Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Salaam kwenu.
Ni kweli lengo la kupigania Uhuru wa Tanganyika, lilikuwa kuwafanya wananchi ama raia kuwa huru kuchagua aina ya uongozi na viongozi wanaotaka, kujiamulia mambo yao ya Kiuchumi, Kisiasa na Kiutamaduni bila kuingiliwa na kikundi ama mataifa ya nje.
Lakini tujiulize hapa, baada ya uhuru kupatikana. Nini kilitokea?
Tujiulize, je tambo hizo ndizo zilizopelekea kumfukuza mkoloni ili tutengeneze kikundi cha wahuni watakaojimilikisha nchi kama wameiokota jangwani?
Tusipozinduka leo, tutaendelea kusubiri hisani za Rais ambapo ndiye anayeonekana kumiliki kila kitu bila kuhojiwa na yeyote.
I rest my case

- Je Watanganyika walikuwa huru kufanya shughuli za siasa ama waliamuliwa aina ya siasa ya kuifuata?
- Je Watanzania walikuwa huru kuchagua mfumo wa namna nchi itakavyoendeshwa? Au waliundiwa Katiba kwa utashi wa viongozi?
- Je Watanganyika walikuwa huru kujiamulia namna ya kuuendesha uchumi wa nchi yao au waliamuliwa namna uchumi utakavyoendeshwa?
- Je elimu ya Tanganyika ilikuwa kwa minajili ya kuwanasua watu dhidi ya ujinga?