Matokeo kidato cha nne yamechakachuliwa

Kama kweli hii ni hatari kwa mstakabali wa taifa. Kama ni habari ya kubuniwa tutafakali.
 
Mnashangaza sana! mnailaumu serikali kwa sababu gani katika hili? siku hizi kwani kuna wanafunzi ? mwanafunzi wa kiume amevaa KATA K , mwanafunzi wa kike amechonga nyusi SKIRT IMEVALIWA KIUNONI ! kutwa kwenye internet cafee na kutwa kwenye facebook! mbona hamuulizi hayo? ukiuliza utaambiwa utandawazi ! kwa kweli Serikali si ya kulaumiwa hata kidogo ! labda uniambie vijijivi ambapo hakuna huduma kama mijini madawati na venginevo lakini haya pia yalikuwepo tokea enzi za Nyerere! tena afadhali hata sasa hivi tunawashukuru Vodacom na makampuni mengine kwa kufikisha vitu hivi karibu na jamii za vijijini! nadhani tukae chini wazazi tujiulize ni kwanini watoto wanafeli badala ya kuwatupia lawama seriali nadhani MNAIONEA!
Juzi nilikuwa sehemu hivi nikaona watoto wa shule fulani kama International school hivi ni shule ya siku nyingi ambayo inaheshimika sana! nikawaona mtoto wa kike ametoboa hereni tatu sikio moja, amesuka rasta, wamekaa na watoto wa kiume wakila kwenye mgahawa pale Regency Hospital ! nilisikitika sana kuona mandhari ya wale wanafunzi ! kwa kweli inasikitisha ! bidii ya wazazi inatakiwa sana katika hii generation wenyewe wanajiita .COM GENERATION !

Nilishawahi kusema hata kama wakifaulu Mungu atashangaa. Hakuna shule bila nidhamu. Watoto wengi hawana nidhamu ya shule. Wako busy na simu, movies, facebook na hakuna anaejali. si wazazi wala wao. Nasema tena watafeli tu, na ndio stahili zao. Sijui tunajenga taifa gani. Hakuna nidhamu ya shule. Kama serikali au yeyote atabadilisha matokeo wanamdanganya nani? Wanawadanganya watakaowapa maksi. Nadhani hata wakifeli wote wapewe wanachostahili. Call spade a spade. Tuwafundishe hawa vijana kwa kuwaonyesha ukweli.
 
sidhani kama mama Ndalichako anaweza fanya ujinga huu. By the way standardization ni moja ya njia za taaluma hii.
 
Tunashukuru sana kwa taarifa yako nzuri mkuu. Tunaomba uendelee kutujulisha kila litakaloendelea kutokea kutoka kwa hao wala nchi. Big up sana mkuu
 
Ukimya wangu humu jamvini ulinisogeza karibu na Wasahihishaji wa Mitihani ya Kidato cha nne.Wasahihishaji wamenidokeza kuwa kutokana na kufanya vibaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza Oktoba mwaka jana kuliko hata mwaka uliotangulia 2010,Serikali iliamua kufanya 'Standardization' ya kuua rasmi elimu ya Tanzania.Habari zilizonifikia zinasema kuwa Daraja D limehesabiwa kuanzia alama 15,C-35,B-55 na A-75 badala ya 21,41,61 na 81 inavyotakiwa kuwa kwa madaraja husika.Kulitokea mvutano wa wazi katika kikao hicho cha 'kustandardize'.Serikali imelenga kutangaza kuwa Matokeo ni mazuri na ufaulu umepanda.Inajiandaa kujisifu kwa takwimu.Baraza haliko tayari kwa hilo.Mvutano.Hii ndio sababu hasa ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.Mwenye macho haambiwi tazama.
Toa sababu nyingine lakini sio kuchelewa matokeo,matokeo huwa yanatoka wiki ya mwisho ya Januari au wiki ya kwanza ya Februari
 
Nilishawahi kusema hata kama wakifaulu Mungu atashangaa. Hakuna shule bila nidhamu. Watoto wengi hawana nidhamu ya shule. Wako busy na simu, movies, facebook na hakuna anaejali. si wazazi wala wao. Nasema tena watafeli tu, na ndio stahili zao. Sijui tunajenga taifa gani. Hakuna nidhamu ya shule. Kama serikali au yeyote atabadilisha matokeo wanamdanganya nani? Wanawadanganya watakaowapa maksi. Nadhani hata wakifeli wote wapewe wanachostahili. Call spade a spade. Tuwafundishe hawa vijana kwa kuwaonyesha ukweli.

NGOJA NI KAZIE KABISAAAA: WATAFELI SAAAAAAAAAAAANA MPAKA AIBU..aliekaribu na mtoto wa secondari amuulize sientific name yake na sio ya human being..we muulize yake..,kama ataweza.!
 
Ukimya wangu humu jamvini ulinisogeza karibu na Wasahihishaji wa Mitihani ya Kidato cha nne.Wasahihishaji wamenidokeza kuwa kutokana na kufanya vibaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza Oktoba mwaka jana kuliko hata mwaka uliotangulia 2010,Serikali iliamua kufanya 'Standardization' ya kuua rasmi elimu ya Tanzania.Habari zilizonifikia zinasema kuwa Daraja D limehesabiwa kuanzia alama 15,C-35,B-55 na A-75 badala ya 21,41,61 na 81 inavyotakiwa kuwa kwa madaraja husika.Kulitokea mvutano wa wazi katika kikao hicho cha 'kustandardize'.Serikali imelenga kutangaza kuwa Matokeo ni mazuri na ufaulu umepanda.Inajiandaa kujisifu kwa takwimu.Baraza haliko tayari kwa hilo.Mvutano.Hii ndio sababu hasa ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.Mwenye macho haambiwi tazama.

Hii ndiyo Tanzania nchi inayokumbatha mabaya na haifuati sheria wala katiba
 
Hicho kitu siyo kigeni, sema namna ya kufanya standardization kama wamekiuka taratibu ndiyo itakuwa hovyo kabisa!! watakuwa wanaiaibisha taaluma ya ualimu. Hakunaga kitu kama kushusha alama ili watu wafaulu, watu wanafanya calculation kama standard deviation & Variance etc ili kuamua mwenye nyingi ashuke au apande kwa kiasi gani.
 
acha kudanganya watu na taarifa zisizo rasmi. Mara umekaa kimya sana humu ulikuwa unafanya ufuatiliaji wa matokeo. Wewe mwenyewe hata posts zenyewe chache halafu unadanganya kwamba ulikuwa kimya.

Hata kama wamestandardize matokeo, kwani nani kakuambia ni vibaya kufanya hivyo? Si mara zote standardization inakuwa na negative impacts kwa wahusika. Ikifanywa fairly na kwa malengo/makusudi sahihi wala haina madhara. Labda tu kwasababu haujui system ya elimu ilivyo kuanzia primary - vyuo vikuu na si tu kwamba standardization inafanyika tu tanzania kama ipo, isipokuwa inaweza ikafanywa popote lkn kitu kikubwa ni nini sababu za kufanya hivyo.

Hivyo usipaze sauti sana kama ni kitu kibaya ktk jamii. Inakuwa mbaya pale ambapo sababu hasa za kufanya hivyo si za msingi au haiko fair kwa wote wanaohusika katika hilo.

Mbona umekuwa mkali sana na mwenye kumwaga shutuma ukitoka mapovu? Kama ni jambo zuri na la kawaida, wanabishana nini?

RED: Kustandadaiz matokeo ni janja ya kuficha uozo wa kushuka kwa kiwango cha ufundishaji, sasa sijui ni lipi zuri unaloliona hapo wewe mwenzetu mwenye akili sana. (Should we CHANGE the FACE or FACE the CHANGE?) Tunataka kumdanganya nani? Wahitimu wa kustandadaiz wakiwa madaktari, tutawalaumu na wao wakistandadaiz dozi kwa wagonjwa? Hapa nakupa 0%.

BLUE: Usiniambie uongo ukifanywa fairly inakuwa ukweli. Acha nikusaidie hili. Ikiwa wanafunzi wote walikosea kufuata maelekezo lkn majibu ya mtihani yakawa sawa, ningeunga mkono jambo hili kwani yawezekana kulikuwa na kosa ktk maandalizi na si kwamba uelewa wa wanafunzi ni mdogo. Lkn inapotokea 28/100 wamefaulu, basi hilo ni tatizo la ufundishaji na tunatakiwa tukabiliane nalo na si kudanganya umma.

GREEN:
Kumbe unaua kuwa inakuwa mbaya ikiwa sababu za kufanya hivyo sio za msingi, sasa juu ya nini ukawa mkali hivyo? Mbona mimi sikuelewi unasimamia wapi?

What I think of YOU:
You are pathetic. Nafikiri tumeona kwa kipindi hiki jinsi serikali inavyofanya mambo yake kimtindo kwa kujaribu kuwazuga wananchi. Nakupa mifano:
1. Mgomo wa madaktari ulipoanza, uongozi wa hospitali ya Muhimbili (kwa siku mbili za kwanza) waliwaambia waandishi wa habari kuwa mambo pale hospitali ni shwari na huduma zinaendelea kama kawaida. Nafikiri sasa majibu unayo kama ni shwari au si shwari.
2. Kila leo utasikia kutoka kwa wazungu na vibaraka wao ambao ndio wanatuongoza kuwa pato la Taifa limepanda na maisha ya mtanzania yameboreka. Lkn ukiingia mtaani, mambo ni tofauti. Na hata huo uchumi wa nchi ni kichekesho. Lkn serikali inapopongezwa na wazungu wanaojiandaa kuomba vibali vya kuchimba madini yetu, watu kama wewe mnajiunga kushangilia ilhali maisha yenu yanaendelea kuwa mabaya.

Kwa kifupi, watu wa namna yako ukweli hauna maana kwao badala yake unapenda maneno matamu. Ungefurahi kuambiwa mwanao kapata Division I ilhali ni mjinga wa mwisho kwa jinsi ambavyo ulikuwa huna time nae akiwa shuleni. Unanichosha bure, endelea kuishi kwa takwimu za serikali.
 
Hicho kitu siyo kigeni, sema namna ya kufanya standardization kama wamekiuka taratibu ndiyo itakuwa hovyo kabisa!! watakuwa wanaiaibisha taaluma ya ualimu. Hakunaga kitu kama kushusha alama ili watu wafaulu, watu wanafanya calculation kama standard deviation & Variance etc ili kuamua mwenye nyingi ashuke au apande kwa kiasi gani.
Mmmmh! Kumshusha mwenye nyingi hiyo sijawahi sikia!
 
Mbona umekuwa mkali sana na mwenye kumwaga shutuma ukitoka mapovu? Kama ni jambo zuri na la kawaida, wanabishana nini?

RED: Kustandadaiz matokeo ni janja ya kuficha uozo wa kushuka kwa kiwango cha ufundishaji, sasa sijui ni lipi zuri unaloliona hapo wewe mwenzetu mwenye akili sana. (Should we CHANGE the FACE or FACE the CHANGE?) Tunataka kumdanganya nani? Wahitimu wa kustandadaiz wakiwa madaktari, tutawalaumu na wao wakistandadaiz dozi kwa wagonjwa? Hapa nakupa 0%.

BLUE: Usiniambie uongo ukifanywa fairly inakuwa ukweli. Acha nikusaidie hili. Ikiwa wanafunzi wote walikosea kufuata maelekezo lkn majibu ya mtihani yakawa sawa, ningeunga mkono jambo hili kwani yawezekana kulikuwa na kosa ktk maandalizi na si kwamba uelewa wa wanafunzi ni mdogo. Lkn inapotokea 28/100 wamefaulu, basi hilo ni tatizo la ufundishaji na tunatakiwa tukabiliane nalo na si kudanganya umma.

GREEN:
Kumbe unaua kuwa inakuwa mbaya ikiwa sababu za kufanya hivyo sio za msingi, sasa juu ya nini ukawa mkali hivyo? Mbona mimi sikuelewi unasimamia wapi?

What I think of YOU:
You are pathetic. Nafikiri tumeona kwa kipindi hiki jinsi serikali inavyofanya mambo yake kimtindo kwa kujaribu kuwazuga wananchi. Nakupa mifano:
1. Mgomo wa madaktari ulipoanza, uongozi wa hospitali ya Muhimbili (kwa siku mbili za kwanza) waliwaambia waandishi wa habari kuwa mambo pale hospitali ni shwari na huduma zinaendelea kama kawaida. Nafikiri sasa majibu unayo kama ni shwari au si shwari.
2. Kila leo utasikia kutoka kwa wazungu na vibaraka wao ambao ndio wanatuongoza kuwa pato la Taifa limepanda na maisha ya mtanzania yameboreka. Lkn ukiingia mtaani, mambo ni tofauti. Na hata huo uchumi wa nchi ni kichekesho. Lkn serikali inapopongezwa na wazungu wanaojiandaa kuomba vibali vya kuchimba madini yetu, watu kama wewe mnajiunga kushangilia ilhali maisha yenu yanaendelea kuwa mabaya.

Kwa kifupi, watu wa namna yako ukweli hauna maana kwao badala yake unapenda maneno matamu. Ungefurahi kuambiwa mwanao kapata Division I ilhali ni mjinga wa mwisho kwa jinsi ambavyo ulikuwa huna time nae akiwa shuleni. Unanichosha bure, endelea kuishi kwa takwimu za serikali.

Poin noted.
Chukua soda hapo dukani kwa Mangi,
mwambie aandike kwenye bili ya Mphamvu.
Sawasawa?
 
Back
Top Bottom