Mashindano ya U-miss TZ!

Kiukweli hayo mashindano huwadhalilisha sana kina dada,nikiangalia jinsi wanavyojinadi kwa kubenjua viuno vyao kwa mbwembwe huwa nacheka sana.
 
Cha kushangaza sana,eti mratibu wa mashindano haya ni AL-HAJJ,anaitwa al-hajj Hashim Lundenga.Mufti Simba anamwangalia al-hajj huyu na wala hajawahi kumuita Bakwata japo kuja kumpa nasaha njema tu sisemi kumuadhibu,lakini akiwahiwa kutangaza mwezi na wenzake ugomvi mkubwa kweli mpaka anakusanya waandishi wa habari na TBC anafika kuwaeleza kuwa yeye peke yake ndio mwenye mamlaka ya kutangaza mwezi.Haya ya Lundenga alhaji kaziba macho na masikio kana kwamba hayamuhusu.

Huyo si kawekwa kikaragosi tu kinaganga njaa, wenyewe ni wahindi, na hakuna siri.
 
Back
Top Bottom