Matusi ya Lema na Matusi ya Lusinde ni Matusi Yetu na Unafiki Wetu!

Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Hata hivyo nina ushabiki mkubwa kupindukia kwa CHADEMA. Sikubaliani na matumizi ya kauli za "Mwanamke huyu si mwaminifu kwenye ndoa hivyo........" hata kama haya si matusi dhahiri. Mi namwona Lema kama mbunge mtata sana. Ukiachana na suala hili la Dr Burian kitendo cha Lema kukataa dhamana na kujipeleka mahabusu (ikumbukwe alishawishiwa sana na akina Dr Slaa akubali dhamana) kilinifadhaisha sana. Hivyo tuhuma kuwa Lema alitukana au alitoa kauli zenye mwelekeo huo hazinishangazi (Sina ushahidi (huenda nafanya ushabiki tu)).

CHADEMA wamekuwa wakibambikiwa kesi na kutikiswa hapa na pale. Paradoxically, CCM hawajui kuwa "kila mtu" anajua! Dr Slaa alikashifiwa sana wakati wa uchaguzi hata Jakaya alichangia sana katika kuongea kauli za HOVYO (herufi kubwa) "msiwachague wanaotaka kwenda Ikulu kwa kutembea juu ya maiti za watu." Hata kama Jakaya kaiba kura, hata kama kashinda kihalali; hata kama Mzee wa Upako, Askofu wangu Kilaini na Mwinjilisti Kulola wamemwita chaguo la Mungu, MZEE KIKWETE ALIONESHA KIWANGO KIDOGO SANA CHA BUSARA. Kauli za watu wa aina ya Lema, Kikwete, Lusinde na wenzao zinaleta tensions zisizokuwa na ulazima kwa nchi. Siku hizi siasa imekuwa "politicized" kwelikweli.

Nitoe angalizo tu kuwa MATUSI yaendelee kuwa sera ya CCM.CDM wana nafasi nzuri ya kusikilizwa na wananchi... waitumie nafasi hii vizuri. Kama CDM watalazimika kujadili mambo "binafsi" ya mtu sina tatizo na hilo ila lazima yawe na uhusiano na welfare ya nchi.
Hatutaki habari za mimba hapa. Hata hivyo usafi wa kimaadili wa mgombea waweza kuhojiwa but kwa habari ya Dr Burian, Lema hakuwa na sababu za kuzungumzia mambo ya mimba ya Dr Burian (kwa ubaya au kwa uzuri).

Nawaombea mafanikio CHADEMA, hata wasipofanikiwa leo au kesho, watabaki katika kumbukumbuku zangu kuwa walijaribu. Hili naliweka katika maandishi. Na kwa hakika kabisa nitachangia maboresho fulani kwa CHADEMA kupitia taaluma na talents zangu, this is guarranteed.

Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki Tanganyika.
 
as usual.....Lema na washabiki wake na siasa za 'harakati na confrontational politics to the maximum'

eti mahakama 'haiko fair' mbona Tsere alipoenda kupinga ubunge wa Dr.Slaa...mahakama imeonekana imetenda haki?
Dr.Slaa aliposhinda????

na mifano mingi tu mingine.......

sasa ukweli ni kuwa siasa za kishabiki na kufurahisha jukwaa bila kuwa makini na sheria zinasemaje

zitawaponza Chadema.........Mbona Mnyika anaweza kuongea bila matusi?

hivi ni mara ngapi Mdee na Lema wameambiwa bungeni kufuta kauli zao
lakini sio Mnyika????/

mbona hili lipo waazi kabisa????????

kuzungumza masuala ya jinsia ya Batilda ni kosa la kisheria....tena hili wanawake wanaharakati walilipigia debe saana?

sheria zilivyo huwezi kumuita mgombea wa kike 'malaya' hata kama ni kweli 'malaya'....

wafuasi wengi wa CDM wameng'ang'ania kusema tu ni kweli kazaa nje ya ndoa as if hiyo ni sera ya CDM...

Waberoya i doubt kama unaeleweka humu.....na wengi....
 
Matusi ni hatari sana na wote wanaotumia matusi majukwaani walaaniwe. Mambo aliyofanya Lusinde kule Arumeru yalikuwa ya hatari tungeweza kujikuta tunarudia uchaguzi kama Siyoi angeshinda. Walaaniwe wote wanaotumia matusi kwakuwa wanatuingiza kwenye gharama zisizo za lazima.
 
Ivi tumefikaje hapa?
Ok.
1. Ikulu nayo imeporomosha matusi kwa Lema nayo tuifanyaje?
2. Mkapa aliwashushia matusi wapinzani, sheria inasemaje juu yake?
Usitaarabu wetu sasa unapimwa kwa kitu gani?
 
Reformer, ulitaka Chenge afungwe miaka mingapi kwa kosa la barabarani? Hebu kapitie kidogo vifungu ndugu usijekuwa unalalamika kwa vitu usivyovijua!
 
Tusiwe waropokaji wazuri bali tuwe wachangia hoja wazuri Hukumu ya Lema ina walakini kwa sababu muhusika mkuu hajalalamika Kingine tuangalie na garama jamani fedha hizo zingefanya mambo ya maendeleo. Bado taifa halijawa na uongozi imara.
 
Waberoya umeongea vizuri sana.

Mdee, Sugu, Lema nao ni watukanaji na wenye kutumia lugha mbovu mbovu kwa wapinzani wao.

Na kwa sisi kuwashangilia na hata kuwatukuza wakati mwengine kunaonyesha tu sisi Watanzania ni watu wa aina gani. Hatuna integrity.

Mtu kama Mdee kumwita Wassira Sokwe-mtu ni aibu........kwa misingi yote iliyopo ya kibinaadamu

Kwani Wasira anaonekana je? Mbona mimi sielewi!!!
 
The Boss, siyo wote lazima wawe sawa. Kuna watu kama Rambo wanafanya kazi na Obama ila ni ngumi mkononi. Wakati mwingine kwenye chama wanatakiwa wawepo watu wasema ovyo kwa kazi fulani ila tu wahakikishe wasivuke mpaka.

3D: Tupo pamoja sana. Ila kwa Tanzania bado nasisitiza kuwa tulikuwa tunatakiwa tuanze na kuwahukumu watoa Rushwa, takrima, kuchakachua kura nk ambazo huwa zinajulikana na kuna ushahidi wa waziwazi. Tukiangalia tu Igunga, tuliona Mkapa akigawia watu Wali wa Maharage. Na anasema waziwazi kuwa "TAKURURU, mtuache tuwape watu chakula...." ila nashangaa mbona leo haendi kupikia watu wa Igunga wali?

Billy Clinton, alikuwa na hatia ya waziwazi maana alidanganya akiwa kwenye KIAPO. Ila wenzetu wakaona tu apigwe faini na si kumuondoa madarakani. Nashukuru hili limeanza sasa maana watu watakuwa wanarekodiwa kwenye hotuba zao na mwisho wa siku wanapandishwa kizimbani.

Nakubaliana na nyie kuwa matusi hayatakiwi ila si kosa la kumfanya mtu aondolewe ubunge. Juzi Mwanza karibu Wabunge wauawe na waliofanya hivyo wanajulikana ila hadi leo hii kimya. Wangelikuwa ni Chadema na wakafungwa, kuna watu wangelikuja hapa na kutetea kuwa walivunja sheria. Haya ya Mwanza yapo mengi sana na ndipo sisi tunapata sana shaka kuwa kama Lema angelikuwa ni CCM na kutoa maneno hayo, wala asingelifanywa kitu. Hizi sheria za Tanzania zina macho kwa Wapinzan tu ila kwa CCM, zinaona giza (film ya Yomba Yomba).

Mwisho, Wapinzani kumbukeni kuwa mnapigana na CHAMPION na hivyo, kama hutamuweka chini (knock-out) basi hupati ushindi. Inatakiwa mpigane haswa na kuwa Wasafi kuzidi wao maana watawawinda kwa kila hali.

Tunaona hata usafi wa Mnyika na Tundu Lisu, nao wako mahakamani. Sijui huko itatumika sheria ipi na watu waje hapa kuitetea.
 
Na mm najiandaa kwenda kumshtaki lusinde kwa niaba ya Slaa, Mbowe, Nassari, na Lema!

hapana usiende kumshtaki Lusinde kwa niamba ya Slaa, Mbowe na Lema......kamshtaki Lusinde kwa kutoa lugha ya matusi kwenye ardhi yetu, mbele ya watoto wetu.shtaki kama mtanzania aliyekasirishwa na hili swala!!!

all the best
 
Tatizo tanzania kila kitu ni siasa hivyo hata wanataaluma maamuzi yao yanategemea upepo wa siasa kwa wakati huo....na hii yote imesababiswa na ccm kwa kuwalazisha watalamu wetu kufanya maamuzi kwa maslai yao.!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mie sijapata ushahidi wa matusi ya Lema, ila ya Lusinde nimeyasikia tena anatukana mbele ya watoto wa shule za msingi!! Isitoshe sheria ilihitaji uthibitisho, tena wa kina, maranyingine tusijifanye kuwa sisi ni safi tufuate vilivyo safi unafiki unakuja pale uma wenyewe hauna ule uthibitisho, kusikia fulani katukana basi ukahukumu na kuogopa kuitwa mnafiki. kama ndivyo hivyo tukichunguza sana kila mtu atakuanaongea lugha ya matusi, na kila mtu atakuwa mnafiki!!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
The Boss, siyo wote lazima wawe sawa. Kuna watu kama Rambo wanafanya kazi na Obama ila ni ngumi mkononi. Wakati mwingine kwenye chama wanatakiwa wawepo watu wasema ovyo kwa kazi fulani ila tu wahakikishe wasivuke mpaka.

3D: Tupo pamoja sana. Ila kwa Tanzania bado nasisitiza kuwa tulikuwa tunatakiwa tuanze na kuwahukumu watoa Rushwa, takrima, kuchakachua kura nk ambazo huwa zinajulikana na kuna ushahidi wa waziwazi. Tukiangalia tu Igunga, tuliona Mkapa akigawia watu Wali wa Maharage. Na anasema waziwazi kuwa "TAKURURU, mtuache tuwape watu chakula...." ila nashangaa mbona leo haendi kupikia watu wa Igunga wali?

Billy Clinton, alikuwa na hatia ya waziwazi maana alidanganya akiwa kwenye KIAPO. Ila wenzetu wakaona tu apigwe faini na si kumuondoa madarakani. Nashukuru hili limeanza sasa maana watu watakuwa wanarekodiwa kwenye hotuba zao na mwisho wa siku wanapandishwa kizimbani.

Nakubaliana na nyie kuwa matusi hayatakiwi ila si kosa la kumfanya mtu aondolewe ubunge. Juzi Mwanza karibu Wabunge wauawe na waliofanya hivyo wanajulikana ila hadi leo hii kimya. Wangelikuwa ni Chadema na wakafungwa, kuna watu wangelikuja hapa na kutetea kuwa walivunja sheria. Haya ya Mwanza yapo mengi sana na ndipo sisi tunapata sana shaka kuwa kama Lema angelikuwa ni CCM na kutoa maneno hayo, wala asingelifanywa kitu. Hizi sheria za Tanzania zina macho kwa Wapinzan tu ila kwa CCM, zinaona giza (film ya Yomba Yomba).

Mwisho, Wapinzani kumbukeni kuwa mnapigana na CHAMPION na hivyo, kama hutamuweka chini (knock-out) basi hupati ushindi. Inatakiwa mpigane haswa na kuwa Wasafi kuzidi wao maana watawawinda kwa kila hali.

Tunaona hata usafi wa Mnyika na Tundu Lisu, nao wako mahakamani. Sijui huko itatumika sheria ipi na watu waje hapa kuitetea.

adhabu ya matusi unataka iwe nini??

je hiyo adhabu ilikuwepo kwenye sheria kabla ya Lema?

Je tuna standard gani inayoonyesha tusi la namna gani liwe na hukumu gani??

kipimo cha utu wetu kinapimwa na wamarekani na taratibu zao??
 
Waberoya umeongea vizuri sana.

Mdee, Sugu, Lema nao ni watukanaji na wenye kutumia lugha mbovu mbovu kwa wapinzani wao.

Na kwa sisi kuwashangilia na hata kuwatukuza wakati mwengine kunaonyesha tu sisi Watanzania ni watu wa aina gani. Hatuna integrity.

Mtu kama Mdee kumwita Wassira Sokwe-mtu ni aibu........kwa misingi yote iliyopo ya kibinaadamu

Webby,
Tatizo ni Pro-Chadema wanataka tuchukizwe na matusi ya Lusinde halafu tufurahishwe na matusi ya Lema haiwezekani hata kidogo.

Mahakama imesema Lema alithibitika kutenda kosa la kutumia maneno yasiyostahili kwenye kampeni zake.

Ebu tujikumbushe maneno ya Lema "Dr Burian sio mwanamke mwaminifu aliyezaa nje na kupata mimba nje ya ndoa".

Hayo maneno ya Lema ni "Illegal Campaign" inatosha kutengua matokeo ya uchaguzi kwa mujibu wa kifungu 114 cha sheria ya uchaguzi inayozungumzia Illegal.

DU YOTE NAUNGA MKONO KWELI KUKU AKIHARISHA AAA ILA NI BATA TUUU

USHABIKI BWANA MTU WAKE AKIHARISHA AA KAJAMBA
 
Kuna tatizo kuu la msingi ambalo nisiposema dhamiri yangu itanihukumu na sitakaa kimya kwa sababu wengine wameamua kukaa kimya.

Jamii ya Tanzania iko kwenye ugonjwa mkubwa na tusipoudhibiti huu ugonjwa hakuna wa kutusaidia. Tunaiumiza jamii, tunaharibiu vizazi vijavyo kwa kisingizio cha mabadiliko!

Sera ya chadema si matusi!! Sera ya chadema ni mabadiliko, sijawahi kuona Slaa akitoa matusi ya nguoni, sijawahi kuona Mbowe akitoa matusi ya nguoni, wala sijawahi kuona Zito akitukana, these people they are still high in their positions na popular kwenye siasa na wanaaminika kwenye jamii kwa kuleta mabadiliko

Ila nimemsikia Mdee akitukana( personally nilimkataza) , nilimsikia Lema akitukana, tumeona Sugu akitukana mpaka kujirekodi!! Hawa ndio wabunge wetu, ndio tuliowapa dhamana ya kuongoza taifa letu kwa nafasi zao…ila wanatukana, wakitukana hawa ni sawa??

Nani kasema?

Kuna uwezekano mkubwa akina Mbowe, slaa hawawezi kuwadhibiti akina Lema, kwa sababu ya kuwaonea aibu!! Unapopagawa na siasa na kuona kila unachotukana kinashangiliwa, basi jamii nzima inakuwa imeoza! Msikilize Lusinde utaamini!

ILA; Ukiwa mpinzani lazima uangalie zile nafasi/chances/ opportunities ambazo adui yako anaweza kuzitumia kukuangamiza!

Kama CCM wametumia mahakama kumuondoa adui yao Lema, it is okay na wametumia karata yao vizuri sana.

Lakini kama si CCM na mahakama, je matusi yanakubaliwa katika jamii yetu??

Hivi Mdee, sugu, Lema na Lusinde tofauti yao ni nini??

Na sisi wataka mabadiliko , ukweli wa mioyo yetu na matusi uko wapi? Kuwa tutukane tu kwa sababu kwa kufanya hivyo ndio tunahimiza moto wa mabadiliko??

Matusi mangapi yanatukanwa humu ndani? Wanaotukana ni akina nani? Je wakipewa uongozi hawatatukana kwa sababu ni viongozi? Yaani uongozi una mechanism ya kuzuia matusi biologically? Matusi tumeyakubali, tunaishi nayo, tunalala nayo kila kona ya nchi yetu si kwa hao niliowataja, yako kila kona, kwenye madaladala, kwenye michezo name it!

Lema ameadhibiwa na mahakama, Lusinde ameadhibiwa na wananchi-ambao wengi wao wanatukana, mwisho wa siku wote ni watukanaji! Ikifika hatua tukaona Lema ni shujaa tunakuwa tumevua akili zetu na utu wetu na kuuweka kando na sisi……..tunaishi kinafiki , tuna post kinafiki kwani usafi na intergirty is not part of our life!!

In this case mahama iko clean..tena wanapongezana, hivi..juzi tu tumelia Lusinde anatukana-tukasema kila kona na kulaani, leo hii Lema anavuliwa ubunge kwa kutukana tunaona ubaya?? Kweli??

hujaacha tu kuandika pumba?
 
Rudieni uchaguzi tu, tuwaoneshe cha moto.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
The Boss, siyo wote lazima wawe sawa. Kuna watu kama Rambo wanafanya kazi na Obama ila ni ngumi mkononi. Wakati mwingine kwenye chama wanatakiwa wawepo watu wasema ovyo kwa kazi fulani ila tu wahakikishe wasivuke mpaka.

3D: Tupo pamoja sana. Ila kwa Tanzania ...............................

Ni vigumu kukubaliana kwa kila kitu, ikitokea hivyo huwa ni kwa matukio machache sana. Ulichoandika hapa ni moja ya matukio yatokeayo kwa uchache kwani nakubaliana nawe kwa ASILIMIA MIA MOJA, katika kila neno, sentensi na hata mpangilio wa kile ulichosema.

WELL SAID MKUU!!
 
Kuna tatizo kuu la msingi ambalo nisiposema dhamiri yangu itanihukumu na sitakaa kimya kwa sababu wengine wameamua kukaa kimya.

Jamii ya Tanzania iko kwenye ugonjwa mkubwa na tusipoudhibiti huu ugonjwa hakuna wa kutusaidia. Tunaiumiza jamii, tunaharibiu vizazi vijavyo kwa kisingizio cha mabadiliko!

Sera ya chadema si matusi!! Sera ya chadema ni mabadiliko, sijawahi kuona Slaa akitoa matusi ya nguoni, sijawahi kuona Mbowe akitoa matusi ya nguoni, wala sijawahi kuona Zito akitukana, these people they are still high in their positions na popular kwenye siasa na wanaaminika kwenye jamii kwa kuleta mabadiliko

Ila nimemsikia Mdee akitukana( personally nilimkataza) , nilimsikia Lema akitukana, tumeona Sugu akitukana mpaka kujirekodi!! Hawa ndio wabunge wetu, ndio tuliowapa dhamana ya kuongoza taifa letu kwa nafasi zao…ila wanatukana, wakitukana hawa ni sawa??

Nani kasema?

Kuna uwezekano mkubwa akina Mbowe, slaa hawawezi kuwadhibiti akina Lema, kwa sababu ya kuwaonea aibu!! Unapopagawa na siasa na kuona kila unachotukana kinashangiliwa, basi jamii nzima inakuwa imeoza! Msikilize Lusinde utaamini!

ILA; Ukiwa mpinzani lazima uangalie zile nafasi/chances/ opportunities ambazo adui yako anaweza kuzitumia kukuangamiza!

Kama CCM wametumia mahakama kumuondoa adui yao Lema, it is okay na wametumia karata yao vizuri sana.

Lakini kama si CCM na mahakama, je matusi yanakubaliwa katika jamii yetu??

Hivi Mdee, sugu, Lema na Lusinde tofauti yao ni nini??

Na sisi wataka mabadiliko , ukweli wa mioyo yetu na matusi uko wapi? Kuwa tutukane tu kwa sababu kwa kufanya hivyo ndio tunahimiza moto wa mabadiliko??

Matusi mangapi yanatukanwa humu ndani? Wanaotukana ni akina nani? Je wakipewa uongozi hawatatukana kwa sababu ni viongozi? Yaani uongozi una mechanism ya kuzuia matusi biologically? Matusi tumeyakubali, tunaishi nayo, tunalala nayo kila kona ya nchi yetu si kwa hao niliowataja, yako kila kona, kwenye madaladala, kwenye michezo name it!

Lema ameadhibiwa na mahakama, Lusinde ameadhibiwa na wananchi-ambao wengi wao wanatukana, mwisho wa siku wote ni watukanaji! Ikifika hatua tukaona Lema ni shujaa tunakuwa tumevua akili zetu na utu wetu na kuuweka kando na sisi……..tunaishi kinafiki , tuna post kinafiki kwani usafi na intergirty is not part of our life!!

In this case mahama iko clean..tena wanapongezana, hivi..juzi tu tumelia Lusinde anatukana-tukasema kila kona na kulaani, leo hii Lema anavuliwa ubunge kwa kutukana tunaona ubaya?? Kweli??
ni kweli kabisa m2 mzima
 
Waberoya, Mahakama haijamkomoa Lema na CDM,lakini imeikomoa serikali ili iandae uchaguzi mdogo,ambapo hadi mie nimekomolewa kwani na mimi pia ni kati ya serikali kwa mujibu wa Abraham Lincoln. Said Mecky Sadick(Dar RC),wakati wa kampeni Lindi mjini alitoa maneno machafu na ya kibaguzi dhidi Mbunge wa sasa kwa tiketi ya CUF Bw. BARUANI akisisitiza wananchi wasimchague ubunge kwa sababu ya Ualbino wake na akisisitiza kuwa albinism ni LAANA. Point ya msingi CCM wameshika MPINI wa kisu na wapinzani wameshika MAKALI,ndio maana lolote wanajiamulia kwa mabavu. SOURCE: The Guardian,Sunday,November,7,2010.
 
Tatizo ni Pro-Chadema
wanataka tuchukizwe na matusi ya Lusinde halafu tufurahishwe na matusi ya Lema haiwezekani hata kidogo.

Mimi ni Pro-CDM lakini sikubaliani na kauli za Lema.

Hayo maneno ya Lema ni "Illegal Campaign" inatosha kutengua matokeo ya uchaguzi kwa mujibu wa kifungu 114 cha sheria ya uchaguzi inayozungumzia Illegal.

Wadau wa sheria wanasema kosa alilotiwa hatiani Lema ni "Illegal Campain" ambalo kifungu husika ni 108 na si 114 (Illegal Practice) aliyosema Jaji.

DU YOTE NAUNGA MKONO KWELI KUKU AKIHARISHA AAA ILA NI BATA TUUU

CCM si bata tu bali Mabata yenye roho mbaya, mbona kesi za rushwa zinapigwa danadana? Soma post ya Sikonge hapo juu (No.68).
 
Back
Top Bottom