Miaka takribani 50 ya Uhuru Tanzania: Ni yapi ya kujivunia?

WAZO ZURI

Lazima upate shida ndio upate na raha,hiyo ndio democracy,muache mbowe atengeneze jina na atie akili,kwani hata viongozi wa Cuf ZANZIBAR waliwekwa ndani sana na kupigwa,na mpaka sasa wametulia wenyewe wameunagana na ccm sasa jahazi letu la zanzbar linaaza safari mpya.

Na sisi wazanzbari tunapigania nchi yetu juu ya mkoloni mwezi tanganyika ambayo inatutawala kwa jina la tanzania,naamini iko siku tutapata uhuru wetu kama munao dai nyie watanganyika kwa ccm.

Sisi lengo letu tuvunje muungano tubakie na zanzbar yetu.
 
Hapa Tanganyika haitawaliki tena,watatumia bakora,risasi,mahakama,vifaru,magereza mwisho watakimbia wao wenyewe,tuwe tayari kuifia nchi yetu...tumeishaanza hatuna budi kumaliza hata kama watasalia wawili
 
Jana ndugu zanguni mida ya jioni nilikuwa narudi home,ila tukakutana na foleni na tukaa zaidi ya masaa 3,mzee mmoja akaanzisha mada akasema kutokana na matatizo mbali mbali tuliyo nayo bora mkoloni arudi,maana umeme shida,maji safi hakuna,reli haifanyi kazi,hospitalini hakuna dawa,elimu mbovu,umaskini unazidi kila kukicha,bara bara mbovu,viongozi hawawajibiki ipasavyo,yule mzee akasema pia ccm wakiri kuwa nchi imewashinda na akatoa mfano ukiwa baba wa familia na ukaona watoto wako wanaenda kudoea chakula kwa jirani ni kwamba baba familia imekushinda.Ndugu wana jf nyie mnamaoni gani kutokana na matatizo mengi tuliyonayo hapa nchini je mkoloni arudi au asirudi?
 
Wahindi na makaburu wameshikilia sector muhimu hapa nchini, but hilo hamlioni. Sijui mnataka mkoloni aje kwa njia gani tena
 
Bila trip zake mngekufa njaa! Baba anaenda kutafuta, unataka akae tu nyumbani?
Mbona hapa nyumbani tunazo rasilimali za kutosha,tatizo ni kwamba hatuzitumii rasilimali zetu vizuri,hizo safari anazozifanya kiranja mkuu ni za kwenda kuwaita wageni waje kuchota rasilimali zetu,mfano sasa hivi kila siku wanyama pori wanahamishwiwa arabuni na kiranja mkuu anaona lakini hachukui hatua.Safari za nje za kiranja mkuu hazina tija zifutwe kwani ni matumizi mabaya ya kodi za watanzania.
 
Arudi tu bora tuwe watumwa.

watu wanshakuwa watumwa ndani ya nchi yao......
mfano: Zain imeuzwa kwa Wahindi ikawa airtel, vitengo karibu vyote vinavyoajiri watu wengi vimebinafsishwa kwa wahindi wengine na matokeo yake vitengo vyote sasa vinaongozwa na wahindi....ni wasanii hao! wanatangaza nafasi za ndani na kusema wanataka mtu mwenye uzoefu wa miaka zaidi 14 wakati wanajua kuwa telecommunication industry ni changa sana TZ kwa maana imeanza kuchanganya miaka ya 2001 hivyo wote wakikosa sifa mhindi analetwa mara moja....IT wamepewa IBM ya India,Operations/networks wamepewa NSN ambayo inaongozwa na wahindi, customer care wamepewa spanco ya india...
unyapara is back ....wahindi wanachofanya ni kurubuni baadhi ya mamanager walobaki ili waafiki kuleta wahindi hata ambao sio professionals....mhindi anayejua excel pekee anasifiwa kuwa bora kuliko wahindisi wanne walotoka udsm!!!serikali imelala usingizi mzito,wananchi nao wanakoroma...watakapoamka watakuta wanauzwa kama enzi za utumwa tena madalali watakuwa weusi wenzetu kama walivofanya machifu uchwara wa enzi hizo....
mweeeeeeeee!!!
 
Jana ndugu zanguni mida ya jioni nilikuwa narudi home,ila tukakutana na foleni na tukaa zaidi ya masaa 3,mzee mmoja akaanzisha mada akasema kutokana na matatizo mbali mbali tuliyo nayo bora mkoloni arudi,maana umeme shida,maji safi hakuna,reli haifanyi kazi,hospitalini hakuna dawa,elimu mbovu,umaskini unazidi kila kukicha,bara bara mbovu,viongozi hawawajibiki ipasavyo,yule mzee akasema pia ccm wakiri kuwa nchi imewashinda na akatoa mfano ukiwa baba wa familia na ukaona watoto wako wanaenda kudoea chakula kwa jirani ni kwamba baba familia imekushinda.Ndugu wana jf nyie mnamaoni gani kutokana na matatizo mengi tuliyonayo hapa nchini je mkoloni arudi au asirudi?

kwa namna yoyote ile, mkoloni hakubaliki.

hapa tulipo kwanza kama Watanzania tuko chini ya mkoloni....Mkoloni Mweusi. Tofauti yao na yule wa zamani(Mkoloni Mweupe) ni hizi:

  1. Wakati mkoloni mweupe alijenga mashule, hospitali, barabara, reli na miundo mbinu mengine, huyu mkoloni wa Mweusi anaharibu kwa kuvunja na kuhujumu miundombinu hiyohiyo. Hii ni kusema kwamba kama mkoloni mweupe alipiga hatua 10 mbele; mkoloni mweusi anapigaa hatua kumi kurudi nyuma. Mwisho wa siku mlinganyo sahili uta-balance na tutajikuta tuna zero katika kila kitu.
  2. Wakati mkoloni mweupe alileta dini ili wanadamu tuishi kwa staha na kuchukuliana, mkoloni mweusi anatumia dini kutukashifisha na kutugombanisha ili atutawale.
Ukoloni ni ukoloni tu. Kama Watanzania hatupashwi kujishusha hadhi kiasi hicho cha kutamani mkoloni mweupe arudi.


Mimi nadhani kwanza tukatae na wala tusitamani mkoloni mweupe kurudi, na pia tumng'oe mkoloni mweusi.

Acha ujuha; tumia vema kura yako 2015. Mkoloni mweusi anajulikana. Sina haja ya kumtaja.

My Take: Mkoloni mweusi na mkoloni mweupe lao moja. Ujio wa Bush, Mana Clinton, Bill Gates, Familia ya Mfalme wa Qatar kwa ufadhili wa mkoloni mweusi ni kielelezo tosha kuwa hawa jamaa (mkoloni mweupe na mweusi) wameamua kushirikiana kutumaliza WaTZ.

Amkeni!
 
Mkoloni Arudi wawachape hawa wanaojiita sisiem, vibaka na wanyonyaji wakubwa wa mali za watanzania! Ktk kpind cha mkoloni nchi ilikua inasonga mbele nowday hakuna kitu. Wanalipana posho na misafari isiyo na tija. ETI UKARABATI WA IKULU SH. Bilion 10? Duh!
 
Bila trip zake mngekufa njaa! Baba anaenda kutafuta, unataka akae tu nyumbani?
Labda kina Lizzy1 sio sisi. Chakula chenyewe cha msaada wanatoa kilo 3 kwa kaya kwa msimu teh! dodoma pale chamwino ikulu wagogo wanakufa kwa njaa, wanasindia zambarau. Mkoloni arudi!
 
Ni vyema kwa watakao changia hoja ya Mkoloni arudi au asirudi watambue yafuatayo:
  • Ukoloni ni ile hali ya nchi moja kuitawala nchi nyingine kwa lengo la kukusanya "viasili uchumi" kwa faida yake. Hapa utaona nguvu, mali na kila chenye faida kikiondoka kutoka nchi inayotawaliwa.
  • Huduma za jamii kama reli, hospitali, barabara n.k vinavyopatikana/vilivyojengwa wakati wa ukoloni ni ili kutimiza lengo la msingi ambalo ni kukusanya "viasili uchumi" kwa faida ya wakoloni.
Pia ni vyema wote tukatambua pamoja na kwamba hakuna "mwelewa" atakeyesema bora ukoloni tutambue kwanini tumefikia mahali swali hili linaweza kuibua mjadala:
  • Ubinafsi wa wale walio na dhamana ya kuongoza na kukosa uwazi katika Utawala. Hii imetuletea matabaka katika jamii na mipango ambayo sio ya kutatua matatizo ya wananchi bali yakutimiza lengo la "kamisheni" (10%)
  • Kukosa Uongozi. Ukilinganisha wakati nchi inatawaliwa na sasa utatambua kwamba sasa hivi hatuna Viongozi kwa kila nafasi ya uongozi. Jiulize kama mkuu wa wilaya hajawahi kufanya kazi serikalini anawezaje kuwaongoza wenzie DAS,DMO,DEO,DAO nk ambao ni watendaji wa muda mreru serikalini???Hata utaratibu wa kupokea na kutoa maamuzi hataujua..
  • Kukosa utaratibu wa namna ya kupata viongozi. Sasa hivi wananchi wa kawaida wanadharau kubwa kwa viongozi walio wengi wanaoteuliwa kwasababu namna walivyopatikana ni utata mtupu. Miguno wakati uteuzi unafanywa imekua ni jambo la kawaida. Maswali kama Hata huyo????ni ya kwaida sana kwa wateuliwa kwasababu wanatoka miongoni mwetu na tunawafahamu.
  • Sababu tatu za awali zinatuleta kwenye udhaifu usio kifani wa huduma za jamii. Ni ulimbukeni ulioje eti hospitali ya mtu binafsi itoe huduma bora kuliko hospitali ya taifa. Mtu kuwa na nyumba iliyobora kuliko mifereji iliyo nje ya nyumba yake.Ninachosema hapa ni kwamba iweje kitu cha mtu mmoja kiwe bora kuliko kitu chetu wote??? au iweje mtu awe na nguvu kuliko kundi la watu?
  • Huduma za jamii zilikua bora wakati wa ukoloni kwa waliozifikia na hili ndilo litoalo picha nzuri ya wakati wa ukoloni
Kama ilivyo kwa wenzangu wengi ndani na nje ya JF Nahisi naiona njia ya kufikia hali iliyobora kwa watanzania lakini sina nguvu wala namna ya kuanza safari.
 
kiongozi wewe upo dunia ipi? maana wakoloni walisha rudi kitambo kwa style ya uwekezaji. ndio wanaotufanya sisi watanzania tusielewane kwa kwa baadhi ya viongozi kutusaliti kwa mali zetu sisi wananchi kwa kuingia mikataba feki, style hiyo hiyo ndiyo waliyoitumia walipokuja kwa kivuri cha umishionari na u explorers waliwatumia machif wachache kuingia nao mikataba feki. kwahiyo mkuu acha utawala wa ccm hata kama ingekuwa chadema style ni hiyo hiyo, na kama style ya chadema isingekuwa hiyo basi CDM isingekuwa na mahusiano ya dhati na CDU +chama cha akina makeni wauwaji wakimarekani. chama cha dhati na wananchi hakihitaji kuwa na support na wakoloni huo ndio ufedhuli wenyewe.
 
Najua Nyerere akiona thread hii ataua mtu, maana aliwafukuza wanafunzi Udsm walipomwambia hivyo. Leo narudia, kwa Tanzania tulipofikia, afadhali ya mkoloni, potelea mbali!!!!!!!!!!!
 
yupi muingereza,mjerumani au muarab?kwa mimi bora mjerumani alijenga miundombinu na mashamba makubwa ya biashara
 
Kama ilivyo desturi yetu tunapenda sana rahisi rahisi, badala ya kupigana kuweza kuwaangusha wazushi katika serikali sisi tunalilia kuja kutawaliwa tena. Mkoloni si mtu mzuri as a 'puppet master' he is causing so much distraction in Africa leo tena tukampe na uongozi wa ndani may be we got issues after all.
 
Back
Top Bottom