Mbunge wa Ushetu apiga magoti kuomba maji ya ziwa Victoria. Waziri amjibu "Samia ametoa pesa mkandarasi anakuja"

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,051
49,736
20240110_072322.jpg

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani Mkoani Shinyanga amemuangukia Waziri wa Maji Jumaa Aweso akimuomba maji kwani Amesema Wilaya Majimbo yaote ya Mkoa wa Shinyanga yamefikiwa na Mji ya kutoka Ziwa Victoria isipokuwa Jimbo lake.

Akiongea Kwa unyenyekevu, uchungu na masikitiko bwana Cherehani amesema kati ya Kata 15 za Jimbo lake Kata 11 hazina maji hivyo kuwa Changamoto kubwa Kwa Wananchi wake.

Akijibu Maombi hayo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema tayari Rais Samia amesikia Kilio Cha Wana Ushetu na Serikali Imetoa maelekezo ya kutangazwa tenda haraka ambapo ndani siku 30 mkandarasi atakuwa site kuanza usambazaji wa Maji Kwa Wananchi maji ya uhakika kutoka Ziwa Victoria.


My Take: Kuelekea Uchaguzi tutaona Mengi, wale wote waliopitishwa na Jiwe kama hawakuwa na sifa ndio imekula kwao.

View: https://www.instagram.com/p/C16S-qIrvkt/?igsh=MXJzdXVjOGE5ZGEwbQ==
 
Nchi imejaa wabunge wajinga kama huyu unategemea maendeleo yatatoka wapi? maji ni kodi za wananchi na siyo hisani ya Samia
Kama huna maarifa utaishia kuwa mpumbavu.

Kwa hiyo maji yasipoletwa na kipaombele kikapelekwa kwingineko utafanyaje wewe mwenye Akili?
 
Siasa ngumu sana! Yaani Mwanaume kabisa, tena Mbunge anapiga Magoti ili kuomba kitu! Huko ni kujidhalilisha na kujishusha thamani, Wapiga kura wake lazima wamdharau kwa hilo.
Kazi gani ambayo ni rahisi kwako?
 
Kazi za kujiajiri hazina mambo kama hayo, ukitegemea za kuajiriwa lazima kuna wakati utanyenyekea Watu na kushusha thamani yako.
Hizo hizo ambazo kuanzia mtendaji wa Kijiji ni boss wako Hadi Rais ? Ukimuona mtu wa Serikali unakuwa mpole.

Pia hazina pesa Wala heshima kama kazi za siasa
 
Hizo hizo ambazo kuanzia mtendaji wa Kijiji ni boss wako Hadi Rais ? Ukimuona mtu wa Serikali unakuwa mpole.

Pia hazina pesa Wala heshima kama kazi za siasa
Si zote, kuna Mtu anafuga Kuku, ataanzaje kuwa mpole akimuona Mtu wa Serikali kama huyo Mtendaji wa Kijiji?

Lakini pia sijasema kwamba Kazi za Siasa hazina Pesa, nilichoona ni ugumu wake hasa nikirejelea kitendo cha huyo Mbunge kupiga Magoti.
 
Si zote, kuna Mtu anafuga Kuku, ataanzaje kuwa mpole akimuona Mtu wa Serikali kama huyo Mtendaji wa Kijiji?

Lakini pia sijasema kwamba Kazi za Siasa hazina Pesa, nilichoona ni ugumu wake hasa nikirejelea kitendo cha huyo Mbunge kupiga Magoti.
Kupiga Magoti na kuogelea kwenye mavi ya kuku kipi Bora? Na Kwa pesa gani? 😂😂
 
Kiufupi anaupiga mwingi sana.

Ujinga ni kudhani Mama anaweza maliza matatizo yenu yaliyowashinda Kwa miaka zaidi ya 60 ndani ya miaka 4.
Hilo ni lako mimi naona hajafanya chochote zaidi ya kuimbiwa nyimbo ambazo yeye hazipendi kuzisikia maana anajua anaingizwa chaka na machawa ili hali ana kazi kubwa mbeleni!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom