Mdee naye amkana Zitto na Urais...

Kwamba kama zitto ana uwezo mkubwa hilo halina mjadala......Ila jinsi magazeti yalivyoaandika katika mtazamo wa kuleta mtafaruku kuelekea 2015 ni tatizo

Hao wabunge niliwaweka katika kundi la waliofilisika kisiasa.....bora kama kuna waliokana.Ni wakati wa umoja ndani ya chama kuelekea 2015.

Jana Niliandika

Kama hao wabunge wamemu-endorse kwa sababu ya ujana na ushkaji tu basi 'WAMEFILISIKA KIMAWZAZO/KISIASA'
Wabunge vijana wa aina hiyo ni janga na ni embarrasement kwa vijana wote.Vijana ni jobless,hawana clear future na wanasiasa wanataka kuwatumia kumaliza game zao.Ipo siku tutaamua hatima yetu kwa mtu wa bunduki badala ya sanduku la kura katika mazingira yenye hila za mafisadi na usalama wa Taifa uliokosa intergrity.Sijutii/sitajutia kauli hii.....

We donn't give a damn wheather the president is young or Old.what we need is maturity and guts to step on thug's toes...

Maswala ya kutumia vijana kama mtaji hayatakubalika.Tunachohitaji ni focus kama chama cha Siasa kwa jinsi gani tuiondoe CCM madarakani 2015 kwa umoja wetu.

What's so special?hao waliomu-endorse wamefanya nini hadi iwe issue?

This is where we make mistakes, a young man ruling doesnt imply a change, come to think of it a great population of our young men are into fraudulent activities., what Tanzania need is a man with vision. Either young or old. We need someone that will spark up some changes via critical decisions. There is just a botton of ingenuity that needs to be pushed in this country.

The average Tanzania youth has over the past 2 decades been pushed down and stripped of all forms of responsibility that they have started thinking, acting and communicating as children. If we don't get our act right and take control of our future; our destiny, which is our country, we'll soon be further demoted to the level of toddlers.

All Tanzania need is a good man who is not afraid to step on toes and of course with a clear focus.

Talking about a young man ruling this country, well, i think that might just be me, hahaha

Mkuu nilihifadhi andiko lako la jana, hakika uliliona kwa macho ya tatu, watu makini wametuonyesha udhaifu wa wale tunaowategemea upo wapi!

Najaribu kushawishika na moja ya andiko la mdau mmoja kuwa baadhi ya wanahabari hupewa fedha na kushurutishwa waandike kwenye magazeti yao kile wanasiasa wetu wakitakacho, na zaidi ikadaiwa kuwa mwanasiasa huiandika yeye mwenyewe habari ka moja kwa moja gazetini na kushawishi itolewe!

Sasa mpaka hapa picha sio la kihidi tena lisiloisha bali ni la kizungu na steringi kesha uawa!
 
ITS BETTER WAGOMBEA WAANZE LEO KUJITANGAZA TUWACHANE VYEMA. Tunahitaji kiongozi wa kuendeleza nchi sio chama.
 
ndio sababu imenifanya kwa mwaka wa pili sasa kutosoma gazeti lolote la tanzania, errors
 
ccm haiwezi kufa peke yake maana ni chama kikongwe,itaenda pamoja na baadhi ya walio nje ya ccm,mashirika ya umma na ya binafsi.Kifo cha mtu mzima kina mshindo mkuu.Hata Yesu si aliuwawa pamoja na wengine wawili (wakristo wanajua)? Labda Zito na Mwananchi wataisindikiza ccm kaburini hatuwezi jua,Tutajua mda sii mda maana dalili ya mvua ni mawingu.
 
Zitto anajua maana ya Camaign ni Come Pain!
Ili 'Come' na sasa ina 'Pain'..
Sipendi aina yake ya siasa anayoifanya kiukweli.
 
Kuomba samahani ni ukomavu jamani Mwananchi, Tido Mhando unajishushia hadhi hivi hivi.
 
Basi hilo gazeti linajipotezea heshima yake!...Nakala ya leo wanamwomba msamaha Membe!...makosa makosa makosa!

namsubili na Filikunjombe.......ila waliyasema haya maneno, sema Mhariri kaweka "header ambayo hawaitaki". Tuangalie chanzo
 
Siamini gazeti ninaloliaminia kwa habari za ukweli kabisa leo hii ninaanza kupotea njia....



Waandishi wa gazeti hili mchwara walibeba tuzo zote za wanahabari nikashangaa sana. lakini sasa nimejua hili gazeti liko kifisadi zaidi

 
Zitto anajua maana ya Camaign ni Come Pain!
Ili 'Come' na sasa ina 'Pain'..
Sipendi aina yake ya siasa anayoifanya kiukweli.

Subiri usikie upande wa pili wa Zitto......acha vurugu na wewe! Naamini Zitto hatakaa kimya kwani akikaa kimya na wengine wamekana itaaminika yeye.....
 
Kimbunga,

kuongelea urais 2015 hakuna tatizo.Na nimekuwa nikipinga watu kusema hakuna vijana wenye uwezo wa kuwa Rais.Pia nimepinga mara nyingi matumizi ya hoja ya ujana tu. CHADEMA kuchukua dola 2015 tunahitaji aggressive movement.Hakuna aggressive movement bila umoja.Let us convince the mass.we should now refrain from confuse the mass.Falsafa ya if you cant convince them confuse them inaweza kutumika intentionally au accidentally lakini ikaleta damage kubwa
Tumekusikia msemaji wa Zitto, kwani nani anauvunja umoja?
 
Du kmbe hili ni gazeti la udaku, nilikuwa napenda sana kulinunua, sasa basii, kumbe wanaweza kuwa maajent wa magamba, poleni sana. Ila ombeni msamaha mkiri kabisa kuwa mmekosa na hamtarudia tena, imani yetu itarudi.
 
Halima Mdee ninayemjua asingeweza kutamka upumbavu kama ulivyoandikwa na Mwananchi.Big Up Mdee kuumbua wanafiki.
 
Unajua kwa nini nampenda Dr. W. Slaa????? Ni kwa sababu amemaliza ujana....alafu kuna muda huyu mzeee anaweza ku"foka".Pia inaonyesha haingii ikulu kwa ajili ya kulipizana visasi.Kitu kingine inaonyesha anaweza kuongeza straight...na ana busara.

Ila hawa wengine...Mwandosya,Sitta,Mwakyembe,Lowasa,Membe,January,Zitto...Nk, wao wataingia ikulu...na kuanza kufanya ujana (kwa vijana) na kulipizana visasi na kusahau matatizo ya watanzania. Wakati sisi kuanzia 2015....hatutakuwa na muda wa kuangalia visasi.

Mtazamo wa uongozi ulio na yote haya ni wa Dhaifu. Mwendo ni ujana na Visasi kwa miaka kumi. Mkirudia haya, tutasaga meno.

Na pia zito asisahau kua, yuko hapo leo kwa sababu ya CDM na wala sio CDM iko hapo kwa sababu yake.
 
Nassari na Mdee wakiletewa mkanda unao onyesha wakiyatamka hayo wanayoyakana watakubali?

Weka huwo mkanda tutajua nani mkweli nani muongo,. Gazeti ama hawo waliyokanusha, jiulize ni kwanini wamekanusha? kama ni kweli wamefanya hivyo.....
 
Siamini ila nasikia zitto kamwaga mzigo wa maana aliopewa na ccm na mafisadi kwa ajili ya kuvuruga cdm....kwa hiyo mimi sishangai habari hizi kwani nilikuwa najua tangu awali........
Zitto kijana hatari sn 30%cdm na 70%ccm.....watch out
 
Kwenye barua yake kwenda kwa uongozi wa juu wa gazeti la mwananchi, hii ni sehemu ya barua yake.

Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wanachama wa chama changu, CHADEMA, ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote. Napenda kuwa mmoja wa Watanzania makini na viongozi wanaojua wajibu, ikiwemo kufanya nini na kusema nini, mahali gani na wakati gani.

*

Nimependezwa na kauli hii kwani CHADEMA inaongozwa kwa Katiba na Kanuni ambazo wanachama wake wanapaswa kuzifuata... Hongera Mh. Mdee kwa kufunguka kama alivyofanya Dogo Janja (Nassari) cha msingi kufahamu haya magazeti yametumwa na yanatumiwa na MAFISADI kuwachafua wapigangaji wa CHADEMA.
 
Kwenye barua yake kwenda kwa uongozi wa juu wa gazeti la mwananchi, hii ni sehemu ya barua yake.



Nasikitika kutumia nafasi hii kukuandikia kukutaarifu kuwa gazeti lako la Mwananchi la Julai 23, 2012, katika habari yake iliyoongoza ukurasa wa kwanza (lead story) limenilisha maneno na kunikuu isivyo sahihi.



Katika habari hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho “Wabunge wamsafishia Zitto njia ya urais 2015,” gazeti lako limeandika hivi “Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.”



Gazeti lako pia katika aya iliyofuata limenukuu kuwa mimi nimesema;

*“Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee”



Nasikitika kusema kuwa gazeti lako limeandika habari zisizo za kweli kwa kunilisha *maneno na kudai kuwa mimi ndiye nimesema maneno hayo, kisha kuyaweka kwenye nukuu, likisema kuwa ni nukuu yangu. Sijajua nia au kusudio la gazeti lako kuamua kupotosha ukweli na kushindwa kabisa kuninukuu kwa usahihi, kama inavyotakiwa katika misingi ya taaluma ya habari.



Nasikitika pia kusema kuwa gazeti lako ambalo limeonekana kujijengea heshima miongoni mwa wasomaji wa kada mbalimbali nchini na hivyo linapaswa kuwa mfano wa kuigwa, linaweza kusigina misingi ya uandishi wa habari na hususan katika kufuata maadili ya taaluma hii muhimu, kwa kiwango cha kufanya moja ya dhambi kubwa ya kukilisha maneno chanzo cha habari.



Kwa ajili ya kutunza heshima ya gazeti lako, lakini pia kwa ajili ya maslahi mapana ya taaluma ya habari na jamii ya Watanzania, nakuandikia kulitaka gazeti lako likanushe maneno liliyoninukuu katika toleo hilo la Julai 23, 2012. Ni vyema sana hilo likafanyika kwa uzito unaostahili kama ilivyoandikwa katika toleo hilo.



Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wanachama wa chama changu, CHADEMA, ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote. Napenda kuwa mmoja wa Watanzania makini na viongozi wanaojua wajibu, ikiwemo kufanya nini na kusema nini, mahali gani na wakati gani.



Nakutakia utekelezaji mwema katika hilo.

*



Kama hata mwananchi wako hivi sasa hli ni mbaya kwa vyombo vyetu vya habari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom