Barua ya wazi kwa ndugu Mwita Waitara Mwikabe

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
Ndugu yangu Mwita Mwikabe,

Ili kuweka barua yangu kwako katika muktadha niliokusudia, nikujulishe tu kwamba siyo ya kisiasa na haijatoka CDM maana mimi sio mwanachama wa chama chochote cha upinzani wala CCM. Hivyo nakuandikia kama mtazania na kijana mwenzako tuliyeishi pamoja pale Mlimani ukisoma shahada yako ya kwanza ya elimu.

Nimemsikiliza Mh Polepole alipokua anakutambulisha na kisha nimekusikiliza wewe kwa makini huku nikihakikisha sipitwi na hata neno moja. Kama inavyoweza kuwa kwa watanzania wengi, niwe mkweli kwamba nimeshtuka sana kukuona na kukusikiliza ukitoa maelezo ya kuhama chama. Ila wakati nakusiliza, sijajua kwa nini, lakini nikakumbuka jinsi ulivyotugeuka wakati tunapigania maslahi yetu katika uanzishwaji wa bodi ya mikopo ukiwa kiongozi/rais wa DARUSO tene baada ya kukupigania upate urais kwa hoja yako kubwa kwamba wewe ni mtoto wa maskini na uliutaka urais kwa maslahi yetu. Tuache hayo. Ninaomba nikuulize maswali kadhaa:

La kwanza: katika maelezo yako ya kwa nini umejitoa CDM na kuhamia CCM ni shida uliyoipata baada ya kuonesha nia ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama. Umeonesha kuwa ulikua na kiu kubwa ya kuwa mwenyekiti na kuhakikishiwa na Mh Mbowe kwamba hutaupata na utashughulikiwa. Sasa kiu yako ya kuwa mwenyekiti wa chama cha siasa imekwisha au unahama nayo CCM? Je CCM wamekuhakikishia utapewa nafasi ya kua mwenyekiti? Unapojitazama unadhani utakua mwenyekiti wa CCM baada ya miaka mingapi ijayo? Au uenyekiti ulikua na hamu nao ukiwa CDM tu lakini sio huko ulikwenda? Kwa kua Mh Polepole kakutangazia kwamba wanachama wa chama chake wote ni sawa na haijalishi mtu kajiunga lini anapewa nafasi kama anastahi, hebu jaribu kugombea Urais 2020 au katoe mapendekezo kwamba JPM awe rais tu na Mwenyekiti awe mtu mwingine na wewe uwe mmoja wa wagombe.

La pili: Kama ilivyo kwa wengine wengi waliohama CDM nawe umeibuka na mambo matano ambayo tumezoea kuyasikia. Moja ni chama kukosa ofisi; mbili ni matumizi mabaya ya fedha za chama na akishutumiwa mwenyekiti Mbowe; tatu ni chama kuwa kampuni yake; nne ni yeye kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu na tano ni yeye kuhusika/kuhusishwa na kifo cha Wangwe. Mambo haya naona ni ngonjera wanazokarishiwa kila wanaohama CDM. Sasa nikuulize kidogo: haya mambo umeyajua leo? Mbona yote yalikuwepo tangu unajiunga na chama na ulipogombea ubunge? Kama Mbowe anahusika na kifo cha Wangwe inakuaje yeye kashindikana hata kushtakiwa tu mahakamani kwa miaka yote hiyo? Ana nguvu gani zinazowafanya polisi, DPP, wasiojulikana, mahasimu wake wa kisiasa, na wengine wote washindwe kumpandisha mahakamani kwa mauaji? Fedha za chama ni mali ya umma.. inakuwaje serikali na vyombo vyake vimeshindwa kumshtaki kwa wizi na ufisadi wakati hesabu zinakaguliwa kila mwaka? Huoni kwamba wewe ulikua sehemu ya mauji ya Wangwe kwa kuwa kwenye chama kilichomua huku ukijiua? Au wazee wa jadi ndio wamekupa hiyo taarifa jana usiku wakikutambikia? Usomi na critical thinking uliyosema unavyo mbona siviooni vikitumika hapa?

La tatu: Umesema CDM hakuna demokrasia na ukifanya jambo unahojiwa? Ni chama gani kisichobana wanachama wake au kuwa na mikakati yao ya kukabiliana na wapinzani wao? Hivi CCM wanakubali kila kitu? Kuna uhuru? Mbona Mh Rais alimwita mbunge aliyekwenda kumsalimia Lema jela kuwa ni msaliti? Ule ni uhuru? Mbona mwenyekiti wa CCM Mh Rais juzi kawatisha wabunge wa kanda ya kusini na waziri mkuu tena hadharani kwa sababu tu walihoji jambo lenye tija na mantiki kwa wananchi? Huo ni uhuru? Wanachama wangapi wa CCM wamefukuzwa kwa kuhoji au kufanya mambo yaliyoonekana ni kinyume na chama chao? Unakumbuka katibu Mkuu wa CCM Mukama alipokwenda Dodoma kuwatisha wabunge walikua wameibua baadhi ya hoja za kifisadi bungeni? Unakumbuka JPM juzi akimjibu Nape kwamba kama anadhani CCM itashindwa sababu ya korosho ahame? Umewasikia wabunge wangapi wa CCM waliompa pole Lissu tangu apigwe risasi? kwa nini?Usomi, critical thinking na ujuaji uliosema unao, mbona vinapingana na huu ukweli?

La nne: Wewe na Mh Polele mumeongelea habari ya ukabilia CDM na kuelekeza shutuma kwa Mbowe kuhusu ukabila. Mbona wewe maelezo yako yamejaa ukabila na ukanda? Umeongelea habari ya watu wa Mara kuumizwa na CDM bila maelezo. Umesema utaongea na wekurya wenzako nao watoke CDM. Umesema umekutana na wakurya wa DSM kabla ya maamuzi na umefanyiwa matambiko na wazee wa kikurya.Huoni fikra zako zimejaa ukabila na umimi pekee? Wakurya ndio walikupa kura pekee DSM? Ubunge uliupata kwa kufanyiwa matambiko ya kikurya? Mbona elimu, degree, critical thinking na kutokua mjinga havionekani hapa?

La tano: mbona hujaongelea lolote kuhusu uminywaji mkubwa wa haki za binadamu a chama unachokifuata? Tena tofauti na CDM ambao huenda munachimbana biti kwenye vikao vyenu, CCM inatumia polisi, jeshi, usalama na vyombo vingine vya dola kuminya uhuru wa kujieleza, kuhoji, na habari kwa wananchi wote. Unasemaje kuhusu wizi wa kura za wazi kwenye chaguzi za marudio, watu kuwekwa ndani ovyo, kupigwa, na hata wengine kupoteza maisha? Wazee wa kimila walikuambia kwamba Lissu aliwahi kupigwa risasi na serikali imegoma hata kumlipia matibabu? Au wamekujulisha ni Mbowe kahusika?

La sita: umesema Mbowe hajawahi kwenda kumsalimia Lissu kwa kuwa anamwona anautaka uenyekiti wake. Ni Kweli? wazee wa mila na wakurya wenzako hawajakumbia kwamba Mbowe alikaa naye hospital Nairobi hadi tukaanza kuhoji anafanya nini huko badala ya kuja kuongoza chama chake na kuongoza kambi bungeni? Wazee wa mila hawajakuambia alivyopambana akatibiwe nje na amekua akipigania maslahi yake hadi leo? Ulitaka aende kulala Ubelgiji pia? Wewe umekwenda Ubelgiji mara ngapi? au nawe hujaenda kwa kuwa unamwona Lissu ni adui angekubana kwenye uenyekiti?

La saba: Umetaja vyeo Lukuki ambavyo ulikua navyo CDM Zaidi ya Ubunge. Ulivipataje kama hakuna demokrasia na viongozi wanapatika kwa kuchomekwa tu? Nawe ulikua umechomekwa? Kama kwa nafasi zote hizo umeshindwa kukisaidia chama katika yale uliyoona ni kasoro, unadhani CCM ndio utaweza? Mbona hapa sioni akili za kisomi zilivyotumika?

La nane: Umesome Mbowe amekua mwenyekiti wa chama kwa miaka 20.. hii ni kweli? Hivi Bob Makani alikua nani na alimaliza lini uongozi wake kama mwenyekiti? au wazee wa kikurya walikudanyanya miaka ya uongozi wa Mbowe wakati wa tambiko?

La tisa: Umedai mishahara yetu haijabadilika (haijapunguzwa) lakini tunalalamika hali ngumu. Kuonesha wewe ni Msomi umedai hiyo inaonesha kuna shida mahali maana tumeminywa mianya ya deal. Hivi hizi ndio fikra za elimu kweli hizi na za mtu anayejiita Msomi na aliongoza wasomi? Kwa hiyo kwa usomi wako athari ya ugumu wa maisha inatokana na mishahara tu? Umewahi kusikia au kusoma kitu kinaitw amfumko wa bei? Unajua athari zake kwenye uchumi? Unajua ni asilimia ngapi ya bidhaa tunazotumia hapa kwetu zinatoka nje na huko zitokazo zinapanda bei kila mara kwa kiasi gani? Unaweza ukatumia degree yako kujiuliza hii ina athari gani kwa mtanzania ambaye kipato chake hakikui? Iko wapi degree na crtical thinking katika hili?

La mwisho: kwa maelezo ya Mh Polepole na wewe mwenyewe, ni wazi unakwenda kugombea tena ubunge Ukonga na umeahidiwa kushinda. Ni wazi upatikanaji wa ushindi wako hautatofautina na ule wa Kindononi na Siha. Hivi unadhani hayo ndio mafanikio ya kisiasa? Kijana mdogo kama wewe kuingizwa bungeni kwa nguvu za dola unadhani ni mafanikio na baraka? Hiki ndicho matambiko ya kikurya yamekutuma kukifanya?

Nisikuhoji sana ila naomba nimalize barua yangu kwako kwa kukuambia tu kwamba umehama chama kwa hoja dhaifu sana, za kizembe, za kitoto, laini, na zenye kila dalili kwamba kuhama kwako ni tunda la ama kuhongwa au kushawishiwa na dola kwa ahaidi ya kulindwa, kupewa vyeo, na maslahi mengine. Na kwa ajili ya hayo, basi jiandae huko mbeleni maishani hasa baada ya uongozi wa Mh JPM kwisha maana utakua na mengi ya kujutia na yajayo yatakushangaza.

Fikisha salamu huko uendako.

Ni mimi Mtumishi wa Uma
 
Last edited:
Ndugu yangu Mwita Mwikabe,

Ili kuweka barua yangu kwako katika muktadha niliokusudia, nikujulishe tu kwamba siyo ya kisiasa na haijatoka CDM maana mimi sio mwanachama wa chama chochote cha upinzani wala CCM. Hivyo nakuandikia kama mtazania na kijana mwenzako tuliyeishi pamoja pale Mlimani ukisoma shahada yako yakwanza ya elimu.

Nimemsikiliza Mh Polepole alipokua anakutambulisha na kisha nimekusikiliza wewe kwa makini huku nikihakikisha sipitwi na hata neon moja. Kama inavyoweza kuwa kwa watanzania wengi, niwe mkweli kwamba nimeshtuka sana kukuona na kukusikiliza ukitoa maelezo ya kuhama chama. Ila wakati nakusiliza, sijajua kwa nini, lakini nikakumbuka jinsi ulivyotugeuka wakati tunapigania maslahi yetu katika uanzishwaji wa bodi ya mikopo ukiwa kiongozi wa DARUSO hata baada ya kukupigania upate urais kwa hoja yako kubwa kwamba wewe ni mtoto wa maskini na uliutaka urais kwa maslahi yetu. Tuache hayo. Ninaomba nikuulize maswali kadhaa:

La kwanza: katika maelezo yako ya kwa nini umejitoa CDM na kuhamia CCM shida uliyoipata baada ya kuonesha nia ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama. Umeonesha kuwa ulikua na kiu kubwa ya kuwa mwenyekiti na kuhakikishiwa na Mh Mbowe kwamba hutaupata na utashughulikiwa. Sasa kitu yako ya kuwa mwenyekiti wa chama cha siasa imekwisha au unahama nayo CCM? Je CCM wamekuhakikishia utapewa nafasi ya kua mwenyekiti? Unapojitazama unadhani utakua mwenyekiti wa CCM baada ya miaka mingapi ijayo? Au uenyekiti ulikua na hamu nao ukiwa CDM tu lakini sio huko ulikwenda?

La pili: Kama ilivyo kwa wengine wengi waliohama CDM nawe umeibuka na mambo matatu ambayo tumezoea kuyasikia. Moja ni chama kukosa ofisi; mbili ni matumizi mabaya ya fedha za chama na akishutumiwa mwenyekiti Mbowe; tatu ni chama kuwa kampuni yake; nne ni yeye kuwa mwenyekiti kwa muda mrefu na tano ni yeye kuhusika/kuhusishwa na kifo cha Wangwe. Mambo haya naona ni ngonjera wanazokarishiwa kila wanaohama CDM. Sasa nikuulize kidogo: haya mambo umeyajua leo? Mbona yote yalikuwepo tangu unajiunga na chama na ulipogombea ubunge? Kama Mbowe anahusika na kifo cha Wangwe inakuaje yeye kashinidikana hata kushtakiwa tu mahakamani kwa miaka yote hiyo? Ana nguvu gani zinazowafanya polisi, DPP, wasiojulikana, mahasimu wake wa kisiasa, na wengine wote washindwe kumpandisha mahakamani kwa mauaji? Fedha za chama ni mali ya umma.. inakuwaje serikali na vyombo vyake vimeshindwa kumshtaki kwa wizi na ufisadi wakati hesabu zinakaguliwa kila mwaka? Huoni kwamba wewe ulikua sehemu ya mauji ya Wangwe kwa kuwa kwenye chama kilichomua huku ukijiu? Au wazee wa jadi ndio wamekupa hiyo taarifa jana usiku wakikutambikia? Usomi na critical thinking uliyosema unavyo mbona siviooni vikitumika hapa?

La tatu: Umesema CDM hakuna demokrasia na ukifanya jambo unahojiwa? Ni chama gani kisichobana wanachama wake au kuwa na mikakati yao ya kukabiliana na wapinzani wao? Hivi CCM wanakubali kila kitu? Kuna uhuru? MbonaMh Rais alimwita mbunge aliyekwenda kumsalimia Lema jela kuwa ni msalili? Ule ni uhuru? Mbona mwenyekiti wa CCM Mh Rais juzi kawatisha wabunge wa miko ya kusini na waziri mkuu hadharani kwa sababu tu walihoji jambo lenye tija na mantiki kwa wananchi? Huo ni uhuru? Wanachama wangapi wa CCM wamefukuzwa kwa kuhoji au kufanya mambo yaliyoonekana ni kinyume na chama chao? Unakumbuka katibu Mkuu wa CCM Mukama alipokwenda Dodoma kuwatisha wabunge walikua wameibua baadhi ya hoja za kifisadi bungeni? Unakumbuka JPM juzi akimjibu Nape kwamba kama anadhani CCM itashindwa sababu ya koroho ahame? Umewasikia wabunge wangapi wa CCM waliompa pole Lissu tangu apigwe risasi? kwa nini?Usomi, critical thinking na ujuaji uliosema unao, mbona vinapingana na huu ukweli?

La nne: Wewe na Mh Polele mumeongelea habari ya ukabilia CDM na kuelekeza shutuma kwa Mbowe kuhusu ukabila. Mbona wewe maelezo yako yamejaa ukabila na ukanda? Umeongelea habari ya watu wa Mara kuumizwa na CDM bila maelezo. Umesema utaongea na wekurya wenzako nao watoke CDM. Umesema umekutana na wakurya wa DSM kabla ya maamuzi na umefanyiwa matambiko na wazee wa kikurya.Huoni fikra zako zimejaa ukabila na umimi pekee? Wakurya ndio walikupa kura pekee DSM? Ubunge uliupata kwa kufanyiwa matambiko ya kikurya? Mbona elimu, degree, critical thinking na kutokua mjinga havionekani hapa?

La tano: mbona hujaongelea lolote kuhusu uminywaji mkubwa wa haki za binadamu a chama unachokifuata? Tena tofaurti na CDM ambao huenda munachimbana biti kwenye viako vyenu, CCM inatumia polisi, jeshi, usalama na vyombo vingine vya dola kuminya uhuru wa kujieleza, kuhoji, na habari kwa wananchi wote. Unasmeajie kuhusu wizi wa kura za wazi kwenye chaguzi za marudio, watu kuwekwa ndani ovyo, kupigwa, na hata wengine kupioteza maisha? wazee wa kimila walikuambia kwamba Lissu aliwahi kupigwa riasa na serikali imegoma hata kumlipia matibabu? Au wamekujulisha ni Mbowe kahusika?

La sita: umesema Mbowe hajawahi kwenda kumsalimia Lissu kwa kuwa anamwona anautaka uenyekiti wake/ Kweli? wazee wa mila na wakurya wenzako hawajakumabia kwamba Mbowe alikaa naye hospital Nairobi hadi tukaanza kuhoji anafanya nini huko bada ya kuja kuongoza chama bungeni? Hawakukuambia alivyopambana akatibiwe nje na amekua akipigania maslahi yake hadi leo? Ulitaka aende kulala Ubelgiji pia? Wewe umwekdna Ubelgiji mara ngapi? au nawe hujaenda kwa kuwa unamwona Lissu ni adui angekubana kwenye uenyekiti?

La saba: Umetaja vyeo Lukuki ambavyo ulikua navyo CDM Zaidi ya Ubunge. Ulivipataje kama hakuna demkrasia na viongozi wanapatika kwa kuchomekwa tu? Nawe ulikua umechomekwa? Kama kwa nafasi zote hizo umeshinda kukisaidia chama katika yale uliyoona ni kasoro, unadhani CCM ndio utaweza? Mbona hapa sioni akili za kisomi zilivyotumika?

La nane: Umesome Mbowe amekua mwenyekiti wa chama kwa miaka 20.. hii ni kweli? Hivi Bob Makani alikua nani na alimaliza lini uongozi wake kama mwenyekiti? au wazee wa kikurya walikudanyanya miaka ya uongozi wa Mbowe wakati wa tambiko?

La mwisho: kwa maelezo ya Mh Polepole na wewe mwenyewe, ni wazi unakwenda kugombea tena ubunge Ukonga na umeahidiwa kushinda. Ni wazi upatikanaji wa ushindi wako hautatofautina na ule wa Kindononi na Siha. Hivi unadhani hayo ndio mafanikio ya kisiasa? Kijana mdogo kama wewe kuingizwa bungeni kwa nguvu za dola unadhani ni mafanikio na baraka?

Nisikuhoji sana ila naomba nimalize barua yangu kwako kwa kukuambia tu kwamba umehama chama kwa hoja dhaifu sana, za kizembe, za kitoto, laini, na zenye kila dalili kwamba kuhama kwako ni tunda la ama kuhongwa au kushawishiwa na dola kwa ahaidi ya kulindwa, kupewa vyeo, na maslahi mengine. Na kwa ajili ya hayo, basi jiandae hukoi mbeleni maishani hasa baada ya uongozi wa Mh JPM kwisha maana utakua na mengi ya kujua na yajayo yatakushangaza.

Fikisha salamu huko uendako.

Ni mimi Mtumishi wa Uma
Aisee, kama tumefkia hapo ATAPATA TABU SANA
 
Hivi ukianzisha thread ukijitanabaisha mimi ni mwanachama wa chama fulani ni dhambi. Mbona kuna akina malisa na Yeriko wanajulikana wazi ni wanachama na hakuna anewabughuzi. Hi tabià ya watu kujifanya hawana vyama unaniudhi sana. Nasisitiza WANAJIFANYA HAWANA VYAMA (THEY PRETEND)
 
Hayo mengine huwa tunayaacha pembeni. Ujumbe umeeleweka? Hilo ndilo la muhimu.
 
Duh, nimekuelewa sana!!
 
Hapo
IMG_20180728_141055_430.jpg
 
Back
Top Bottom