Mgombea Urais matumizi yaongeza hadi Bil 5

Chukulia Rostam na mi pesa yake ya wizi sijui halali, akiamuwa akanunua mchele kila familia jimboni kwake , si anatumia fedha zake bwana kuna kosa hapo??

Hii sasa ni rushwa!

pamoja na fedha ni zako, lakini kuna mazingira ambayo serikali inabidi kulimiti utumiaji na namna unavyozitumia fedha

Isipokua mazingira ya ufisadi, au rushwa sio haki kumlimiti mtu kwa mfano kununua muda wa kujinadi kwenye TV ni rhuksa hata zaidi 1 bil.

Mfano Poland ukimpa fedha omba omba hawa ma homeless polisi wakikuotea unampa pesa umekwisha.
Kama sio ufisadi nadhani hapa Poland wanaingilia uhuru wa mtu

Kila tendo lina namna yake ya kulitafsiri hata kama mali ni yako.Japo sina uhakika kabisa fedha ni ya serikali ama mtu anayeimiliki.
Huna uhakika kwa sababu sheria hii ni mbovu! Ingekua nzuri isingekua na utata
 
Ni kosa kama lengo la kugawa mchele ni kununua uongozi

sasa hiyo utaipima je? kama alitaka kwa ajili ya uongozi ama alitaka kusaidia kwa fedha zake masikini?? maana masikini wanaohitaji msaada wapo wakati wote wakati wa kampeni na wakati usio kampeni.

Kifupi tunahitaji sheria inayoenda mbali zaidi ya kudhibiti hata matumizi ya mtu binafsi.

inatakiwa sheria kwenda mbali zaidi isiishie hapo tu kwenye mambo ya uchaguzi, na napendekeza sheria iingie ndani zaidi hata mtu akijenga nyumba inabidi apeleke ankara jinsi alivyopata fedha hizo na jinsi alivyolipa kodi.

Nimekupa mfano Poland ukimpa fedha homless na polisi wakikuotea umekwisha. Na ukiwa na kiwanda cha mikate ukaamuwa hiyo mikate kuwagawia watu itakubidi uilipie ushuru mikate yote uliyogawa.
 
sasa hiyo utaipima je? kama alitaka kwa ajili ya uongozi ama alitaka kusaidia kwa fedha zake masikini?? maana masikini wanaohitaji msaada wapo wakati wote wakati wa kampeni na wakati usio kampeni.

Kifupi tunahitaji sheria inayoenda mbali zaidi ya kudhibiti hata matumizi ya mtu binafsi.

inatakiwa sheria kwenda mbali zaidi isiishie hapo tu kwenye mambo ya uchaguzi, na napendekeza sheria iingie ndani zaidi hata mtu akijenga nyumba inabidi apeleke ankara jinsi alivyopata fedha hizo na jinsi alivyolipa kodi.

Nimekupa mfano Poland ukimpa fedha homless na polisi wakikuotea umekwisha. Na ukiwa na kiwanda cha mikate ukaamuwa hiyo mikate kuwagawia watu itakubidi uilipie ushuru mikate yote uliyogawa.
Ndiyo maana wenye akili walifuta takrima........kila nchi na sheria zake ya Poland waachie wa Polish
 
inatakiwa sheria kwenda mbali zaidi isiishie hapo tu kwenye mambo ya uchaguzi, na napendekeza sheria iingie ndani zaidi hata mtu akijenga nyumba inabidi apeleke ankara jinsi alivyopata fedha hizo na jinsi alivyolipa kodi.

Hapa unazungumzia kama fedha ni halali zimepatikana kihalali na kodi imelipwa...Hii ni sawa kabisa lakini si kuthibit matumizi . Sheria ilipaswa kuchunguza kama hizo fedha zimepatikana kihalali basi na sio za EPA or Kagoda!
 
Hii sasa ni rushwa!



Isipokua mazingira ya ufisadi, au rushwa sio haki kumlimiti mtu kwa mfano kununua muda wa kujinadi kwenye TV ni rhuksa hata zaidi 1 bil.


Kama sio ufisadi nadhani hapa Poland wanaingilia uhuru wa mtu

Huna uhakika kwa sababu sheria hii ni mbovu! Ingekua nzuri isingekua na utata

sema ni mbovu kwa misingi ipi? kama ni ubovu wake utakuwa je wakati inatumika kwa wote?? Karibu kila sheria ni mbovu ilaa kwa vile ina apply kwa wote inageuka kuwa nzuri.Itakuwa mbovu tu mara itakapo toa upendeleo.
 
Ndiyo maana wenye akili walifuta takrima........kila nchi na sheria zake ya Poland waachie wa Polish

Ni kweli kabisa
Na ndio maana ya kwetu ni ya kwetu ktk kampeni mwisho ni bilioni moja. Na ndio maana kule mwanzo nilishangaa mjumbe mmoja akisema hii sheria haiko kote kote duniani wakati akisahau ya kwetu ni ya kwetu na yao ni ya kwao.

Mie binafsi ningependa kama ikiongezwa sheria juu ya hiyo ya kumonitor matumizi ya fedha with respect na kipato chako.Isiishie hapo tu kwenye uchaguzi japo hiyo ni hatua moja mhimu.teh teh
 
Hapa unazungumzia kama fedha ni halali zimepatikana kihalali na kodi imelipwa...Hii ni sawa kabisa lakini si kuthibit matumizi . Sheria ilipaswa kuchunguza kama hizo fedha zimepatikana kihalali basi na sio za EPA or Kagoda!

Hata kama umeipata fedha kihalali inabidi ,wakudhibiti jinsi unavyoitumia.

Mfano akija jamaa na fedha zake nyingi kihalali, akaja akazinunua fedha nyingiiii karibu zote za Tsh na akazipiga moto ama akazichimbia shimoni tu kwa mda fulani.
Unafikiri ni nini kitatokea? hapa najaribu kukuvuta ktk picha halisi.
 
kumbuka hiyo elfu 20 inajumlisha matangazo, malipo ya watendaji, vitendea kazi n.k ! Nyie subirini kutawaka moto huko hadi mshangae. Sasa kitakachofanyika ni kuwa, wale wenye uwezo sasa hivi wataandaa vitendea vyao vya kazi sasa hivi, yaani wataingia gharama yote sasa hivi! wale wenzangu na miye sasa watakaotaka kusubiri muda maalumu ndio watajikuta wanazidiwa 100:1 halafu watalalamika "sheria ile ya gharama ya uchaguzi mbaya".. mimi nitakuwa nimeshika popcorn yangu na togwa!
Je, nikiwa na magari yangu binafsi matano (yenye thamani ya zaidi ya TSh.100,000,000) nikayatumia katika kampeni zangu za ubunge, nitakuwa nimevunja hii sheria au la?! Wanatumia kigezo gani kusema gharama zote za uchaguzi ni milioni 40?
 
Je, nikiwa na magari yangu binafsi matano (yenye thamani ya zaidi ya TSh.100,000,000) nikayatumia katika kampeni zangu za ubunge, nitakuwa nimevunja hii sheria au la?! Wanatumia kigezo gani kusema gharama zote za uchaguzi ni milioni 40?

Nafikiri hawahesabu hivo,
gharama za kuedeshea mfano kununua mafuta, matengenezo n.k.

wewe ukiwa na chopa lako la bilion 100 ok. lakini lisinywe mafuta ya thamani ya bilioni moja na zaidi.
 
Nafikiri hawahesabu hivo,
gharama za kuedeshea mfano kununua mafuta, matengenezo n.k.

wewe ukiwa na chopa lako la bilion 100 ok. lakini lisinywe mafuta ya thamani ya bilioni moja na zaidi.

Itabidi tununue machopa yanayotumia Solar na Upepo.

Magari yanayotumia umeme/Gas. Sijui watafahamu vipi gharama zake?
 
Itabidi tununue machopa yanayotumia Solar na Upepo.

Magari yanayotumia umeme/Gas. Sijui watafahamu vipi gharama zake?

Sasa ukinunua machopa yanayotumia solar maana yake gharama ya uendeshaji haijavuka bilioni .teh teh teh
 
Labda tuwasaidie kuelewa "Election Expenses" ni nini:

Sheria inasema:
7.-(1) The term "election expenses" means all funds
expended or expenses incurred in respect of the conduct and
management of nomination process, election campaign and
election by a political party, candidate or Government and·
include
(inataja vitu mbalimbali)

na
(2) All funds used for promotional art groups for
purposes of presentation of a candidate to voters including the
cost of providing food, drinks, accommodation or ~portation
which has been reasonably incurred by a candidate for members
of his campaign team shall be deemed to constitute election
expenses.
Ina maana gharama za TOT ni sehemu ya Gharama za uchaguzi!

Ili kuelewa "Funds" ni nini, sheria inatumia Sec. 12(1) kutolea mfano na inafafanua:

(2) The term "funds" as used in subsection (1) shall be
construed to include:
(a) money;
(b) a motor vehicle;
(c) an aircraft;
(d) transportation;
(e) T-shirts;
(f) a flag;
(g) printing, publication or distribution of leaflets,
brochures or any other publications;
(h) broadcasting, radio or television equipment;
(i) provision of food or drinks;
(j) promotional art groups; and
(k) any other thing intended to be used for furtherance
of election campaigns.

Lakini haya yanaweza kukufanya ufikirie kuwa mgombea anaweza kutumia "gharama" zake mwenyewe. Si kweli. Sheria inasema hivi waziwazi..

14.-(1) All expenses to be incurred during the nomination
process within the political parties shall be borne out by a political
party concerned.

Na kama watu wasiojali Katiba za vyama vya siasa na utaratibu wao wa kufanya uteuzi wa wagombea sheria yenu inasema:
(2) For the purpose of this section, the Minister shall, in
consultation with the Registrar and political parties with full
registration, make uniform regulations which shall be observed
during the nomination process by all political parties
.

Lakini huyu Minister si naye aweza kuwa ni mgombea wa chama cha siasa? Kwanini tuamini kuwa maamuzi yake hayatakuwa ya kubeba Chama chake?
 
pix.gif

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa.

WANASIASA wa vyama mbalimbali vya upinzani wamependekeza matumizi kwa wagombea katika kampeni za uchaguzi mkuu ziongezwe, kwa maana fedha zilizopendekezwa na Serikali ni kidogo...
Serikali ilipendekeza gharama za matumizi ya mgombea urais yasizidi Sh bilioni moja, huku ubunge na udiwani gharama zikiwa zinategemea eneo la jimbo, idadi ya watu na hali ya miundombinu.

Katika majadiliano ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi yaliyomalizika Dar es Salaam, jana, wanasiasa hao walisema gharama zilizowekwa hazilingani na hali halisi ya sasa na wala haziendani na kupanda kwa gharama za maisha mwaka hadi mwaka kutokana na sababu mbalimbali, likiwamo ongezeko la watu na ukame.

Aidha, walisema sheria hiyo inatakiwa kufanyiwa marekebisho ya kina ili isilete usumbufu siku za baadaye kwa kutakiwa kubadilishwa kutokana na ongezeko la mahitaji au kupanda kwa gharama za maisha.

John Mnyika wa Chadema alisema viwango vilivyopendekezwa ni vidogo kutokana na maeneo mengine kuwa na majimbo makubwa na vituo vingi vya uchaguzi, hivyo Sh bilioni moja haitatosheleza shughuli zote za uchaguzi.

“Chadema tulifanya kampeni katika uchaguzi uliopita na tulitumia zaidi ya Sh milioni 700 na hatukuzunguka majimbo yote, hivyo Sh bilioni moja kwa sasa ni kiwango kidogo ikilinganishwa na gharama za maisha zilivyopanda, labda angalau Sh bilioni mbili au tatu,” alisema.

Alisema pamoja na viwango hivyo kuwa vidogo, lakini kinachopaswa kuangaliwa zaidi ni matumizi sahihi ya gharama ambapo pia alisema sheria hiyo imechelewa kujadiliwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo alisema ni ngumu kufanya makadirio ya gharama za uchaguzi kwa sababu kila chama kina mapendekezo yake ya jinsi ya kufanya kampeni ambapo wengine hutumia matangazo mengi kwenye vyombo vya habari na wengine magari na helikopta kufuata wananchi.

“Ni ngumu sana kufanya makadirio ya gharama za uchaguzi maana hata wananchi nao wana mtazamo tofauti, sasa hivyo mtu huwezi kuwaendea kwa miguu tu, wengine wanalazimika wakati mwingine kutumia magari na wengine helikopta,” alisema.

Alisema tatizo si fedha ila kinachopaswa kuangaliwa ni jinsi inavyotumika na kueleza kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakizitumia kununua watu na wengine kuzigawa kama njugu wakati wa kampeni za uchaguzi.

“Kwa kipindi cha nyuma, tumekuwa tukivumilia uchaguzi wa aina hiyo ila kwa sasa uchaguzi wa ‘kumwaga’ fedha utadhibitiwa na wengi waliokuwa wakifanya hivi ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maana walikuwa wanaona uongozi ni pesa,” alisema.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Wilbrod Slaa, alisema uchaguzi ujao unaonekana kuwa mgumu kutokana na sheria hiyo na kueleza kwamba ingawa lengo ni kuzuia rushwa, lakini fedha hizo ni kidogo.

Aidha, wadau hao walitaka kifungu cha kuwapo kwa watu maalumu wa kampeni kubadilishwa, kutokana na kifungu kinachoonesha kwamba baada ya watu hao kutambuliwa, hatatakiwa mtu mwingine kumnadi mgombea kama si mwanakampeni.

Walisema hiyo ni kuwanyima Watanzania haki za msingi za kumnadi mgombea wanayemtaka na wakataka mgombea anapohitaji kubadilisha watu wanaomkampenia kutoomba kibali upya na badala yake kutoa taarifa tu kwa Mamlaka iliyopo.

Rais wa Tadea, John Chipaka, alisema haina haja ya kubanwa kwa fedha hiyo na badala yake wananchi wasimamie uchaguzi wenyewe na kutoa taarifa kwa wanaogawa vitenge au sukari, ili wapewe kura maana hao ndio wanaoua maendeleo ya nchi kutokana na kutorudi kuwaangalia wanapochaguliwa.

CHANZO: HABARILEO
 
WASOMI wamesema mapendekezo yaliyotolewa na serikali ya kutaka matumizi ya mgombea urais yasizidi Sh1 bilioni katika uchaguzi, ni kiini macho na kwamba yamelenga kumsaidia rais aliye madarakani na kuwakandamiza wapinzani wake.

Pia, wamesema kwa upande mwingine mapendekezo yanaashiria kuwaengua wagombea wenye kipato kidogo na kuwaacha wenye kipato kikubwa.

Kauli ya wasomi inatokana na mapendekezo ya serikali kuhusu kanuni na utaratibu wa matumizi ya sheria mpoya ya gharama za uchaguzi iliyosainiwa kwa mbwembwe wiki moja iliyopita na Rais Jakaya Kikwete. Kanuni za taratibu hizo zilijadiliwa kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Karimjee ukishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na asasi za kiraia.

Mbali na pendekezo hilo la kutaka wagombea urais watumie kiasi hicho cha fedha kuanzia kwenye mchakato wa uteuzi ndani ya chama hadi katika kampeni, serikali imependekeza kuwa gharama kwa wagombea ubunge na udiwani zitegemee eneo la jimbo, idadi ya watu pamoja na hali ya miundombinu.

Katika mapendekezo hayo matumizi ya wagombea ubunge yanatakiwa kuwa kati ya Sh10 milioni na Sh40 milioni huku udiwani ikiwa ni kati Sh1 milioni hadi Sh10 milioni.

Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, wasomi hao, Dk Benson Bana, Profesa Mwesiga Baregu na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam(UDSM), Bashiru Ally, walisema uwepo wa sheria ya gharama za uchaguzi ni muhimu lakini utekelezaji wake kivitendo ndio utakoa kuwa na matatizo na kwamba kiwango cha fedha kilichopendekezwa kinaashiria kuwaengua wagombea wenye kipato kidogo na kuwaacha wenye kipato kikubwa.

Ally alisema endapo mapendekezo hayo yakipitishwa wanasiasa watakuwa wamejiingiza katika mtego na kwamba kiwango cha Sh1 bilioni tu kutumika katika mchakato wa kuteuliwa na chama hadi kampeni hakitawezekana kutokana na hali halisi ya mazingira ya nchi.

"Huu ni mtego waliotegewa wanasiasa... haiwezekani Sh1bilioni tu zikatumika kuanzia mchakato wa kuteuliwa na chama na hadi kampeni kwa kuzunguka nchi nzima kwa mgombea wa urais," alisema Ally.

"Haya yote ni kama kiini macho. Pia, kiwango cha fedha kilichopendekezwa kinaashiria kuwaengua wagombea wenye kipato kidogo na kuwaacha wenye kipato kikubwa," alisema Ally.

Ally, ambaye ni mchambuzi wa siasa za ndani na nje ya nchi, alifafanua kwamba kutokana na mfumo wa fedha wa nchi ulivyo, ni vigumu kwa mgombea kudhibitiwa kutumia kiasi chochote cha fedha.

"Financial flow (mtiririko wa kifedha) wa nchi haupo imara. Hadi sasa hauwezi kutambua nani kaingiza kiasi hiki na katumia kiasi hiki," alisema Ally na kuhoji: "Mgombea anaweza kutumia zaidi ya kiwango alichowekewa na nani anaweza kujua hilo."

Naye Profesa Baregu alisema pamoja na mambo mengine, sheria hiyo ingeanisha mambo ambayo hayatakiwa katika kampeni.

"Nimeshangaa hayo mapendekezo lakini nilifikiri kuwa pamoja na mambo mengine sheria hiyo ingeainisha mambo machafu ambayo hayahitajiki katika kampeni, lakini si kung'ang'ania kuweka kiwango maalumu cha matumizi ya fedha," alisema Profesa Baregu.

Naye Dk Bana alisema kutokana na ukubwa wa nchi, mazingira pamoja na miundombinu gharama hizo ni ndogo na kwamba mwenye kuweza kumudu kiasi hicho ni mgombea urais yeyote atakayekuwa madarakani na kipindi chake cha miaka kumi ya urais bado hakijamalizika.

"(Mgombea urais aliye madarakani) Atatumia hata rasilimali za serikali ili kumudu kufanya kampeni nchi nzima, lakini si kwa wagombea wa upinzani," alisema Dk Bana, ambaye ni mtaalamu wa sayansi ya siasa.

Dk Bana alisema katika utafiti uliofanywa na Redet kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, wagombea wa urais walitumia si chini ya Sh1.5 bilioni huku wabunge walitumia kati yaSh 60 milioni hadi Sh100 milioni.


http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18708
 
Fedha za kusaka urais ni bilioni 5/-.

Ni mara tano ya pendekezo la Tendwa
headline_bullet.jpg
Ubunge nao sasa ni Sh. milioni 50
headline_bullet.jpg
Vyama vyawasilisha mapendekezo



Cheyo%285%29.jpg

Mwenyekiti wa United Democratic Party UDP), John Cheyo



Hatimayep; mvutano kati ya vyama vya siasa na Msajili wa vyama hivyo nchini kuhusu fedha anazopaswa kutumia mgombea urais kuanzia mchakato wa kuteuliwa na chama hadi kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu, umefikia tamati baada ya kukubaliana kwamba, zisizidi Sh. bilioni tano.
Makubaliano hayo, ni moja ya maazimio kadhaa yaliyofikiwa katika mkutano wa pamoja kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa na vyama hivyo uliofanyika kwa siku mbili mfululizo, jijini Dar es Salaam, kuanzia Jumatatu wiki hii.
Wanasiasa hao walikutana na Tendwa katika siku hizo kwa lengo la kujadili rasimu ya kanuni na taratibu zitakazotumika wakati wa uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi iliyotiwa saini na Rais Jakaya Kikwete Machi 17, mwaka huu.
Habari zilizopatikana baadaye zinaeleza kuwa mara baada ya majadiliano marefu, Tendwa na wanasiasa hao walikubaliana kimsingi, kwamba mgombea urais atumie fedha zisizozidi Sh. bilioni tano, kuanzia mchakato wa kuteuliwa na chama hadi kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Kabla ya makubaliano hayo kufikiwa, Tendwa alipendekeza kuwa mgombea wa urais asitumie zaidi ya Sh. bilioni moja, lakini pendekezo hilo lilipingwa na vyama vya siasa, kwa maelezo kuwa kiasi hicho ni kidogo na kwamba hakiwezi kumwezesha mgombea kumudu gharama za kumfikisha katika maeneo yote ya nchi.
Kwa mujibu wa maazimio kati ya Tendwa na vyama vya siasa, fedha anazopaswa kutumia mgombea wa kiti cha ubunge zimegawanywa kulingana na jimbo.
Katika mgawanyo huo, wadau hao wamekubaliana kuwa mgombea atakayewania kiti hicho katika majimbo yaliyoko makao makuu ya mkoa, fedha atakazotumia zisizidi Sh. milioni 50.
Atakayewania kiti hicho katika majimbo yaliyoko katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza zisizidi Sh. milioni 40.
“Kuhusu majimbo mengine, itategemea na wananchi,” kilisema chanzo chetu mara baada ya kikao hicho.
Chanzo hicho kimefafanua kuwa maeneo yenye wananchi kuanzia 150,000 hadi 300,000, fedha anazotakiwa kutumia mgombea wa kiti hicho zisizidi Sh. milioni 45.
Pia maeneo yenye wananchi kuanzia 100,000 hadi 150,000, fedha anazotakiwa kutumia mgombea ubunge zisizidi Sh. milioni 35, wakati wananchi walio chini ya idadi hiyo, ni Sh. milioni 25.
Hata hivyo, kiwango anachopaswa kutumia mgombea udiwani hakikuweza kubainishwa katika makubaliano hayo, lakini awali Tendwa alipendekeza zisizidi Sh. milioni 10.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa baada ya mkutano huo wa siku mbili kuhitimishwa jana, Tendwa na wadau hao watakutana tena Aprili 6, mwaka huu kwa ajili ya kutoa baraka za mwisho makubaliano yaliyofikiwa.
Habari zinasema kuwa baada ya hapo, rasimu ya makubaliano hayo itapelekwa kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya kutiwa saini ili kuwa kanuni.
Awali, wakikosoa mapendekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa yaliyotaka mgombea urais asitumie zaidi ya Sh. bilioni moja, viongozi wa vyama vya siasa walisema kiasi hicho ni kidogo na hakiwezi kumwezesha mgombea urais kufika mikoa yote 26.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Matson Chizii, alipendekeza angalau kiasi hicho kiongezwe hadi kufikia Sh. bilioni 10 ili zimwezeshe mgombea kuwafikia wananchi katika maeneo yote ya nchi.
Aliongeza kuwa Sh. bilioni moja haziwezi kutosha kukodisha magari na mafuta ya kuzunguka mikoa yote 26 na kwamba kiasi hicho kwa mtu anayegombea urais kinaweza kukatika kwa kampeni za mikoa miwili tu.
Mwenyekiti wa United Democratic Party UDP), John Cheyo, alisema ingawa ni vigumu kufanya makadirio ya gharama halisi za mgombea urais, kiasi kilichotajwa na Tendwa ni kidogo sana kwa kuwa kugombea nafasi hiyo ni jukumu zito.
Alisema kutokana na miundombinu mibovu, inakuwa vigumu kuwafikia wananchi, hivyo baadhi ya wagombea hulazimika kutumia helikopta ambayo ni gharama kubwa kuikodisha.
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, alisema kwa gharama ya Sh. bilioni moja haiwezi kuwa rahisi kwa mgombea urais kwani gharama za maisha zimepanda kwa kiwango kikubwa.
Alipendekeza angalau kiwekwe kiwango cha Sh. bilioni tano kwa mgombea urais na Sh. milioni 50 kwa wagombea wa ubunge.
Mwakilishi wa NCCR-Mageuzi, Beati Mpitabakana, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, alisema kiasi hicho hakitoshi na alipendekeza kiongezwe hadi kufikia angalau sh. bilioni tano.
Rais wa Tanzania Democratic Alliance (Tadea), John Lifa Chipaka, alisema kiasi hicho ni kidogo sana na kupendekeza kiongezwe hadi kufikia Sh. bilioni tano.
Mwenyekiti wa Chama cha Ustawi Tanzania (Chausta), James Mapalala, alisema Sh. bilioni tano hazitoshi kwa mgombea urais ambaye chama chake ni kipya na hakijawa na mtandao mkubwa wa nchi nzima.
Hata hivyo, Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, alitofautiana na wenzake kwa kusema kiasi hicho (cha sh. bilioni moja) kinaweza kutosha kama vyama hivyo havitahonga wapiga kura na alitoa mfano kuwa mwaka 2005, Chadema ilitumia sh. milioni 700 katika kampeni zake.
Naye Tendwa alisema ofisi yake ilitoa mapendekezo hayo ili wadau wayajadili, lakini kiasi hicho si uamuzi wa mwisho kama baadhi ya watu walivyotafsiri.



CHANZO: NIPASHE
 
Sasa pia mkumbuke kuwa sheria hii inabana zaidi baadaye (siku tisini) lakini kabla ya hapo mtashuhudia CCM ikifanya fundraising kubwa n.k Kila ninavyoangalia ninachoona ni kuwa sheria hii itaiumiza CCM zaidi na hasa wagombea wapya ambao majina yao hayajulikani sana.

Mwanakijiji CCM walishaanza matumizi ya kampeni siku nyingi kwani walishakuwa na insider information kuhusu hii sheria mpya. Si unakumbuka magari 200 waliyoagiza hivi karibuni na kupata tax exemption za TRA. Ukichukua grarama ya TZS 100 million kwa kila gari hapo unaongelea jumla ya TZS 20 Billion tayari zimetumiwa na CCM kujiandaa na kampeni zinazokuja.

Watu walioingia madarakani kwa njia ya rushwa hawawezi kamwe kuendesha vita dhini ya rushwa za uchaguzi.
 
By Dominic Nkolimwa


John%20Tendwa(2).jpg

Registrar of Political Parties John Tendwa



Political parties and the office of the Registrar of Political Parties have agreed on 5bn/-as the election expenses ceiling for Presidential candidates.
According to a reliable source from the two-day meeting between the political parties and the registrar discussing the implementation of the Election Expenses Act 2010, the amount was agreed after a long debate.
It was also agreed that expenses for each parliamentary candidate in constituencies located at regional headquarters should not exceed 50m/-, while in Dar es Salaam and Mwanza, a candidate's expenses should not exceed 40 million/-.
Political party delegates argued that candidates in constituencies at regional headquarters would be forced to spend more due to poor infrastructure.
The delegates also agreed that parliamentary candidates for a constituency having between 150,000 and 300,000 voters should not exceed 45 million/- in expenses.
The source added it was agreed that candidates in constituencies with 100,000 to 150,000 voters, should spend not more than 35m/-, while those in constituencies with less than 100,000 voters should spend not more than 25m/-.
The agreement will again be discussed at another meeting between the registrar and political parties, before it is sent to the prime minister for signing, ready for implementation.
According to the Election Expenses Act 2010, in order to combat dirty money and corruption during the elections, no support either financial or material from abroad will be allowed for any party, 90 days or three months before the general elections.
In a by-election no support either material or financial will be allowed for any party, 30 days before the elections.
One of the guidelines issued by the office of the Registrar of Political parties as part of the implementation of the Election Expenses Act 2010 states that presidential candidates in the general elections will not be allowed to enlist more than 50 people in their campaign teams, a move designed to check corruption.
According to the guidelines, parliamentary contestants would be limited to a campaign team of not more than 20 people while those vying for ward councillorship would be allowed to put up a team of not more than ten people.
Speaking at yesterday's meeting, the Registrar of Political Parties John Tendwa underlined the need for all political parties to respect and adhere to the requirements of the new law.
Representatives of the parties proposed that the Registrar provide special forms which would be used to report candidates bribing voters.
President Kikwete signed into law last Wednesday the Financing of Election Bill aimed at plugging loopholes often used by candidates to win through corrupt means.
The general elections are scheduled for October.




Wameshtuka bilioni moja ni changa la macho. Mabango na tisheti zitatengenezwa na nini pia kanga na kofia?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom