa nchi kuegemea zaidi kwenye siasa kuliko kujali utaalamu,
na kuwafanya wananchi wa Tanzania kuishi kwenye kiza kinene baada ya kujitokeza jinai ya
kugawiwa umeme.


Inawezekanaje nchi yenye vyanzo vyake yenyewe vya umeme, kuwa na mgawo wa umeme?

Uchumi wa Tanzania unaporomoka kwa kasi kubwa kutokana na ukosefu wa nguvu ya umeme
wa uhakika pamoja na kuwa madini ya Uranium yanayotengeneza nishati ya nyuklia yanapatikana
kwa wingi Tanzania. Madini ambayo kwa nchi kama Iran na Korea yanatumika kwenye uzalishaji
nguvu za umeme kwa njia ya nyuklia.

Mgao huu wa umeme licha ya kudhoofisha uchumi wa taifa na wa mtu mmoja mmoja unasababisha
uharibifu na uchafuzi wa mazingira. Majenereta yanayofanya kazi mchana kutwa mijini yamekuwa
yanachafua mazingira kwa moshi na hata kelele.
 
Na unaangalia viongozi wanatoa matamko wakicheka cheka maana hili hawalioni kama tatizo
 
Miaka 50 ya uhuru kwa mafisadi(tunaowaita viongozi) kuitafuna kwa fujo nchi yetu hata kuvimbiwa na hatimaye kututapikia,na sisi tukifurahia style ya utapikaji wao kwa UZEZETA WETU...
 
Nitangulie kuwaomba radhi wana Jf ambao mtakuwa mmekwazika kwa hoja yangu hii, lakini sina namna ya kubadilisha kile kilichoko kwenye fikra zangu.
Yeyote ambaye anapata raha katika nchi hii bila shaka wazo langu ni la kipumbavu na halina maana kwake iwapo ni mbinafsi, lakini mtu huyo huyo kama anapata raha lakini anawafikiria watanzania wenzake wanaopata taabu na mashaka bila shaka hili ni wazo na hoja nzuri kwake.
KWANINI TUTAWALIWE UPYA?
Licha ya ukatili wao lakini ni jambo lisilopingika kwamba Wakoloni walifanya mengi tena kwa kasi kubwa kuliko zama hizi za hawa wakoloni weusi (CCM), ukiangalia barabara nyingi ambazo tunazitumia sasa hivi asili yake ni ukoloni, hebu jiulize kama kazi hii wangepewa ‘CCM' inangekuwaje?
Ni wazi kwamba ingechukua muda mrefu, isingefanyika au tungeshuhudia vichochoro badala ya barabara. Hebu angalia mambo yaliyofanywa na wakoloni, kwanini nisitamani tuje kutawaliwa upya. Hawa waliopo si viongozi bali ni watawala pia, we si unaona vyeo vyao? Afisa tawala mkoa na wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni wanajeshi. Kwanini wajaze nafasi hizo kwa wanajeshi wakati vijana wengi wanamaliza na kjukosa ajira? Kwanini waweke makapteni na mameja wastaafu?
Wazo la kutamani nchi yetu itawaliwe sana linanijia ninapoiona hali halisi ya nchi yetu inavyozidi kuwa mbaya, Umeme, maji ufisadi n.k ni miongoni mwa vitu vinavyolitafuna taifa kwa kiasi kikubwa. Tena hao mafisadi wenyewe wako tayari kukimbizia fedha katika mabenki ya nje na ikitokea wakafa fedha hupotelea huko!
Narudia tena hali jinsi ilivyo natamani hii nchi irudi tena katika mikono ya wakoloni. Yako mengi naweza kuandika kuipa nguvu hoja yangu lakini sipendi kuwachosha
Ahsanteni!.
 
Mkuu mimi nakuunga mkono kwani nchi hii inahitaji viongozi kama DC Mnali ambaye aliwachapa viboko walimu pale waliposhindwa kufaulisha kwa uzembe wa makusudi! Adhabu ya viboko isiishie kwa watoto mashuleni tu hata kwa makatibu wakuu na wakurugenzi wanaotorosha wanyama na wote wasiowajibika wapewe adhabu hiyo ambayo ni muafaka kabisa kwa wakati tulionao!
 
Naunga mkono hoja kwa sababu mkoloni akirudi yatajiri yafuatayo,
  • FAIDA----
  1. Atajenga reli za kisasa na kuleta treni za umeme kumrahisishia usafiri
  2. Atajenga viwanja vya ndege vya kisasa na kuleta Boeing mpya
  3. Atajenga barabara za kisasa flying over za kutosha
  4. Atajenga bwawa kubwa linaloanzia baharini ili kuondoa mgao wa giza kumpa ufanisi wa kazi
  5. Atatoa elimu bure kama zamani
  • HASARA--
  1. Atatorosha twiga, faru, swala...
  2. Atatorosha tanzanite, almasi, dhahabu,
  3. Atatuachia mahandaki ya kufa mtu
naona kama faida ni nyingi kuliko hasara au,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Tujiulize na tutafakari kati ya CCM na Mkolonoi, je ni serikaloi gani imeweza kumpatia mwananchi maisha yenye unafuu?
Tukipata jawabu tuchukue maamuzi magumu
 
Yet another crapulous argument from apparently an alky who seems to have been sick from katzenjammer and now he's finding a way of getting rid of it.
 
Bora mkoloni aisee angalau hela ilikuwa na thamani si sasa hivi mambo ovyo tu tumechoka
 
Back
Top Bottom