USHETU: Kamati ya Siasa Yaridhishwa na Kasi ya Maendeleo Ushetu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

USHETU: Kamati ya Siasa Yaridhishwa na Kasi ya Maendeleo Ushetu

Wananchi katika Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wahaswa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan pamoja na Chama cha Mapiduzi CCM katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa katika ziara ya kamati ya siasa ya mkoa huo ambapo wamekagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Mabala amesema, katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia, ni fedha nyingi zilizotolewa kwaajili ya maendeleo ikiwa ndio utekelezaji wa Ilani ya hicho katika kutatua kero na changamoto za Wananchi na kwamba Kamati imeridhishwa na usimamizi wa miradi iliyotolewa na serikali.

Akizungumza katika Ziara hiyo Mbunge wa jimbo la Ushetu @cherehaniemmanuel amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa Fedha ya Miradi katika Elimu, Afya Maji na Miundombinu lakini sambamba na hilo amekuwa anasikiliza kero za Wananchi kwani kuwapa Miradi pekee bado haitoshi kukamilisha utekelezaji wa Ilani Ya Chama.

Amesema hadi sasa amefanya jumla ya mikutano 252 katika kata zote za Jimbo hil na ameseikiliza na kutatua Kero mbalimbali za Wananchi kwa kushirikiana na watumishi wa Halmashauri na Madiwani na Kwamba hiyo ndio chachu ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Nae Mkuu wa wilaya ya Kahama @mboni_mhita amesema lengo la Kamati hiyo ya siasa kufanya ziara ni kujionea utekelezaji wa miradi ambayo iliahidiwa na chama cha mapinduzi wakati wa uchaguzi huku akimpongeza Mbunge Cherehani kwa kufanikisha kupata miradi mingi ya maendeleo.

Kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga Imefanya ziara katika Jimbo la Ushetu na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa vyumba vya madarasa, Bweni, Ukumbi na Matundu ya Vyoo katika Shule ya Sekondari Dakama, ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa Shule ya msingi Ukune na Jengo la dharura katika Hospital ya Halmashauri Ushetu.
WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.09.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.10.jpeg
    50.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.13.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.13.jpeg
    54.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.13(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.13(1).jpeg
    28.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.09(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.09(1).jpeg
    30.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.13(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-21 at 02.43.13(2).jpeg
    48.2 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom