Matusi ya Lema na Matusi ya Lusinde ni Matusi Yetu na Unafiki Wetu!

Hii Habari ya Lema kila mtu anajifanya ni analyst na mwandishi mzuri,

lakini aingii akilini kulinganisha ya Lusinde na ya Lema, na kama kuna mwandishi mzuri ama analyst anaelinganisha vitu basi angeweka hapa ni kipi alichokisema Lema (ambacho ni tusi) ukilinganisha na cha Lusinde

Lakini cha muhimu pia tujiulize na kuanalyze hicho alichokisema Lema (ambacho ni tusi) ndilo lililomvua Ubunge?

kwa hiyo kutukana kidogo is okay, ila kutukana sana si sawa?? mnataka ushahidi wa matusi ya lema ili hali amevuliwa ubunge na mahakama kwa kutukana matusi!!! what a joke
 
Waberoya unafikiri sana na hujawa addicted na politics za Bongo.Siasa zetu huwa za kulewa na chongo turns to Kengeza.Binafsi wote wenye matatizo ya kufanana wawajibishwe tu yaani Mkapa(kama kuhoji uhalali wa Vicent ni tusi),Vicent Nyerere (kama kumuhusisha mkapa na kifo cha Kambarage ni tusi),Mndee,Sugu,Lema, Lusinde wote ni ''manzi ga nyanza''
 
Leta data ikiwezekana audiovisual tuwashughulikie. Isije ikawa matusi hayo ni ukweli unaotolewa na mdee , lema na sugu dhidi ya mafisadi leta data hapa
 
Batilda kuambiwa kazaa nje ya ndo si tusi...privided hajaahi kuja court kukanusha....ila kumwabia mtu ...KAMA KAJ..EA nitus dhahari hata mtoto anajua....usitake kulinganisha manano ya LEMA na matusi ya LUSINDE
 
Hii bongo mjomba usiumizwe kichwa huhitaji genius kueleza kwanini mahakama imetoa maamuzi ya kesi immediately baada ya matokeo ya arumeru. Hivyo ni visa vya mama au baba ubaya, kajibu mapigo au siyo period. Wasijifanye mahakama ni chombo huru. Fikiria kesi ile ya burushi aliyekaa siku 40 tu baada ya kumuua mswahili rujewa. Escort toka mby full mzinga ffu waliotapakaa kila mahali kudhibiti hasira za wananchi. Eti it was just a natural justice lema kufukuzwa ubunge tumuogope mola siku moja atatoa hukumu saa hiyohiyo hapo mahakamani. Misukumo ya serkali ipo sana kama siyo mbona kesi zingine zimelala usingizi wa pono. Kulikoni hapa?
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
We Macho mlendemko hebu jaribu kutofautisha mambo badala ya ku-generalize issues, matusi ya Lusinde haya influence chochote kwenye hukumu ya Lema, na nnashangaa kuona mnadai hapa ushaidi wa Lema kama alituka kweli au la hali mnajua kabisa Lema alimshambulia mgombea wa CCM kwa kashfa za kutokua mwaminifu katika ndoa yake am sure mahakama haikukurupuka kutoa hukumu bila ushaidi wa kutosha, au na nyie mnataka ushaidi uwekwe kwenye youtube ndo muamini?
 
WanaJF,

Nimerudia kusikiliza rekodi ya hotuba ya Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera (CCM) wakati akimwaga MATUSI katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Ngarasero. Nimeandika zaidi ya sentensi 15, ambazo ni matusi au zina viashiria vya lugha ya matusi.

Karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Mh. Mkama amesikika akitetea kwamba Lusinde alikuwa anajibu hoja za wapinzani wake, CDM.

Aidha jana, tarehe 5/4/12, ubunge wa Mh. Godbless Lema (Arusha Mjini, CDM), umetenguliwa kwa kile kinasemwa kufanya kampeni bila kuzingatia maadili ya kampeni, ikiwepo matumizi ya lugha inayotafasiriwa kwamba ni matusi. Jambo zuri tu, kama kweli tunataka kulenga kampeni za kistaarabu!

Katika dk 16:06 zilizorekodi hotuba ya Lusinde kama ilivyo katika mtandao, nimetambua mambo haya kama matusi au lugha ya matusi, wastani wa karibu sentinsi/tusi moja katika kila dk moja aliyotumia kuongea Lusinde:-

  1. Kuda-dada-deki (amerudia karibu mara sita).
  2. Wewe umekuwa ukiwachanja chale mpaka matakoni (akimlaumu Prof. Majimarefu).
  3. Hata wao ni mashoga basi, (akihusisha kutoga masikio na suala la ushoga).
  4. Nani hafahamu kwamba mbunge wa Arusha mjini aliolewa kule mahabusu/amepata bwana, (akihusisha Lema kuwa mahabusu na kwamba aliolewa), (ikiwa ni sodomization kwa tafsiri yangu).
  5. Dk. Slaa alitimuliwa uPadri baada ya kuwatia mimba wanakwaya. (akimtukana Dk. Slaa moja kwa moja)
  6. ***** huyu - Vicent Nyerere, ana akili mbovu. (akimtukana Mh. Vicenti Nyerere)
  7. Ameliwa -------- siye hatusemi. (ikimaanisha kuwa sodomized, iwapo sikujua anamtukana Vicent Nyerere au Godbless Lema).
  8. Acheni ushamba nyie. (akiwatukana wananchi, ambao wanaonyesha kuwa wafuasi wa CDM)
  9. Washamba wakubwa nyie x 2. (akiwatukana wananchi)
  10. Washamba wakubwa ----, Dk. Slaa mshamba mkubwa, akivaa kombati, anakuwa kama kajinyea. (akimtukana Dk. Slaa)
  11. Viongozi wa CDM vichaa wa kulogwa. (akiwatukana viongozi wa CDM)
  12. Dk. Slaa anatishia kujamba wakati anaharisha. (akimtukana Dk. Slaa)
  13. Sera ya CDM ni sera ya jogoo, jogoo linamuahidi kuku gauni, huku lenyewe hata chupi halina. (akikitukana chama kwa ujumla wake).
  14. Mbowe anasema ana uchungu, kwani ana mimba? (akimtukana Mbowe)
  15. Mbowe pigwa mimba! Slaa pigwa mimba! Nasari pigwa mimba! (akiwatukana Mbowe, Slaa na Nasari).

Sasa, nimeambiwa kupitia vyombo vya habari kwamba watu 3 ndiyo waliomfungulia mashtaka Mh. Godbless Lema, kufanya illegal practices katika kampeni wala siyo aliyeshindana naye katika ubunge Batilda Burian, vema. NANI WATAMFUNGULIA MASHTAKA LUSINDE KWA KUFANYA ILLEGAL PRACTICES katika kampeni za Arumeru Mashariki kama kweli tunatendeana haki?

Sentensi na maneno ya viashiria vya matusi niliyotaja mnaweza kuyafanyia uchambuzi zaidi, na kurudia kuisikiliza hotuba ile ili kujenga hoja vizuri. Najua kuna mdau alikwisha uliza hoja kama hii humu mtandaoni, lakini sijui hatua gani zimeendelea kuchukuliwa.

Nasisitiza wanasiasa kujenga hoja za msingi wakati wa kampeni. Ushahidi unajionyesha wengi wamekuwa wanajikita zaidi katika kumshambulia mgombea kuliko kushambulia-kwa uchambuzi na mikakati mambo ambayo ni matatizo na changamoto katika maendeleo ya wananchi. Lusinde alitumia zaidi ya dk 15, kushambulia watu, sio kushambulia kwa uchambuzi na mikakati matatizo ya wanaArumeru Mashariki.

Kwa mzaha kabisa, Katibu Mkuu wake anaunga mkono kwamba huko ilikuwa kujibu hoja za wapinzani wake. Hapa unajua unashindwa kutafsiri hekima na busara ya kiongozi mkuu wa chama, katika kukiwezesha chama chake kupaa na kuaminiwa. Sijui bwana, SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA!


Perecy Ugula
MwanaJF Mchanga,
Email: ugulapp@yahoo.co.uk
Simu: +255 766 082388

perecy,wewe ni zaidi ya great thinker!
Waberoya yu sahihi kimantiki,kwa maana hakuna justification ya mtu yeyote kutukana!
Lakini,WANAO DAI LEMA katukana,wameshndwa kutoa ushahd timilifu usio na shaka kama ulivyo fanya!
U are Unique!
 
Matusi ya lusinde kila mtu ameona.unaweza kutudhibitishia kuwa Lema ametukana?walalamikaji walidai hivyo lakini mimi sijaona uthibitisho wowote walioitoa kuithibitishia mahakama kuwa Lema alitukana?

Tuheshimu taaluma za watu.Tambua kuwa Lema alikuwa na Mwanasheria wake sawa na upande wa walalamikaji.Shauri hili limechukua muda,mjadala wa kisheria,rasilimali fedha na hatimaye maamuzi kutolewa.

Nani alikwambia ushahidi ili ukamilike na uwe accurate sharti CD ionyeshwe.Testification ni suala pana na linautaratibu wake mpaka kukubaliwa Mkubwa.
 
sisi kwenye hili jukwaa tusingependa habari ndefu na hotuba ndefu! tunaomba utupe ushahidi wa matusi ya lema,sugu na mdee! usiweke habari ndefu isiyo na vielelezo! tunakushuru kwa kuandika ujumbe mzuri ila tusaidie ushaidi uliyo nao!. Amani kwako
Msitake kuishi kinafki kama kweli ni mfatilia siasa unajua kabisa mdee, lema, na sugu hawana kauli nzusi
 
well said hakuna justification ya mtu yeyote kutukana hasa kiongozi, mimi ni mwanaccm ila nalaani kitendo cha lusinde, basi msiwe wanafiki kwamba hata sugu nae hamuoni matusi yake?
 
Kuna tatizo kuu la msingi ambalo nisiposema dhamiri yangu itanihukumu na sitakaa kimya kwa sababu wengine wameamua kukaa kimya.

Jamii ya Tanzania iko kwenye ugonjwa mkubwa na tusipoudhibiti huu ugonjwa hakuna wa kutusaidia. Tunaiumiza jamii, tunaharibiu vizazi vijavyo kwa kisingizio cha mabadiliko!

Sera ya chadema si matusi!! Sera ya chadema ni mabadiliko, sijawahi kuona Slaa akitoa matusi ya nguoni, sijawahi kuona Mbowe akitoa matusi ya nguoni, wala sijawahi kuona Zito akitukana, these people they are still high in their positions na popular kwenye siasa na wanaaminika kwenye jamii kwa kuleta mabadiliko

Ila nimemsikia Mdee akitukana( personally nilimkataza) , nilimsikia Lema akitukana, tumeona Sugu akitukana mpaka kujirekodi!! Hawa ndio wabunge wetu, ndio tuliowapa dhamana ya kuongoza taifa letu kwa nafasi zao…ila wanatukana, wakitukana hawa ni sawa??

Nani kasema?

Kuna uwezekano mkubwa akina Mbowe, slaa hawawezi kuwadhibiti akina Lema, kwa sababu ya kuwaonea aibu!! Unapopagawa na siasa na kuona kila unachotukana kinashangiliwa, basi jamii nzima inakuwa imeoza! Msikilize Lusinde utaamini!

ILA; Ukiwa mpinzani lazima uangalie zile nafasi/chances/ opportunities ambazo adui yako anaweza kuzitumia kukuangamiza!

Kama CCM wametumia mahakama kumuondoa adui yao Lema, it is okay na wametumia karata yao vizuri sana.

Lakini kama si CCM na mahakama, je matusi yanakubaliwa katika jamii yetu??

Hivi Mdee, sugu, Lema na Lusinde tofauti yao ni nini??

Na sisi wataka mabadiliko , ukweli wa mioyo yetu na matusi uko wapi? Kuwa tutukane tu kwa sababu kwa kufanya hivyo ndio tunahimiza moto wa mabadiliko??

Matusi mangapi yanatukanwa humu ndani? Wanaotukana ni akina nani? Je wakipewa uongozi hawatatukana kwa sababu ni viongozi? Yaani uongozi una mechanism ya kuzuia matusi biologically? Matusi tumeyakubali, tunaishi nayo, tunalala nayo kila kona ya nchi yetu si kwa hao niliowataja, yako kila kona, kwenye madaladala, kwenye michezo name it!

Lema ameadhibiwa na mahakama, Lusinde ameadhibiwa na wananchi-ambao wengi wao wanatukana, mwisho wa siku wote ni watukanaji! Ikifika hatua tukaona Lema ni shujaa tunakuwa tumevua akili zetu na utu wetu na kuuweka kando na sisi……..tunaishi kinafiki , tuna post kinafiki kwani usafi na intergirty is not part of our life!!


In this case mahama iko clean..tena wanapongezana, hivi..juzi tu tumelia Lusinde anatukana-tukasema kila kona na kulaani, leo hii Lema anavuliwa ubunge kwa kutukana tunaona ubaya?? Kweli??
Kamanda naona umeweka nyama za kutosha kwenye makala yako.Unaweza toa angalau clip moja ya ushahidi wa matusi ya Lema na Mdee kama ilivyofanyika kwa Lusinde?. Umenifunua kumbe Mdee na Lema nao ni watukanaji ! !
 
perecy,wewe ni zaidi ya great thinker!
Waberoya yu sahihi kimantiki,kwa maana
hakuna justification ya mtu yeyote kutukana!
Lakini,WANAO DAI LEMA katukana,wameshndwa kutoa ushahd timilifu usio na shaka kama ulivyo fanya!
U are Unique!


Nadhani ingekuwa vyema kama tukipata Nakala ya hukumu.Baada ya kuisoma tunaweza kujadili mengi tukihusisha Wanasheria wa JF (Members).Nasema hivi kwa sababu wengi wetu hapa hatukuweza kuifatilia kesi hii kwa umakini kwa maana ya kushiriki mahakamani.Hii si kwa sababu ya kutokujali bali majukumu ya kikazi na kimaisha kutuzinga.

Wenye ushahidi wa kutosha kisheria dhidi ya Lusinde wanaweza kupeleka shauri hili mahakamani kwa jinsi wanavyoona lina mashiko.Lusinde ni kijana aliyekaa kwa muda kidogo Tarime hivyo sishangai hata mazingira,elimu na ulimbukeni kumuathiri kisiasa.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Umesema mengi sana juu ya cdm, mbona huoni juu ya Mkapa, Wassira, Mchemba na Sendeka? Unafiki haukufai.
 
sikujua kama na wewe gamba mkuu !

yan unataka lema na lusinde wawe treated the same? how dare u??

embu weka huo ushahidi wa matusi ya lema hapa n the rest nways!
 
Mkuu Gaijin,

Si kweli hapo kwenye RED. Mdee hajamwita Wassira Sokwe. Nina uhakika asilimia 100. Maneno ya Mdee, unaweza kuyaweka kwenye mstari unaogawanya matusi na si matusi. Mwingine anaweza kuyachukulia kama matusi na mwingine si matusi.

Hata Lusinde kusema Dr. Slaa akitembea kama amejinyea, haina maana kasema kuwa Dr. Slaa kajinyea. Ila tu neno lenyewe kujinyea, hapo ndipo linaleta utata na ni sawa na neno Sokwe mtu.

Mtu akija na kusema "...anapotembea ni kama Malaika (Kabibi - Sam Mangwana)" haina maana huyu binti kashakuwa Malaika.

Sugu matusi yake unaweza kubishana sana maana Wasanii duniani huwa wanapewa kihuruma fulani hivi na kuruhusiwa kuuvuka mstari wa Wananchi wengine. Anaweza kutania, kutukana nk. Tuliona hata Jammie Fox akimshambulia Obama kuwa hajui kucheza na tena White House. Sasa wewe mwenzangu mie nenda ufanye huo utani. Sugu kwenye matusi tusimchanganye sana na sanasana BASATA inabidi wale naye sambamba ingawa nayo siku zote italeta ugomvi.
Waberoya umeongea vizuri sana.

Mdee, Sugu, Lema nao ni watukanaji na wenye kutumia lugha mbovu mbovu kwa wapinzani wao.

Na kwa sisi kuwashangilia na hata kuwatukuza wakati mwengine kunaonyesha tu sisi Watanzania ni watu wa aina gani. Hatuna integrity.

Mtu kama Mdee kumwita Wassira Sokwe-mtu ni aibu........kwa misingi yote iliyopo ya kibinaadamu
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Kwa ujumla lugha za matusi zimejengeka sana katika siasa zetu.Imefikia hatua ambayo watu wanadai ''ukitaka watu wajue umekula nini jana usiku'' nenda kwenye siasa.

Maadili ya wachaguaji kwa maana ya Wananchi nayo yameshuka kweli kweli.Wananchi katika kampeni wanapenda kusikia ''mipasho'' tu tena story za mitaani.Sera kwao ni sawa na kupoteza muda lakini ufarijika kusika fulani kafanya hivi,bwabwa,heleni,bongo fleva,mke wa mtu ...oooooh kimada.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Waberoya umesema vizuri, lakini ushahidi wa matusi ya Lema uko wapi? Hebu tuwekeeni hapa ushahidi wa Matusi ya Lema.
 
[Q
UOTE=Sikonge;3639657]Mkuu Gaijin,

Si kweli hapo kwenye RED. Mdee hajamwita Wassira Sokwe. Nina uhakika asilimia 100. Maneno ya Mdee, unaweza kuyaweka kwenye mstari unaogawanya matusi na si matusi. Mwingine anaweza kuyachukulia kama matusi na mwingine si matusi.

Sikonge

Napata shida kidogo kukupata kwa kile unachojaribu kuharalisha hapa.Tambua siasa ni disciplinary code of conduct na players wake ni waomba kura na wapiga kura.Huwezi kusema eti wasanii wanahurumiwa kutumia lugha zao za kitaa katika jukwaa la siasa.

Tusi ni tusi tu na adhabu yake ni pale anayetukanwa ama jamii ikilichukulia kama tusi na si utani.Tujenge heshima tunapokuwa majukwaani kwani wanaotusikiliza ni (wazee,vijana,watoto,baba,mama,wakwe n.k).Siasa za kihuni hazikubaliki kwa namna yeyote.
Hata Lusinde kusema Dr. Slaa akitembea kama amejinyea, haina maana kasema kuwa Dr. Slaa kajinyea. Ila tu neno lenyewe kujinyea, hapo ndipo linaleta utata na ni sawa na neno Sokwe mtu.

Mtu akija na kusema "...anapotembea ni kama Malaika (Kabibi - Sam Mangwana)" haina maana huyu binti kashakuwa Malaika.

Sugu matusi yake unaweza kubishana sana maana Wasanii duniani huwa wanapewa kihuruma fulani hivi na kuruhusiwa kuuvuka mstari wa Wananchi wengine. Anaweza kutania, kutukana nk. Tuliona hata Jammie Fox akimshambulia Obama kuwa hajui kucheza na tena White House. Sasa wewe mwenzangu mie nenda ufanye huo utani. Sugu kwenye matusi tusimchanganye sana na sanasana BASATA inabidi wale naye sambamba ingawa nayo siku zote italeta ugomvi.[/QUOTE]
 
Wanasheria wapenda haki, jiungeni tumshitaki Lusinde avuliwe ubunge kwa kutoa matusi ya aibu jinsi hiyo. Je inawezekana mkafanya hivyo kwa niaba yetu?
 
Back
Top Bottom