Uchambuzi jadidi: Zitto ni Prof. Lipumba kuelekea 2020?

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Nianze kusema mapema kabisa mimi ni mchambuzi huru, ninayetazama Siasa za Tanzania katika mizania ya uhalisia wake na kujaribu kujenga hoja kulingana na miktadha inayokuwa inajitokeza. Uchambuzi wangu hapa utalenga zaidi kuzitazama Siasa za upinzani kuelekea mwaka 2020 na possible trends ambazo zinaweza kujitokeza. Nikiri pia mapema hapa, ninachokiandika hapa ni kutokana na kuzisoma hulka na tabia binafsi za wanasiasa lakini zenye kujenga dhana pana ya mwelekeo wa Siasa zetu.

Tukio la Maalim Seif Sharif Hamad kuachana na chama alichokiasisi cha CUF na kujiunga na chama chenye utata katika uasisi wake cha ACT Wazalendo ingawa kimeleta mtikisisko katika siasa za Tanzania kilitazamiwa. Kama alivyoeleza Hamad mwenyewe, kwa wadadisi na wafuatiliaji wa mambo halikua jambo la kushangaza na ghafla sana hasa ikizingatiwa mgogoro uliokuwapo ndani ya CUF uliufanya upande wake Maalim kushika makali ya kisu hivyo kumlazimisha kiongozi huyu nguli wa Siasa za Zanzibar kuanza kufikiria mapema mbadala wa jukwaa la kuendeleza harakati zake.

Lakini kilichokua hakitazamiwi na wengi, ni kiongozi huyu na kundi lake kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo, chama ambacho kama nilivyoeleza hapo awali mbali na kuwa na utata katika kuanzishwa kwake, ni kichanga sana ukiKIlinganisha na chama kikuu cha upinzani cha CAHADEMA na hakijawahi kuwa katika mkondo wa ushirika na vyama vya upinzani ukiacha mienendo ya hivi karibuni kama ya tukio la muswada wa vyama vya siasa, kile kilichoitwa Azimio la Zanzibar na zaidi kiongozi wake mkuu Zitto Kabwe kuanza kulia na ‘wapinzani wenzake’ hasa CHADEMA ambao wameingia kwenye mtego wa mkono wa dola.

Hapa lazima ieleweke kwamba kuanzishwa kwa chama cha ACT-Wazalendo kulikuja kutokana na waasisi wake kama Prof. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe, Alberto Msando, Samson Mwigamba, Anna Mghwila na wengine wengi kufukuzwa kutoka chama Kikuu cha Upinzani cha CHADEMA kwa tuhuma ambazo zilibatizwa jina la ‘Usaliti’ na ‘Uanzishwaji wa Mpango wa kupindua uongozi halali wa chama’. Hata hivyo, kabla ya kutimuliwa kwao ndani ya CHADEMA, kulikua na historia kubwa ya misigano ya kiutendaji baina ya kundi hili na chama chao hicho (CHADEMA) ambayo ilipelekea wanasiasa wa aina ya Julianza Shonza (Naibu Waziri kwa sasa), Habib Mchange (Mkurugenzi katika magazeti ya Tanzanite), Ibrahim Chagulani na wengineo kufutwa uanachama.

Kuanzishwa kwa chama cha cha ACT-Wazalendo kulitazamwa kama pigo kubwa kwa CHADEMA na wachambuzi wengi wa mambo ya Siasa za Tanzania walikuwa wakitazamia mpasuko mkubwa wa chama hiki ingawa baadaye kilibaki imara pamoja na kutetereka kiasi baadhi ya maeneo hasa Mkoa wa Kigoma anakotokea Zitto Kabwe. Ni chambuzi hizi ndizo zilipelekea kuibuka kwa dhana kama za ‘ACT-Wazalendo ni CCM B’, ‘Wasaliti’ na ile ya chama hiki kuwa ni ‘mali ya vigogo wa CCM’ ambao walikuwa wanajiandaa kuchepuka mara baada ya kukatwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea urais ndani ya chama hiki kikongwe mwaka 2015.

Ingawa dhana hizi zilionekana kama ‘propaganda hami’ (Defensive Propaganda) kutoka CHADEMA na washirika wake lakini kwa kiasi kikubwa leo zinaweza kuwa bado zinaacha mashaka ndani ya Siasa za Upinzani. Kwanini? Ninavyoandika sasa, karibu viongozi wote waasisi wa chama hiki cha ACT-Wazalendo na wale waliofukuzwa chama cha CHADEMA ama wameteuliwa katika nyadhifa mbalimbali za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na CCM au ni washirika wakubwa wa chama hiki tawala tena katika mazingira ya ushirika ambao unaularua kwelikweli upinzani.

Hata Zitto mwenyewe katika kipindi cha mwanzo cha Utawala wa Serikali ya awamu ya tano, alikuwa akiwang’ong’a wapinzani huku akisifia utendaji wa serikali ya CCM. Tukio kubwa la kukumbukwa ni siku Rais John Pombe Magufuli alipofanya ziara mikoa ya Kigoma na Tabora ambapo ZZK alisimama Jukwaani katika tukio la uwekaji jiwe la msingi mradi wa maji Kigoma na kumwaga sifa kedekede kwa JPM na kuwananga wapinzani hususani CHADEMA ambao walionekana kupinga approach ya Serikali ya awamu ya tano katika kuendesha nchi. Ni katika ziara hii pia Rais JPM alimsifia David Kafulira kwa kuibua sakata la ufisadi wa Akaunti ya Tegeta-ESCROW na kumwambia ‘waliokuita tumbili wao ndiyo watageuka tumbili’. Leo Kafulira ambaye ni zao la CHADEMA na ‘mshirika’ wa Zitto Kabwe naye ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

Ingawa wataalam wa Siasa wanasema ‘Siasa huamuliwa zaidi na nyakati’ na kwamba ‘Siku moja ni mwaka katika siasa’ pia ‘Siasa haina adui au rafiki wa kudumu’ bado kiongozi huyu mkuu wa ACT-Wazalendo ana kazi kubwa ya kuwaaminisha watu makini juu ya mazongwe yote haya. Ana kila sababu ya kuprove beyond doubt kwamba he is the right person to be trusted na washirika wengne wa vyama vya upinzani. Na hapa ndipo palipo na hoja kuu ambayo ninaelekea kuhitimisha nayo.

Baada ya washirika wake wakuu ‘kumkimbia’ na kuteuliwa kuitumikia Serikali ya CCM, Zitto Kabwe alianza kuwa mwiba kwa Serikali, bila woga na mara nyingi maandiko yake katika mitandao ya kijamii amekua akimtaja rais JPM moja kwa moja tena kwa lugha kali zenye kejeli huku akiwa na kashikashi chache sana za kidola ukilinganisha na wapinzani wengine. Tukio la hivi karibuni tu ni kumtaja rais JPM katika suala la utoaji misaada kwa majirani zetu wa Zimbabwe, Zambia na Msumbiji kwa kutumia maneno kama ‘Ushamba’ na ‘Ushetani’. Ingawa yaweza isiwe hoja sana kutokana na kuibuka kwa matukio kadhaa ya kisiasa ambayo yanawaunganisha zaidi wapinzani, bado kasi ya Zitto Kabwe katika hili la kumshambulia JPM moja kwa moja imekua kubwa na tuseme ndiyo kwa kiasi kikubwa imerejesha imani yake kwa viongozi wengine wa upinzani vikiwemo vyama washirika wa UKAWA.

Hili sambamba na kujiweka karibu sana na shambulio la Tundu Lisu ndilo kwa kiasi kikubwa limerejesha ‘imani ya wengi’ katika ushirika wa vyama vya upinzani unaojengeka sasa na pengine baadaye. Hapa ndipo alianza kufanya mazungumzo mazungumzo na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani bila kusahau kutano lake la siri ofisni kwa Edward Ngoyai Lowasa aliyekua mgombea wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 kupitia CHADEMA na washirika UKAWA kabla hajatangaza kurejea CCM. Lowasa pia ameondoka akiwa ameshiriki kinachoitwa azimio la Zanzibar sambamba na vyama washirika vya upinzani.

Kwa msingi huu, kuingia kwa Maalim Seif Sharif na kundi lake la Zanzibar kwenye chama hiki cha ACT-Wazalendo kunampa rasmi Zitto Kabwe turufu kubwa ya kuamua ushirika wa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Hii ina maana kwamba ACT-Wazalendo imekubali kuibeba CUF Zanzibar ndani yake na Zitto Kabwe ndiye kabaki kuwa Lipumba wa CUF hii ndani ya ACT-Wazalendo.

Hulka za Zitto Kabwe mara nyingi hujionesha katika majivuno ya kuwa bora zaidi kuliko wengine, kujibrand kama central pillar, kujiapiza na ndoto yake ya muda mrefu kutaka kuwa rais wa Tanzania, kutaka kuwa dominant katika aspects mbalimbali na zaidi katika kuamini fikra zake ni mujarab na omega. Hili ndilo pengine lilipelekea kuwepo kwa cheo cha Kiongozi Mkuu ndani ya Chama chake cha ACT-Wazalendo ambacho kinawafanya Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Chama chake kuwa ceremonials na wasio na nguvu yoyote ya maamuzi.

Na hili ndilo linafanya wadadisi wengi kusubiri kwa hamu kubwa kitachotokea katika ‘muunganiko huu’ hasa ikizingatiwa uwepo wa wa tetesi za kusajili vigogo kutoka Chama cha Mapinduzi ambazo kama ni kweli basi tunaweza kuona picha halisi za ushirika huu wa upinzani kuelekea 2020. Vigogo hawa waweza kuwa turufu ya kutengeneza himaya binafsi ya vyama vya upinzani kuelekea 2020 kuliko ushirika na kwa maana hiyo kama hawataingia na kumezwa katika ‘mikakati ya ushirika wa vyama’ basi wataingia kama wasambaratishaji wa ushirika. Ikumbukwe Tundu Lisu naye kasimama katikati kama sole candidate na challenger wa chama tawala kuelekea mwaka 2020 na ametengenezewa picha hii. Hapa ndipo Zitto Kabwe aweza kutoka kama Lipumba wa mwaka 2015.

Mchakato wa kuwapata wagombea wa Uchaguzi Mkuu wa JMT na Zanzibar wa ndani ya CHADEMA unaacha maswali juu hatma ya ushirika na vyama vingine vya siasa. Nalazimika kuliongeza zaidi andiko hili.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa akisema ni chama chake pekee chenye nia na uwezo wa kukamata dola. Ameeleza wazi kwamba vyama vingine vya upinzani vinalenga viti vya ubunge na udiwani tena kwa idadi isiyozidi viti vitano. Hata hivyo, awali CHADEMA kupitia Katibu Mkuu wake John John Mnyika kilitangaza kukaribisha vyama vyenye nia thabiti ya kushirikiana kukiondoa CCM madarakani.

Hata hivyo, ukiutazama mchakato unavyokwenda wa kuwapata watia nia na wagonbea ni dhahiri CHADEMA inacheza karata ya kuvitega tu vyama vingine. Mtego wa CHADEMA umeilenga ACT ya ZZK. Kwamba CHADEMA kuamua kuutenga mchakato wa uchaguzi pande mbili, Zanzibar na Tanganyika (Tanzania Bara) ni hatimaye kumweka ZZK kwenye mtego mkuu. CHADEMA inalenga kuiunga mkono ACT upande wa Urais wa Zanzibar ili hatimaye kulazimisha turufu ya ZZK na ACT isiyo na nguvu bara kwenye urais wa JMT huku ushindani wa ubunge na udiwani ukibaki wazi kwa ushindani bila ushirika. Swali ni Je ZZK atakuwa tayari? Hivi karibuni amekuwa akitoa kauli zinazoashilia kuamua kugombea urais huku wakati huohuo akilitaja mara kwa mara jina la Bernard Membe.
 
Siasa siku zote ni upepo uvumao. Usishangae siku moja Magufuli naye akajiunga ACT WAZALENDO.
 
Nguvu kubwa itakayotumika Sasa ni kuichonganisha ACT WAZALENDO na CHADEMA kwa Sababu ya LIPUMBA na SEiF yashapita.
 
Utashangaa sasa ukiambiwa Kujiunga kwa Maalim Seif ACTW kulipata baraka zote za viongozi wa Chadema, na baadhi walishiriki katika kuandaa mpango huo.
 
Ku
Nianze kusema mapema kabisa mimi ni mchambuzi huru, ninayetazama Siasa za Tanzania katika mizania ya uhalisia wake na kujaribu kujenga hoja kulingana na miktadha inayokuwa inajitokeza. Uchambuzi wangu hapa utalenga zaidi kuzitazama Siasa za upinzani kuelekea mwaka 2020 na possible trends ambazo zinaweza kujitokeza. Nikiri pia mapema hapa, ninachokiandika hapa ni kutokana na kuzisoma hulka na tabia binafsi za wanasiasa lakini zenye kujenga dhana pana ya mwelekeo wa Siasa zetu.

Tukio la Maalim Seif Sharif Hamad kuachana na chama alichokiasisi cha CUF na kujiunga na chama chenye utata katika uasisi wake cha ACT Wazalendo ingawa kimeleta mtikisisko katika siasa za Tanzania kilitazamiwa. Kama alivyoeleza Hamad mwenyewe, kwa wadadisi na wafuatiliaji wa mambo halikua jambo la kushangaza na ghafla sana hasa ikizingatiwa mgogoro uliokuwapo ndani ya CUF uliufanya upande wake Maalim kushika makali ya kisu hivyo kumlazimisha kiongozi huyu nguli wa Siasa za Zanzibar kuanza kufikiria mapema mbadala wa jukwaa la kuendeleza harakati zake.

Lakini kilichokua hakitazamiwi na wengi, ni kiongozi huyu na kundi lake kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo, chama ambacho kama nilivyoeleza hapo awali mbali na kuwa na utata katika kuanzishwa kwake, ni kichanga sana ukiKIlinganisha na chama kikuu cha upinzani cha CAHADEMA na hakijawahi kuwa katika mkondo wa ushirika na vyama vya upinzani ukiacha mienendo ya hivi karibuni kama ya tukio la muswada wa vyama vya siasa, kile kilichoitwa Azimio la Zanzibar na zaidi kiongozi wake mkuu Zitto Kabwe kuanza kulia na ‘wapinzani wenzake’ hasa CHADEMA ambao wameingia kwenye mtego wa mkono wa dola.

Hapa lazima ieleweke kwamba kuanzishwa kwa chama cha ACT-Wazalendo kulikuja kutokana na waasisi wake kama Prof. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe, Alberto Msando, Samson Mwigamba, Anna Mghwila na wengine wengi kufukuzwa kutoka chama Kikuu cha Upinzani cha CHADEMA kwa tuhuma ambazo zilibatizwa jina la ‘Usaliti’ na ‘Uanzishwaji wa Mpango wa kupindua uongozi halali wa chama’. Hata hivyo, kabla ya kutimuliwa kwao ndani ya CHADEMA, kulikua na historia kubwa ya misigano ya kiutendaji baina ya kundi hili na chama chao hicho (CHADEMA) ambayo ilipelekea wanasiasa wa aina ya Julianza Shonza (Naibu Waziri kwa sasa), Habib Mchange (Mkurugenzi katika magazeti ya Tanzanite), Ibrahim Chagulani na wengineo kufutwa uanachama.

Kuanzishwa kwa chama cha cha ACT-Wazalendo kulitazamwa kama pigo kubwa kwa CHADEMA na wachambuzi wengi wa mambo ya Siasa za Tanzania walikuwa wakitazamia mpasuko mkubwa wa chama hiki ingawa baadaye kilibaki imara pamoja na kutetereka kiasi baadhi ya maeneo hasa Mkoa wa Kigoma anakotokea Zitto Kabwe. Ni chambuzi hizi ndizo zilipelekea kuibuka kwa dhana kama za ‘ACT-Wazalendo ni CCM B’, ‘Wasaliti’ na ile ya chama hiki kuwa ni ‘mali ya vigogo wa CCM’ ambao walikuwa wanajiandaa kuchepuka mara baada ya kukatwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea urais ndani ya chama hiki kikongwe mwaka 2015.

Ingawa dhana hizi zilionekana kama ‘propaganda hami’ (Defensive Propaganda) kutoka CHADEMA na washirika wake lakini kwa kiasi kikubwa leo zinaweza kuwa bado zinaacha mashaka ndani ya Siasa za Upinzani. Kwanini? Ninavyoandika sasa, karibu viongozi wote waasisi wa chama hiki cha ACT-Wazalendo na wale waliofukuzwa chama cha CHADEMA ama wameteuliwa katika nyadhifa mbalimbali za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na CCM au ni washirika wakubwa wa chama hiki tawala tena katika mazingira ya ushirika ambao unaularua kwelikweli upinzani.

Hata Zitto mwenyewe katika kipindi cha mwanzo cha Utawala wa Serikali ya awamu ya tano, alikuwa akiwang’ong’a wapinzani huku akisifia utendaji wa serikali ya CCM. Tukio kubwa la kukumbukwa ni siku Rais John Pombe Magufuli alipofanya ziara mikoa ya Kigoma na Tabora ambapo ZZK alisimama Jukwaani katika tukio la uwekaji jiwe la msingi mradi wa maji Kigoma na kumwaga sifa kedekede kwa JPM na kuwananga wapinzani hususani CHADEMA ambao walionekana kupinga approach ya Serikali ya awamu ya tano katika kuendesha nchi. Ni katika ziara hii pia Rais JPM alimsifia David Kafulira kwa kuibua sakata la ufisadi wa Akaunti ya Tegeta-ESCROW na kumwambia ‘waliokuita tumbili wao ndiyo watageuka tumbili’. Leo Kafulira ambaye ni zao la CHADEMA na ‘mshirika’ wa Zitto Kabwe naye ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.

Ingawa wataalam wa Siasa wanasema ‘Siasa huamuliwa zaidi na nyakati’ na kwamba ‘Siku moja ni mwaka katika siasa’ pia ‘Siasa haina adui au rafiki wa kudumu’ bado kiongozi huyu mkuu wa ACT-Wazalendo ana kazi kubwa ya kuwaaminisha watu makini juu ya mazongwe yote haya. Ana kila sababu ya kuprove beyond doubt kwamba he is the right person to be trusted na washirika wengne wa vyama vya upinzani. Na hapa ndipo palipo na hoja kuu ambayo ninaelekea kuhitimisha nayo.

Baada ya washirika wake wakuu ‘kumkimbia’ na kuteuliwa kuitumikia Serikali ya CCM, Zitto Kabwe alianza kuwa mwiba kwa Serikali, bila woga na mara nyingi maandiko yake katika mitandao ya kijamii amekua akimtaja rais JPM moja kwa moja tena kwa lugha kali zenye kejeli huku akiwa na kashikashi chache sana za kidola ukilinganisha na wapinzani wengine. Tukio la hivi karibuni tu ni kumtaja rais JPM katika suala la utoaji misaada kwa majirani zetu wa Zimbabwe, Zambia na Msumbiji kwa kutumia maneno kama ‘Ushamba’ na ‘Ushetani’. Ingawa yaweza isiwe hoja sana kutokana na kuibuka kwa matukio kadhaa ya kisiasa ambayo yanawaunganisha zaidi wapinzani, bado kasi ya Zitto Kabwe katika hili la kumshambulia JPM moja kwa moja imekua kubwa na tuseme ndiyo kwa kiasi kikubwa imerejesha imani yake kwa viongozi wengine wa upinzani vikiwemo vyama washirika wa UKAWA.

Hili sambamba na kujiweka karibu sana na shambulio la Tundu Lisu ndilo kwa kiasi kikubwa limerejesha ‘imani ya wengi’ katika ushirika wa vyama vya upinzani unaojengeka sasa na pengine baadaye. Hapa ndipo alianza kufanya mazungumzo mazungumzo na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani bila kusahau kutano lake la siri ofisni kwa Edward Ngoyai Lowasa aliyekua mgombea wa kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 kupitia CHADEMA na washirika UKAWA kabla hajatangaza kurejea CCM. Lowasa pia ameondoka akiwa ameshiriki kinachoitwa azimio la Zanzibar sambamba na vyama washirika vya upinzani.

Kwa msingi huu, kuingia kwa Maalim Seif Sharif na kundi lake la Zanzibar kwenye chama hiki cha ACT-Wazalendo kunampa rasmi Zitto Kabwe turufu kubwa ya kuamua ushirika wa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Hii ina maana kwamba ACT-Wazalendo imekubali kuibeba CUF Zanzibar ndani yake na Zitto Kabwe ndiye kabaki kuwa Lipumba wa CUF hii ndani ya ACT-Wazalendo.

Hulka za Zitto Kabwe mara nyingi hujionesha katika majivuno ya kuwa bora zaidi kuliko wengine, kujibrand kama central pillar, kujiapiza na ndoto yake ya muda mrefu kutaka kuwa rais wa Tanzania, kutaka kuwa dominant katika aspects mbalimbali na zaidi katika kuamini fikra zake ni mujarab na omega. Hili ndilo pengine lilipelekea kuwepo kwa cheo cha Kiongozi Mkuu ndani ya Chama chake cha ACT-Wazalendo ambacho kinawafanya Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Chama chake kuwa ceremonials na wasio na nguvu yoyote ya maamuzi.

Na hili ndilo linafanya wadadisi wengi kusubiri kwa hamu kubwa kitachotokea katika ‘muunganiko huu’ hasa ikizingatiwa uwepo wa wa tetesi za kusajili vigogo kutoka Chama cha Mapinduzi ambazo kama ni kweli basi tunaweza kuona picha halisi za ushirika huu wa upinzani kuelekea 2020. Vigogo hawa waweza kuwa turufu ya kutengeneza himaya binafsi ya vyama vya upinzani kuelekea 2020 kuliko ushirika na kwa maana hiyo kama hawataingia na kumezwa katika ‘mikakati ya ushirika wa vyama’ basi wataingia kama wasambaratishaji wa ushirika. Ikumbukwe Tundu Lisu naye kasimama katikati kama sole candidate na challenger wa chama tawala kuelekea mwaka 2020 na ametengenezewa picha hii. Hapa ndipo Zitto Kabwe aweza kutoka kama Lipumba wa mwaka 2015.
Kuna hoja hapa
 
Umeandika ukweli ambao watu hujibaraguza kama wamesahau. Labda tuombe msuguano kati ya jiwe na waasisi wa asili wa ACT ndani ya CCM uendelee. Wakipatana tuhesabu maumivu kwa wapinzani. Na ndio itakuwa kifo cha democracy TZ.
 
Uchqmhuzi murua, makini hongers sana.
 
He is some how Senior when you Talk about opposion parties in Tanzania '' For ACT is it true or False that he is senior to them'' Amekwepa mishale mingi kwenye Siasa za upinzani nadhani anastahiri kuwa Kiongozi mkuu kwenye chama chake
 
Back
Top Bottom