Gerald
JF-Expert Member
- Nov 14, 2007
- 290
- 46
Nakumbuka wiki iliyopita uongozi mzima wa Chadema ulikuwa uje kufungua ofisi ya kata ya Olorien- Chadema lakini kutokana na kikao cha dharula ilibidi uongozi mzima uwepo Dar es Salaam hivyo uzinduzi huo ukahairishwa mpaka wiki hii
Kwa mtazamo wangu ofisi kama hizi za kata zinatakiwa kufunguliwa na wenyeviti wa mikoa hivyo mheshimiwa tunaomba upumzike kwa hilo na kuwaachia viongozi wa mkoa
Binafsi ningependa kukuona ukizindua ofisi za mikoa na wilaya badala ya hizi za kata. Kifupi ni kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawajui hata ofisi za chadema za mikoa zilipo na pia ofisi zenye bado hazikidhi mahitaji ya chadema kikubwa kama chadema. Tunawaomba uongozi mfanye mikakati ili chama kiweze kuwa na ofisi zinazoeleweka ambapo ndo tutapenda mheshimiwa Mwenyekiti uje kufungua badala ya hizi za kata
Nashukuru na natumaini utakuwa umenielewa
Katika mada yako umepungukiwa na mawazo yakinifu mara usije kufungua ofisi za kata, mara fungua za mikoa, mara ofisi zenu azieleweki zilipo. je uonii kuwa ni chama kinachostawi na machungu ya umaskini, haki na usawa? mbona hicho kinachojulikana ofisi zake hawalipi kodi? na hua wanatumia majengo rasilimali za wananchi bure? sasa kipi bora hapo weee mtoa mada. Jambo lolote linaweza kufanyika ila inategemea mipango ya chama au unaogopa kuja kupata wafuasi wengi zaidi uko nini?
Tumekutuhumu wewe kachori