Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,850
- 155,799
CCM oyeeeee
Ukimya wangu humu jamvini ulinisogeza karibu na Wasahihishaji wa Mitihani ya Kidato cha nne.Wasahihishaji wamenidokeza kuwa kutokana na kufanya vibaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza Oktoba mwaka jana kuliko hata mwaka uliotangulia 2010,Serikali iliamua kufanya 'Standardization' ya kuua rasmi elimu ya Tanzania.Habari zilizonifikia zinasema kuwa Daraja D limehesabiwa kuanzia alama 15,C-35,B-55 na A-75 badala ya 21,41,61 na 81 inavyotakiwa kuwa kwa madaraja husika.Kulitokea mvutano wa wazi katika kikao hicho cha 'kustandardize'.Serikali imelenga kutangaza kuwa Matokeo ni mazuri na ufaulu umepanda.Inajiandaa kujisifu kwa takwimu.Baraza haliko tayari kwa hilo.Mvutano.Hii ndio sababu hasa ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.Mwenye macho haambiwi tazama.