Mdee naye amkana Zitto na Urais...

ngurati

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
221
240
Kwenye barua yake kwenda kwa uongozi wa juu wa gazeti la mwananchi, hii ni sehemu ya barua yake.

Nasikitika kutumia nafasi hii kukuandikia kukutaarifu kuwa gazeti lako la Mwananchi la Julai 23, 2012, katika habari yake iliyoongoza ukurasa wa kwanza (lead story) limenilisha maneno na kunikuu isivyo sahihi.

Katika habari hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho “Wabunge wamsafishia Zitto njia ya urais 2015,” gazeti lako limeandika hivi “Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.”

Gazeti lako pia katika aya iliyofuata limenukuu kuwa mimi nimesema;

“Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee”

Nasikitika kusema kuwa gazeti lako limeandika habari zisizo za kweli kwa kunilisha maneno na kudai kuwa mimi ndiye nimesema maneno hayo, kisha kuyaweka kwenye nukuu, likisema kuwa ni nukuu yangu. Sijajua nia au kusudio la gazeti lako kuamua kupotosha ukweli na kushindwa kabisa kuninukuu kwa usahihi, kama inavyotakiwa katika misingi ya taaluma ya habari.

Nasikitika pia kusema kuwa gazeti lako ambalo limeonekana kujijengea heshima miongoni mwa wasomaji wa kada mbalimbali nchini na hivyo linapaswa kuwa mfano wa kuigwa, linaweza kusigina misingi ya uandishi wa habari na hususan katika kufuata maadili ya taaluma hii muhimu, kwa kiwango cha kufanya moja ya dhambi kubwa ya kukilisha maneno chanzo cha habari.

Kwa ajili ya kutunza heshima ya gazeti lako, lakini pia kwa ajili ya maslahi mapana ya taaluma ya habari na jamii ya Watanzania, nakuandikia kulitaka gazeti lako likanushe maneno liliyoninukuu katika toleo hilo la Julai 23, 2012. Ni vyema sana hilo likafanyika kwa uzito unaostahili kama ilivyoandikwa katika toleo hilo.

Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wanachama wa chama changu, CHADEMA, ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote. Napenda kuwa mmoja wa Watanzania makini na viongozi wanaojua wajibu, ikiwemo kufanya nini na kusema nini, mahali gani na wakati gani.

Nakutakia utekelezaji mwema katika hilo.
 
Basi hilo gazeti linajipotezea heshima yake!...Nakala ya leo wanamwomba msamaha Membe!...makosa makosa makosa!
 
ukisoma maneno ya mdee na ya nassari yote yanaonekana kuwa sawa.....mwananchi ni watu wa ajabu sana
 
Siamini gazeti ninaloliaminia kwa habari za ukweli kabisa leo hii ninaanza kupotea njia....
 
Nilishangaa kuiona hyo habari katka gazeti la mwananchi tu wakati lile tamasha halikuwa la siri.
Nimeshtuka zaidi kuona habari hyo imeandkwa siku 5 baada ya tamasha.
 
Maigizo ya siasa yanaendelea, tusubiri tuone kilicho nyuma ya pazia....
 
Tido amelipotezea heshima mwananchi, kisa zitto na mipango yao haramu. Bora niwe mdau wa shigongo kwa kuwasoma akina wema na Almasi tu.
 
Mimi sioni shida ya haya maneno..ila hii ni ishara ya watu kutomwamini Zito..kwani hata kama hakuyasema haya maneno and she believe Zito anaweza kunahaja gani ya kuomba gazeti kukanusha.. Nimeanza kujijazia majibu yangu mwenyewe kwa hili..
 
ukisoma maneno ya mdee na ya nassari yote yanaonekana kuwa sawa.....mwananchi ni watu wa ajabu sana

Sishangai inaonekana hiyo ndo style ya Viongozi wengi wa Chadema kunakili (Copy and Paste) tokea walivyokuwa Chuoni kwa wale waliobahatika kukanyaga
 
Mleta hoja hii tittle "Mdee naye amkana Zitto na urais,soma hapa" inahusikaje sasa na habari yenyewe....kwa uelewa wako ukirejea ulichoandika Mdee amemkana Zitto au amelikana gazeti la Mwananchi na habari waliyoitoa,mnapiga kelele Zitto na mbinu chafu-Zitto na mbinu chafu, kumbe nyie ndo mna mambinu machafu,shauri yenu zote hizo ni point za ushindi kwa Wapinzani wenu
 
zitto yeye anaamini mwananchi na raia mwema ndio magazeti pekee yenye habari huru Tanzania,,,kisa yanamwandika kama anavyotaka, kajamaa hakana tofaouti na Lyatonga! KIGOMA ALL STARS OYEEE!!
 
Damage imeshafanyika tayari. MWANANCHI wataomba radhi lakini habari ya Zitto itakumbukwa zaidi ya ile ya kuomba radhi. Kuna haja sasa Zitto mwenyewe ajitokeze na akiri kwamba walichoandika Mwananchi sio walichosema Nassari na Mdee.

Zitto
akiendelea kukaa kimya, tutahisi yeye ndiye anaye-engineer hii kitu
 
Mimi sioni shida ya haya maneno..ila hii ni ishara ya watu kutomwamini Zito..kwani hata kama hakuyasema haya maneno and she believe Zito anaweza kunahaja gani ya kuomba gazeti kukanusha.. Nimeanza kujijazia majibu yangu mwenyewe kwa hili..


Kama Mdee hakuyasema hayo maneno basi shida ipo, kwa nini gazeti lijitungie habari, au un ataka kutueleza nini, mimi sikuelewi kabisa. nani alikwambia she believes zitti anaweza?
 
Hizo ni kazi za afisa habari na wala sio wahusika personaly.kamaujumbe ni mje haiitaji kubadili kitu
 
ngurati Hivi hayo maneno yana ubaya gani hadi yakanushwe? Kwani mtu akisema Zitto anafaa kuwa kiongozi wa nchi kuna ubaya gani? Ningekuwa mimi Mdee wala nisingehangaika kukanusha kwa kuwa hakuna neno ovu wala tusi hapo. Lakini kwa kuwa kuuongelea Urais ndani ya CDM hasa ukihusishwa na Zitto ni taboo basi naona akina Mdee wamebanwa mbavu hadi wanakanusha.

Hata kama Mdee hakusema lakini naamini ndani ya moyo wake hayo ndio maoni yake.
 
Last edited by a moderator:
Siamini gazeti ninaloliaminia kwa habari za ukweli kabisa leo hii ninaanza kupotea njia....
mkuu hili gazeti siku hizi nalisoma kwa kutumia simu. nimeacha kununua nakala ssb ya bei yao. bado ni gazeti makini lkn wafanye marekebisho ktk mambo km hayo. au nalo lipo kwenye payroll ya ile billion moja ya kuiangamiza CDM?:yawn:
:yawn:
 
Damage imeshafanyika tayari. MWANANCHI wataomba radhi lakini habari ya Zitto itakumbukwa zaidi ya ile ya kuomba radhi. Kuna haja sasa Zitto mwenyewe ajitokeze na akiri kwamba walichoandika Mwananchi sio walichosema Nassari na Mdee.

Zitto
akiendelea kukaa kimya, tutahisi yeye ndiye anaye-engineer hii kitu

Halafu you call yourself a "Consultant" Consultant my d**k...uliona wapi statement iliyotolewa kimakosa ikimnukuu mtu X ikakanushwa na mtu Y? wameshakanusha wenyewe sasa wewe unatuletea habari gani hapa,au ilimradi na wewe uingize jina la Zitto kwenye comment yako?
 
Back
Top Bottom