Mdahalo kati ya Freeman Mbowe na Hamad Rashid ITV

Labda utusaidie ni ipi RANGI Halisi ya Chadema?...maana nawe umechukua madai yaliyokuwa yanatumiwa na CCM kuwapaka CUF...ila nyinyi Chadema mkipakwa na rangi waliopakwa CUF "mnaruka"

Wewe ulitaka CUF mwaka huu ZNZ wafanye nini? watu wamefanya kura ya maoni, wewe ulitaka watu wauwane...?
Duh, mkuu wangu lugha inakupiga chenga au ndio makusudi kwa sababu nimewazungumza CUF...Chadema wao siku zote wanalia hawana Udini nakama kweli hawana basi ni jukumu lao wenyewe kutuonyesha hawana Udini kwa sababu najua fika CUF ni chama cha aina gani. CUF ni wabaguzi toka maswala ya kimuungano kuzungumzia zaidi ya Zanzibar na Waislaam kiasi kwamba hata Ufisadi haikuwa kero kwenu.

Napwapongeza tu kwa sababu hamjifichi nyuma ya pazia lolote mkitangaza Udini na Uzanzibar lakini kwa kazi yenu wepesi sana kupachika wengine pia udhaifu wa chama chenu. Nawajua fika mkuu wangu kazi yenu kubwa ni kutafuta kuitumia dini na Uzanzibar ili mpate nafasi ndani ya uongozi kwani kwa unafiki huo hamkuanza leo..
 
.

Binafsi, siwapendi CUF na wala siwaamini kama kweli ni chama kinachowakilisha wananchi, ni chama kinachotumia kero za wananchi hasa waislaam ili kujiweka katika nafasi nzuri ya Upinzani. Na ushahidi wa malalamiko yangu umeonekana mwaka huu wakati Seif Sharrif Hamad alipokubali kuchukua makamu wa rais wa Zanzibar, cheo ambacho hakiwezi kuboresha sera za CUF kwa aina yeyote ile. Wizara walizopewa zote hazina maana hata kidogo na kwa miaka mitano mingine Wazanzibar watatawaliwa na serikali isiyokuwa na Upinzani - viongozi wake walichounda ni nasaba ya Usultan.

Chadema wanachotakiwa kufanya ni kukijenga chama pale kinapopwaya na kwa maelezo haya nadhani wanafahamu fika Ujinga ulokwisha jengwa na wananchi kiasi kwamba kura nyingi walizopoteza zimetokana na tuhuma hizo..Ni muhimu waweke mkazo kuwavuta wananchi (wapigakura) na sio ushirika wa vyama.
- Ni mtazamo wangu

Mkandara,
Hata kama huwapendi CUF lakini jaribu kuwa objective, angalau kidogo. Hivi wizara ya afya haina maana?
 
Mzee Mkandara, (Sorry kukuita mzee ni kwa sababu ya busara yako nyingi:teeth:)
Kilichonifurahisha katika post yako hii ni kuona sasa umefungua macho na kuona kitu kilichokuwa kinatuletea utofauti siku kidogo zilizopita. Nacho ni muungano wa vyama hivi viwili. Nakumbuka ulikuwa msitari wa mbele kuhakikisha vinaungana kwa namna yoyote ile, mbali na kilio chetu kwamba si vema waungane. Nakumbuka hata ule mfano wako kwamba CUF ni kama mke wa ndoa wa CCM.
Lakini nimefurahi ku note kuwa sasa na wewe umeliona hilo la ndoa batili ambayo Chadema wanataka kujifunga nayo na CUF. Sioni sababu tena hata kwa nini kuwe na mdahalo. Wakati wa mdahalo nadhani umekwisha na Chadema need to work for wananchi na sio midahalo isiyo na tija hii ya kutupotezea muda.
Mkuu wangu labda hukunielewa...Mara nyingi hutazama mbele zaidi ya hivi vinavyoelea. Kama unakumbuka nilisema CUF sii chama cha Visiwani tu kipo bara na kina sehemu ambazo wananchi wengi wamekipigia kura. Chadema kkama chama kinachotazama ushindi mwaka 2015 ni lazima kitumie akili zaidi kujihusisha na wananchi haswa wapenzi wa CUF kwa kuwaonyesha mapenzi yasiyokuwa na ubaguzi kwa sababu tu CUF Zanzibar imekubaliana na CCM..

Tatizo la mjadala ule ulopita ni kwamba wanaChadema wengi hapa wamekitazama chama CUF, badala ya wanachama wa CUF Tanzania nzima ambao ndio muhimu zaidi ya huyo Hamad Rashid au wajumbe wabunge wa Zanzibar walitutosa ila hao wachache hata kama ni wawili kutoka bara basi hawa wana repesent hesabu kubwa ya wananchi wakazi wa kusini. Kwa hiyo, ndicho nilicholenga mimi zaidi ya ushirikianao ambao Chadema wenyewe waliutaka kisha kukataa kwa sababu CUF walitaka vyama vingine vishirikishwe...

Sababu mlizozitoa wakati ule ni baada ya CUF kukataa ndio sikukubaliana nazo kwani sababu zote hizi zilikuwepo hata kabla Chadema haijaomba washirikiane. Sasa maadam Chadema walikwisha kataa kuweka ushirika na CUF kwa sababu hizi (tukizungumzia leo hii) sioni sababu kabisa ya kuwepo mdahalo na chama ambacho mnakishutumu kwa kuungana na CCM. Kama ingekuwa kabla ya shutuma hizi ningesema waendelee kuongea zaidi lakini mkuu wangu walipofika sasa hivi hawahitaji tena kutiana vidoe vya macho..
 
Mh Freeman Mbowe, atakaa sehemu maalum iliyotulia ili ajiandae kwa mdahalo, hii ni strategy ya marekani ambapo chadema huwa wanaitumia ili kuongea kitu chenye mantiki kwa jamii na kinachopimika na huo utaalam umesababisha Chadema kupaa kwa kasi maana maelezo yao mengi yamefanyiwa utafiti na unaokubalika ndani ya chama. Kuna wachache ktk chadema ambao hawatumii mkakati huu nao wako wanaelimishwa taratibu. Big up Mbowe, big up chadema. Safari inaanza kesho, vox media keep it up!!
 
Mkandara,
Hata kama huwapendi CUF lakini jaribu kuwa objective, angalau kidogo. Hivi wizara ya afya haina maana?
Mkuu labda nisome tena.. CUF watafanya nini tofauti na CCM ikiwa sera zinazotumika ni za CCM. Kuna tija gani zaidi ambayo wewe unaiona toka wizara ambayo haizalishi isipokuwa mzigo kwa serikali na wananchi hivyo CCM wamekupeni mzigo huo kuubeba.

Elimu na Afya ni muhimu sana lakini kama CCM leo wakiwapa Chadema wizara hizo chini ya utawala wa CCM itakuwa vichekesho vitupu..
 
Ndani ya CUF kuna wapenzi wa madaraka na kuna watu hawawezi kukaa bila ya madaraka .Watu wote tegemeo la mageuzi ndani ya CUF wao ni madaraka kwanza ndiyo mfano Hamad Rashid naona hawezi kuishi Bungeni bila ya madaraka au anatimiza ahadi zao na makubaliano ya CCM ndiyo maana vurugu zote hizi .Maalimu kesha pata Ulaji kesha tulia na CUF kwisha kazi maana anatekeleza sera za CCM hawezi kupinga lolote na huku bara wanataka Chadema kuwa kama CUF hapana watuache wao waendelee na kusaka madaraka na kuingia makubaliano na CCM.Tutasikia hiyo weekend wao wana agenda gani .
Sure!!!
 
Mkuu labda nisome tena.. CUF watafanya nini tofauti na CCM ikiwa sera zinazotumika ni za CCM. Kuna tija gani zaidi ambayo wewe unaiona toka wizara ambayo haizalishi isipokuwa mzigo kwa serikali na wananchi hivyo CCM wamekupeni mzigo huo kuubeba.

Elimu na Afya ni muhimu sana lakini kama CCM leo wakiwapa Chadema wizara hizo chini ya utawala wa CCM itakuwa vichekesho vitupu..
Nimekupa heshima kubwa kwa bandiko hili
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.

Kama umeme utakuwepo maana kwa wiki hii sehemu nilipo usiku umeme hakuna na wala hakuna taarifa yoyote ya kuelezea sababu ya kukosekana kwake
 
Angalizo wanaJF, wakati wa mdhalo turudishe kumbu kumbu zetu nyuma kwa CUF walivyo wanaendesha shughuli zao za kisiasa bara na visiwani. Mfano; hawakuitambua serikali ya zenji mpaka walipo ahidiwa ulaji!
 
Utakuwa poa nataka kumsikia aliyekuwa kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani mjengoni akisema nini mara baada ya chama chake kufunga ndoa na chama cha mapinduzi, si ajabu akasema wameamua kufunga ndoa na CCM kuutokana na rais wa awamu ya tano yuko na sera kama za cuf akisahau kuwa 2005- 2010 rais alikuwa kikwete pia awamu ya nne.

CUF wanataka wawemo kwenye kambi ya upinzani. CADEMA wamebana. Sasa CUF wnakuja na vigezo vya kwanini wao nao wasiwemo kwenye kambi hiyo na CHADEMA wanakuja vigezo kwanini wawe wao peke yao. It will be very Intresting.
 
Hapa upinzani uko hatarini,haileti maana yoyote kuwa na such debate!

upinzani hauko hatarini bali upinzani bandia sasa ndio hatarini hii ndio dmkrasia mwanangu Wananchi ili tupate uwanja mpana lazima walumbane kwa hoja Nini watatufanyia nasi tutapima hoja na kuamua kumbe chama fulani ni pumba tu hawana maono!
 
Duh, mkuu wangu lugha inakupiga chenga au ndio makusudi kwa sababu nimewazungumza CUF...Chadema wao siku zote wanalia hawana Udini nakama kweli hawana basi ni jukumu lao wenyewe kutuonyesha hawana Udini kwa sababu najua fika CUF ni chama cha aina gani. CUF ni wabaguzi toka maswala ya kimuungano kuzungumzia zaidi ya Zanzibar na Waislaam kiasi kwamba hata Ufisadi haikuwa kero kwenu.

Napwapongeza tu kwa sababu hamjifichi nyuma ya pazia lolote mkitangaza Udini na Uzanzibar lakini kwa kazi yenu wepesi sana kupachika wengine pia udhaifu wa chama chenu. Nawajua fika mkuu wangu kazi yenu kubwa ni kutafuta kuitumia dini na Uzanzibar ili mpate nafasi ndani ya uongozi kwani kwa unafiki huo hamkuanza leo..

Wakiwa pemba cuf wanadai kwamba walaaah wapemba tunabaguliwa na serkali ya zanzibar na ya muungano yaheeee Wakija zanzibar wanaanza kunadi zanzibar imegeuzwa kijiji cha tanganyika sio nchi lazima turudishe utaifa wa wazanzibar Wakivuka bahari kuja bara wesha badilika na kutangaza waislamu wanaonewa jameni walaaah waislamu wanaonewa Takbir kunja ngumi waislam tunaonewa hee! hiyo ndio picha halisi ya ciyuefu wanangu kaeni chonjo na watu ambao sirini wana malengo yao mahsusi walio yaficha!
 
Lazima tujiulize kwa nini chadema wameunda kambi bila kuwashirikisha vyama vingine hii sio sawa wako CUF,TLP,UDP na NSSR
Je hii ni ubinafsi wa Mbowe na wenzake?
 
Wadau nimepokea email na nawasilisha kwenu kama nilivyopokea.

Wapendwa,
Salamu kwenu nyote na nashukuru kwa jinsi Jukwaa hili linavyojumuisha watu wakabadilishana mawazo juu ya mambo tofauti ya maisha.

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.

eeh Mungu naomba tanesco wasitutende kutukatia umeme wao.amen
 
Lazima tujiulize kwa nini chadema wameunda kambi bila kuwashirikisha vyama vingine hii sio sawa wako CUF,TLP,UDP na NSSR
Je hii ni ubinafsi wa Mbowe na wenzake?

Cuf wana serikali ya mseto na CCm huko Zanzibar. So CUF wamepoteza sifa ya kuwa chama cha upinzani. wataipingaje ccm nao wanashirikiana Zanzibar? TLP mmesikia anaisifia ccm waziwazi, UDP yeye silently ana support ccm, Mbatia wa nccr haeleweki. Sio vema kuwalaumu CHADEMA. Hiyo ndio hali halisi.
 
Muheshimiwa hamad ndio anaingia hapa nasikia kelel huko nje hope ni freeman aikaeli mbowe anaingia hapa

mdahalo utaanza muda si mrefu
 
Back
Top Bottom