Mdee naye amkana Zitto na Urais...

Basi hilo gazeti linajipotezea heshima yake!...Nakala ya leo wanamwomba msamaha Membe!...makosa makosa makosa!
Sijui Mwananchi wanakusudia kufanya nini kupitia habari zao za kutengeneza. Hawana shabaha kama Kova aliyemtumia Gwajima badala ya kuwatumia Uamsho... Badala ya kuwatumia watu kama kina Selasini, John Shibuda, Mhonga Said na Juliana Shonza wao wanamtumia Mdee na Nassari huku wakijua kuwa wale ni madogo janja?
 
Mwananchi gazeti kiboko Salim A. Salim hatalisahau, wakati anagombea Urais na Mwandosya na Kikwete ilipigwa Photoshop yake hakuamini.

Mimi nachosema hukoCDM sasa kutachemka ni kwa nini wanaomuunga mkono Zitto kwenye Urais baada ya siku 3 wanakanusha?

Huu ukanda wa Kaskazini uangalieni sana, una nia ya kutoa Raissasa mwachieni na wengine km kina Zitto kua ubaya gani M-Ha au M-Manyema kutawala? basi hata uenyekiti wa Chama au KUB (Kiongozi wa Upinzani Bungeni)
 
ngurati Hivi hayo maneno yana ubaya gani hadi yakanushwe? Kwani mtu akisema Zitto anafaa kuwa kiongozi wa nchi kuna ubaya gani? Ningekuwa mimi Mdee wala nisingehangaika kukanusha kwa kuwa hakuna neno ovu wala tusi hapo. Lakini kwa kuwa kuuongelea Urais ndani ya CDM hasa ukihusishwa na Zitto ni taboo basi naona akina Mdee wamebanwa mbavu hadi wanakanusha.

Hata kama Mdee hakusema lakini naamini ndani ya moyo wake hayo ndio maoni yake.

Mkuu unatisha kweli. Imani ya wengi ni kuwa anayeweza kuangalia ya moyoni ni Mungu pekee. Loh! katika hili umejipa uwezo mkubwa kupitiliza. Ikiwa kweli mwenyewe anayedaiwa kusema hayo maneno amekanusha wewe ni nani uamue kuwa hayo ndiyo maneno yake? Kweli unatisha!

Lakini pia imeandikwa kuwa "Mungu hadhihakiwi kwa kuwa apandacho mtu ndicho atakachovuna". Tusiwe wasahauifu. Zitto alisema kuwa atagombea uraisi si mwaka huu bali 2010 wakati akijinadi kugombea ubunge huko Kigoma "kwa mara ya mwisho". Kuwa safari nyingine atakuja kama mgombea uraisi yaani 2015.

Ikumbukwe kuwa wakati huo mgombea wa CHADEMA alikuwa Dr. Slaa. Hii maana yake nini? Yeye alijua kuwa Dr. Slaa hatashinda. Lakini kosa alilolifanya ambalo linaonyesha kuwa hajakomaa kisiasa ni kupanda mbegu kwa kutokumuunga mkono mgombea wa chama chake. Huwezi wewe kutaka kuungwa mkono ili hali wewe huwezi kuwaunga wenzio. Huko ni kupanda mbegu mbaya na msimu wa mavuno umeanza.

Huyu Bwana pia amekuwa akisifiwa sana kuwa ni mtendaji mzuri - sijui ni kwa utendaji upi uliotukuka? Lakini kama hawezi kujenga umoja, kila kitu na kila siku yeye ni ubinafsi tu na kujifagilia yeye ujue kuwa hafiki mbali. Unapojiona kuwa wewe tu ndiye unayefaa, ujue una kasoro kubwa sana.

Tuliwahi kutahadharishwa kuwa ukiona mtu anakimbilia sana ikulu muepuke kama ukoma, tukapuuza. Maonyo hayo hatukuzingatia kama taifa na kwa miaka kumi tunakiona cha moto.

Kama ni zigo, bazi Zitto ni zigo zito, libebeni mnaotaka kufanya hivyo.
 
Ben hapa umesukumwa umesukumwa na upofu wa kufikiri
. Zitto anaweza kuwa na uwezo mkubwa kwenye mambo mengine lakini sio urais

wewe ndiyo uliyesukumwa na upofu wa kufikiri.nisome kwa makini na kunielewa.....
 
Mkuu unatisha kweli. Imani ya wengi ni kuwa anayeweza kuangalia ya moyoni ni Mungu pekee. Loh! katika hili umejipa uwezo mkubwa kupitiliza. Ikiwa kweli mwenyewe anayedaiwa kusema hayo maneno amekanusha wewe ni nani uamue kuwa hayo ndiyo maneno yake? Kweli unatisha!
Lakini pia imeandikwa kuwa "Mungu hadhihakiwi kwa kuwa apandacho mtu ndicho atakachovuna". Tusiwe wasahauifu. Zitto alisema kuwa atagombea uraisi si mwaka huu bali 2010 wakati akijinadi kugombea ubunge huko Kigoma "kwa mara ya mwisho". Kuwa safari nyingine atakuja kama mgombea uraisi yaani 2015. Ikumbukwe kuwa wakati huo mgombea wa CHADEMA alikuwa Dr. Slaa. Hii maana yake nini? Yeye alijua kuwa Dr. Slaa hatashinda. Lakini kosa alilolifanya ambalo linaonyesha kuwa hajakomaa kisiasa ni kupanda mbegu kwa kutokumuunga mkono mgombea wa chama chake. Huwezi wewe kutaka kuungwa mkono ili hali wewe huwezi kuwaunga wenzio. Huko ni kupanda mbegu mbaya na msimu wa mavuno umeanza.
Huyu Bwana pia amekuwa akisifiwa sana kuwa ni mtendaji mzuri - sijui ni kwa utendaji upi uliotukuka? Lakini kama hawezi kujenga umoja, kila kitu na kila siku yeye ni ubinafsi tu na kujifagilia yeye ujue kuwa hafiki mbali. Unapojiona kuwa wewe tu ndiye unayefaa, ujue una kasoro kubwa sana. Tuliwahi kutahadharishwa kuwa ukiona mtu anakimbilia sana ikulu muepuke kama ukoma, tukapuuza. Maonyo hayo hatukuzingatia kama taifa na kwa miaka kumi tunakiona cha moto.
Kama ni zigo, bazi Zitto ni zigo zito, libebeni mnaotaka kufanya hivyo.

Mkuu una maana Zitto hakumuunga mkono Dr. Slaa?
 
Zitto, endelea na majukumu yako ya kitaifa na wala usihangaike kusema neno ktk thread hii. We know and every decent Tzanian knows kuwa You can lead this nation...yaani ni kwamba una UWEZO.

Simply you can do, yes you can! Sis Halima usiogope kusema kilicho wazi... ni vema pia sisi vijana hasa tuliofika darasani...tukawa na uzalendo wa kusema kweli ili tuwafahamishe umma kilicho bora.

Tuwe na mioyo hiyo... ili tulipeleke taifa hii mbele ktk maendeleo. Let do justice to ourselves by speaking out whole truth.
 
Mimi nawashangaa sana hawa Nasari na Mndee, mbona wao hawatuelezi walisema nini pale jukwaani isipokuwa madai tu kwamba gazeti limepotosha... Mimi nataka kujua wao wanadai walisema nini ktk tamasha lile tofauti na gazeti hili maana najua kabisa hili ni kundi la vijana wanaoamini mageuzi ya nchi hii yataletwa na vijana na wapo pamoja na Zitto...

Sasa swala limekuwa la chama na kujenga uzito kwao wanamkimbia Zitto wakati binafsi sioni ubaya wowote isipokuwa dhana ya ujana tu..Ile sifa ya Ujana kuwa sababu, kila mmoja wao anaikimbia sasa..
 
Kwenye barua yake kwenda kwa uongozi wa juu wa gazeti la mwananchi, hii ni sehemu ya barua yake.

Nasikitika kutumia nafasi hii kukuandikia kukutaarifu kuwa gazeti lako la Mwananchi la Julai 23, 2012, katika habari yake iliyoongoza ukurasa wa kwanza (lead story) limenilisha maneno na kunikuu isivyo sahihi.

Katika habari hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho “Wabunge wamsafishia Zitto njia ya urais 2015,” gazeti lako limeandika hivi “Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.”

Gazeti lako pia katika aya iliyofuata limenukuu kuwa mimi nimesema;

“Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee”

Nasikitika kusema kuwa gazeti lako limeandika habari zisizo za kweli kwa kunilisha maneno na kudai kuwa mimi ndiye nimesema maneno hayo, kisha kuyaweka kwenye nukuu, likisema kuwa ni nukuu yangu. Sijajua nia au kusudio la gazeti lako kuamua kupotosha ukweli na kushindwa kabisa kuninukuu kwa usahihi, kama inavyotakiwa katika misingi ya taaluma ya habari.

Nasikitika pia kusema kuwa gazeti lako ambalo limeonekana kujijengea heshima miongoni mwa wasomaji wa kada mbalimbali nchini na hivyo linapaswa kuwa mfano wa kuigwa, linaweza kusigina misingi ya uandishi wa habari na hususan katika kufuata maadili ya taaluma hii muhimu, kwa kiwango cha kufanya moja ya dhambi kubwa ya kukilisha maneno chanzo cha habari.

Kwa ajili ya kutunza heshima ya gazeti lako, lakini pia kwa ajili ya maslahi mapana ya taaluma ya habari na jamii ya Watanzania, nakuandikia kulitaka gazeti lako likanushe maneno liliyoninukuu katika toleo hilo la Julai 23, 2012. Ni vyema sana hilo likafanyika kwa uzito unaostahili kama ilivyoandikwa katika toleo hilo.

Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wanachama wa chama changu, CHADEMA, ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote. Napenda kuwa mmoja wa Watanzania makini na viongozi wanaojua wajibu, ikiwemo kufanya nini na kusema nini, mahali gani na wakati gani.

Nakutakia utekelezaji mwema katika hilo.
Nimepapenda sana hapo kwenye red
 
Bora amkane hebu ona uhusiano wa Zitto na Jack Zoka, tuwe macho na uhusiano wao

Uhusiano kati ya Zitto na Jack Zoka ambao uliwekwa wazi na vyombo mbalimbali ni taarifa mbaya kwa wanasiasa na wananchi wanaoipenda taifa lao la Tanzania. Uhusiano huu wa Zitto na Jack Zoka ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa TISS (usalama wa taifa) umeripitiwa kuwa na historia ndefu tangu wakati wa uchaguzi mkuu.

Wakati Zitto anajitapa kuwa anatetea maslahi ya wananchi, mshirika wake wa chanda na pete Jack Zoka anatuhumiwa na wanasiasa na wanachi kufanya kazi ya kuwadhuru badala ya kulilinda taifa. Kama mshirika wa Zitto anadhuru wananchi ni wazi kuwa naye Zitto ana masalahi binafsi na mabaya kwa wananchi.

Maana ukitaka kujua tabia ya mtu, uliza tabia ya rafiki yake. Ni jambo la kusikitisha Zitto kuwa na uhusiano na huyu mfanyakazi wa usalama wa taifa anayedhuru watu na wakati huohuo anajidai kuwa ni mpambanaji.

Uhusiano wa Zitto na Jack Zoka ulishawekwa wazi kuwa walikuwa wanawasiliana kwa simu mara kwa mara wakati wa kipindi cha uchaguzi. Tuwe macho na urafiki wao na ambao si mwema hata kidogo kwa wanasiana na wananchi wenye uchungu na taifa letu.
 
Hizi taasisi za habari may be zinatumika na watu kwa nia ovu? mi sikutegemea kwa gazeti kama mwananchi ktoa hbr ya kizushi vile! Duh! kweli kila kitu ni kigeugeu
 
ngurati Hivi hayo maneno yana ubaya gani hadi yakanushwe? Kwani mtu akisema Zitto anafaa kuwa kiongozi wa nchi kuna ubaya gani? Ningekuwa mimi Mdee wala nisingehangaika kukanusha kwa kuwa hakuna neno ovu wala tusi hapo. Lakini kwa kuwa kuuongelea Urais ndani ya CDM hasa ukihusishwa na Zitto ni taboo basi naona akina Mdee wamebanwa mbavu hadi wanakanusha.

Hata kama Mdee hakusema lakini naamini ndani ya moyo wake hayo ndio maoni yake.
Kwa CCM maneno hayo hayana madhara, lakini kwa CDM yako nje ya utaratibu, kumbuka kile ni chama makini.
 
Kwa CCM maneno hayo hayana madhara, lakini kwa CDM yako nje ya utaratibu, kumbuka kile ni chama makini.

Umakini si kufinyanga demokrasia ya maoni. Yaani kuongelea Urais imekuwa ni kukosa umakini. Zitto anasema chama bado hakina mgombea lakini kuna watu ndani ya chama na washabiki tayari wana mgombea wao kwapani! Hapo ndipo penye shida
 
Bora amkane hebu ona uhusiano wa Zitto na Jack Zoka, tuwe macho na uhusiano wao

Uhusiano kati ya Zitto na Jack Zoka ambao uliwekwa wazi na vyombo mbalimbali ni taarifa mbaya kwa wanasiasa na wananchi wanaoipenda taifa lao la Tanzania. Uhusiano huu wa Zitto na Jack Zoka ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa TISS (usalama wa taifa) umeripitiwa kuwa na historia ndefu tangu wakati wa uchaguzi mkuu.

Wakati Zitto anajitapa kuwa anatetea maslahi ya wananchi, mshirika wake wa chanda na pete Jack Zoka anatuhumiwa na wanasiasa na wanachi kufanya kazi ya kuwadhuru badala ya kulilinda taifa. Kama mshirika wa Zitto anadhuru wananchi ni wazi kuwa naye Zitto ana masalahi binafsi na mabaya kwa wananchi.

Maana ukitaka kujua tabia ya mtu, uliza tabia ya rafiki yake. Ni jambo la kusikitisha Zitto kuwa na uhusiano na huyu mfanyakazi wa usalama wa taifa anayedhuru watu na wakati huohuo anajidai kuwa ni mpambanaji.

Uhusiano wa Zitto na Jack Zoka ulishawekwa wazi kuwa walikuwa wanawasiliana kwa simu mara kwa mara wakati wa kipindi cha uchaguzi. Tuwe macho na urafiki wao na ambao si mwema hata kidogo kwa wanasiana na wananchi wenye uchungu na taifa letu.

Hapo pekundu, ahaa! ndiyo maana Stella Vitunguu alisema Chadema ndio waliomtesa Dr. Ulimboka. Naona sasa mahusiano ya Zoka na Zitto kumbe! Dunia ya ajabu!
 
Ramadhani Semtawa anajua kufanya kazi za Zitto Kabwe....
Niliisoma hiyo habari, kwa kiasi fulani naliuona mkono wa Zitto katika kuiandika.
Naujua vizuri sana uandishi wa Zitto, alichofanya Semtawa ni kuisukuma kama ilivyo!
Shame on you!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom