Miaka 50: Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele...

IMG_1142.jpg



Kwanini? Magari Tunayo na Wazungu wanayaendesha kwenye barabara zetu.
 
uchumi wa data za kwenye makaratasi ni hatari sana, mi naona uchumi unadorora -- tunashindwa kufanya exportation - tumeua viwanda kwa makusudi kuwapa wawekezaji wa kihindi.

Sasa tunaangiza kila kitu toka nje yaani hadi vijiko, sahani, vikombe, peni, karatasi nk.-- na ndiyo maana sh yetu inayumba kila siku. Ila ukimuuliza Mkulo atakupekulia mafali yake data zake anayotembea nayo kila siku kwamba uchumi wetu unakuwa kwa 7% kila mwaka na tunafanya vizuri sana.
 
Tanzania imepiga hatua kubwa kufuta umaskini katika miaka 50 kuliko nchi nyingi kwa muda huo. Hata Merekani, ambayo ni nchi tajiri duniani, mpaka miaka 150 baada ya Uhuru walikuwa bado wanatabaka la umaskini kubwa kuliko ilivyo Tanzania kwa sasa.
 
1. Ari mpya
2. Kasi mpya
3. Nguvu mpya
4. Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania
5. Ari zaidi
6. Kasi zaidi
7. Nguvu zaidi
8. Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele....!!!!!??????
Matatizo juu ya matatizo!
 
Tujitokeze kwenye sherehe za miaka 50 ya uhuru tukiwa tumebeba mabango ya kuikosoa serikali
 
Kuna mambo ambayo hata sisi wenyewe inatakiwa tubadilike! sisi kama watanzania ndio tunaotakiwa tufaidike na rasilimali zetu na hao viongozi ni kikundi cha watu wachache tu ambao tuliwaamini na kuwapa ridhaa ya kutuongoza sasa wameshindwa.Kama wewe ndo mwenye mali na unamwajiri mtu hatimizi ambacho wewe unataka au haendani na malengo yako ni kazi ndogo tu hakufai na unatakiwa kumfukuza. sasa inatakiwa tuwe na nia thabiti ya jambo hili tusiishie kulalamika tu watu tuliowapa watuongoze wameshindwa wanajali masilahi yao zaidi sasa sisi kama wananchi ambao ni waajiri wao hawatufai inatakiwa tuwaondoe kabla hali haijaendelea kuwa mbaya zaidi.Tutajikuta hatuna kitu maana kila mtu anakuja kuchuma hapa kwetu hakuna anayekuja kuleta maendeleo, hapa wawekezaji fuatilia miradi wanayofanya utasikitika wanatuona majuha shamba la bibi! inchi hii ukija kuwekeza utapewa kila unachohitaji na kodi nafuu au bure kabisa..
 
wamethubutu kutuhadaa,wameweza kutufanya wajinga na wanasonga mbele kutuburuza kama tumelala!Uongo wa asbh eti miaka 50 ya uhuru wa TZ wakati toka TZ izaliwe ina umri usiozidi miaka 47 na Tanganyika ingekuwepo ndo miaka 50 ila imeshakufa!wamethubuu,wameweza na wanasongd mbele kwa kutunyima umeme wa uhakika,sukari kupanda bei kila siku,mafuta aina zote bado tete kila kitu kizungumkuti
 
Tujitokeze kwenye sherehe za miaka 50 ya uhuru tukiwa tumebeba mabango ya kuikosoa serikali
<br />
<br />
Tushindwe kuikosoa serikali kwenye kura tukaweze kuikosoa kwenye maandamano??? Mi naona hata hawa CDM wanahangaika tu, acheni kampeni za maandamano, jitahidini kumfundisha mwananchi, nina hakika kama waTZ wangekua na elimu na ufahamu walau wakujua imact na mchango wa kura yake kwa m2 pacpo kuangalia chama i dont thnk kama wangekua wamepiga kura walivyo piga,mwaka juzi, Ujinga wa MtZ ndo unakula pande yake, na uelewa wake ndo utamkomboa, Hakuna cha CCM, CDM, WALA CUF wala chama chochote, icpokua kura ya mtz kwa m2 sahihi, na elimu ya kumjua huyo m2 sahihi,
 
Kwa hali ilivyo sasa labda tumethubutu na kuweza kula rushwa kubwa kubwa tukaendelea kubaki salama
 
Wana JF, labda mi sina shukrani, labda cjaweza kuchambua inavyo pasa, lkn inaweza kuwa na maana nanyi mkakagua hii miaka 50, ni vipi kama wangebaki wakoloni? Wkt mwingine najaribu kuvuta hisia za maumivu ya kutokua na uhuru kuliko wapata mababu ze2,kweli napata machungu, lkn naona ni heri wangekuwepo zaidi, maana kwangu mm uhuru umeturudisha nyuma miaka 40, ninavyo kwakua tuna tabia ya kuangalia tunayoita maendeleo pacpo kuangalia madhara yake au kulinganisha na madhara yake, km vle, global warming, femine, hunger, deseases, kwangu mm yanayoitwa maendeleo heti kuna jitihada zilizo fanywa.... Ni heri Tz ingeachwa km ilivyo pangekua na maendeleo ya kweli, kwa WaTZ, mioyoni, mwilini, kwenye mazingira na kwa viumbe wengine nk, hayo xangekua maendeleo, lkn c ilivyo sasa km itafanyika tathmini, wanao jigamba watafungwa na Mungu kwa kuita uharibifu maendeleo, labda wenze2,
 
mkuu, wengine si watu aisee, ni viatu tu
<br />
<br />
Mi nadhani anayejua historia ndo ana nafac nzuri ya kuponda pongeza za maendeleo, kwakua majanga yaliyo letwa mi nina hita purukushani za uchafuzi, na uharibifu heti kulenga maendeleo ikiwemo u2nzi wa sera mbovu, au sera nzuri kucmamiwa vbaya, ufujaji wa mali, poor management of natural resources, uongozi mbovu, mcngi wa mfumo mbovu wa elimu, ubinafsi, matumizi mabaya ya elimu kwa walio bahatika kupata elimu nk. Na zaidi ya haya km yupo mwenye ushuhuda chanya kuliko hasi km ilivyo bac hiyo historia haimo vtabuni, hapo cpingi nami nitashangilia miaka 50.
 
No no no
1- Hatujathubutu, kwani hadi leo baadhi yetu ni watumwa ndani ya nchi yetu, tunanyanyaswa,
tunaonewa na tunauliwa na hao hao wazungu kupitia sisi wenyewe ( mauaji ya Tarime)
2- Hatujaweza, hadi leo bajeti yetu inategemea wazungu achilia mbali misaada n.k.
3- Hatujasonga mbele ukilinganisha na tulioanza nao au tulio waacha nyuma.(Kenya, Rwanda)
TUMETHUBUTI
  • Kupanga miradi mikubwa ya maendeleo yenye kuleta tija kwa wananchi
TUMEWEZA
  • Kutekeleza miradi hiyo mfano:
1. Upanuzi mkubwa wa sekta ya Elimu;
  • shule za msingi zaidi ya 15,000 kuanzia uhuru hadi leo
  • shule za sekondari kutoka chini ya 200 wakati wa uhuru mpaka zaidi ya 4,000 hadi sasa
  • vyuo vikuu kutoka 0 wakati tunapata uhuru mpaka zaidi ya 40 hivi sasa
  • vyuo vya ufundi vya kumwaga
2. upanuzi mkubwa katika sekta ya Afya
  • madaktari kutoka 12 wakati tunapata uhuru mpaka zaidi ya 1500 hivi sasa
  • ujenzi wa zahanati kila kijiji umefikia kiwango kikubwa kwani vimesalia vijiji vichache mno
  • ujenzi wa vituo vya afya kila kata umefanywa pia kwa kiwango cha kuridhisha
  • zaidi ya asilimia 90 ya wilaya zetu zina hospitali za wilalya
  • hospitali za mikoa zaidi ya 18 katika kila mkoa isipokuwa michache tu
  • hospitali za rufaa KCMC, MBEYA, BUGANDO, KIBONG'OTO na Milembe zimeboreshwa
  • Upanuzi mkubwa wa Hospitali ya Taifa ya muhimbili ikijumuisha uwekaji wa vifaa vya kisasa vya upasuaji wa moyo, ubongo na uti wa mgongo pamoja na Kinywa na Meno
  • zaidi ya madaktari bingwa 28 wamepatiwa mafunzo nje ya nchi kwa ajili ya kufanya upasuaji wa moyo
3. Upanuzi mkubwa wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami
  • kuongeza idadi ya ma-Engineer kutoka 2 wakati tunapata uhuru mapka zaidi ya 500 hivi sasa
  • mpaka sasa zaidi km 12,000 za barabara nchini kote zipo katika hatua mbalimbali ya kujengwa kwa kiwango cha Lami
4. Kuboresha kilimo bora nchini
  • maafisa ugani zaidi ya 4000 wameajiliwa na kusambazwa nchi nzima
  • wakulima wanawezeshwa pembejeo, matrekta na mikopo kwa ajili ya kuendeleza kilimo chao
TUNASONGAMBELE
  • kuendeleza mafanikio yaliyopatikana
  • kuendelea kubuni miradi mipya hasa kuimarisha sekta ya uchukuzi, nishati na madini
  • kuiwezesha STAMICO ili isimimamie vyema uchimbaji wa madini nchini
  • Kuiwezesha sekta binafsi ili ijuhusishe kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi yetu kupitia mpango wa PPP
  • Kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi unaendana sanjali na kupunguza umasikini wa kipato kwa wananchi
MAMBO YOTE HAYO HAMRIDHIKI? MBONA HAMNA SHUKURANI NYIE!
 
Tanzania imepiga hatua kubwa kufuta umaskini katika miaka 50 kuliko nchi nyingi kwa muda huo. Hata Merekani, ambayo ni nchi tajiri duniani, mpaka miaka 150 baada ya Uhuru walikuwa bado wanatabaka la umaskini kubwa kuliko ilivyo Tanzania kwa sasa.

Naona unatumia masaburi kufikiria, hizo data umezitoa wapi?
 
SWALI? hivi mi najiuliza?? Kwa malinganizo, yale walofanya wakoloni kwa kipindi wakiwepo hapa kulingana na muda, na tulinganishe na miaka ye2 walipo tuacha wenyewe! Mimi naona kama ni maendeleo, tuliua hata yale waloanzisha kwa kac kubwa hata km hatukua na utaalamu wa kutosha,
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru imetolewa leo,ambayo ni 'Tumethubutu,Tumeweza na tunasonga mbele' Je iko relevant na Tanzania ya leo miaka 50 baada ya Uhuru?
labda tuseme wamethubutu kuiba,wameweza na wanasonga mbele
 
Miaka 50 ya uhuru ni uhuru wa wakoloni weusi wa tabaka kandamizi.
Uhuru ni wa jk na tabaka lake. Hatuutambui uhuru huo katika madhila haya.
Mwisho wao waja.
 
Wamethubutu kuuza nchi, kuhadaa watanzani, kugawana nyadhifa.
Wameweza kuficha matlilooni nje ya nchi kwa msaada wa serikali
wanasonga kuiibia nchi yetu na kujimegea maeneo makubwa ya ardhi yetu.
 
Back
Top Bottom