Mbowe hawezi kukwepa lawama za kukosa adabu na kutukana matusi ya nguoni kunakofanywa na vijana wake wa CHADEMA

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,301
9,727
Ndugu zangu Watanzania,

Wakati mwingine huwa ni aibu sana,fedheha kubwa sana pale unapoweza ukawa unasikiliza mkutano wa hadhara wa CHADEMA unaohutubiwa na vijana wake huku mitaani.kiukweli inasikitisha sana na inaleta maswali mengi sana kichwani juu ya maadili ya kiuongozi yanayotolewa na kufundishwa ndani ya CHADEMA kwa vijana wake ambao ndio viongozi wa kesho.

Kinachokuwa kinatawala na kutoka katika vinywa vya vijana hao huwa ni matusi matupu tena matusi ya nguoni,ni lugha za ukakasi na za aibu kubwa sana ambayo unakuwa unaona wewe unayesikiliza.huwa najiuliza mimi binafsi kuwa hivi hawa vijana hawawezi kuzungumza na kujenga hoja bila kutukana matusi kwa viongozi wetu na watu wengine? Kwamba Huwa haiwezekani kupeleka na kufikisha ujumbe kwa wananchi bila kutukana matusi? Kwamba hawawezi kujenga hoja za kuwashawishi watu bila matusi? Kwamba hawawezi kueleweka kwa watu wasipotukana matusi?

Ni vipi na namna gani mbowe anawalea vijana wake? Anawafundisha nini akiwa nao kwenye vikao vya ndani? Anafurahia matusi yanayotolewa na vijana wake kwenda kwa watu wengine wanaotofautiana nao mitizamo na itikadi? Amewahi kuwaonya? Je wamemshinda au anawaogopa? Shida nini kukosa huku adabu na hekima kwa vijana wa CHADEMA? Je malezi mabaya toka kwenye familia zao? Kama ni malezi mabaya kutoka kwenye familia zao, iweje wawe ni vijana wa CHADEMA pekee waliokosa adabu ,hekima ,busara na staha na kutukana matusi kama vichaa au wendawazimu?

Je, CHADEMA ni kimbilio la vijana waliozibuka akili na kuvuta mibangi bila kikomo? Je CHADEMA imejaa vijana ambao wameshindikana kutoka katika familia zao? Je CHADEMA ni mrundikano wa vijana walioathirika kisaikolojia,waliokosa malezi pamoja na kujikulia tu bila uangalizi wa aina yoyote ile? Inawezekana vipi kijana unayejitambua ,mwenye adabu ,hekima,busara,staha,aibu na hofu ya Mungu ukawa unatukana matusi na kuandika matusi makubwa kiasi kile katika mitandao ya kijamii kuwatukana watu waliokuzidi umri na ambao wanaweza kulingana na wazazi wako au kuwazidi kabisa? Kwani huwezi ukamkosoa mtu kwa staha pasipo kumporomoshea matusi ya nguoni na kumdhalilisha?

Unapata wapi ujasiri wa kumtukana mtu matusi ya nguoni utafikiri kuna kosa kubwa? Kutofautiana tu mitizamo ndio umdhalilishe mtu? Kukosolewa tu ndio iwe nongwa? Kwanini pia vijana wa CHADEMA wanaona ufahari sana na kumpongeza sana na kumuona shujaa na jasiri mtu anayetukana matusi makubwa makubwa viongozi wetu pamoja na wale wanaotofautiana mitizamo katika mambo fulani fulani? Kwamba watanzania wote tuwe na mawazo sawa na kuwaza sawa wakati wote kama mazuzu?

Mimi naona Mbowe alikuwa na nafasi kubwa sana na ya kipekee sana kuwakuza vijana wake kiuongozi wakawa na adabu,hekima,busara,staha na utulivu wajengapo hoja ama kuandika katika kurasa zao za mitandao.angewafunda na kuwakemea au kuwafundisha namna ya kujenga hoja badala ya kushambulia watu kwa matusi.sasa kinachoonyesha kwa sasa ni kama Mbowe anawaogopa vijana wake kuwaambia ukweli kwa hofu kuwa wataanza kumshambulia kwa matusi na kejeli na kumtaka ajiuzulu na kuwaachia chama chao.

Lakini pia nimefanya uchambuzi wangu binafsi na wa kina kwa kutumia akili yangu nikabaini kitu kingine kuwa kwa muda mrefu Mbowe amekuwa akiwatumia vijana hawa katika kuwashughulikia mahasimu wake na washindani wake walioonekana kukimendea na kukinyemelea kiti cha uenyekiti.ambapo amekuwa akiwatumia vijana wake kupeleka mashambulizi ya lugha za aina zote kuanzia matusi, udhalilishaji pamoja na tuhuma za kupikwa ,uzushi,uongo na kuwapaka matope wapinzani wake ndani ya chama kwa kutumia vinywa vya vijana hawa.

Hivyo kama amewatumia katika michezo haramu na mibaya ya kuumiza wapinzani wake na akafanikiwa kuendelea kusalia katika kiti hicho cha Uwenyekiti kwa miaka 20 ,maana yake ni kuwa hawezi kuwa na ujasiri wala uwezo wala nguvu wala kifua wala sauti ya aina yoyote ile kuwakemea au kuwaonya vijana hawa kuwa waache matusi. kwa sababu ni matusi hayo hayo ndiyo waliyoyatumia kumuokoa yeye kudondoshwa au kupata ushindani mkali katika kinyang'anyiro cha Uwenyekiti. ndio sababu anaamua kukaa kimya hata kama hapendi matusi hayo ya vijana wake.na kama akizungumza hawezi kuzungumza kwa ujasiri au nguvu au sauti ya mamlaka na akaeleweka na hao vijana,zaidi zaidi watamdharau tu moyoni mwao na kumpuuza. na ndio sababu ya kuendelea kwa hali hii ya matusi miongoni mwa vijana wa CHADEMA.

Hali hii ya matusi inayofanywa na vijana wa CHADEMA kwa sasa inawakwaza sana Watanzania,inawakera sana maana hakuna mtanzania anayependa kusikia habari za matusi ya nguoni.au hakuna kijana anayeweza kufurahia kuona mzazi wake au mama yake akitukanwa matusi ya nguoni na vijana wadogo mitandaoni bila sababu ya msingi.hii ndio sababu CHADEMA inakuwa inaonekana kama chama cha kihuni huni tu kilichojaa na kusheheni wahuni. Lakini ikumbukwe ya kuwa wahuni hawa na waliokosa adabu na kutukana matusi leo ndio watakaokuwa viongozi kesho ndani ya CHADEMA.hivyo chama kitaendelea kukosa mvuto na ushawishi kwa watu kwasababu kitakuwa hakina hoja ya msingi kuwashawishi watu kuwaunga mkono zaidi ya matusi tu ambayo hakuna jamii inayoweza kufurahia jambo hilo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania wote kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Sidhani kama kuna vijana wanaongoza kwa matusi kama UVCCM. Ni hawahawa walioandika mabango ya “Hakuna cha kujinyea wala kujikojolea, Hapa Kazi Tu!” kwenye kampeni za mwaka 2015 kumdhihaki marehemu mzee Lowassa.

Na hawahawa wakasema hawataki viwete ikulu kwenye kampeni za 2020 kumdhihaki T. Lissu. Hiyo ni baadhi ya mifano tu.

E068CB54-68CB-4496-90E8-4CB0E64162D5.jpeg
 
Mi nafikiri wengi wanaotukana Sio CHADEMA..
Ni watu tu wenye fikra na hasira na Maisha..

Na hata uluvyosema baadhi ya Viongozi wa CHADEMA kukosa Adabu na Hekima Mbele ya watu wengine na Uongozi wa Nchi..Hiyo ndo Inamfanya Mbowe awe na hofu Kuachia CHAMA maana akiachia tu chama bila kuandaa au kufundisha watu wa kuwaachia Chama kitafutika na kupogea kama CUF
Lucas mwashambwa
 
Mi nafikiri wengi wanaotukana Sio CHADEMA..
Ni watu tu wenye fikra na hasira na Maisha..

Na hata uluvyosema baadhi ya Viongozi wa CHADEMA kukosa Adabu na Hekima Mbele ya watu wengine na Uongozi wa Nchi..Hiyo ndo Inamfanya Mbowe awe na hofu Kuachia CHAMA maana akiachia tu chama bila kuandaa au kufundisha watu wa kuwaachia Chama kitafutika na kupogea kama CUF
Lucas mwashambwa
Kama ameshindwa kutengeneza viongozi wanaoweza ongoza chama katika nafasi ya uwenyekiti ,basi amini ya kuwa ni ngumu sana kuandaa viongozi hao kwa sasa,zaidi zaidi ni kuwa kitakachokuwa kinafanyika ni janja janja ya yeye mbowe kusalia kwenye kigoda chake alichorithishwa..
 
Ndugu zangu Watanzania,

Wakati mwingine huwa ni aibu sana,fedheha kubwa sana pale unapoweza ukawa unasikiliza mkutano wa hadhara wa CHADEMA unaohutubiwa na vijana wake huku mitaani.kiukweli inasikitisha sana na inaleta maswali mengi sana kichwani juu ya maadili ya kiuongozi yanayotolewa na kufundishwa ndani ya CHADEMA kwa vijana wake ambao ndio viongozi wa kesho.

Kinachokuwa kinatawala na kutoka katika vinywa vya vijana hao huwa ni matusi matupu tena matusi ya nguoni,ni lugha za ukakasi na za aibu kubwa sana ambayo unakuwa unaona wewe...
Kile chama ni cha wahuni ni matusi na ujuaji mwingi kidogo mbowe huwa ana busara ila vijana wake huku chini hamna kitu mabingwa wa matusi sijui wenyewe kwa akili zao mbovu wanaona ndio ujanja huwa nashindwa kuwaelewa
 
..Na Samia hawezi kukwepa lawama za Bashite kununua makalio makubwa.

..Pia Samia hawezi kukwepa lawama za hali ngumu ya uchumi inayowakabili Watanzania.
Zamani ulikuwaga unajenga hoja nzuri sana huku jukwaani.lakini siku hizi sijuwi umepatwa na nini? Mimi nahisi labda anayetumia jina na ID hii kwa sasa siyo yule wa awali .
 
Back
Top Bottom