Mroojr
Member
- Nov 15, 2010
- 65
- 8
Moja ya mada nzuri za kujadili na kuzitolea maoni ni kama hii.Kiukweli mzee washiriki wote ni wana dini zao,siku hizi kila mtu ana dini yake.Sipaswi kuwalaum sana washiriki pengine hawajafikishiwa vizuri ubaya wa jambo lenyewe na viongozi wao wa dini.Kwa upande 1 mimi naweza kuwalaumu hata viongozi wa dini,wamebeba majukumu yasiyo yakwao zaidi na kusahau majukumu hasa ya kwao.We angalia kama kina Mufti simba anagombania wadhifa wakutangaza mwezi jambo dogo tu la kurekebisha wameshupaa kweli,wakati watoto wa kiislam wengi wanashiriki na hafanyi jitihada yoyote kuwanusuru.Waangalie kina Kadinal Pengo kila mara wanailaum serikali,nchi inakwenda pabaya sijui kuna hili na lile wakati watoto wa kikristo wengi wanashiriki wala hawafanyi jitihada zozote kunusuru janga hili.Hayo ni maoni wangu kwa hili.