Mgombea Urais matumizi yaongeza hadi Bil 5

Sheria inazungumzia hivi:

(3) For the purposes of subsection (2), "campaign team"
means a group of' persons formed by a candidate in the
nomination process or a contested election for purpose' of
presenting or assisting that candidate in the election campaigns,
who have been approved-
(a) in the case of a Presidential candidate, by the
Registrar;
(b) in the case of a Member of Parliament, by the
District Administrative Secretary; and
(c) in the case of a Councilor, by the Ward Executive
Officer.

Hili ni jambo moja Dr. Slaa amelionesha kwenye ile mada nyingine: Ni kwanini Timu yangu ya kampeni ipatiwe kibali (kuruhusiwa) na mtumishi wa serikali? Kwa mfano, timu ya kampeni ya Mbunge X badala ya kukubaliwa na chama chake tunaambiwa ikubaliwe na Katibu Tawala wa Wilaya? kwanini? Na akikataa?

Sheria inasema:
9.-(1) A candidate shall be required to disclose at least
seven days before the nomination day-
(a) in the case of a Presidential candidate, to the
Secretary General;
(b) in the case of a candidate for the post of a Member
of Parliament and a member of the Council, to the
District Party Secretary,
of a political party which sponsored that candidate the amount of
funds which the candidate-
(i) has in his possession; and
(ii) expects to receive,
intends to use as election expenses.

Kwanini sheria ina presume kuwa vyama vyote vina mfumo sawasawa (swali hili amelihoji Dr. Slaa vile vile). Kama Chama kingetaka kuwa na utaratibu mwingine wa kutoa taarifa za fedha, utaratibu huo umeharibiwa na Sheria hii.

Sheria hiyo hiyo inajiharibia yenyewe pale inaposema hivi:

(5) The disclosure of funds made pursuant to the
provisions of this Act shall be confidential and shall· not be
divulged except when such information is the ,subject of a
complaint or a complaint lodged by the Registrar or investigation
initiated by the Registrar or if it is the subject of proceedings in
the court of law.

Kwanini sheria iamue tena kufanya siri mambo haya? Kwanini isiseme kuwa taarifa zote za fedha ni public record? Je, wananchi hawana haki ya kujua nani kachangia chama gani na kiasi gani? Kwanini iwe hadi kuwa na malalamiko au kesi?

Angalieni sheria yenu inavyosema:

11.-(1) A political party may, for the purposes of
financing election expenses, appeal for and receive voluntary
donations from any individual or organisation, in and outside the
United Republic, provided that the source of every donation,
exceeding shillings one million for an individual donor and
shillings two million for an organization shall, within thirty days
of its receipt, be disclosed to the Registrar by the Board of
Trustees of the political party concerned.

Swali, itakuwaje kama mtu mmoja atachangia shilingi 999,999? je atatakiwa to disclose to the registrar? Itakuwaje kama taasisi itachangia 1,999,999 je itatakiwa itoe taarifa?

Itakuwaje mtu ana milioni 20 kutoka nyumba moja na akaamua kuigawa kwa ndugu zake mbalimbali ili kila mmoja achangie less than 1 milioni kutakuwa na tatizo lolote?

sehemu ndogo ya nne ya kifungu hicho inadokeza hivi:

(4) For the purpose of voluntary donations, a candidate
may receive or accept donation for election expenses from an
individual person or organisation.

Cha kushangaza sheria haisemi mgombea mwenyewe anaweza kupokea kiasi gani na kama anatakiwa kutangaza kiasi anachopokea au la na kama anatakiwa afungue akaunti ya kuweka fedha ya election na kama atatakiwa kulipia kampeni yake kutoka akautni hiyo au la kama inavyotaka kwenye chama.

Angalia hii:

14.-(1) All expenses to be incurred during the nomination
process within the political parties shall be borne out by a political
party
concerned.
(2) For the purpose of this section, the Minister shall, in
consultation with the Registrar and political parties with full
registration, make uniform regulations which shall be observed
during the nomination process by all political parties.

Kweli hakuna tatizo hapa? Je, mgombea mtarajiwa atatumia fedha zake wakati gani?

Angalia baadhii ya adhabu:

26. Any person who commits an offence under this Act to
which no specific penalty is prescribed shall on conviction be
liable to-
(a) in the case of a political party, to a fine not
exceeding shillings three million;
in the case of a candidate, to a fine not exceeding
shillings one million;
in the case of an organization, corporation or
institution, to a fine not exceeding shillings five
million.

Basically.. sheria haitoi adhabu ya kumtisha mtu; ila inaonekana taasisi au shirika linapata adhabu zaidi kuliko wanasiasa! na hakuna kifungo (ukiondoa makosa ya kutumia nguvu ambapo kifungo hakitazidi miaka miwili).
 
Why do you confine yourselves with this nonsense? Uchaguzi uchaguzi uchaguzi! Basi kama uchaguzi ni muarobaini mezeni basi kutwa mara tatu.
 
Hebu amagalieni hii ya UK(Representation of the People Act 1983) Sections 72 to 90 control the total election expenses that can be spent on behalf of a candidate.

During the time limit of the election, all money spent on the promotion of a candidate must be authorized by his election agent. This includes the cost of holding public meetings, organising public displays, issuing advertisements, circulars, or otherwise presenting the candidate's views and the extent or nature of his backing or disparaging another candidate. It does not include travel expenses from home or similar personal expenses.

The expenses limit for the campaign (which is enforceable due to it all having to be authorized by one person) is £100,000 for a parliamentary by-election, but is approximately £5,483 plus either 6.2p or 4.6p for every registered voter in the district.

So short na si sheria mama ni sub section tu...sisi ni muswada mzima...imagine taifa kubwa hivyo halioni hii kitu kama ni issue
 
Mimi watanzania nawashangaa kweli

Hivi bilioni moja haimtoshi mtu kutembea tanzania nzima wakati wa kampeni??

Bado nawashangaa pia wanaoishangaa kanuni hii, kila siku wamekuwa wakilalama kwamba ccm haiweki mazingira sawa kwa wagombea kwa sababu wana rasilimali nyingi wamezishikilia, leo hao hao ccm wamekubali wakasema sasa kiwango cha kutumia fedha kiwe sawa ,bado watu wanalalamika.

Hivi ninyi ccm wakiruhusu kila mmoja atumie fedha zake ,nyie mnaolalamika leo mtaweza kushindana na ccm kujitangaza kwa kutumia fedha???

Najuwa hamlalamiki kuhusu usawa, najuwa wamewabana kutumia helikopita kama kitega uchumi cha kuchota kodi za wananchi.
MkamaP tatizo hapa si nani ana pesa kiasi gani tatizo ni matumizi yake yaani nidhamu ya pesa watu walichokuwa wanalalamika ni jinsi CCM walivyokuwa wanatumia pesa kununua wapigakura kugawa Tshirt kanga na kofia bure hawakulalamika kwa nini CCM wana pesa nyingi
 
headline_bullet.jpg
Vyama vyasema bilioni haitoshi
headline_bullet.jpg
CCM wataka ifikie Sh. bilioni 10
headline_bullet.jpg
Wapinzani wataka Sh. bilioni tano

Vyama vya Siasa vimekosoa mapendekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, kuwa mgombea wa urais asitumie zaidi ya Sh. bilioni moja kuanzia mchakato wa kuteuliwa na chama hadi kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu, kwa maelezo kuwa kiasi hicho ni kidogo.
Wakizungumza jana na Nipashe, viongozi wa vyama hivyo walisema kiasi hicho ni kidogo na hakiwezi kumwezesha mgombea urais kufika mikoa yote 26.
Wanasiasa hao juzi na jana walikutana na Tendwa kujadili rasimu ya kanuni na taratibu zitakazotumika wakati wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Matson Chizii, alipendekeza angalau kiasi hicho kiongezwe hadi kufikia Sh. bilioni 10 ili zimwezeshe mgombea kuwafikia wananchi katika maeneo yote ya nchi.
"Hao waliopendekeza kiasi hicho walikisia tu bila kwenda kuona hali halisi na sijui vigezo walivotumia …waangalie gharama za kufikia kata zote kwa jimbo moja inakuwa kiasi gani, mafuta, vipaza sauti, vipeperushi, picha za wagombea na wasifu wa wagombea," alisema Chizii. Aliongeza kuwa Sh. bilioni moja haziwezi kutosha kukodisha magari na mafuta ya kuzunguka mikoa yote 26 na kwamba kiasi hicho kwa mtu anayegombea urais kinaweza kukatika kwa kampeni za mikoa miwili tu.
"Mgombea urais ana majimbo 232 ambayo lazima ayafikie wakati wa kampeni zake, sasa atakuwa na miujiza gani ya kuyafikia hayo yote kwa bilioni moja tu, ni kweli tunataka kudhibiti rushwa, lakini kuwawekea wagombea kiasi kidogo siyo dawa ya rushwa na kwa mawazo yangu, naona mtu akiwekewa kiwango kikubwa ndipo ataachana na kutoatoa rushwa," alisema Chizii.
Mwenyekiti wa United Democratic Party UDP), John Cheyo, alisema ingawa ni vigumu kufanya makadirio ya gharama halisi za mgombea urais, kiasi kilichotajwa na Tendwa ni kidogo sana kwa kuwa kugombea nafasi hiyo ni jukumu zito.
Alisema kutokana na miundombinu mibovu, inakuwa vigumu kuwafikia wananchi, hivyo baadhi ya wagombea hulazimika kutumia helikopta ambayo ni gharama kubwa kuikodisha.
"Mimi nimegombea urais, najua ugumu wake, unajua ukigombea pia lazima utumie vyombo vya habari, huna ujanja lazima ujitangaze na matangazo ni gharama kubwa sana," alisema na kuongeza:
"Tusiogope mgombea kutumia fedha nyingi, isipokuwa tuangalie anazitumiaje, kama atazitumia kununua watu ni kosa, lakini akizitumia kuwafikia watu na kuwaeleza sera zake kuna tatizo gani hapo?"
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, alisema kwa gharama ya Sh. bilioni moja haiwezi kuwa rahisi kwa mgombea urais kwani gharama za maisha zimepanda kwa kiwango kikubwa.
Alipendekeza angalau kiwekwe kiwango cha Sh. bilioni tano kwa mgombea urais na Sh. milioni 50 kwa wagombea wa ubunge.
Alitoa mfano kuwa Sh. milioni 20 zilizopendekezwa na Tendwa haziwezi kufika popote kwa mgombea ubunge kwani baadhi ya majimbo ya mijini yana vituo hadi 800 vya kupigia kura hivyo mgombea lazima awalipe mawakala wake wote. "Siku ya uchaguzi tu yenyewe unaweza kutumia milioni nane kuwalipa mawakala, sasa haiwezekani mgombea ubunge kutumia milioni 20 kwa kampeni zake zote," alisema Mnyika.
Mwakilishi wa NCCR-Mageuzi, Beati Mpitabakana, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, alisema kiasi hicho hakitoshi na alipendekeza kiongezwe hadi kufikia angalau Sh. bilioni tano.
Alisema kutokana na miundombinu kuwa mibovu, wagombea wanalazimika kukodi magari ya uhakika na wakati mwingine ndege ili kufika kwa wakati kwenye mikutano ya kampeni.
Rais wa Tanzania Democratic Alliance (Tadea), John Lifa Chipaka, alisema kiasi hicho ni kidogo sana na kupendekeza kiongezwe hadi kufikia Sh. bilioni tano. Alisema mgombea urais lazima awe na wapambe wa kumsaidia kufanya kampeni mikoa yote 26, hasa pale ambapo hawezi kufika yeye mwenyewe hivyo fedha nyingi lazima zitumike.
"Mimi mwenyewe kama nagombea urais kwanza nahitaji timu ya watu 100 wa kunisaidia na Sh. bilioni tano za kampeni, hawa watanisaidia kuandaa mikutano yangu nchi nzima sio kwamba watakuwa nyuma yangu wanakula na kunywa tu, watafanya kazi na lazima wale na walale na utawapa posho, maana wana familia zao," alisema Chipaka.
Mwenyekiti wa Chama cha Ustawi Tanzania (Chausta), James Mapalala, alisema Sh. bilioni tano hazitoshi kwa mgombea urais ambaye chama chake ni kipya na hakijawa na mtandao mkubwa wa nchi nzima.
Alisema kugombea urais kunahitaji fedha nyingi zaidi ya zilizotajwa na Tendwa kwani mgombea anatakiwa kuwafikia wapiga kura wengi ambao wamesambaa mikoa yote 26.
"Kwa vyama vipya, bilioni moja siyo kitu ila wenzetu CCM hata ukiwapa milioni 100 inawatosha maana wana mtandao wa nchi nzima, ila mimi Mapalala hata nikipewa milioni 200 tu nigombee urais nitamchachafya hata mgombea aliyepewa bilioni moja," alisema.
Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willbroad Slaa, alisema kiasi hicho kinaweza kutosha kama vyama hivyo havitahonga wapiga kura na alitoa mfano kuwa mwaka 2005, Chadema ilitumia Sh. milioni 700 katika kampeni zake. Alisema kwa kiasi hicho walikodi helikopta, magari na kujaza mafuta kila siku kwa kuwa hawakuwa wakitoa rushwa kama vinavyofanya baadhi ya vyama.
"Nasema bilioni moja inaweza kutosha, inategemea unataka kufanya nini, kama unataka kuhonga honga na kununua wapiga kura, hizo haziwezi kukufikisha popote na hapo ndipo patamu maana waliozoea kuchapisha kanga, fulana, kofia na kugawa ovyo watashindwa, walidhani hii sheria itawabana wapinzani tu kumbe itawabana hadi wao,"alisema Dk. Slaa.
Naye Tendwa aliiambia Nipashe kuwa ofisi yake ilitoa mapendekezo hayo ili wadau wayajadili, lakini kiasi hicho si uamuzi wa mwisho kama baadhi ya watu walivyotafsiri.
"Jamani nilichotoa ni mapendekezo tu na hawa wadau ndio wanapaswa kujadili na waseme kama kiasi hicho ni kidogo au kikubwa. Sikusema kwamba kiasi hicho kinatosha, wanaoweza kusema kinatosha au hakitoshi ni wao ambao huwa wanaenda kugombea, sio mimi na ndio maana tuko hapa kujadiliana," alisema Tendwa.
Alisema ofisi yake itawapa muda wanasiasa hao kuendelea kutoa mapendekezo yao hadi keshokutwa na yatachukuliwa na kufanyiwa kazi.
Alisema Aprili 6, mwaka huu, kikosi kazi cha ofisi yake kitakaa kuangalia kama mapendekezo ya vyama vya siasa yamefanyiwa kazi na kisha watamwandikia Waziri na baadae rasimu hiyo itapelekwa kwa Waziri Mkuu ili asaini na ianze kutumika kama kanuni halali.
"Maoni yao yote tutayachukua, maana hii kanuni inawahusu wao, wao ndio wanaokwenda kugombea hivyo lazima tuwasikilize na ikishakuwa kanuni sasa tutaanza kubanana kwa wale wanaokiuka," alisema Tendwa.
 
MkamaP tatizo hapa si nani ana pesa kiasi gani tatizo ni matumizi yake yaani nidhamu ya pesa watu walichokuwa wanalalamika ni jinsi CCM walivyokuwa wanatumia pesa kununua wapigakura kugawa Tshirt kanga na kofia bure hawakulalamika kwa nini CCM wana pesa nyingi

Mkuu
Sijakuelewa ama na wewe hujanielewa ama hatuelewi kwa pamoja nini tunachokitaka ktk Tanzania.

Mkuu kwa uelewa wangu sheria kama hiyo inasaidia sana ,kudhibiti uiibaji wa fedha ,ila wanaolalamika ni kwamba inawabana kupata mirija ya kufyonza fedha.

Chukulia mfano huu, mimi nina fedha za wafadhili nashindwa jinsi gani ya kuzifisadi na pia kufisadi fedha za wananchi kwa kutumia sheria halali lakini kiufisadi.

Nagombea urais naenda kukodi AIR BUS NAIROBI, kule naelewana nao kwamba kwa kawaida kukodi kwa siku hizo ni bilioni 1 sisi tunaandika bilioni 5 moja yao ya uhalali kujumlisha moja yao cha juu, mimi nachukuwa 3 natia mfukoni.

Hilo inamaana hamlioni kabisa??
Tatizo la viongozi wetu wanayajuwa majibu sahihi kabisa ya kututoa ktk umasikini, lakini wakiyatumia majibu sahihi kutatua tatizo yataziba mianya yao kujiribikizia fedha, ndivyo vivyo ilivyo kwa watanzania wote wanapoona mirija inazibwa wanakuja juu.

Ndio maana mie na mtazamo wangu, kutokana na ninavyoona kwamba mkombozi wetu hajapata kupatikana, hawa wote wanaopiga makelele ni kwa sababu nafasi zao za kufisadi bado finyu.

Japo mie sio mtaaramu wa sheria na pia si mtaaramu wa takwimu, lakini kutokana na kahesabu na kafizikia kadogo naona sheria ni nzuri kabisa.Hiyo sheria naona itakuwa mbaya kama wakiimplement kwa mazingira tofauti mfano CCM wanaruhusiwa bilioni 10, CHADEMA milioni 1 na CUF milion 5.Hapo nafikiri ndipo tutasema sheria mbaya.

Lakini hata kama ni sheria mbaya lakini ina apply kwa wote kwa kiasi na condition zilezile, hiyo bado ni sheria nzuri na yenye pivot sahihi.

Mfano unapofanya experiment yako under vaccum na ukiwa na object mbili na kifaa ulichofanyia experiment ni kibovu na ukapata majibu si sahihi under the same conditon na hata ukienda ukafuata na ukapata kifaa kizuri na ukachukuwa vipimo tena under the same condition majibu yatakuwa proportional na yale ya kifaa kibovu na kifaa kizuri with respect na object.
 
Hapo ndipo walipotia chumvi hii sheria, kuweka kiwango cha pesa na idadi ya wapambe ni kuonyesha kuwa hii sheria haikubaliki na haitekelezeki...hivi nchi gani kuna sheria ya namna hii labda tujifunze?....ukiangalia tu idadi ya mikoa ya tanzania na chukulia viongozi wa vyama wa mikoa (mwnykt,katb,mweka hazina,mwenezi) wako wa 4 na mikoa 26, ukisema hawa ndio wasindikizzaji wa raisi tu tayari wamezidi 50, na kama ni raisi kutumia idadi hiyo ya watu walewale kila mkoa basi gharama zake zitakuwa zaidi ya bil 1, hivi jk anafikiria nini? Je msajili atakuwa na uwezo wa kumuadhabisha pale tutakapo peleka malalamiko???
Mpaka sasa wapo wagombea wanatumia mamilioni kujinadi majimboni...na hata raisi nae anatimu ishaanza kuweka mambo sawa je record zake zipo? Maana hii sheria ni kabla na baada ya uteuzi....
 
Sheria nzuri, yawezekana kabisa duniani kote hakuna hiyo sheria lakini ndivyo vivyo kote dunianiani hakuna nchi nyingine kama Tanzania.

Wapambe wengi wa nini? hao waliotanabaishwa hapo juu yani 50, kwanza ni wengi mno wa nini wote hao.?? kama si ufujaji wa fwedha???
 
Inaweza kumtosha kama ataitumia peke yake!

Kwa sababu haijaweka kiwango sawa!

Si waruhusu uone wakatavyoumizana CCM wenyewe; kwani aliyedhurika zaidi kwama 2005 ni nani, si CCM?

walioingiza magari 200 na watakoingiza pikipiki nyingine lukuki wakati huu si ndiyo wenye kushikilia mfuko wa kodi za wananchi?

Magari 200 na hizo pikipiki zinaweza kuwa chini ya bei la sijui chopa ama helkopita la mzee mmoja alilolinunulia chadema. Na hata hivyo

Hii sheria nafikiri hailimiti chama kumiliki vifaa bali inalimiti kutumia fedha nyingi wakati wa kampeni.

watu wanatumia fedha kama fimbo kujitwalia madaraka na wakati huohuo watu wengine wanatumia kapeni kujitunishia fedha kwa kutumia mianya ambayo imo ndani ya sheria.

Hii sheria binafsi naiona ipo sahihi maana kutangaza sera za chama Tanzania nzima hakuzidi hata hiyo bilioni moja.
 
Mkuu
Sijakuelewa ama na wewe hujanielewa ama hatuelewi kwa pamoja nini tunachokitaka ktk Tanzania.

Mkuu kwa uelewa wangu sheria kama hiyo inasaidia sana ,kudhibiti uiibaji wa fedha ,ila wanaolalamika ni kwamba inawabana kupata mirija ya kufyonza fedha.

Chukulia mfano huu, mimi nina fedha za wafadhili nashindwa jinsi gani ya kuzifisadi na pia kufisadi fedha za wananchi kwa kutumia sheria halali lakini kiufisadi.

Nagombea urais naenda kukodi AIR BUS NAIROBI, kule naelewana nao kwamba kwa kawaida kukodi kwa siku hizo ni bilioni 1 sisi tunaandika bilioni 5 moja yao ya uhalali kujumlisha moja yao cha juu, mimi nachukuwa 3 natia mfukoni.

Hilo inamaana hamlioni kabisa??
Tatizo la viongozi wetu wanayajuwa majibu sahihi kabisa ya kututoa ktk umasikini, lakini wakiyatumia majibu sahihi kutatua tatizo yataziba mianya yao kujiribikizia fedha, ndivyo vivyo ilivyo kwa watanzania wote wanapoona mirija inazibwa wanakuja juu.

Ndio maana mie na mtazamo wangu, kutokana na ninavyoona kwamba mkombozi wetu hajapata kupatikana, hawa wote wanaopiga makelele ni kwa sababu nafasi zao za kufisadi bado finyu.

Japo mie sio mtaaramu wa sheria na pia si mtaaramu wa takwimu, lakini kutokana na kahesabu na kafizikia kadogo naona sheria ni nzuri kabisa.Hiyo sheria naona itakuwa mbaya kama wakiimplement kwa mazingira tofauti mfano CCM wanaruhusiwa bilioni 10, CHADEMA milioni 1 na CUF milion 5.Hapo nafikiri ndipo tutasema sheria mbaya.

Lakini hata kama ni sheria mbaya lakini ina apply kwa wote kwa kiasi na condition zilezile, hiyo bado ni sheria nzuri na yenye pivot sahihi.

Mfano unapofanya experiment yako under vaccum na ukiwa na object mbili na kifaa ulichofanyia experiment ni kibovu na ukapata majibu si sahihi under the same conditon na hata ukienda ukafuata na ukapata kifaa kizuri na ukachukuwa vipimo tena under the same condition majibu yatakuwa proportional na yale ya kifaa kibovu na kifaa kizuri with respect na object.
Ndiyo maana nilikuambia tatizo si kuwa na pesa tatizo ni matumizi yake.
 
Serikali inaweza kuchukua hatua dhidi ya fedha chafu, lakini kuzuia au kudhibiti matumizi ya fedha halali za mwananchi ni kuingilia uhuru wake wakikatiba! Rais aliye-sign na watungaji wa sheria hii wamedhalilisha ueledi wao. Sheria hiii ni kichekesho, haitekelezeki na inakiuka uhuru wackikatiba wa mwananchi
 
Serikali inaweza kuchukua hatua dhidi ya fedha chafu, lakini kuzuia matumizi ya fedha halali za mwanachi ni kuingilia uhuru wake wakikatiba! Sijua hivyo viwango ndio thamani za hizo nyadhifa hizo? Sheria hii nikichekesho tupu! Haitekelezeki na inakiuka uhuru kikatiba wa mwanachi
Wakimaliza hii ya uchaguzi watakuja ya harusi mwisho laki 2
 
Ndiyo maana nilikuambia tatizo si kuwa na pesa tatizo ni matumizi yake.

Ndiyo
Ndio maana wameona ktk matumizi ya kawaida ya kupiga kapeni bilioni moja inatosha.sasa tatizo la wanaong'aka ni nini??
 
Serikali inaweza kuchukua hatua dhidi ya fedha chafu, lakini kuzuia au kudhibiti matumizi ya fedha halali za mwananchi ni kuingilia uhuru wake wakikatiba! Rais aliye-sign na watungaji wa sheria hii wamedhalilisha ueledi wao. Sheria hiii ni kichekesho, haitekelezeki na inakiuka uhuru wackikatiba wa mwananchi

Chukulia Rostam na mi pesa yake ya wizi sijui halali, akiamuwa akanunua mchele kila familia jimboni kwake , si anatumia fedha zake bwana kuna kosa hapo??

pamoja na fedha ni zako, lakini kuna mazingira ambayo serikali inabidi kulimiti utumiaji na namna unavyozitumia fedha.

Mfano Poland ukimpa fedha omba omba hawa ma homeless polisi wakikuotea unampa pesa umekwisha.

Kila tendo lina namna yake ya kulitafsiri hata kama mali ni yako.Japo sina uhakika kabisa fedha ni ya serikali ama mtu anayeimiliki
 
Back
Top Bottom