Matokeo Kidato cha Nne 2014 yametoka: Sekondari ya Kaizirege yaongoza

Kupata Matokeo Haya,

Bofya hapa

Jiridhishe kwa kutembelea NECTA

Siku hizi hakuna Divisions, na tafsiri ya GPA ni hii hapa kwenye jedwali, Distinction ndio kama Division I ukipenda.

http://www.necta.go.tz/files/utaratibu_wa_kutunuku.pdf
GPA
DISTINCTION
MERIT
CREDIT
PASS
FAIL
3.6 - 5.0
2.6 - 3.5
1.6 - 2.5
0.3 - 1.5
0.0 - 0.2

Qualifying Test (QT): Tembelea HAPA


UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA
KUTUMIA MFUMO WA GPA


1. Mfumo wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average - GPA)

Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake.
GPA hutokana na masomo saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo matatu (3) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03 kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.

Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.

Utaanza kutumika kupanga madaraja ya ufaulu katika Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2014 na Kidato cha Sita (ACSEE) 2015.

2. Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa
Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu (3) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni ifuatayo:

GPA =
Jumla ya Uzito wa gredi za masomo
------------------------------------------------
Idadi ya Masomo

Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D.

3. Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo wa GPA
Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA) kutakuwa na madaraja manne ambayo ni Distinction, Merit, Credit na Pass.

Daraja la juu la ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass kama ilivyoainishwa katika Jedwali lifuatalo:
attachment.php

Mfano; Mtihani wa Kidato cha Nne, mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili (B), English (C), Physics (C), Chemistry (C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo saba aliyofanya vizuri.

Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07), Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la Merit. Katika Mtihani wa Kidato cha Sita mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction.

4. Manufaa ya kutumia Mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA);
Kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa aina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia Elimu ya Msingi hadi Elimu ya Juu;

Matokeo yaliyo katika mfumo wa wastani wa pointi kwenye cheti yatarahisisha kazi ya udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika ngazi za juu za mafunzo na Mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ni rahisi kueleweka kwa wadau wa kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na GPA kubwa ndiye aliye na matokeo mazuri kuliko aliye na GPA ndogo.

Maelezo zaidi kuhusu GPA yanapatikana katika tovuti ya Baraza la Mitihani (www.necta.go.tz).

=====================




Wale waliokuwa wakitokwa povu na kuandamana ili Dr. ndalichako aondoke NECTA, vipi safari hii wamepata marks za bure au bado hawajasaidika!
 
mikagati,

Hakulipia ada ya mtihani......hiyo ni changamoto, hivyo sasa hivi atatakiwa kulipa ada ikiambatana na adhabu ambayo jumla yake ni Sh. 95,000.00 ( http://necta.go.tz/Documents/Results/FOMU_YA_MATOKEO.pdf) .

Wakati angelipa katika muda husika ingekuwa kama inavyo oneshwa hapa chini.

Registration Fees

Type of ExaminationRegistration Fees
Normal RegistrationLate Registration With Penalty
Certificate of Primary Examination
(English Medium)
TZS. 15,000N/A
Qualifying TestTZS. 30,000TZS. 40,000
Certificate of Secondary Education ExaminationTZS. 50,000TZS. 65,000
Advanced Certificate of Secondary School ExaminationTZS. 50,000TZS. 65,000
Grade A Teacher Certificate ExaminationTZS. 50,000TZS. 65,000
Diploma in Secondary Education ExaminationTZS. 50,000TZS. 65,000

NOTE: The above fees are applicable for the specified dates in the registration periods.

Source: http://www.necta.go.tz/registration#fees


Description of "Star Codes" Used by NECTA in Examination Results


  • * S==> Results suspended pending clarification of observed anomalies either in candidates' entry details, involvement in cases of irregularities or misconduct in the examination.Results suspended due to centers or schools' failing to meet registration requirements (i.e. centers with less than 35 candidates).



  • * E==> Results withheld, pending proof of candidates' payment of requisite Examination fees.



  • * I==>INCOMPLETE Results due to candidates' missing Continous Assessment (CA) scores in all subjects offered.



  • I ==>Incomplete results due to candidates' missing Continous Assessment(CA) scores in one or more subjects offered but not all.



  • * W ==>Results withheld/nullified or cancelled due to proven candidate's involvement in cases of dishonesty or irregularities before, during or after the examinations.



  • * T ==>Results suspended due to candidates' attempting one or more subjects not registered for (pirate candidate).



  • ABS ==>Candidate missed to take the Exam.



  • FLD ==>Candidate failed the Exam.



  • X ==>Candidate did not appear to take the exam for the particular registered subject.
 
Last edited by a moderator:
Mbona haya matokeo yako biased kidini inakuwaje top 10 candidates nzima wajae makafiri, hata shule top 10 wamejaa makafiri, lakini shule worse zote zinatokea maeneo yenye waislam wengi, jamani waislam wenzangu tusikubali MFUMOKRISTO utatumaliza

Pigeni kitabu, wakristo sie tunaamini pia elimu dunia ni muhimu ili kuishi kwenye hii dunia ngumu. Kama mnategemea miujiza kufaulu bila maandalizi imekula kwenu na mtaendelea kua wa mwisho,

kwanza hizo islamic seminaries zenu wanakomalia sana itikadi badala ya mtaala wa elimu asa mtaongozaje sasa. Njelekela Islamic seminary wametuaibisha Kigoma
 
Well...

ungetoa japo mfano wa mwanafunzi mmoja aliyeonewa...


Mbona haya matokeo yako biased kidini inakuwaje top 10 candidates nzima wajae makafiri, hata shule top 10 wamejaa makafiri, lakini shule worse zote zinatokea maeneo yenye waislam wengi,

jamani waislam wenzangu tusikubali MFUMOKRISTO utatumaliza
 
Pigeni kitabu, wakristo sie tunaamini pia elimu dunia ni muhimu ili kuishi kwenye hii dunia ngumu. Kama mnategemea miujiza kufaulu bila maandalizi imekula kwenu na mtaendelea kua wa mwisho,

kwanza hizo islamic seminaries zenu wanakomalia sana itikadi badala ya mtaala wa elimu asa mtaongozaje sasa. Njelekela Islamic seminary wametuaibisha Kigoma

Mkuu Niko sofya hapa sokoni njoo ule tano.
 
Kumbe Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ndivyo walivyofanya hivi.......wametumia mfumo wa GPA yan Grade Point Average kwahiyo mtahiniwa mwenye maksi nying ndio aliye faulu kwani A=5 ,B+=4,B-=3,C=2,D=1,E=0.5,F=0 kwahiyo wanaangalia masom saba 7 uliyoyafaulu wanajumlish then wanagawanya kwa idadi itakayopatkana ndio GPA ya mtahniwa.

Mfano Biology B, Chemistry C, History C, Kiswahili B, English B, Mathematics C, Civics B, Kwahiyo ikichukuliwa idadi ikagawanywa kwa 7 18/7 mtahniwa anakuwa na GPA ya 2.5 ambayo ni credit!

Wenye uelewa zaidi ya huu naomba tushirikiane kuelewesha wadogo zetu na wale wasioelewa.

Wengi wanalalamika kuwa wakiulizwa na wazazi wao wanashindwa kuwaelewesha so kazi kwenu.

Asante.
 
Mbunge mmoja kapost hii kitu, nawe itafakari ili upate, mwelekeo:

ila matokeo ya kidato cha nne ni uozo mtupu. People are too clever,Matokeo yametolewa kwa mfumo wa GPA ambazo watahiniwa/wahitimu wenyewe hawawezi kuzichanganua ili kujua GPA husika inamaanisha nn, na wameenda mbali zaidi kwa kutoa GPA zisizofanana hata kidogo na zile za vyuo ili hata kaka zao, dada zao au wazazi wa hao wahitimu wasiweze kuzichanganua.
Walisema madaraja yatakua hivi...
0.0-0.1 Fail
0.2-1.5 Pass
1.6-2.5 Credit
2.6-3.5 Merit
3.6-5 Distinction
Kutokana na zile pass ambazo mtu anakua amepata kwenye somo husika, kwa kufuata mtiririko huu ufuatao...
A>>> 75 - 100
B+>> 60 - 74
B>>> 50- 59
C>>> 40 - 49
D>>> 30 - 39
E>>> 20 - 29
F>>> 0 - 19
Kwa maana hiyo utapata ukipata marks kulingana na grade hizo utakua umeangukia kwenye mojawapo ya alama hizi...
A=5
B+=4
B=3
C=2
D=1
E=0.5
F=0
Lakini tatizo bado lipo, kwa wale wataalamu wa kukokotoa wakijaribu kutumia alama hizo kukokotoa matokeo ya mtu wanakuta alichoandikiwa kama ni Pass au distinction hakifanani na ukokotozi sahihi, kwa mfano...
Mtu aliyepata
CIVICS - C
HIST - C
GEO - C
KISWA - B
ENGL - B
PHY - B
CHEM - B
BIO - B
MATH - D
Ukikokotoa kulingana na mfumo wao na grade zao zilivyopangwa unapata 2.44 ambayo ni credit, ila wao wanamuandikia 2.7 ambayo ni Merit. Kuna tatizo hapa.
Nadhani waTz tumekua wajinga sana, hauwezi kumpa mtu matokea ambayo hata yy hayaelewi.

ELIMU NI BURE
 
GPA inakokotolewa kwa kuangalia masomo saba aliyofaulu vizuri sio yote.

Soma hii link hapa chini, mbona vitu vingine mnatupia lawama ambazo hazina msingi, namna ya ku-calculate GPA imewekwa kwenye website ya NECTA

http://www.necta.go.tz/files/utaratibu_wa_kutunuku.pdf

Hivyo basi kwa alama ulizoweka hapa ana B tano na C mbili (masomo saba aliyofaulu vizuri)

GPA = ((5 x 3) + (2 x 2))/7 = 19/7 = 2.71 = 2.7

Kuweni na objectivity vitu vingine viko wazi ila ukitanguliza chuki bila kufuatilia hata kidogo ni kwanini inakuwa hivyo utakuwa huwezi kuelewa.


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...yametoka-sekondari-ya-kaizirege-yaongoza.html

Mbunge mmoja kapost hii kitu, nawe itafakari ili upate, mwelekeo:

ila matokeo ya kidato cha nne ni uozo mtupu. People are too clever,Matokeo yametolewa kwa mfumo wa GPA ambazo watahiniwa/wahitimu wenyewe hawawezi kuzichanganua ili kujua GPA husika inamaanisha nn, na wameenda mbali zaidi kwa kutoa GPA zisizofanana hata kidogo na zile za vyuo ili hata kaka zao, dada zao au wazazi wa hao wahitimu wasiweze kuzichanganua.
Walisema madaraja yatakua hivi...
0.0-0.1 Fail
0.2-1.5 Pass
1.6-2.5 Credit
2.6-3.5 Merit
3.6-5 Distinction
Kutokana na zile pass ambazo mtu anakua amepata kwenye somo husika, kwa kufuata mtiririko huu ufuatao...
A>>> 75 - 100
B+>> 60 - 74
B>>> 50- 59
C>>> 40 - 49
D>>> 30 - 39
E>>> 20 - 29
F>>> 0 - 19
Kwa maana hiyo utapata ukipata marks kulingana na grade hizo utakua umeangukia kwenye mojawapo ya alama hizi...
A=5
B+=4
B=3
C=2
D=1
E=0.5
F=0
Lakini tatizo bado lipo, kwa wale wataalamu wa kukokotoa wakijaribu kutumia alama hizo kukokotoa matokeo ya mtu wanakuta alichoandikiwa kama ni Pass au distinction hakifanani na ukokotozi sahihi, kwa mfano...
Mtu aliyepata
CIVICS - C
HIST - C
GEO - C
KISWA - B
ENGL - B
PHY - B
CHEM - B
BIO - B
MATH - D
Ukikokotoa kulingana na mfumo wao na grade zao zilivyopangwa unapata 2.44 ambayo ni credit, ila wao wanamuandikia 2.7 ambayo ni Merit. Kuna tatizo hapa.
Nadhani waTz tumekua wajinga sana, hauwezi kumpa mtu matokea ambayo hata yy hayaelewi.

ELIMU NI BURE
 
na hivi hesabu sijuijui yani napatashida sana kuelewa huu uzi embu fafanueni kwa maneno matupu basi
 
Back
Top Bottom