Mdee naye amkana Zitto na Urais...

Hongera Mdee huu si wakati wa kutibua Chama kwa migawanyiko ya makundi ya Urais wazi wazi. Acha CCM waweweseke!
 
Mwananchi wamechemka sana
Wahariri wa magazeti mengi wanaweza kujaribiwa kuongeza chumvi au hata kuandika mambo kinyume na ukweli ili kuongeza mauzo ya gazeti (wote huwa, ktk nyakati tofauti, wanachemka). Tutaendelea kuwashauri kutanguliza maslahi ya taifa katika kazi zao za kuhabarisha wenye nchi (wananchi). Lazima waombe radhi kwa uzito ule ule!
 
Nadhani kila mtu angependa kuhukumiwa kwa kauli na matendo yake.
Kuongelea Urais sio tatizo, tatizo ni pale chombo cha habari kinachoaminika kama Mwananchi kinapoleta habari zinazoonekana ni za kutunga.

Mwananchi ina dhima ya kuthibitisha au kukanusha kuhusu habari za Wabunge hao.
Hakika jambo hili limeleta sintofahamu kubwa katika jamii hata kama ni sehemu tu ya jamii.

Tido Mhando, tunapokuwa na chombo cha habari kilichomzulia Membe maneno na sasa kusemekana kuwawekea maneno wabunge ni jambo la hatari sana. Sina hofu na gazeti hilo kupoteza umaarufu, hofu yangu ni kuliona likitumika vibaya.
Tunajua nguvu ya media na madhara yatokanayo kama yale ya Rwanda, na hapo ndipo ninaona mwananchi linajaribu kutupeleka.

Ingawa ni suala binafsi nina hakika Chadema wana mkanda mzima wa kilichozungumzwa. Hili kulikalia kimya kwa kuogopa ogomvi na media ni hatari kubwa sana. Huko twendako Mwananchi litakuja na habari hatari zaidi.
Ningeshauri Chadema kama chama wawasiliane na wabunge wao na watoe kauli kwa umma juu ya hili kwa njia za kistaarabu tu.
 
Kimbunga,

kuongelea urais 2015 hakuna tatizo.Na nimekuwa nikipinga watu kusema hakuna vijana wenye uwezo wa kuwa Rais.Pia nimepinga mara nyingi matumizi ya hoja ya ujana tu. CHADEMA kuchukua dola 2015 tunahitaji aggressive movement.Hakuna aggressive movement bila umoja.Let us convince the mass.we should now refrain from confuse the mass.Falsafa ya if you cant convince them confuse them inaweza kutumika intentionally au accidentally lakini ikaleta damage kubwa

hivi we muhanga wa BAVICHA bado upo tu? Kila siku nakwambia kuwa siasa zako hizo za kucope na kupaste kwa wakina malema ipo siku zitakuzima kwani ukiona tu Zitto basi moyo wako ulia yoriyori kwani we na Zitto lenu 1 tu la kuunda makundi na kutumia ticket ya ujana kulaghai mass that y hata kamati kuu ya CDM iliwashtukia ikawaondoa kwenye uchaguzi wa BAVICHA, hapo past nilikukubali sana kwa hoja zako ila sasa huna tena jipya na sijui ule mpango wako wa kuhamia CHAUMA umeishia wapi.

We ni another disaster ndani ya CDM.
 
Kama Mdee hakuyasema hayo maneno basi shida ipo, kwa nini gazeti lijitungie habari, au un ataka kutueleza nini, mimi sikuelewi kabisa. nani alikwambia she believes zitti anaweza?

Waulizeni hao wanahabari wa Mwananchi, kuna habari zinazoongelewa kila mara kuwa Zitto huandika habari zinazmhusu yeye mwenyewe, na kisha kuzipelekeka kwenye vyombo vya habari ambavyo vina wapambe wake. Kwa hiyo sishangai kama hata huyo aliyeandikwa kama mwandishi wa hiyo habari akawa hajui kama yaliyoandikwa kwa jina lake kweli yalisemwa au hayakusemwa. Mtu ambaye anastahili kutoa jibu ni Zitto. Tido Mhando lazima afanye kazi ya ziada kuwaondoa waandishi wanaotumiwa na wanaharakati wa mbio za Urais. Kama habari hizi za kuwa Zitto hujiandikia habari zake mwenyewe na kisha kuwahonga waandishi wa habari ili wazitoe kama zilivyo ni za kweli, basi itabidi tujiulize mara mia, 'huyu anayewahonga waandishi wa habari, akiupata huo uongozi anaoutafuta kwa mbinu zote, nzuri na chafu, atafanya nini? Huyu atakuwa kweli ni mpiga vita rushwa? Kwa sasa atahonga vyombo vya habari lakini akiupata uongozi nadhani atavilazimisha.
 
Halafu ile kukusanya wasanii wa kigoma (Ukabila) eruption yake ndo hii! yani zitto huu ndo ulikuwa mpango?? kuutengeneza ukabila kisha kuuwaalika wabunge wenzio waudhibitishe katika magazeti uliyokuwa ameyapanga ukisaidiwa na ikulu! Kumbuka we zitto, JK alitumia sana magazeti ili aingie ikulu! leo yuko wapi??? aibu tupu! hata kama kajilimbikizia mimali ya kutosha wapi heshima yake ilipo kama si rais aliyeshindwa kulionhgoza taifa kwa kuendekea wizi na visasi kwa wakosowaji wake! sasa na wewe zitto ndo unataka kutumia njia hiyo hiyo kuutaka urais??? vyombo vya habari??haya tutaona.
 
zitto ana urafiki wa karibu sana na mhariri wa mwananchi DENIS MSAKI, na mara nyingi wameripotiwa na interijensia ya cdm wakikutana sinza ktk pub ya msaki iliyopo jirani na wanyama hotel.
 
Sishangai inaonekana hiyo ndo style ya Viongozi wengi wa Chadema kunakili (Copy and Paste) tokea walivyokuwa Chuoni kwa wale waliobahatika kukanyaga

Mkuu, yaonekana umekwenda shule na wewe pia.
Kwani kuna ubaya gani wa ku-copy and paste?
Elimu zote ndivyo zilivyo. Ukim-quote mtu lazima uandike kama alivyosema, Uki-state law au principle lazima usiache hata neno usije kupindisha maana.
Sasa sijui ni elimu gani unayoizungumzia wewe?
 
Tuacheni propaganda, tuongee real issues.Matatizo yakujadili watu badala ya issues ndo haya sasa.Mwenzako alieibuka kama MIC ya Nasari kafuata flow kama yako.Sisi wanasayansi tynaweza ku-draw a simple conclusion, MMETUMWA NA MTU MMOJA.Sasa sijui mnajuana na mwenzako,angalieni hata posho inawezekana tofauti,wakati dhambi ni sawa!!!

Hembu scan hiyo barua ya mdee na umwambie mwenzako afanye hivo kwa hio ya Nasari.ACHENI PROPOGANDA,cdm mambo sio shwari. Young bloods are tired of policing, chama cha Mbowe na Slaa-madogo wameshastukia
CCM poor perfomers lkn sio cha ukoo, kina sura ya kitaifa.Rais ajae KKKT,mpende msipende MMASAI
 
ndugu wananch nyie c ndo mlikuwa mnamshangilia TIDO? leo viko wapi jamani? Mnamuona mbaya kisa zitto? Go go zito our next president
 
Huu ni mjezo mchafu wa ZITTO KABWE mwenyewe asitupotezee muda inaonekąna kama kamuhonga mwansdishi wa habari naye muhariri kaitoa kama ilivyo, katika mwendo huu wa ukombozi Zitto atakuwa ni tatizo anatamaa sana sa na uongozi.
 
Damage imeshafanyika tayari. MWANANCHI wataomba radhi lakini habari ya Zitto itakumbukwa zaidi ya ile ya kuomba radhi. Kuna haja sasa Zitto mwenyewe ajitokeze na akiri kwamba walichoandika Mwananchi sio walichosema Nassari na Mdee.

Zitto
akiendelea kukaa kimya, tutahisi yeye ndiye anaye-engineer hii kitu

Nafikiri kuna thread iliyoanzishwa na Zitto mwenyewe akizungumzia habari hiyo. Endelea ku-browse utaipata. Lakini hata hivyo tunahitaji unedited video tujionee sisi wenyewe siku hiyo. Kuna mtu hapa ataumbuka tu.
 
Zitto ana video amesema ataibandika kwenye blog yake.Anasema walichoandika mwananchi ni kweli.So video ndo mwamuzi wa mwisho kwenye kuukata huu mzizi wa fitna.
 
Back
Top Bottom