Mengi na Uanachama wake CCM

wewe naye! hivi hujui level ya interlect ya posters wengine ndani ya JF?

halafu mnataka watu wafanye serious analysis humu

for what?

mtu ana post the whole article bila source link wala comment yake

Source link nimeweka mwishoni mwa post na comment ndio hii ninayokuandikia wewe, umeridhika?
 
Buchanan, pale unapochagua kutumia "breaking news" prefix kwenye habari unayotundika,ni nini haswa kinakuongoza kufanya hivyo? Jamani, kwanini tusiwe wastaarab na kujaribu kuelewa matumizi ya hiyo prefix?!

Toa shule badala ya kulaumu, ni wakati upi inakuwa breaking news na wakati upi sio? Nafikiri ni suala dogo kuelimishana kuliko kuanza ku-divert mada unnecessarily!
 
Breaking News....Nalo hili tuanze kuelimishana kuwa linahusu nini na linatumika mahala gani??By the way,why you chose to use it in the first sight!?Habari ya kutoka gazetini tena linalopatikana online na lipo available tangu alfajiri(EAT),jioni hii unataka kuiita ni breaking news?
 
Breaking News....Nalo hili tuanze kuelimishana kuwa linahusu nini na linatumika mahala gani??By the way,why you chose to use it in the first sight!?Habari ya kutoka gazetini tena linalopatikana online na lipo available tangu alfajiri(EAT),jioni hii unataka kuiita ni breaking news?

Ok, ndugu yangu nimekubali mapungufu! Ubarikiwe!
 
Mengi kila wakati huwa anawazidi akili CCM. Amefanikiwa kumweka JK mfukoni kwa kumkejeli kuwa anapiga vita ufisadi. Wakati huohuo anawanyima wakina Makamba usingizi kwa kauli zake tata na hamna wanachoweza kumfanya. Cha kujiuliza ni anajipanga kwa lipi 2010 kwenye hii move? Maana licha ya kuombwa msamaha yaishe na viongozi wa Dar bado amehamisha uanachama wake kwenda Moshi mjini (na sio Hai). Mh tusibiri tuone...

.
 
...Nadhani mwaka kesho kutachimbika huko Kilimanjaro maana naskia pia Michael Ngaleku Shirima yuko mbioni kugombea jimbo la Rombo kwa kupitia CCM!

Shirima na Mramba ni marafiki wakubwa na business partners. Kambi ya Mramba ndio imeshinda uongozi wa chama jimboni na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa watu wa CCM walioshinda ni wa kwake. Hizi rumours zinaweza kuwa kweli kwani kesi za ufisadi zikimbana Mramba itakuwa rahisi kwa Shirima kumrithi kama mgombea maana machinery tayari ipo.

.
 
Kulikoni Mzee Mengi kuamishia tawi Kilimanjaro
Nimesoma habari kutoka gazeti la Tanzania daima na nimeona Bw. Mengi amehamishia uanachama wake toka tawi lake la CCM la Kisutu kuelekea Kilimanjaro! Je huu ni mwanzo wa yeye kuingia rasmi kwenye siasa yaani kugombea Ubunge na kama ni hivyo je ni jimbo gani atagombea? Nathani huu ni muda muafaka kwa wana Chadema kukaa mkao wa kula haswa Mzee Ndesa-pesa na Bw. Mbowe maana hiki ni kisiki cha mpingo kikiamua kugombea Ubunge katika majimbo hayo yaani Moshi Mjini au Hai kinachukua kiulaini.

Ila sidhani kama itakuwa ni wazo zuri kwa demokrasia hapa nchini maana sijui Mzee Ndesa-pesa atamjibu nini huyu Mengi katika kupokonya tonge mdomoni? Maana mara ya mwisho alimwambia Prof. Maghembe atamrudisha kwa miguu kipindi atakachosubuthu kunusa jimbo lake! Sasa tumeona amenunua copters kama maandalizi ya kulinda hilo jimbo! Nadhani mwaka kesho kutachimbika huko Kilimanjaro maana naskia pia Michael Ngaleku Shirima yuko mbioni kugombea jimbo la Rombo kwa kupitia CCM!
 
Shirima alishakanusha kujiingiza siasa na Mramba is done, gone case. Mengi katika kujipendekeza kisawasawa anakwenda kuongoza kikosi cha ukombozi kugomboa majimbo ya Moshi akisaidiana na Aggrey Marealle ili onekane shujaa kuliko familian ya Mangi Mkuu
 
Ni kwa sababu akina Simba hapo Dar walisema hawamtambui yeye kama mwana CCM!
 
Huyu Mengi sasa ni mnafiki asitumie siasa kwa maslahi yake ya biashara anathani pesa zake ndo zitampa kila kitu ngoja Ndesa-pesa amchachafye! wanathani watamtoa kirahisi enhe? Kilimanjaro si kama majimbo mengine! Wanaangalia loyalty ya muhusika! sio kwa maslahi binafsi!
 
Huyu Mengi sasa ni mnafiki asitumie siasa kwa maslahi yake ya biashara anathani pesa zake ndo zitampa kila kitu ngoja Ndesa-pesa amchachafye! wanathani watamtoa kirahisi enhe? Kilimanjaro si kama majimbo mengine! Wanaangalia loyalty ya muhusika! sio kwa maslahi binafsi!

Mbona hueleweki Geza!! Ona sentensi yako zako za awali in red "Nathani huu ni muda muafaka kwa wana Chadema kukaa mkao wa kula haswa Mzee Ndesa-pesa na Bw. Mbowe maana hiki ni kisiki cha mpingo kikiamua kugombea Ubunge katika majimbo hayo yaani Moshi Mjini au Hai kinachukua kiulaini.

Ila sidhani kama itakuwa ni wazo zuri kwa demokrasia hapa nchini maana sijui Mzee Ndesa-pesa atamjibu nini huyu Mengi katika kupokonya tonge mdomoni?"

Kifungu hicho unaonesha ni jinsi gani Mzee Mengi alivyo kisiki cha mpingo!!! Few minutes later unabadilika, let's see this in blue:

" Huyu Mengi sasa ni mnafiki asitumie siasa kwa maslahi yake ya biashara anathani pesa zake ndo zitampa kila kitu ngoja Ndesa-pesa amchachafye! wanathani watamtoa kirahisi enhe? Kilimanjaro si kama majimbo mengine! Wanaangalia loyalty ya muhusika! sio kwa maslahi binafsi"

Where du stand Geza?!! For me, kama ni kweli amehamishia uanachama K'njaro basi ni dalili ya kutojiamini kv mpiganaji anayejiamini can fire from any angle!! c unakumbuka Lyatonga yuleeeeee, wa miaka ya 90?!

Alipokuja TMK kugombea kila m2 akashangaa, hata nami nikajiuliza Mrema na TMK wapi na wapi!!! few years later huyoooo, kwao, akaua vilevile!!! Isitoshe, sizani kama analenga ubunge, labda preparation ya 2015, lakini c atakuwa babu sana!!!!
 
Huyu Mengi ni mtu hatari sana na anatakiwa kuangaliwa na kumuelewa janja yake. sidhani kama ananyemelea jimbo huko Moshi bali ukifuatilia nyendo zake utaona kama anajiimarisha kitaifa. Hivyo tusimshangae mkisikia anaibuka na kutaka kugombea urais.

Kumbuka kuwa aliwahi kumtumia sana Mchungaji Mtikila ila ipitishwe hoja ya mgombea binafsi na walishinda kesi mahakama kuu lakini mtandao uliwang'amua na kuikatalia hoja hiyo. Angalia jinsi anavyoliyumbisha bunge huku akijiweka chiiiiniiii, ha mzee mjanja sana huyu
 
Kunatesi kwamba R. mengi anakusudia kumpindua ubunge nDESAMBURO ktk ubunge 2010 kwa hivyo Chadema kupoteza ubunge Jimbo hilo.Kwa inavyoonyesha ni sawa na Kusukuma Mlevi tu, yaani Ndesamburo kuangushwa na mengi

1.Rekebisha heading ya bandiko, ni Ndesamburo, not Lisamburo.

2.Nina mashaka na ukweli wa habari hii, maana huyu Mengi alishakataa kujiingiza huko toka mapema.
3.That could be a stomach blow...Msitupe pressure kabla ya wakati bana!...
 
Mengi ashakataa kujiingiza katika siasa, na mpaka juzi hivi alirudia tena kauli hizo wakati akimjibu Sofia. Please mods get rid of this!
 
Aingie RASMI kwenye SIASA kuliko anavyofanya sasa. Tunamhitaji Berlusconi wetu hapa.
 
I wish I could one day understand this old man.
Sasa kama hajihusishi na siasa, mbona anahamishia Tawi huko k'njaro?
come on Mengi speak up! Tulishazoea hotuba zako. wewe si umeamua kuwa unatuhutubia ITV tunakusikiliza. Kwanza nashangaa nani alikuruhusu uwe unahutubia wananchi?
 
Huyu Mengi sasa ni mnafiki asitumie siasa kwa maslahi yake ya biashara anathani pesa zake ndo zitampa kila kitu ngoja Ndesa-pesa amchachafye! wanathani watamtoa kirahisi enhe? Kilimanjaro si kama majimbo mengine! Wanaangalia loyalty ya muhusika! sio kwa maslahi binafsi!

Huyu Mengi ni mtu hatari sana na anatakiwa kuangaliwa na kumuelewa janja yake. sidhani kama ananyemelea jimbo huko Moshi bali ukifuatilia nyendo zake utaona kama anajiimarisha kitaifa. Hivyo tusimshangae mkisikia anaibuka na kutaka kugombea urais. Kumbuka kuwa aliwahi kumtumia sana Mchungaji Mtikila ila ipitishwe hoja ya mgombea binafsi na walishinda kesi mahakama kuu lakini mtandao uliwa ng'amua na kuikatalia hoja hiyo. Angalia jinsi anavyoliyumbisha bunge huku akijiweka chiiiiniiii, ha mzee mjanja sana huyu


Simtetei Mengi, ila kabla hamjamshambulia kwa kejeli na kashfa ni vema mkatumia hoja zenye mshiko kutushawishi.

Ni wapi Mengi katamka kuwa anautaka urais? Ni wapi na lini kasema anagombea ubunge?

Ndugu Jimmy, Mengi si mbunge, tafadhali tueleze ni jinsi gani analiyumbisha bunge ilhali si mbunge?
 
Ndugu Jimmy, Mengi si mbunge, tafadhali tueleze ni jinsi gani analiyumbisha bunge ilhali si mbunge?

Naona kama umeuliza majibu??? Sijui kama uko TZ hapa?? Mengi, Mb. Likokola,VICOBA, Ilani ya CCM wanavyozunguka nayo!!!
 
I wish I could one day understand this old man.
Sasa kama hajihusishi na siasa, mbona anahamishia Tawi huko k'njaro?
come on Mengi speak up! Tulishazoea hotuba zako. wewe si umeamua kuwa unatuhutubia ITV tunakusikiliza. Kwanza nashangaa nani alikuruhusu uwe unahutubia wananchi?

wewe sasa umeamua kutuchekesha, alitakiwa kuomba ruhusa???????? je wewe nani kakurusu kusikiliza hotuba zake????
 
Back
Top Bottom