Masoud Kipanya na kifo cha imani ya msalaba

Kutokana na imani yake, sidhani kama ana sifa ya kukosoa imani ya watu wengine. So kwa upande wangu nimechagua kumpuuza. Maana ameingilia mambo yasiyomhusu.
Very true iwe kweli au uongo mambo ya Kanisa hayamuhusu masoud kwa sababu ni muislam hajui chochote kuhusu ukristo kwa hiyo alitakiwa apite kule kimya kimya
 
Massoud Kipanya anatukosea wakristo. Yeye ni Muslim. Bible inasema, ya kaisari mwachie kaisari. Ndio mkuu wa KKT alidhibitisha. Kuja na katuni kama hiyo ni kwenda kunyume na biblia. Wakristo wote wanaohijua kweli huwa hawapambani na kaisari. Kipanya kabla ya kutoa katuni awaulize wakristo wa kweli.
Ina maana Desmond tutu, Martin Luther king Jr nk. hawakuwa wakristu? KKKT imetawaliwa na tamaa ya mali na madaraka
 
Inaonekana humfuatilii Masoud Kipanya na katuni zake. January 15 aliposti hii?
MASOUD JANUARY 15.jpg
 
Massoud Kipanya anatukosea wakristo. Yeye ni Muslim. Bible inasema, ya kaisari mwachie kaisari. Ndio mkuu wa KKT alidhibitisha. Kuja na katuni kama hiyo ni kwenda kunyume na biblia. Wakristo wote wanaohijua kweli huwa hawapambani na kaisari. Kipanya kabla ya kutoa katuni awaulize wakristo wa kweli.
wewe mfia dini mchana wa leo umekula?
 
Hapa masoud haeleweki kwa jamii ya kikristo sababu yeye ni muislam, wapi na wapi na imani ya msalaba? Habari ya msalaba waachiwe wanaohusika na imani hiyo kama imezama au iko hai
 
Hicho kibonzo kingekuwa kinahusu upande wa pili halafu kikawa kimechorwa na Mgalatia sasa, yaani muda huu watoto wa nyumba ndogo ya Ibrahim mama yao akiwa Hajra wangeshaingia barabarani wakiandama wakidai kwamba mtume kadhalilishwa.
 
Katuni ya kipanya haipo kwa KKKT kama wengi wanavyodhani bali ni ujumbe namna miradi aliyoiacha Magufuli inavyosuasua na mingine imekufa kabisa
 
Hicho kibonzo kingekuwa kinahusu upande wa pili halafu kikawa kimechorwa na Mgalatia sasa, yaani muda huu watoto wa nyumba ndogo ya Ibrahim mama yao akiwa Hajra wangeshaingia barabarani wakiandama wakidai kwamba mtume kadhalilishwa.
Kwa nini mnapenda kurudia rudia hayo maneno? Inakuwa kama watanzania na uoga wa kufanya maandamano.
 
Anamaanisha magari ya mwendo kasi UDART
Mkuu hata mimi nimepata tafsiri kama yako kupitia kibonzo hicho.

Ni kweli hapo rangi ya basi hilo kubwa la bluu ni dhahiri kuwa shirika la UDART ni kama lipo nusu ya kuelekea kuzikwa kwake rasmi. Safari yake ya mwisho kuelekea kuzikwa kaburini ni kama vile imefikia nusu.

Kibonzo hiki kinaonyesha shimo la kaburi na huku msalaba ukitumika tu kama alama maarufu inayowekwa kaburini mara baada ya kifo na kuzikwa rasmi kwa mpendwa ndugu yetu.

Kutokuwepo kwa waombolezaji na wazikaji hapo kaburini, hii ni kutokana na shirika kutelekezwa na serikali. Hivyo marehemu aliachwa ajifie yeye mwenyewe na hata sasa anapoelekea safari yake ya mwisho kaburini ni kama hakuna anayeangaika naye.
 
Back
Top Bottom