Jasho la Damu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 956
- 120
Salaam JF
Haya ni maono yangu juu ya kiongozi mkuu wa chama cha ACT hayausiani na utabiri wala njozi yoyote. Mhe ZZK kama utasoma uzi huu yakupasa ufunge mkanda kubadili haya maono. Maono haya nimeyaweka katika dhana ya mapigo 3.
Mapigo hayo ni kama yafuatayo;
1. Kuanzishwa kwa UKAWA
Hili ni pigo lililofuta kabisa upepo wa ZZK kuhama na kuitikisa CDM. Wachambuzi wengi wa siasa akiwemo yeye mwenyewe ZZK waliamini kuhama/kufukuzwa kwa ZZK CDM kungeleta maafa makubwa ndani ya cdm, ni kweli ulitikisa cdm kwa muda mfupi lkn dhana ya UKAWA ilpokuja ilikufuta katika headlines za media zetu na huo ukawa mwanzo wa ZZK kusahaulika.
2. LOWASA kuhamia CDM/UKAWA
Mhe ZZK hili ni pigo ambalo hutakaa ulisahau katika maisha yako yote ya siasa. LOWASA ni tunda ulilokuwa unalisubiri muda mrefu liive ili ulimenye na kula uongeze afya ya chama chako cha ACT lkn kwa bahati mbaya mtoto wa mjini ambaye ni mwalimu wako wa siasa Freeman A. Mbowe amekupiga bao dk za mwisho wakati unasubiri tunda LOWASA lianguke uliokote, yeye kalipandia juu na kuliwai kulichuma. Amini amini nakuambia Hili pigo litakutesa na litazaa pigo la 3 litakalokufuta kabisa kwenye siasa. Ukiona Dr. Kitila Mkumbo akiwapongeza cdm kumchukua LOWASA ujue safari ya ikulu imekaribia
3. KUKOSA UBUNGE
Mhe ZZK omba Mungu Serukamba asibadili mawazo akaamua kugombea kupitia UKAWA, ubunge utabaki historia kwako. Naiona nguvu kubwa ya UKAWA ambayo hutaweza kuizuia kuchukua jimbo utakalogombea ama majimbo yote ya kigoma. Pia pole zangu zimwendee Mhe Machali naona safari hii ameamua kupishana na bahati ya Ubunge tutakumis sana bungeni.
USHAURI
Tafuta mashauriano na UKAWA ikiwezekana muombe radhi Mbowe akipokee chama chako ndani ya UKAWA. Nina imani mbowe yupo tayari kukusamehe na kukurudisha kundini kwani yeye ndiye aliyekutoa kisiasa.
Wenu
Jasho la damu
cc: Zitto