Miaka takribani 50 ya Uhuru Tanzania: Ni yapi ya kujivunia?

hii ilikuwa kwenye ufunguzi wa tawi la chuo cha mipango......nina pics nyingi sana!!wabunge karibu wote walishiriki kwenye activity..kulikuwa na uchaguzi wa tawi la st john, then kufungua tawi......ukizitaka nyingine nipe email adress yako...nina picha nyingi za chadema activities dodoma...
 
Siyo siri tena kuwa hali ya watanzania waliowengi ni mbaya bin taabani bin
kwishiney kama siyo mufilisi. Kwanzia mijini hadi vijijini,mahakamani hadi
magerezani,mashuleni hadi mavyuoni,mahospitalini hadi kwa waganga wa jadi.
maofisini hadi mitaani nk. yaani kote huko hali ni tete ile mbaya. Mengi tume
zungumza kuhusiana na hali mbaya hii kupitia matv,radio,magazeti na mablog
lakini hakuna chochote kilichobadilika! sanasana ufisadi ndiyo unaongezeka na
watu tunazidi kupungua kwa vifo vya njaa,magonjwa na kulipuliwa na mabomu
huku mafisadi wakiishi kama wako peponi. Yaani kwa ufupi watanzania tupo hoi
bin menyemenye. walionacho wanazidi kujiongezea na tusiokuwanacho hata kile
kidogo tunanyang'anywa! Sasa je,kwahali hii tuliyonayo ya kukatisha tamaa bin
choka mbaya ni nani aichukue hii nchi kati ya watu hawa 3?
1.Ni bora jeshi (jwtz) waishike nchi na watutawale kidikteta?
2.Au serikali ya ccm iendelee tu kututawala kwa kutuua na mateso?
3.Au ni bora tuwaombe wakoloni warudi kuja kututawala huku wakiiba utajiri wetu? - Nawasilisha wajahmeni

wakoloni wenye upendo kama akina Williamson Diamonds Ltd hawapo tena fika Buzwagi ujionee, kufa hatufi ila cha moto tunakipata fresh. TULIE NA NEC:rain::rain:
 
haya wadau, ngoja niwape kwa ufupi. ilikuwa ufunguzi tawi la chadema tawi la chuo cha mipango...155 Halima mdee akiwapasha waheshimiwa waprotokali kuwa kizazi kipya ni digital na sio analogue, 148..bango lililomchinja shibuda na kumzuia mbowe asimpe uwaziri kivuli, 203 diwani kata ya igogo ambaye anasoma mwaka wa 4 ud akiwapa shavu vijana, 116 regia mtea akiwapa moyo wanawake na wasichana...192 na 200 mbegu zilizopandwa na tumaini jipya kwa taifa...ebu wasome machoni kwao hakuna mchezo sasa...258 mnyika akimwaga nondo kwa umakini..168 mwenyekiti wa tawi la chuo cha mipango na katibu wa shirikisho la bavicha vyuo vikuu kanda ya kati aliyemwaga sumu moja kwa moja kuwa shibuda abakize malezi yake huko huko CCM..185 profesa kahigi akiaga maana ilikuwa kwa shift....225 kichwa mkurugenzi wa bunge wa chadema john mrema na aliyekuwa mgombea wa vunjo john mrema akihutubia....344 wabunge vijana kutoka zanzibar wa kuteuliwa ambao wamewahakikishia vijana kuwa tangu waingie chadema hawajawahi kuambiwa wabadilishe dini!!
mnataka nyingine?
 

Attachments

  • IMAG0155.jpg
    IMAG0155.jpg
    301.2 KB · Views: 29
  • IMAG0148.jpg
    IMAG0148.jpg
    262.2 KB · Views: 35
  • IMAG0203.jpg
    IMAG0203.jpg
    347.6 KB · Views: 29
  • IMAG0116.jpg
    IMAG0116.jpg
    261.5 KB · Views: 28
  • IMAG0154.jpg
    IMAG0154.jpg
    224.1 KB · Views: 34
  • IMAG0147.jpg
    IMAG0147.jpg
    275.4 KB · Views: 29
  • IMAG0192.jpg
    IMAG0192.jpg
    307.2 KB · Views: 31
  • IMAG0200.jpg
    IMAG0200.jpg
    353.6 KB · Views: 38
  • IMAG0258.jpg
    IMAG0258.jpg
    333.6 KB · Views: 26
  • IMAG0168.jpg
    IMAG0168.jpg
    223.2 KB · Views: 25
  • IMAG0185.jpg
    IMAG0185.jpg
    221.8 KB · Views: 31
  • IMAG0255.jpg
    IMAG0255.jpg
    359.7 KB · Views: 31
  • IMAG0344.jpg
    IMAG0344.jpg
    239.8 KB · Views: 30
haya wadau, ngoja niwape kwa ufupi. ilikuwa ufunguzi tawi la chadema tawi la chuo cha mipango...155 Halima mdee akiwapasha waheshimiwa waprotokali kuwa kizazi kipya ni digital na sio analogue, 148..bango lililomchinja shibuda na kumzuia mbowe asimpe uwaziri kivuli, 203 diwani kata ya igogo ambaye anasoma mwaka wa 4 ud akiwapa shavu vijana, 116 regia mtea akiwapa moyo wanawake na wasichana...192 na 200 mbegu zilizopandwa na tumaini jipya kwa taifa...ebu wasome machoni kwao hakuna mchezo sasa...258 mnyika akimwaga nondo kwa umakini..168 mwenyekiti wa tawi la chuo cha mipango na katibu wa shirikisho la bavicha vyuo vikuu kanda ya kati aliyemwaga sumu moja kwa moja kuwa shibuda abakize malezi yake huko huko CCM..185 profesa kahigi akiaga maana ilikuwa kwa shift....225 kichwa mkurugenzi wa bunge wa chadema john mrema na aliyekuwa mgombea wa vunjo john mrema akihutubia....344 wabunge vijana kutoka zanzibar wa kuteuliwa ambao wamewahakikishia vijana kuwa tangu waingie chadema hawajawahi kuambiwa wabadilishe dini!!
mnataka nyingine?
Mkuu ahsante sana kwa hizi picha! hakika zimenifariji sana. Ila unapoudhuria kwenye matukio kama haya
jaribu kutuhabarisha kupitia hapa hapa JF live chart ili kutupata latest news
 
Yaani Wakoloni weupe wana afadhali kuliko hawa wakoloni weusi kama sisi! Hawa wakoloni weusi hawatuangalii usoni wanatupiga tu ngumi za pua!
 
Maamuzi mengi muhimu ya nchi yetu yanafanywa na taasisi nyingi, zinazoongozwa na mtu mmoja mmoja kwa niaba ya wahusika regardless wananchi wanataka nini. Wananchi kwa ujumla hawana mamlaka yeyote ya kufanya maamuzi dhidi ya nchi yao.

Wao kazi yao ni kupokea maamuzi yanayofanywa na taasisi hizo kwa niaba yao, na nitaelezea vizuri na kwa mifano. Ukiangalia kwa makini si rahisi kwa mgombea wa chama chochote ukiondoa ccm kuweza kuchaguliwa kuwa rais nchi hii kwa sababu moja kuu, nayo ni nafasi ya urais kwa nchi yetu imewekwa chini ya vyombo maalum kama Tume ya uchaguzi ambacho kiko ktk full control yao.

Ofisi ya msajili wa vyama na taasisi nyingine nyingi ziko kwa ajili ya kuweza ku control vyama vya siasa kwa niaba ya wahusika(ccm). Maamuzi makubwa ya taasisi nyingi yamewekwa chini ya mtu mmoja kwa ajili ya wahusika kuwa na full control na chombo husika. Mfano mzuri ni msajili wa vyama anayo mamlaka yeye peke yake kukifuta chama cha siasa. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi peke yake anaweza kuamua nani awe Rais, hii inamaanisha nini kwetu Watanzania? inamaanisha kuwa mamlaka yote ya nchi hii hayako chini ya mimi na wewe kwa maana ya umma bali yako chini ya mamlaka hizi ambazo wahusika wanao ziongoza kwa niaba ya wahusika(CCM), na sisi watanzania tumebaki hatuna freedom kwa maana ya maamuzi juu ya nchi yetu. Kwa hiyo hapa kwenye mabadiliko ya katiba ndio eneo pekee la kuweza kuirudisha nchi hii mikononi mwa wananchi wenyewe na kuzinyanyanga taasisi hizi nguvu ya kuweza kututawala tena kinyume na matakwa yetu.

Hakuna tofauti kati ya mkoloni na CCM kwani mkoloni alitumia taasisi zake alizozi control kukandamiza maamuzi ya wengi kwa niaba ya mabwana zao kama vile CCM inavyozitumia taasisi zake kuwakandamiza walio wengi kwa niaba ya mabwana wachache weusi. Mabadiliko ya katiba Tanzania kwangu mimi ni struggle for independence for our lovely country. CCM inaogopa mabadiliko ya katiba kufanywa na wananchi wenyewe kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kurudisha madaraka ya nchi kwa wananchi badala ya taasisi zake.
 
kila siku huwa ninajiuliza inakuwaje pale mambo yanaposimamiwa na watu weupe yanakwenda sawa iwe ni ujenzi, huduma za afya, huduma za umeme, na nyinginezo nyingi,
tatizo linakuja pale tunapoachiwa wazawa (waswahili) tunaanza kuchakachua hata kama huduma hiyo anaipata mzazi wake kule nyaishozi.
kutakuwa na hujuma kubwa ikiwemo kukata na kuiba miundo mbinu, kama ni umeme tutazima bila hata ya sababu ya msingi ili mradi watu walalame tu, hospitalini tutauza dawa kwa bei ya kutupa ili mradiwa tu wakose huduma mzuri.
ndo maana nauliza kuwa tunahitaji kutawaliwa kwa mara nyingine? Maana wale walioonja matunda ya kutawaliwa ndo waliofanya vizuri kama nyerere, na wengine wengi waliokuwepo kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza hawappo madarakani na uraiani.
tutafakari pamoja.
 
Nimekuelewa hasa unapokuja na njia mbadala ya kutaka kerekebisha hali ya nchi yetu ambayo ipo ukingoni kuzama. Jibu unaloshauri si sahii bali inathibitisha jinsi ulivyokata tamaa. Hatuitaji wakoloni ili tuweze kuendelea ila inabidi tunyanyuke tuwe wakoloni wa viongozi wetu. Hili litakuwa ni moja tu nalo ni kuhakikisha tunaufanya ukoloni kwa kuchagua viongozi ambao tutaweza kuwaeleza tunataka nini, tunataka kwenda wapi, tumechoka na nini, hatutaki wafanye nini, na wajue kuwa uongozi ni msalaba na utumwa kwa wananchi.
 
kwani lini ulipata uhuru? hawajakupa uhuru wa kufanya maamuzi,leo wewe si unashabikia wamarekani wanavyovamia nchi za watu na kufanya wanachotaka? wafaransa waingereza wote unawashabikia. wazee wetu waliwatimua sasa sisi tumewarudisha. Nilisikitika zaidi siku moja Slaa anahojiwa chanel ten akazungumza eti chama chake wanashirikia na republican na kile chama cha uingereza nikajiuliza, kama hichi chama ni cha kuwatetea watanzania walalahoi ambapo ulalahoi wao ni wakihistoria toka enzi za hao jamaa sasa iweje tena tuwakumbatie? Ivi ukisha chukua pesa yao utaweza kupinga matashi yao? viongozi ambao huonesha kupinga upuuzi huo wa kuingiliwa katika maamuzi ya kiinchi na wamarekani hutangazwa vibaya ili kuturubuni akili zetu tumchukie mfano mugabe,gadafi,najadi.
 
Kwa yanayoendelea Tanzania, na mimi natakamani wakoloni warudi, tunaweza kupata Reli nyingine na kupata huduma zaidi. Watu wangapi sasa hivi wanakimbilia Afrika Kusini kwa sababu mkoloni alikataa muda mrefu. Kenya wanatuzidi kwa sababu Mwingereza aliwekeza sana. Mimi natamani Mjerumani arudi Tanzania watu wapate akili. Wewe nchi gani Polisi anaua rahia na anaendelea na kazi. Hata kama ni mwizi polisi kuua ni mwiko.
Jamani Wajerumani njoo tunakufa huku!!!!!!!!!!!!
 
Nimepokea habari ya kukamatwa kwa M/kiti wa CDM Bwana Freeman Mbowe kwa majonzi makubwa sana lakini, huku nikiendelea kutafakari nikasikia Pia Bwana Zitto Kabwe pia yupo rumande ya Polisi Singida na baadaye kuachiwa, ni vyema kila mmoja wetu hasa wana mapinduzi kutafakali hili swala kwa Pamoja na matukio ya kukamatwa kwa Bwana Tundu Lissu, Lema na wenzao wanne huko Tarime pamoja na watanzania wanaokamatwa kila siku katika kila kona za Tanzania bila kosa na kuonewa na polisi na hata kubambikiziwa kesi za uongo kwa ajili ya kuwakomo, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha.

Ninachotaka kusema hapa leo siyo ujinga wa Jeshi la Polisi na jinsi wasivyojuwa hata kazi zao kwasababu ya ama kuendelea kupata mafunzo yenye mbinu walizorithi kwa mkoloni mzungu au kuwa Jeshi kubwa lenye wajinga wengi kwa maana kwa takribani miaka 50 sasa Jeshi hilo liliachwa kuwa la Form Four Failure na Darasa la Saba lakini hata hivyo Form Four wanaojiunga na hilo Jeshi wengi wao wamekuwa ni watu wanaotumia vyeti vya ndugu na jamaa zao huku wao kihalisia ni ama Form Two Failure au aliyeacha shule kwa kuogopa umande wakitokea katika katika mitaa iliyojaa kila aina ya lanaa za kubaka dada na mama zao.

Lengo langu kuu ni kuwe swali mezani! ili wana JF tupeane kumbukumbu sahihi na pia tujue umuhimu wa hawa viongozi wetu kukamatwa, kunyanyaswa na hata kudhalilishwa maana tukisha kujua hilo basi tutapiga moyo konge na tutajua umuhimu wa kuchagua viongozi ambao wapo tayari kunyanyashwa, kuonewa na kudhalilishwa kwa ajili yetu! Tutashagilia na tutakuwa makini katika kila chaguzi kuhakikisha kuwa hao ndio tunao wapa kura zetu zote maana wapo mbele yetu nasi tupo nyuma yao.

Swali langu kwa wana-JF ni kuwa "Nani anajua nchni yoyote katikia Bara la Afrika ambayo ilipata uhuru wa kweli kutoka kwa vyama na watawala waliorithi Ukoloni kutoka kwa Wazungu bila kunyanyashwa, kuonewa, kukamatwa na hata kufungwa jela kwa wapigania uhuru wa Afrika?" Kama hamna basi tujivunie kukamatwa kwa viongozi wetu kwa ajili yetu, tuwape moyo na tuombe Mungu atuongezee viongozi wengi zaidi kama hao.

Kwa wale wasiojua nini maana ya uhuru, ili mjadala husiwape tabu bure, nawapa kiashiria kuwa walichofanya wazungu katika karne ya kumi na tisa ni kukabidhi serikali za nchni za Afrika kwa waafrika na siyo kutoa uhuru kwa wananchni, hatua ya kutoa uhuru kwa wananchni ilipaswa kuanzishwa na wale viongozi waliopokea madaraka kutoka kwa Wazungu, kwa maana hiyo mimi naamini kuwa hata kama ingewezekana kuwapa wananchi uhuru bila wazungu kuondoka ingekuwa best scenario kwangu kuliko hili lililofanyika la kuwandoa wazungu wakati wananchni bado wanaendelea kukosa uhuru na kunyanyaswa pengine hata zaidi ya wakati wa serikali za Wazungu.

Tukijufunza na case za Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Afrika kusini nk. Ni dhahiri kuwa mlango wa uhuru na haki umeanza kufunguka Tanzania, maana bila kukamatwa kwa hao viongozi wetu hatuta fika kunapotaka kwenda. Mfano: Kenya vuguvugu za kuwatoa wakoloni weusi zilianza siku nyingi sana lakini zilipamba moto mwanzoni mwa 1980 huko nyuma na hadi sasa mengi yamendikwa katika historia ya kenya kuanzia kuuwawa kwa Tom Mbuya, Dr. Ouko, kuwekwa kizuizini kwa Laila Odinga hadi vurugu za mauwaji ya 2007/2008 ambayo kwasasa kuna kesi za ICC, ikumbukwe kuwa miongoni mwa waliopo mbele ya ICC yumo Msomali mwenzie Saidi Mwema (ambaye naye kama Said Mwema ndiye alikuwa IGP wa kenya).

Katika hii case ya kenya tunajifunza kuwa wakati kama huu tuwe makini sana maana uhuru upo karibu kufika saa yoyote na dakika yoyote lakini sasa tusiruhu mamluki na vibaraka wa hawa wakoloni kuingia miongoni mwetu! Maana watakapo soma alama za nyakati na kujua kuwa jua halita zama bila ukombozi na uhuru kamili lazima watapandikiza miongoni mwetu watu wao ili baada ya ukombozi wapate ulinzi wa kudumu, hicho ndicho Moi alichomfanyia Raila baada ya kujua fika kuwa hata kwa wizi hawata weza kuiba kura za wakenya alimchomeka Kibaki kibaraka wake miongoni mwa wapigania uhuru ili kujiweka salama mbele ya hasira ya Umma, kutokufahamu kwa wakenya na wanamapinduzi wao kuwa wana mamluki miongoni mwao kumewapa hasara kubwa sana hata kuwafanya hadi sasa kuwa katika nusu uhuru nusu ukoloni.


Kesi ya Uganda imekuwa tofauti kidogo maana wao ilibidi kutumia mtutu ya bunduki kuwaondoa wakoloni weusi. Hii njia ni nzuri lakini pia ina madhara yake ambayo yaweza kuwa sawa kabisa na hii ya kutumia sanduku la kura. Nasema yaweza uwa sawa kabisa pale ambapo yamkini wapigania uhuru watakuwa wanauwawa na kufungwa kila kukicha ni bora kutumia vita ijulikane maana katika vita hata wao watakufa pia.

Madhara waliyopata Uganda kutokana kulazimika kuingia vitani dhidi ya wakoloni weusi ni kuwa nchi haiku stabilize mapema sana ukilinganisha na kesi ya Rwanda ambayo Kagame ameonyesha uimara mapema mno, yawezeka kesi ya Kenya tokea kuanzia kuuwawa kwa Tom Mboya hadi leo ni sawa kabisa na bora kama wangefanya vita na kuwatowa wakoloni hawa kwa vita kuliko njia ya sanduku la kura ilivyo wagarimu.


Kwa kweli mifano ni mingi sana, lakini naomba niliache swali lisimame kama swali, Ni nchni gani Barani Afrika ambayo ilipata uhuru kutoka kwa vyama na watawala waliorithi Ukoloni kutoka kwa Wazungu bila kunyanyashwa, kuonewa, kukamatwa na hata kufungwa jela kwa wapigania uhuru wao? Kama hamna basi tujivune kukamatwa kwa wapigania uhuru wetu.

Tuwe pamoja nao, kila mmoja kwa imani ya Dini yake afunge pamoja nao tuwaombee maana uhuru tunaoutaka hautapatika bila hayo kutokea, hayo yote hana budi kutokea ndipo tutashinda hii vita dhidi ya serikali za kidhalimu.
 
Asante kwa kuwakilisha mkuu ujumbe umefika na tuwaunge mkono bila kuchoka viongozi wetu hasa wale wanaonyesha nia ya dhati kwa kuwatetea wananchi.Nnalilaani jeshi la polisi kwa kutumika Kama kinga kuutetea uongozi mmbaya(wa mabavu)wa ccm kukandamiza haki za wananchi wake Watanzania.
 
Wazo zuri liliotulia. Ukombozi umekuja na huko mlangoni.. Dalili zote zimeshaonekana. Anguko la serikali dhulumati ya Kikwete limefika na haina ubishi kwani majeshi yote yameishiwa nguvu na amri ovyo wanazopewa zisizo na mashiko wala werevu.
Serikali iliyoko madarakani ina wayawaya na imeshakosa werekeo. Imeanza kukosa support ya ndani na sasa inaanzakukosa support ya nje! hizo ni dalili njema za kuanguka kwa serikali yeyote duniani. Mambo haya tutayaona kwa macho yetu......
 
Asante kwa kuwakilisha mkuu ujumbe umefika na tuwaunge mkono bila kuchoka viongozi wetu hasa wale wanaonyesha nia ya dhati kwa kuwatetea wananchi.Nnalilaani jeshi la polisi kwa kutumika Kama kinga kuutetea uongozi mmbaya(wa mabavu)wa ccm kukandamiza haki za wananchi wake Watanzania,nipo tayari kwa lolote na J3 tutaenda huko mahakamani(hapa Arusha)siogopi na sitishwi na chochote bado damu za ndugu zangu zilizomwagika ktk maandamano(tar5/January)zinailia serikali hii dhalimu ya ccm.
 
Asante kwa kuwakilisha mkuu ujumbe umefika na tuwaunge mkono bila kuchoka viongozi wetu hasa wale wanaonyesha nia ya dhati kwa kuwatetea wananchi.Nnalilaani jeshi la polisi kwa kutumika Kama kinga kuutetea uongozi mmbaya(wa mabavu)wa ccm kukandamiza haki za wananchi wake Watanzania.

Wazo zuri liliotulia. Ukombozi umekuja na huko mlangoni.. Dalili zote zimeshaonekana. Anguko la serikali dhulumati ya Kikwete limefika na haina ubishi kwani majeshi yote yameishiwa nguvu na amri ovyo wanazopewa zisizo na mashiko wala werevu.
Serikali iliyoko madarakani ina wayawaya na imeshakosa werekeo. Imeanza kukosa support ya ndani na sasa inaanzakukosa support ya nje! hizo ni dalili njema za kuanguka kwa serikali yeyote duniani. Mambo haya tutayaona kwa macho yetu......

Asante kwa kuwakilisha mkuu ujumbe umefika na tuwaunge mkono bila kuchoka viongozi wetu hasa wale wanaonyesha nia ya dhati kwa kuwatetea wananchi.Nnalilaani jeshi la polisi kwa kutumika Kama kinga kuutetea uongozi mmbaya(wa mabavu)wa ccm kukandamiza haki za wananchi wake Watanzania,nipo tayari kwa lolote na J3 tutaenda huko mahakamani(hapa Arusha)siogopi na sitishwi na chochote bado damu za ndugu zangu zilizomwagika ktk maandamano(tar5/January)zinailia serikali hii dhalimu ya ccm.

Tusiogope jela, hata viongozi wetu wasiogope jela, wanaogopa jela bora warudi CCM maana kila mtu ajue kuwa akuna anayekufa bila kutapatapa na kurusha miguu, hivyo ndivyo hawata kubali kuachia bila vurugu tuwetari kwa lolote baada ya kupiga 2015 hata kama ni kufa kwa kulinda kura na iwe maana historia inatufundisha kuwa hawata kubali kuondoka kistaarabu ingawa wameshindwa.

Kama UN inataka kuepusha yaliyotokea kenya ilete ulinzi wa kura za Watanzani 2015 kuepusha yalitokea kenya iwapo kura zitapigwa bila kubadili katiba.
 
Im ready to die just right now, lakini the moment nnayokufa ndipo hapo ukombozi utakuwa umefika

Hizi za kukamatwa kwa wanaharati ni dalili za mwanzo za ushindi wa 2015 vijana tujiandae kulinda kura hata kama damu itamwagika hadi kutoka nyeupe!
 
Hivi wanharakati wenzangu ni damuipi mnayo ingoja, kuliko hii ya inayoendelea kumwagika? (Arusha & Tarime) Ndio maana serikali ya kikwete haijali, inafanya inavyo taka. Wa tanzania bado ni waoga kazi kupiga midomo tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom