Kurejea kwa Lowassa CCM, pande nne zitanufaika

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
568
1,562
Wanajanvi Habarini.

Jana tumeshuhudia Nguri wa siasa Tanzania bwana Edward Lowassa akirejea katika Chama chake cha zamani ikitokea CDM.
Kuna mitazamo mingi katika hili, mingine Hasi na mingine Chanya kama ambavyo wadau mbalmbali walivyochangia kupitia nyuzi kadhaa kuhusiana na suala hili.
Mimi leo najikita kuangazia Mitazamo chanya ambamo ndani yake kuna Faida itokanayo na huyu mheshimiwa Lowasa kurejea chama chake cha zamani CCM.

1. Faida ya Kwanza ni kwa Lowassa mwenyewe na Familia yake.

Katika sababu kubwa kabisa amboyo imesababisha ndugu huyu kurejea CCM basi ni hii, Kujinusuru yeye mwenyewe na Familia yake dhidi ya Mkono wa Mheshimiwa Jiwe kupitia vyombo na Taasisi mbalmbal za serikari.

Bwana huyu kuondoka CCM ilikua ni pigo kubwa kwa Chama kutokana na ukubwa, Ukomavu na Ushawishi aliona0 katika Siasa za Nchi hii. Hii ilipelekea Mhesimiwa Jiwe aishi kwa wasiwasi wa kisiasa kwani anamtambua vyema mtu huyu na anajua fika hata ndani ya CCM ya sasa bado jamaa huyu ana ushawishi mkubwa.

Sasa ili hali iwe shwari mtu huyu alitakiwa kwa gharama yoyote arudishwe kundini, mbinu za kumshawishi ili arudi kwa hiari ziligonga mwamba ndipo mheshimiwa akaagiza zitumike nguvu kwa kugusa moja kwa moja Masilahi na mali za huyu bwana kama tulivyo shuhudia, pia iliagizwa waguswe ndugu na jamaa zake il tu kumlegeza nguri huyu wa Siasa za Bongo.

Lowassa afanye nini sasa kujinusuru na kuiokoa Familia yake, hakua na namna na wala hakuna machaguo mengi bali ni kujisalimisha na kurejea CCM. Bora Nusu Shari kuliko Shari Kamili.

2. Faida ya Pili ni kwa CCM Yenyewe

Hakuna kitu kilichoisumbua CCM kama bwana huyu kua mbali na udhibiti wa CCM, kwani wanajua madhara ambayo angeyasababisha Indirect kupitia wafuasi wake waliopo na wasiokuepo ndani ya CCM. Huyu bwana alijijengea mizizi imara ndani ya chama na inaweza kuchukua awamu nzima na hata ijayo ili kumaliza kabisa ushawishi wake ndani ya chama hicho.
Sasa ili chama kitulie na kitazame mbele basi ilikua lazima huyu bwana arudishwe kundini vyovyote iwe lazima arudishwe na ndicho kilichotokea.

3. Faida ya Tatu ni kwa Selikari na Nchi kwa Ujumla.

Kama tujuavyo Serikali yetu inaendeshwa kwa mifumo ya Siasa, Msukumo wowote wa kisiasa basi husababisha pia Serikali kua na maamuzi kadhaa ili kukisaidia chama tawala kushinda misukumo hiyo.
Kama tulivyoona Sheria mbalimbali zilitungwa ili kuhakikisha Upinzani unadhibitiwa kwa ukaribu basi leo ujue shabaha kubwa ilikua ni kuhakikisha huyu bwana hana namna ya kufulukuta huko alikohamia.
Sasa kurejea kwake CCM kutaleta Nafuu kubwa kwa Taifa kwani maamuzi kadhaaa yanaweza kubatilishwa ama kulegezwa kwani alieogopwa karejea kundini, usishangae kuona si muda mrefu mikutano ya kisiasa ikaruhusiwa tena, media zikalegezewa kidogo, wapinzani wakapewa ka uhauweni kidogo.
Hivi vikitokea vitalejesha Imani kwa Nchi Hisani nao watarejesha Misaada, Wawekezaji wa nje kuwekeza tena na hatimaye Shilingi yetu kubalance tena.

4. Faida ya Nne ni Kwa Vyama Pinzani Hususani CHADEMA Yenyewe.

Kama tujuavyo kua ilikua ni makosa makubwa sana kwa Upinzani UKAWA hususani CHADEMA kumkaribisha bwana Lowassa, sio kwa sababu ya kashifa alio kua nayo la hasha ni kwa sababu ya hatua ambazo zimechukuliwa na CCM kuhakikisha wanamdhibiti mtu huyu ndio zina madhara makubwa kwa upinzani kuliko hata kashifa yake ya Ufisadi.

Sheria zote zilizochukuliwa dhidi ya Upinzani ilikua kuhakikisha huyu bwana hapewi mwanya wa kufanya Siasa huko aliko, wanasisias walioumia/walioshughulikiwa wao kama wao haikua Shabaha, shabaha alikua bwana huyu Edward Lowassa.
Sasa kurejea kwake CCM ni Hauweni na Nafuu kubwa kwa CHADEMA na Upinzani kwa Ujumla.

CHADEMA kama chama Kikuu cha upinzani inabidi kifurahie zaidi kwa Mtu huyu kuondoka kuliko kusikitika, ni wakati wa Vyama Pinzani kujiangalia na Kuchukua Hatua Sitahiki ili kujijenga zaidi.
Kwa CHADEMA ni wakati wa kujifumua na kujisuka Upya, ikiwezekana Mbowe ajihuzuru na si kwa Ubaya bali kutoa nafasi kwa Fikra Mpya. Amepigana vya kutosha na amejitahidi kukivusha Chama kwa Hatua za Kutosha.

Nampongeza Lowassa kwa kuujua Ukweli, ni kama Yona wa kwenye Biblia aliposema ukweli kua ile Dhoruba yote ni yeye ndie Chanzo ili atupwe Baharini Chombo kitulie. Lowassa kaamua kujitosa ,Upinzani utatulia na kuimalika zaidi.
 
Kwanini mnang'ang'ania mbowe ajiuzuru ...kuna nini kimejificha kwa wanaofosi???

hivi vikitokea vitalejesha Imani kwa Nchi Hisani nao watarejesha Misaada, Wawekezaji wa nje kuwekeza tena na hatimaye Shilingi yetu kubalance tena.

4. Faida ya Nne ni Kwa Vyama Pinzani Hususani CHADEMA Yenyewe.

Kama tujuavyo kua ilikua ni makosa makubwa sana kwa Upinzani UKAWA hususani CHADEMA kumkaribisha bwana Lowassa, sio kwa sababu ya kashifa alio kua nayo la hasha ni kwa sababu ya hatua ambazo zimechukuliwa na CCM kuhakikisha wanamdhibiti mtu huyu ndio zina madhara makubwa kwa upinzani kuliko hata kashifa yake ya Ufisadi.

Sheria zote zilizochukuliwa dhidi ya Upinzani ilikua kuhakikisha huyu bwana hapewi mwanya wa kufanya Siasa huko aliko, wanasisias walioumia/walioshughulikiwa wao kama wao haikua Shabaha, shabaha alikua bwana huyu Edward Lowassa.
Sasa kurejea kwake CCM ni Hauweni na Nafuu kubwa kwa CHADEMA na Upinzani kwa Ujumla.

CHADEMA kama chama Kikuu cha upinzani inabidi kifurahie zaidi kwa Mtu huyu kuondoka kuliko kusikitika, ni wakati wa Vyama Pinzani kujiangalia na Kuchukua Hatua Sitahiki ili kujijenga zaidi.
Kwa CHADEMA ni wakati wa kujifumua na kujisuka Upya, ikiwezekana Mbowe ajihuzuru na si kwa Ubaya bali kutoa nafasi kwa Fikra Mpya. Amepigana vya kutosha na amejitahidi kukivusha Chama kwa Hatua za Kutosha.

Nampongeza Lowassa kwa kuujua Ukweli, ni kama Yona wa kwenye Biblia aliposema ukweli kua ile Dhoruba yote ni yeye ndie Chanzo ili atupwe Baharini Chombo kitulie. Lowassa kaamua kujitosa ,Upinzani utatulia na kuimalika zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema wamenufaika sana maana Edo alikuwa passive na bora amehama mapema kwani angehama kuelekea uchaguzi ingekuwa balaaa
 
Ukweli mchungu bila Mbowe kujiuzulu watu wenye akili hawatakielewa chama.
 
Back
Top Bottom