Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.
Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.

Hiyo ni muhimu saana, ila ndugu zetu TANESCO wasitukatie umeme hapa Arusha muda huo. Haksante kwa info nzuri.
 
well mkuu endelea kutu-update.

Mods kama mnaweza kubadilisha heading ili isomeke vema.
 
Mdahalo ndiyo unaanza.

Nitawaletea issues kwa kadri nitakanyoweza, natumia sime so speed yangu itakuwa siyo kali sana.

BNN
 
mjadala umeshaanza.
swali Bunge lilopita lilikuwa na sura moja ya upinzani bunge hili kuna sura mbili, kwanini?
Mbowe anajimbu kwanza then HR
 
Lazima tujiulize kwa nini chadema wameunda kambi bila kuwashirikisha vyama vingine hii sio sawa wako CUF,TLP,UDP na NSSR
Je hii ni ubinafsi wa Mbowe na wenzake?


Ujinga mwingine bwana, kanuni za bunge zimetamka kabisa kuwa chama cha upinzani kitaunda kambi ya upinzani kama kina 12.5% sasa CDM wana hiyo sifa. Lakini ulitegemea kweli CDM wamshirikishe lyatonga ambaye alikuwa anapigia kampeni kikwete? Ukiujua ujinga wako ukatafuta elimu na ukauacha unakuwa si mjinga tena, lakini ukiung'ang'ania unatoka kuwa mjinga na kufikia upumbavu.
 
mbowe anataja kanuni zinazounda upinzani.
anataja kanuni ile ya ili chama kunde kambi lazima kiwe na 12.5%
na anasema chadema walikuwa na sifa hii
 
slaa anafailia kwa umakini kuliko kawaida
mbowe anazungumzia sfa za kisheria za chadema kuunda kambi ya upinzani, wing wa wabunge kuliko vyama vingine
 
Back
Top Bottom