Mengi na Uanachama wake CCM

Ni kichaa au punguani peke yake anayeweza kubisha kwamba mtu fulani sio mwanachama wa chama fulani. Kadi za vyama hivi zinapatikana kirahisi sana kama karanga au mahindi ya kuchoma mtaani.
Halafu, ofisi za vyama vyetu hivi hazina uwekaji wa kumbukumbu za wanachama wao nzuri kiasi hicho. Kadi za CCM, CHADEMA, CUF,....zinapatikana kirahisi kama laini za voda, tigo, zain,.....
 
Wazushi CCM, kwanza hawana hata utaratibu wa kutunza kumbukumbu za wanachama wao, kadi wanagawa km njugu mtaani bila kurecord popote... leo wanadai ooh tumepita matawi yote hatujaona jina la Mengi, mara ooh mengi ni mwanachama,haya mwingine anaomba msamaha... huu ni usaniii!!
 
Kwa mara nyingine tena nawashangaa hawa the so called strategists wa siasa zetu za Tanzania. Naona kuna watu wanaokotwa okotwa tu wasiojua manafanya nini, eti ndio wanakuwa planners jinsi mambo yaendaje.Asilimia tisini yana back fire badly.Kazi ipo maana hata asiye na macho anaona jinsi mambo yanavyoharibiwa
 
Siku hizo kadi ya CCM ni kama lulu, ukifikiria chama kilianzishwa mapema mwaka huo huo,kuipata ilikuwa kwa mbinde

Naona watu hawaelewi what is going on. Mengi aliwaambia Sofia Simba/Ng'enda/Guninita kuwa kama wanataka kuhakikisha uanachama wake basi waulize kwa viongozi wa ngazi za juu wa CCM. Walipouliza wakaambiwa kuwa wasimchezee Mengi na wathibitishe haraka. Hii inaonyesha kuwa uanachama wa Mengi ni wa siri na unajulikana katika ngazi za juu tu.

Kwa mantiki hiyo hiyo, utakuta Mengi ni mwanachama wa Chadema, TLP, NCCR Mageuzi, Mtikila's Party (jina lake limenitoka) etc. Na uanachama wake katika vyama hivyo pia unajulikana katika ngazi za juu tu.

Kuthibitisha hilo, mtakumbuka hadithi za fedha za Chadema zilizocheleweshwa njiani wakati wa chaguzi ndogo, jinsi Mtikila alipopewa fedha ili afungue shauri mahakamani kuhusu mgombea binafsi etc etc.

Hili la CCM imebidi liwekwe wazi kwa sababu viongozi wa kati wa CCM walifyatuka bila kucheki kuhusu uanachama wa Mengi na maji yakawa tayari yamemwagika ama sivyo wala watu wasingejua kwa uahakika uanachama wa Mengi CCM.

Na kwa kuwa CCM ndio chama tawala ni lazima Mengi awe katika good books with it ama sivyo mambo yake yanaweza kuharibika.
 
tk

Kwa mantiki hiyo hiyo, utakuta Mengi ni mwanachama wa Chadema, TLP, NCCR Mageuzi, Mtikila's Party (jina lake limenitoka) etc. Na uanachama wake katika vyama hivyo pia unajulikana katika ngazi za juu tu

This is a pumba of the day!
 
Bhayandaa,

Hawa viongozi nao wamezidi kulopoka sana wengine itabidi watambue maana ya majina yao kwa mfano Sophia maaana yake ni WISDOM sasa kwakweli yeye hapo si mwelewi kwanini analopoka nadhani hilo sio Jina lake kuna haja ya kwenda milembe kweli tukajue uwezo wake wa akili ukoje

Aibu gani hii viongozi wengi wa CCM wana watu wao ni wachinvimbi na wanao tembeza ftina ndani ya Jumuuiya ya UVCCM na UWT na NEC na CC umbea full ndio chanzo cha viongozi wetu wengu wasiokuwa na ujasili na walioingia madarakani kwa mlango wa nyuma kama unajiamini wananchi wanakupenda na kukuamini wapi unakuwa hujiamini??
 
Hiyo ndio Tanzania yetu, where leaders on the frontline, dare to talk boldly only to think later on!Siyo Kilumbe tu, tukiomba wanajamvi walete quotes za viongozi kuropoka then next day baada ya kufikiri wanasahihisha utashangaa. Kama unakumbuka any of those confusing statements rusha hapa. Tunaanza na Kilumbe, who is next? Kazi kwenu wanajamvi
2.
3.
4.
5.
6.

hivi unafikiri huwa wanafikiria baadae wanayo yasema??? no! no mmojawao ambae ni mjanja mjanja kidogo ndo anamshtua kuwa 'pale ulichemsha'
 
Ndiyo tatizo la kuropoka bila hata kufikiri. the so called Kilumbe Ng'enda hii si aibu kwako sasa? unakurupuka tu ili kuwafurahisha mabwana/ watwana wako ona sasa ulivyoaibika!
Ashakum si matusi; hata anayetaka kutoa ushuzi huangalia na kuhakikisha mazingira kama yanaruhusu, hawezi kutoa ushuzi hovyohovyo kama huu wa Kilumbe, 'Ooo Mengi siyo mwanachama oo orodha ya matawi yote ninayo n.k Unafaa kweli kuwa katibu wewe?
 
Hii inaonyesha kuwa uanachama wa Mengi ni wa siri na unajulikana katika ngazi za juu tu.

Kwa mantiki hiyo hiyo, utakuta Mengi ni mwanachama wa Chadema, TLP, NCCR Mageuzi, Mtikila's Party (jina lake limenitoka) etc. Na uanachama wake katika vyama hivyo pia unajulikana katika ngazi za juu tu.

Haya ni matumizi mabaya ya mantiki; yaani hitimisho lako halijafuata msingi wa hoja yako. Yaani kwa vile Mengi ni mwanachama CCM na siyo siri (kwani inajulikana hadi kadi yake) iweje tena awe mwanachama wa siri kwenye vyama vingine?

Kuthibitisha hilo, mtakumbuka hadithi za fedha za Chadema zilizocheleweshwa njiani wakati wa chaguzi ndogo, jinsi Mtikila alipopewa fedha ili afungue shauri mahakamani kuhusu mgombea binafsi etc etc.

Yaani katika viwango vya ushahidi ndugu yangu ulilosema halithibitishi lolote. Mwingine anaweza kusema "ulisikia zile fedha zilizoibwa kutoka benki fulani"... and?
Hili la CCM imebidi liwekwe wazi kwa sababu viongozi wa kati wa CCM walifyatuka bila kucheki kuhusu uanachama wa Mengi na maji yakawa tayari yamemwagika ama sivyo wala watu wasingejua kwa uahakika uanachama wa Mengi CCM.

Ndilo tatizo la miungu watu ndani ya CCM ambao wanafikiri bila kupigiwa magoti na kulambwalambwa na waumini basi sala haziendi!

Na kwa kuwa CCM ndio chama tawala ni lazima Mengi awe katika good books with it ama sivyo mambo yake yanaweza kuharibika.

Hili lina ukwel kwa kiasi kikubwa. Lakini ukiliangalia utaona linawagusa wengi sana ndani ya chama hicho hata nje yake. It is the nature of the beast
 
Na kwa kuwa CCM ndio chama tawala ni lazima Mengi awe katika good books with it ama sivyo mambo yake yanaweza kuharibika.

You miss the point tk, pengine wewe ni wa juzi.
Siku hizo usipokuwa mwanachama wa CCM katika ngazi yoyote ungejulikana kama mpinga chama, hasa kama shughuli zako zinagusa ofisi za serikali.
Hivyo wanachama walikuwa toka mfagizi wa ofisi hadi Meneja Mkuu au Waziri.
Hivyo si ajabu kuwa Mengi alikuwa mwanachma tika siku hizo chama kilipoanzishwa.
 
Ndiyo tatizo la kuropoka bila hata kufikiri. the so called Kilumbe Ng'enda hii si aibu kwako sasa? unakurupuka tu ili kuwafurahisha mabwana/ watwana wako ona sasa ulivyoaibika!
Ashakum si matusi; hata anayetaka kutoa ushuzi huangalia na kuhakikisha mazingira kama yanaruhusu, hawezi kutoa ushuzi hovyohovyo kama huu wa Kilumbe, 'Ooo Mengi siyo mwanachama oo orodha ya matawi yote ninayo n.k Unafaa kweli kuwa katibu wewe?

Jambo tunajifunza pia ni kwamba usiamini kila unaloambiwa... kumbuka hatat Sophia Simba ambaye ni Waziri alisema kuwa Mengi aliomba uanachama hivi karibuni ... akanyimwa!!!! Na ndio mana mzee mengi alimpa ushauri kuwa awe anauliza kwanza aaaa kabla ya kuropoka
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom