Mengi na Uanachama wake CCM

Hii kali sasa kwani huyu Kilumbe Ngenda si alisema amepita matawi yote ya chama chao DSM hajaona jina la uwanachama la Mengi sasa iweje akakiri? alitumwa na nani kuropoka bila kuwa na uhakika?


Not sure nani kamtuma, but any of these guys
1. RA
2.EL
3.SS (aka Sofia Si-mba)
4
5
6
Add to the list
 
Je, yawezekana hata majina ya Kibunango na Masatu hayamo kwenye daftari alilo nalo Kilumbe Ng'enda linaloorodhesha majina ya wanachama wa CCM ? Vipi na Fairplayer na wana JF wengine wanaojitambulisha kama wakereketwa - iteni press conference kama Mengi alivyofanya, WALT!
 
Kuna vilaza wengi tz lkn yule maza kiboko....yan huwa namsahau kila nnapoambiwa kutaja majina ya mawaziri...cjui mkuu analifikiriaje hili manake sio first time anafuka.....

Ha ha haah .... hutakiwi kumsahau!!Inatakiwa ndio awe wa kwanza kumkumbuka,KWA UJINGA WAKE lakini
 
JEURI iliyoonyeshwa na mfanyabiashara maarufu, Reginald Mengi, mbele ya waandishi wa habari kwa kuweka bayana uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na harakati zake za kukichangia chama hicho kwa hali na mali, inaonekana kukitikisa chama hicho tawala, Tanzania Daima imebaini.
Hali hiyo ya mtikisiko iliendelea kujidhihirisha ndani ya chama hicho jana, baada ya Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng’enda, kutoa tamko ambalo linaonyesha dhahiri kumuangukia mfanyabiashara huyo ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP.
Ng’enda katika taarifa yake ya kurasa mbili kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, alieleza bayana uamuzi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kutangaza rasmi kuutambua uanachama wa Mengi, sambamba na kumuomba mfanyabiashara huyo aendelee kukichangia chama hicho kwa hali na mali.
Kiongozi huyo wa CCM ambaye mara kadhaa katika siku za hivi karibuni amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akipinga hadharani uanachama wa Mengi katika chama hicho, katika tamko lake la jana alionyesha dhahiri kubadili msimamo huo.
Taarifa hiyo ya Ng’ande ambayo inaonekana dhahiri kuwa na maelekezo mahususi kutoka katika mamlaka za juu za chama hicho, imekuja siku chache tu baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, kukaririwa akitilia shaka uanachama wa Mengi ndani ya chama hicho.
Waziri Simba aliyekuwa akizungumza katika kikao cha ndani kati ya wabunge wa CCM na kamati ya maridhiano ya chama hicho inayoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alikaririwa akisema uanachama wa Mengi alioupata hivi karibuni ulikuwa umekataliwa.
Akifafanua katika taarifa yake ya jana, Ng’ande alisema, CCM Mkoa wa Dar es Salaam ilifikia uamuzi wa kuridhia uanachama wa Mengi baada ya matawi mawili ya chama hicho ya Kisutu na Mkunguni kutoa taarifa za kumtambua mfanyabiashara huyo kuwa ni mwanachama wao.
“Baada ya Tawi la Kisutu na Mkunguni kuthibitisha uanachama wa Ndugu Mengi na kuzingatia kwamba jukumu la kumpa mtu uanachama ni la kamati ya siasa ya tawi, kwa hiyo mkoa wetu hauna sababu ya kutotambua uanachama wake,” ilieleza taarifa hiyo ya jana.
Aidha, taarifa hiyo ilisisitiza kwamba, Mengi ataendelea kushirikiana na tawi lake katika kukiimarisha chama hicho, hasa kwa kuendelea kutoa michango yake ya hali na mali kama anavyofanya sasa.
Pia katibu huyo alimpongeza Mengi kwa kitendo chake cha ujasiri alichokifanya kwa kutangaza hadharani uanachama wake tofauti na ilivyo kwa wafanyabiashara wakubwa ambao hawapo tayari kukiri kujiunga na vyama vya siasa.
“Kwa kweli Mengi ameonyesha mfano wa kuigwa, kwani ni nadra sana kwa wafanyabiashara wakubwa wa aina hii kujitokeza na kukiri hadharani uanachama wao kwa vyama vya siasa,” ilisisitiza taarifa hiyo iliyosainiwa na Ng’enda.
Katibu huyo amelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya juzi gazeti moja la kila siku la Kiswahili (si Tanzania Daima), kuandika habari ikimkariri yeye mwenyewe akisema CCM Mkoa wa Dar es Salaam ilikuwa haitambui uanachama wa Mengi.
“Huu ulikuwa ni upotoshaji, jitihada za CCM ni kuhakikisha inaongeza jeshi la wanachama, hivyo hatuwezi kamwe kumpa kisogo mwanachama yeyote,” alisema Ng’enda katika taarifa ya jana akikanusha habari zilizoandikwa juu yake juzi.
Tamko hili jipya la CCM linakuja siku chache baada ya Mengi mwenyewe, mwishoni mwa wiki iliyopita, kutoa tamko akitangaza kwamba amekuwa mwanachama wa CCM mwenye kadi namba B124595 aliyoipata katika Tawi la Kisutu tangu Aprili 18, mwaka 1977, ikiwa ni miezi miwili na ushei tangu chama hicho kilipoasisiwa rasmi, Februari 5, mwaka huo huo.
Mengi ambaye alitoa ufafanuzi huo akijibu kauli za Waziri Simba na kupinga misimamo ya viongozi wengine wa CCM akiwamo Ng’ande na mwenyekiti wake wa Mkoa wa Dar es Salaam John Guninita, alikataa kujibishana, akisema alikuwa hawezi kufanya hivyo dhidi ya mtu mjinga.
Mbali ya hilo, Mengi alipotakiwa kusema iwapo alikuwa ameshawahi kukichangia chama hicho, hakuwa tayari kusema lolote zaidi ya kueleza tu kwamba, viongozi waadilifu wa CCM walikuwa na taarifa zote kuhusu hilo.
Wakati Mengi akisema hayo, taarifa zilizovuja kutoka ndani ya kikao cha pamoja cha wabunge na kamati ya Mwinyi zilimkariri mbunge mmoja akimtetea mfanyabiashara huyo, kwa kuwa mstari wa mbele kukichangia chama hicho tawala na akatoa mfano wa uchaguzi mdogo wa Busanda, ambapo alichangia kiasi cha shilingi milioni 100.



Source: Tanzania Daima
 
JEURI iliyoonyeshwa na mfanyabiashara maarufu, Reginald Mengi, mbele ya waandishi wa habari kwa kuweka bayana uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na harakati zake za kukichangia chama hicho kwa hali na mali, inaonekana kukitikisa chama hicho tawala, Tanzania Daima imebaini.
Mh waandishi wachochezi acha tuu!
 
Sina uhakika kama ni kweli Mengi ni mwanachama wa ccm kwa kuwa swala zima la uanachama ni gumu sana kulisemea hasa kwa mazingira ambayo mengi anajaribu kutuonyesha kuwa amekuwa mwanachama toka mwaka 1977.Kwa kweli huu ni ujinga na uongo mkubwa kwa mtu kudaikuwa yeye ni mwanachama wa ccm huku inajulikana wazi kuwa ccm ilitoa kadi mpya baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama ningi na kadi zote za zamani zilifutwa,yani zile kadi za lazima ambazo mtu alikuwa ata akitaka kwenda kazini au kusafiri nje ya nchi alikuwa anawajibika kuwa ni mwanachama safi wa chama cha mapinduzi.Aidha,kadi yenyewe ya bwana Mengi hakuna mtu alioisoma na kuona kama ina picha yake kwa kushuhudia ile pia yake kubwa kwenye kadi takatifu ya CCM
 
Sina uhakika kama ni kweli Mengi ni mwanachama wa ccm kwa kuwa swala zima la uanachama ni gumu sana kulisemea hasa kwa mazingira ambayo mengi anajaribu kutuonyesha kuwa amekuwa mwanachama toka mwaka 1977.Kwa kweli huu ni ujinga na uongo mkubwa kwa mtu kudaikuwa yeye ni mwanachama wa ccm huku inajulikana wazi kuwa ccm ilitoa kadi mpya baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama ningi na kadi zote za zamani zilifutwa,yani zile kadi za lazima ambazo mtu alikuwa ata akitaka kwenda kazini au kusafiri nje ya nchi alikuwa anawajibika kuwa ni mwanachama safi wa chama cha mapinduzi.Aidha,kadi yenyewe ya bwana Mengi hakuna mtu alioisoma na kuona kama ina picha yake kwa kushuhudia ile pia yake kubwa kwenye kadi takatifu ya CCM

Bwa ha ha ha ha
 
Sina uhakika kama ni kweli Mengi ni mwanachama wa ccm kwa kuwa swala zima la uanachama ni gumu sana kulisemea hasa kwa mazingira ambayo mengi anajaribu kutuonyesha kuwa amekuwa mwanachama toka mwaka 1977.Kwa kweli huu ni ujinga na uongo mkubwa kwa mtu kudaikuwa yeye ni mwanachama wa ccm huku inajulikana wazi kuwa ccm ilitoa kadi mpya baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama ningi na kadi zote za zamani zilifutwa,yani zile kadi za lazima ambazo mtu alikuwa ata akitaka kwenda kazini au kusafiri nje ya nchi alikuwa anawajibika kuwa ni mwanachama safi wa chama cha mapinduzi.Aidha,kadi yenyewe ya bwana Mengi hakuna mtu alioisoma na kuona kama ina picha yake kwa kushuhudia ile pia yake kubwa kwenye kadi takatifu ya CCM

amesema amekuwa mwanachama toka 1977 haimaanishi hana kadi mpya ya CCM! elewa utetezi wake
 
Jana kahamisha uanachama wake toka Kisutu(Dar es Salaam) kuelekea Moshi..Guninita anadai anataka ubunge...
 
• Ahofiwa kulenga nafasi ya kisiasa 2010

na Mwandishi Wetu


HATUA ya Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kutangaza kuwa ni mwanachama wa CCM pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, akiwa na wabunge waliojipambanua kuwa ni wapambanaji wa ufisadi, imezidisha hofu na mgawanyiko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili pamoja na mahojiano ya baadhi ya makada wa chama hicho, vimebainisha hofu iliyoanza kuingia ndani ya chama hicho katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.

Mmoja wa makada aliyezungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kutotaka jina lake liandikwe, alisema baadhi ya wabunge, hasa walio kambi tofauti na ile ya wapambanaji wa ufisadi, wanaona hatua hiyo ni mapambano ya wazi kati ya kambi hizo ambazo hivi sasa zimekuwa zikiwindana na kushutumiana kwa kificho na hadharani.

Anabainisha kuwa kujitokeza hadharani kwa Mengi na kuanza kuzunguka na baadhi ya wabunge, ambao hivi sasa wamejipatia umaarufu kwa madai ya kupambana na ufisadi, kumezidi kuleta mgawanyiko, maana baadhi ya wanachama wanaona hali hiyo inakidhoofisha zaidi chama badala ya kukijenga.

Chanzo hicho kimedokeza kuwa Mengi amekuwa mhimili mkubwa wa baadhi ya wabunge, ambao hivi sasa wamekuwa na wakati mgumu katika majimbo yao, kutokana na kile kinachodaiwa baadhi ya watu kupandikiza watu wao ili wawang'oe katika uchaguzi mkuu.

Miongoni mwa wabunge wanaodaiwa kukabiliana na hali ngumu katika majimbo yao ni Fred Mpendazoe (Kishapu), Christopher ole Sendeka (Simanjiro), Lucas Selelii (Nzega), na wengineo ambao tangu kutokea kwa kashfa ya Richmond wamekuwa wakitembea kifua mbele.

Baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakihusisha juhudi hizo za Mengi na kuwania uongozi wa siasa, licha ya Mengi mara kadhaa kuelezea dhamira yake ya kutotaka kuwania uongozi wowote wa kisiasa hapa nchini, kwa madai kuwa yeye ni mfanyabiashara asiyependa kuingia katika ulingo wa kisiasa.

Mengi alikuwa akihusishwa na kuwania urais, hasa baada ya serikali kubwagwa katika kesi ya kupinga kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika nafasi ya urais.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaainisha kuwa mbali na mfanyabiashara huyo kuzusha hofu na mgawanyiko katika chama hicho tawala, amesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kushughulikiwa kwa wabunge waliopo mstari wa mbele katika mapambano ya ufisadi.

Wanaeleza kuwa uungwaji mkono anaoupata mfanyabiashara huyo na kundi la wabunge analoliunga mkono kutoka kwa wananchi, ndiyo imekuwa silaha kubwa kwa viongozi wakubwa wa CCM kuwashughulikia wabunge wao kwa hofu ya kukosa kura.

Wachambuzi hao wanasema kitendo cha baadhi ya wanachama kujadili na kutaka kadi ya mfanyabiashara huyo aliyoikata hivi karibuni isikubaliwe na chama, lilikuwa ni jaribio muhimu la kuonyesha nguvu ya mfanyabiashara huyo ndani na nje ya chama.

Wanabainisha kuwa hatua ya mfanyabiashara huyo kutangaza wazi kuwa yeye ni mwanachama wa chama hicho tangu mwaka 1977, na alichukulia kadi katika Tawi la Kisutu, Dar es Salaam, iliwachanganya viongozi wengi waliokuwa wakimuona kuwa ni miongoni mwa wafadhili na wanachama wa upinzani.

Wanasema makada waliokuwa wakitaka kadi ya mfanyabiashara huyo isitambulike, walikosa nguvu pale uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam ulipotoa taarifa ya kumtambua Mengi, jambo lililotafsiriwa kuwa ni maagizo kutoka ngazi za juu za chama.

Wakati baadhi ya wanachama wa CCM, wananchi na wapinzani wakishangazwa na kutafakari hatua ya Mengi kutangaza hadharani uanachama wake, mfanyabiashara huyo ameamua kuhamisha uanachama wake kutoka Tawi la Kisutu, Dar es Salaam, kwenda Mkoa wa Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilimanjaro, Jonas Semu, ndiye aliyetoa taarifa za kumpokea Mengi, huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba, akiiambia Tanzania Daima kuwa utaratibu wa kuhamisha uanachama ni wa kawaida na kila mwanachama anayo haki ya kufanya hivyo.

"Huo ni utaratibu wa chama na hata mimi nilipokuwa mkuu wa mkoa nilihamisha uanachama wangu kutoka Kivukoni kwenda Mikocheni, na baadaye nilitaka kuishi katika nyumba yangu mwenyewe nikahamishia tena uanachama wangu huko Tegeta.

"Kama hutahamisha uanachama wako ina maana huwezi kupiga kura za maoni, na ukitaka kugombea ubunge ni lazima uwe mwanachama wa eneo hilo," alisema Makamba.

Wadadisi wa masuala ya siasa wanaweka wazi kuwa ufafanuzi huo wa Makamba na hatua ya Mengi huenda ndiyo ikawa ishara ya mfanyabiashara huyo kuingia katika medani ya kisiasa badala ya kuendelea kuwasaidia baadhi ya wabunge.

Wanabashiri kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ndani ya CCM utakuwa mgumu, kwa kuwa ufa wa kutokuelewana kwa makundi ndani ya chama hicho, umezidi kushamiri na kuingia kwa Mengi kumeongeza chachu ya ugumu.

Aidha, wachambuzi hao wanabainisha kuwa huenda pia hofu ya baadhi ya wanachama ikawa sahihi kuwa Mengi ana lengo la kugombea nafasi ya kisiasa ili apambane na baadhi ya wanasiasa wanaotuhumiwa kwa ufisadi, lakini bado wanaendelea kuwa wawakilishi wa wananchi na chama.

SOURCE: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=10339
 
Buchanan, pale unapochagua kutumia "breaking news" prefix kwenye habari unayotundika,ni nini haswa kinakuongoza kufanya hivyo? Jamani, kwanini tusiwe wastaarab na kujaribu kuelewa matumizi ya hiyo prefix?!
 
Buchanan, pale unapochagua kutumia "breaking news" prefix kwenye habari unayotundika,ni nini haswa kinakuongoza kufanya hivyo? Jamani, kwanini tusiwe wastaarab na kujaribu kuelewa matumizi ya hiyo prefix?!


wewe naye! hivi hujui level ya interlect ya posters wengine ndani ya JF?

halafu mnataka watu wafanye serious analysis humu

for what?

mtu ana post the whole article bila source link wala comment yake
 
Nimesoma habari kutoka gazeti la Tanzania daima na nimeona Bw. Mengi amehamishia uanachama wake toka tawi lake la CCM la Kisutu kuelekea Kilimanjaro! Je huu ni mwanzo wa yeye kuingia rasmi kwenye siasa yaani kugombea Ubunge na kama ni hivyo je ni jimbo gani atagombea? Nathani huu ni muda muafaka kwa wana Chadema kukaa mkao wa kula haswa Mzee Ndesa-pesa na Bw. Mbowe maana hiki ni kisiki cha mpingo kikiamua kugombea Ubunge katika majimbo hayo yaani Moshi Mjini au Hai kinachukua kiulaini.

Ila sidhani kama itakuwa ni wazo zuri kwa demokrasia hapa nchini maana sijui Mzee Ndesa-pesa atamjibu nini huyu Mengi katika kupokonya tonge mdomoni? Maana mara ya mwisho alimwambia Prof. Maghembe atamrudisha kwa miguu kipindi atakachosubuthu kunusa jimbo lake! Sasa tumeona amenunua copters kama maandalizi ya kulinda hilo jimbo! Nadhani mwaka kesho kutachimbika huko Kilimanjaro maana naskia pia Michael Ngaleku Shirima yuko mbioni kugombea jimbo la Rombo kwa kupitia CCM!
 
Ile ni tactical move,kaona jamaa wa Dar wanaweza kuitisha kikao kimizengwe na kumfukuza chamani.Wote tulisikia kauli za Mwenyekiti na Katibu wa Mkoa.Hakuna tena kuaminiana
 
Back
Top Bottom