Mgombea Urais matumizi yaongeza hadi Bil 5

Kuna mechanism gani in place ya kujua kiasi kilichotumika katika uchaguzi?

Hapo kama mhusika ni upinzani basi mahesabu yote yatapatikana lakini kama ni CCM mahesababu yatapigwa factor hata ya 0.5 ili pesa ziwe kidogo.
 
Well.....this is still advantage CCM. How many opposition parties can spend $1billion per election per candidate(correct me if I'm wrong)? I think this is more of a limit on CCM presidential candidates and not presidential candidates as a whole.

By the way.....just thinking out loud.....mheshimiwa anaogopa kuna makundi yanayo weza yakawa na funds zaidi ya za ***** lake? Maana hizi sheria za miezi michache kabla ya uchaguzi zina raise questions nyingi.
MwanaFalsafa1 nafikiri amount ni Tshs Bil.1 na si $1billion symbol ya $ ni ya Dola correct me if I'm wrong
 
Yale magari mapya yaliyoletwa na CCM yataingizwa kwa gharama hizi?

Usiniambie wameagiza tena yale mamonster ya kijani!

Hivi inalipa kweli kununua hayo magari kila miaka mitano wakati miaka 2 baada ya uchaguzi idadi yake huwa inaanza kudundulia sijui ni kwa ajili ya uhafifu wa aina ya magari, matumizi mabaya au?
 
Nili-expect kwamba wabunge wanaogombea majimbo ya vijijini wangepangiwa kiwango kikubwa ukilinganisha na viwango vya kwenye majimbo yaliyo ndani ya makao makuu ya mikoa.

Ukienda nje ya makao makuu ya mikoa (vijijini) barabara ni mbovu sana na hazipitiki kirahisi, kukodi magari kwenye barabara kama hizo ni gharama kubwa ukilinganisha na kwenye barabara nzuri, pia hata matumizi ya mafuta ni makubwa huko vijijini ukilinganisha na mijini.

Idadi ya watu si kigezo cha kutumika kupanga limit ya fedha, bali ni namna gani hao watu wamesambaa. Chukulia kule umasaini ama kwenye jamii za wafugaji ambako kuna vitongoji na mitaa kibao ndani ya kijiji kimoja na huwezi kusema utawapata wote kwa siku moja kwenye kijiji, one has to go kwenye mitaa yao ama vitongoji vyao ili kuwapunguzia usumbufu wa wao kutembea umbali mrefu kwenda kwenye kampeni.

Nikiangalia hicho kipengele pekee ninaona kinakandamiza vyama vya upinzani ambavyo network yake huko vijijini iko weak ukilinganisha na CCM. Kibaya zaidi watendaji wengi wa vitongoji, mitaa na vijiji ni pro-CCM na hivyo ni rahisi kwa watendaji kuwahimiza wananchi kwenda kwenye mikutano ya kampeni za CCM.

Sheria ya Gharama za Uchaguzi imetungwa kwa kukurupuka na ilipitishwa kwa maslahi ya walio madarakani ili waendelee kuchaguliwa kirahisi na kuwazuwia wapya wanaotaka kujitokeza.
 
Fikiria mgombea wa Jimbo fulani la Dar ambapo inapendekezwa kutumia si zaidi ya dola 20,000 basically! are they serious?

hiyo kwa siku tisini kufanya kampeni?
 
- Hii sheria itakua ni kinyume na Bill of Rights ya Constitution yetu maana sasa unaingilia uhuru wa wananchi kutumia mali zao as they see fit, serikali ingesema inataka kuweka kiwango maalum on hela za kampeni toka serikalini kwa mgombea sawa, lakini huwezi wakataza wananchi kutumia hela zao za mifukoni huo ni simply ujamaa jamaa na mazimio azimio,

- Tanzania sasa ni nchi ya kibepari hatuwezi kuanza tena tabia za kuhesabiana visoda vya bia kwenye ma-Bar, serikali inatakwia kuwalinda wananchi na mali zao, lakini sio kuwaamulia namna ya kuzitumia mali zao, that is simply pathetic thinking! na wananchi tukatae kwa nguvu zote mawazo haya mgando! na yaliyopitwa na wakati.

- Wakisharuhusiwa kuwaamulia wananchi namna ya kutumia hela zao kwenye siasa, the next thing watahamia kwenye maisha yao hatuhitaji hizi sheria za ki-stone age!

Respect.

FMEs!
 
mzee ni too late now.. ndiyo wanavyosema kuwa "kilichokwenda kwa mganga" si uliona walivyomzunguka na kupiga picha! Hili litawauma kweli, ndio maana nimeipinga hii sheria toka mwanzo ni kinyume na Katiba.. na watakaoumia zaidi ni wana CCM hasa kwenye kura za maoni..
 
- Wananchi wanaweza kwenda kwenye sheria, kura za maoni safari hii CCM atakufa mtu maana ndio zitakazo amua nani awe mbunge kwenye majimbo yao, na watatumia katiba mpya ya CCM ya wanchama wote wa kata kupiga kura, ukimpa hela kiongozi wa kata kwa niaba ya wengine umeunywa maana wananchi watashituka kuwa kachukua mgawo mzito kuliko anaowagawia, huu uchaguzi wa maoni ya CCM itakua kivumbi sana mwaka huu!

Respect.

FMEs!
 
Fikiria mgombea wa Jimbo fulani la Dar ambapo inapendekezwa kutumia si zaidi ya dola 20,000 basically! are they serious?

hiyo kwa siku tisini kufanya kampeni?

Mzee sikuwa nimezama kwa kina kama wewe ulivyonifungua macho ... this is a joke!

Shilingi milioni 20 ukigawanya kwa siku 90 za kampeni, ni sawa matumizi ya shilingi 220,000/= kwa siku moja!

Laki 2 kwa siku moja ni matumizi ya watu individually na tena wale ambao wana discipline ya matumizi ya fedha. Leo hii ndiyo uweke limit kwamba kwa siku moja mgombea atumie laki 2! Kweli hawa jamaa hawako serious.

Seriously, walitumia vigezo gani kufikia kwenye hiyo figure?
 
kumbuka hiyo elfu 20 inajumlisha matangazo, malipo ya watendaji, vitendea kazi n.k ! Nyie subirini kutawaka moto huko hadi mshangae. Sasa kitakachofanyika ni kuwa, wale wenye uwezo sasa hivi wataandaa vitendea vyao vya kazi sasa hivi, yaani wataingia gharama yote sasa hivi! wale wenzangu na miye sasa watakaotaka kusubiri muda maalumu ndio watajikuta wanazidiwa 100:1 halafu watalalamika "sheria ile ya gharama ya uchaguzi mbaya".. mimi nitakuwa nimeshika popcorn yangu na togwa!
 
Kuna utata mkubw kwneye hii
Kwanza Scope ya neno matumizi na gharama haiko wazi.

Pili nani wa kuthibitisha usahihi au makosa ya taarifa za kimahesabu kwenye Accounts za chama/mgombea fulani. kuna mtu ataleta mahesabu kakodi gari kwa 10,00 kwa siku mwingine atasema kakodi kwa shilingi 5,000 kwa siku kwenye jimbo hilo hilo.

Inabidi wahasibu/ watayarisha mahesabu wapelekwe semina kwa pesa za walipa kodi.

uchaguzi wa mwaka huu utavunja rekodi ya kesi na rufaa. wajitayarishe kuunda na mahakama ya uchaguzi.
 
Mzee sikuwa nimezama kwa kina kama wewe ulivyonifungua macho ... this is a joke!

Shilingi milioni 20 ukigawanya kwa siku 90 za kampeni, ni sawa matumizi ya shilingi 220,000/= kwa siku moja!

Laki 2 kwa siku moja ni matumizi ya watu individually na tena wale ambao wana discipline ya matumizi ya fedha. Leo hii ndiyo uweke limit kwamba kwa siku moja mgombea atumie laki 2! Kweli hawa jamaa hawako serious.

Seriously, walitumia vigezo gani kufikia kwenye hiyo figure?

Unamaanisha sie Civil servants tunatumia laki 2 kwa siku!doh,that is more like our monthly salary mh.

Au na wewe ni katika wale mnaoamini kila anayeendesha corola mjini anapokea mshahara wa milioni 20?!

kwa mindset hii ndio maana hii nchi rushwa haiishi,Mishahara midogo halafu unataka utumie laki 2 kwa siku!!haya masifuri muda si mrefu yatakuwa hayana maana.Huyo mgombea wa ubunge kutumia Laki 2 kwa siku is more than enough,Tatizo tumezoea wagombea wa ubunge kuwa kama wazazi,walezi katika kipindi chote cha uchaguzi.

wanatakiwa wagharamie logistics na other minor costs sio kulipia round za bar au kanga na vitenge
 
Unamaanisha sie Civil servants tunatumia laki 2 kwa siku!doh,that is more like our monthly salary mh.

Au na wewe ni katika wale mnaoamini kila anayeendesha corola mjini anapokea mshahara wa milioni 20?!

kwa mindset hii ndio maana hii nchi rushwa haiishi,Mishahara midogo halafu unataka utumie laki 2 kwa siku!!haya masifuri muda si mrefu yatakuwa hayana maana. Huyo mgombea wa ubunge kutumia Laki 2 kwa siku is more than enough, Tatizo tumezoea wagombea wa ubunge kuwa kama wazazi, walezi katika kipindi chote cha uchaguzi.

wanatakiwa wagharamie logistics na other minor costs sio kulipia round za bar au kanga na vitenge

Mkuu Kimweri,

Naomba tuwe wakweli. Lita moja ya petroli/dizeli ni shilingi ngapi? Na je huyo mtu anahitaji magari mangapi kwa ajili ya kuandaa logistics za kampeni zake ikiwa ni pamoja na kufacilitate movement za kwake na wasaidizi wake? Au atakuwa anaenda kwenye kampeni kwa baiskeli au bajaji?

Kampeni ni pamoja na matangazo kwenye redio, magazeti na TV (esp. sehemu kama Dar ambapo wananchi wana access ya kusoma magazeti, kutazama TV na kusikiliza radio). Kitangazo kidogo kwenye gazeti ni zaidi ya hizo laki 2, je kuweka sera zake kwenye quarter/half/full page ataweza?

Hizo laki 2 hazitoshi kurusha tangazo kwenye TV hata kwa dakika moja.

Bado kuna kuchapisha vipeperushi pamoja na vitu vingine ambavyo vitakuwa vinamtangaza mgombea kwa wananchi pamoja na sera zake.

Bado unasema hizo laki 2 kwa siku zinatosha?

Tatizo la hiyo sheria ni kwamba hata kama mhusika ana hela zake pia inambana, haijalishi kwamba hizo hela ni zake ama zimetoka serikalini, kinachotakiwa ni ku-comply na hiyo sheria na pia aainishe sources za funds zake mapema ili wajue umezipata wapi na kwa njia ipi.

Tatizo siyo kwamba hela zinatolewa na serikali, tatizo ni kiwango. Kama mtu ana uwezo wa ku-raise funds kwa njia halali aruhusiwe kutumia kiwango kitakachomuzesha kujiuza kwa wapiga kura. Kitu ambacho walitakiwa kukiangalia kwa makini ni namna kwanza alivyopata hizo hela kama ni njia halali ama ni ufisadi; pili ni jinsi anavyotumia hizo hela, je anahonga ama anatumia kihali ili ku-facilitate kuuza sera zake kwa wananchi?

Pilau siyo kuuza sera, mafuta, mchele na sukari siyo kuuza sera; lakini kama anatumia hizo hela kwa kuuza sera zake na kujiuza yeye mwenyewe kwa wananchi kwa kutumia media mbali mbali za matangazo na kujiuza (mfano, vipeperushi, matangazo kwenye TV, radioni, kwenye magazeti na wakati mwingine hata t-shirt ama kofia ambazo zina kauli mbiu yake vinaweza kuwa vinamuuza candidate kwa wananchi).

The Act is tricky, itawashika wasio na connections/majina na walio na connections/majina watapeta. Victims wa kwanza zitakuwa ni nominations za CCM. Mwaka 2005 watu walilia na mchezo mchafu wa JK kwenye nominations, hakuna kilichofanywa na akaishia kupeta.

Chaguzi za Jumuiya za CCM zimejaa rushwa lakini kama mtoa rushwa ni "mwenzao", hakuna kitakachofanyika, ila kama mtoa rushwa siyo mwenzao basi lazima ashughulikiwe.
 
Mimi watanzania nawashangaa kweli

Hivi bilioni moja haimtoshi mtu kutembea tanzania nzima wakati wa kampeni??

Bado nawashangaa pia wanaoishangaa kanuni hii, kila siku wamekuwa wakilalama kwamba ccm haiweki mazingira sawa kwa wagombea kwa sababu wana rasilimali nyingi wamezishikilia, leo hao hao ccm wamekubali wakasema sasa kiwango cha kutumia fedha kiwe sawa ,bado watu wanalalamika.

Hivi ninyi ccm wakiruhusu kila mmoja atumie fedha zake ,nyie mnaolalamika leo mtaweza kushindana na ccm kujitangaza kwa kutumia fedha???

Najuwa hamlalamiki kuhusu usawa, najuwa wamewabana kutumia helikopita kama kitega uchumi cha kuchota kodi za wananchi.
 
Mimi watanzania nawashangaa kweli

Hivi bilioni moja haimtoshi mtu kutembea tanzania nzima wakati wa kampeni??

Inaweza kumtosha kama ataitumia peke yake!

Bado nawashangaa pia wanaoishangaa kanuni hii, kila siku wamekuwa wakilalama kwamba ccm haiweki mazingira sawa kwa wagombea kwa sababu wana rasilimali nyingi wamezishikilia, leo hao hao ccm wamekubali wakasema sasa kiwango cha kutumia fedha kiwe sawa ,bado watu wanalalamika.

Kwa sababu haijaweka kiwango sawa!

Hivi ninyi ccm wakiruhusu kila mmoja atumie fedha zake ,nyie mnaolalamika leo mtaweza kushindana na ccm kujitangaza kwa kutumia fedha???

Si waruhusu uone wakatavyoumizana CCM wenyewe; kwani aliyedhurika zaidi kwama 2005 ni nani, si CCM?

Najuwa hamlalamiki kuhusu usawa, najuwa wamewabana kutumia helikopita kama kitega uchumi cha kuchota kodi za wananchi.

walioingiza magari 200 na watakoingiza pikipiki nyingine lukuki wakati huu si ndiyo wenye kushikilia mfuko wa kodi za wananchi?
 
Hizi limits ni at individual level or even at a party level?Itakuwaje kama chama kitatumia zaidi ya hiyo level?
 
Back
Top Bottom