Matokeo kidato cha nne yamechakachuliwa

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ukimya wangu humu jamvini ulinisogeza karibu na Wasahihishaji wa Mitihani ya Kidato cha nne.Wasahihishaji wamenidokeza kuwa kutokana na kufanya vibaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza Oktoba mwaka jana kuliko hata mwaka uliotangulia 2010,Serikali iliamua kufanya 'Standardization' ya kuua rasmi elimu ya Tanzania.Habari zilizonifikia zinasema kuwa Daraja D limehesabiwa kuanzia alama 15,C-35,B-55 na A-75 badala ya 21,41,61 na 81 inavyotakiwa kuwa kwa madaraja husika.Kulitokea mvutano wa wazi katika kikao hicho cha 'kustandardize'.Serikali imelenga kutangaza kuwa Matokeo ni mazuri na ufaulu umepanda.Inajiandaa kujisifu kwa takwimu.Baraza haliko tayari kwa hilo.Mvutano.Hii ndio sababu hasa ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.Mwenye macho haambiwi tazama.
 
Dr.Joyce Ndalichako,Katibu Mtendaji wa NECTA ameonyesha dhahiri kuwa hakubaliani na kutangazwa kwa matokeo yaliyopangwa kwenye chumba cha mkutano.Jamani kwa hali hii tutafika kweli?
 
Serikali magamba wanatafta point angalau wanaweza ongea wananchi wakafurah kutokana ukali wa maisha unaomuandama mwananchi...but you are too late tumeishaelimika tayari!..Mlivyo fanya hivyo ingelikuwa unit za umeme kidogo tungelielewana!
 
Kaka ukistaajabu ya musa utazima kuona samsoni akivunja miamba.. Nilicho sikia mimi ni kwamba eti kwa kuwa shule za kata ndio hasa hufanya vibaya! Hzo ndizo zimelengwa kufanyiwa hyo adjustment ili serikali waonekane wame upgrade ktk kusimamia muamko wa elim. Ndo taifa letu jamani. Litawaliwalo na watu wazima waigizaji na ubishow
 
ukimya wangu humu jamvini ulinisogeza karibu na wasahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne.wasahihishaji wamenidokeza kuwa kutokana na kufanya vibaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza oktoba mwaka jana kuliko hata mwaka uliotangulia 2010,serikali iliamua kufanya 'standardization' ya kuua rasmi elimu ya tanzania.habari zilizonifikia zinasema kuwa daraja d limehesabiwa kuanzia alama 15,c-35,b-55 na a-75 badala ya 21,41,61 na 81 inavyotakiwa kuwa kwa madaraja husika.kulitokea mvutano wa wazi katika kikao hicho cha 'kustandardize'.serikali imelenga kutangaza kuwa matokeo ni mazuri na ufaulu umepanda.inajiandaa kujisifu kwa takwimu.baraza haliko tayari kwa hilo.mvutano.hii ndio sababu hasa ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.mwenye macho haambiwi tazama.

acha kudanganya watu na taarifa zisizo rasmi. Mara umekaa kimya sana humu ulikuwa unafanya ufuatiliaji wa matokeo. Wewe mwenyewe hata posts zenyewe chache halafu unadanganya kwamba ulikuwa kimya.

Hata kama wamestandardize matokeo, kwani nani kakuambia ni vibaya kufanya hivyo? Si mara zote standardization inakuwa na negative impacts kwa wahusika. Ikifanywa fairly na kwa malengo/makusudi sahihi wala haina madhara. Labda tu kwasababu haujui system ya elimu ilivyo kuanzia primary - vyuo vikuu na si tu kwamba standardization inafanyika tu tanzania kama ipo, isipokuwa inaweza ikafanywa popote lkn kitu kikubwa ni nini sababu za kufanya hivyo.

Hivyo usipaze sauti sana kama ni kitu kibaya ktk jamii. Inakuwa mbaya pale ambapo sababu hasa za kufanya hivyo si za msingi au haiko fair kwa wote wanaohusika katika hilo.
 
Hilo wafanyalo wadhani ni kufurahisha watanzania waliochoka na mfumko wa bei na ugumu wa maisha unaosababishwa na uroho na ufisadi!

Hayo ni maandalizi hasira nyingine kwa watanzania!
 
wacha kudanganya kama kufeli watu wamefeli lakini siku zote matokeo yanatoka mwezi wa pili au mwisho wa mwezi
 
Very..... Gud necta and keep it up" 2nafurahi bkoz 4m5 hyo lacn jueni sisi mnaotusaidia na sawa na kumsaidia nyoka so kama mnabisha habari 2taionesha serikali yenu ya magamba(CCM)
 
upumbavu mwingine unaandaliwa.serikali chovu sana hii! Shwaini!

Mnashangaza sana! mnailaumu serikali kwa sababu gani katika hili? siku hizi kwani kuna wanafunzi ? mwanafunzi wa kiume amevaa KATA K , mwanafunzi wa kike amechonga nyusi SKIRT IMEVALIWA KIUNONI ! kutwa kwenye internet cafee na kutwa kwenye facebook! mbona hamuulizi hayo? ukiuliza utaambiwa utandawazi ! kwa kweli Serikali si ya kulaumiwa hata kidogo ! labda uniambie vijijivi ambapo hakuna huduma kama mijini madawati na venginevo lakini haya pia yalikuwepo tokea enzi za Nyerere! tena afadhali hata sasa hivi tunawashukuru Vodacom na makampuni mengine kwa kufikisha vitu hivi karibu na jamii za vijijini! nadhani tukae chini wazazi tujiulize ni kwanini watoto wanafeli badala ya kuwatupia lawama seriali nadhani MNAIONEA!
Juzi nilikuwa sehemu hivi nikaona watoto wa shule fulani kama International school hivi ni shule ya siku nyingi ambayo inaheshimika sana! nikawaona mtoto wa kike ametoboa hereni tatu sikio moja, amesuka rasta, wamekaa na watoto wa kiume wakila kwenye mgahawa pale Regency Hospital ! nilisikitika sana kuona mandhari ya wale wanafunzi ! kwa kweli inasikitisha ! bidii ya wazazi inatakiwa sana katika hii generation wenyewe wanajiita .COM GENERATION !
 
Hii inasikitisha sana na inabashiri tunakoelekea ni kubaya zaidi ya tulipo kielimu sijui kama tutafika salama. Dunia kizingiti yataka mkono wa Mungu kuvuka
 
Kuhusu kuchelewa mi nakataa kwani kila mwaka huwa yanatoka mwishoni wa mwezi huu au mwanzoni wa mwezi wa pili....na kama kweli wamefanya hivyo ELIMU ye2 ndo inazidi kuporomoka.
 
Back
Top Bottom