Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

Huu ni mkakati maalum wa MACCM unaofanywa kwa kudhoofisha elimu nchini. Umeona watoto wao wanatia mguu kwenye shule ambazo watoto wa walala hoi wanasoma? Mtaji wa kuongezeka kwa wapumbavu nchini ni neema kwa MACCM ya kuwawezesha kuitawala Tanzania milele, hawa wapumbavu hawajui kuchanganua mambo kwa kina, hawahoji lolote lile dhidi ya nchi yao wao ni ndiyooooooo kila kukicha.

Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida? (Mfano STRABAG, Nakumatt?)

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!
 
wachina wanamiminika sasa TZ kuchukua nafasi za watema pumba nchini
 
watema pumba wengi wa dar leo hii wamekesha huko kwenye tamasha lao la imooooooooooo!! na wanachekelea.
 
Tunawasaidia vipi?

Kama kuwasema ndiyo tushawasema sana humu na kwengineko, tatizo tumeliona na tumelijuwa, sasa tujadiliane namna ya kuwaokoa.
 
Back
Top Bottom