Namna elimu ya chuo ya Tanzania ni kupoteza muda kwa kijana wa kitanzania hususa ni karne hii.

Mwiba1

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
886
1,941
Ni matumaini yangu mko poa ndugu zangu wana jf and happy independence day ndugu zangu watanzania. Majobless endeleeni kupambana mechi bado halftime, mahustlers endeleeni kusaka tonge hakuna kukata tamaa. Wasomi endeleeni kutafuta kazi n.k

Ninajua juu ya uzi huu basi wasomi na wanazuoni wazee wa madesa wenye itikadi kali ambao ndio wengi humu ndani, mtanijia juu kama tai ya msabato lakini lazima ukweli usemwe.

binafsi uzi huu sijakurupuka bali ni research niliyoifanya kwa muda mrefu katika harakati zangu za mtu mweusi ndani na nje ya Tz. Nimekutana na watu wa aina mbali mbali ikiwemo wafanya biashara, watu maarufu na kadharika lakini wengi wao hawajafika hata highschool. Binafsi nilidrop chuo 2nd year baada ya kuona jamaa yangu aliyeishia form four na kuamua kutumia fursa ya kilimo kilichokuwa kikifanywa na wazazi wake na kufikia hatua ya kuexport parachichi ulaya hapo ndipo nikaona elimu sio ishu nikapiga chini na kujichanganya mapema.

Binafsi mimi ni mtu ninae zungumza na watu tofauti tofauti bila kujali umri, na mara kadhaa hukaa pamoja na wazee kuwasikiliza busara zao.
Mataifa kadhaa niliyotembelea hususa ni mataifa tajiri kama UAE, Ulaya, Marekani, mashariki ya mbali na baadhi ya nchi tajiri hapa africa sikuona wasomi wengi yaani wenye degrees ni wachache sana bali wenye skills ni wengi zaidi ukilinganisha na ilivyo africa mashariki, kati na magharibi ambapo vijana wengi ni degree holders na hawana skill yoyote wako na vyeti tu pumbaf kabisa. Ni kweli zipo kada muhimu tunazohitaji wasomi ili kuendeleza jamii yetu lakini kuna kada ambazo ni kupoteza muda.

Wasomi wengi wa chuo kikuu niliokutana nao katika maisha ya kila siku, hii ikijumlisha ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla wamekuwa wakichelewa sana katika maisha na wengi wao wanatia huruma sana wamekuwa na maisha magumu sana wapiga mizinga ukiachilia mbali kuchelewa kuoa na kuachwa sana na wachumba zao, wengi wao ni heart broken sana na ndio kila siku utawasikia humu ndani wakijiita kataa ndoa, wengi wana stress sana ukiwagusa kidogo wanapanic sana mbali na hivyo ni watumiaji wakubwa wa bajaji, bodaboda na usafiri wa umma lakini pia hata katika hospital za vichaa wamekuwa ni wengi sana kwani wengi wao humalizia stress zao za kukosa ajira kwenye mihadarati ikiwamo bangi, madawa na pombe za jerojero maana hawana hela ya kunywa bia. Katika tafiti zangu za muda mrefu nimegundua ongezeko la wavuta bangi katika jamii linachangiwa kwa kiasi kikubwa na graduates.

Ukweli ni kwamba sio makosa yao walichofeli wengi ni kuingia kwenye mfumo wa mkoloni yaani tango pori walilolishwa babu zetu na kuamini elimu ni ufunguo wa maisha na wao wamekubali kulila. lakini huwa wanajiona wana class flan hivi. Kiukweli sio makosa yao kwani waliaminishwa kuwa degree ndio kila kitu katika maisha lakini wakija mtaani wanakuta juu chini wanachanganyikiwa.

Niko hapa kuwaelimisha vijana wenzangu msio na koneksheni za ajira ya kwamba muda mnaopoteza kusoma highschool na chuo mgeutumia vizuri kufanya tafiti za kibiashara au kutafuta ujuzi sehemu mbalimbali mtafika mbali sana na tutalijenga taifa letu kwa kasi ya ajabu lakini kama kila mmoja atataka kukalia kiti cha kuzunguka tutabaki na taifa la wavivu na wapumbafu kama ilivo hivi sasa, vijana changamkieni fulsa na resourcess tulizo nazo kama vile madini, kilimo, ufugaji , uvuvi na kujiajiri mkiwa bado mnanguvu mtafika mbali, otherwise mtaishia milembe kwa stress za kukosa kazi.
Tuko katika scramble na mwenye kisu kikali ndio mla nyama. Wasomi wameshakuwa wengi sana ajira ni dhahiri hazipo sasa kwanini usitafute skill inayohitajika katika maisha ya kila siku?
Nisingependa kuizungumzia education system ya Tanzania deeply kwani ni uozo unaonuka elimu isiyotambulika hata dizonga tu hapo kwa ndugu zetu. Sasa kwanini upoteze miaka minne UNI alafu uje kuendesha boda si ungeanza kuendesha boda mapema ungekuwa mbali maana waendesha bolt dsm wengi ni degree holders kwa sasa.

Wasomi watapanic wenye busara watalitafakari hili. Wazazi msipoteze hela zenu kusomesha watoto wenu vyuo hivi vya Tz vilivyooza kama hamuwezi kuwapeleka first word countries kusoma basi ni mara mia mkawapa mitaji au mkatumia muda mwingi kuwa coach katika talent zao mtakuwa mmewasaidia sana.

Nimtazamo tu hivyo matusi na dharau sio mahala pake tunaelimishana ukicoment basi weka hoja.
 
Sera ya elimu ya mwaka 2014 inakiri mapungufu mengi sana ya mfumo wetu wa elimu kama mwanafunzi kutumia miaka mingi shuleni, kutoa wahitimu amabao wanamshindani mdogo pamoja na ujuzi N.K lakini hili lishatokea.
My point sisi kama vijana hatuna budi kujipambania malalamiko, kujisusa wakatia maisha ni yako haina maana..... Tupambane vijana wenzangu kuna siku tutabadilisha maisha yetu.
 
I can say you're right. Kwa sababu degree is just a piece of paper hasa hizi degree za bongo zinazotolewa hadi na colleges. Kwa mtazamo wangu watu wenye degree washakuwa wengi and unfortunately wengi wao wanahitaji kuajiriwa tu, nani atawaajiri wote?.... sasa tunahitaji waajiri, serikali peke yake haiwezi kuajiri haya maelfu ya graduates, tunahitaji makampuni na wawekezaji wa ndani wa kutosha.
Education and school are two different things, unaweza kuwa na mtaji wako wa 50m na ukaajiri degree holders ukatumia ujuzi wao.........sasa wakati wao wapo busy kusoma we tafuta pesa/mtaji wa kutosha ili wanapograduate wanarudi mtaani kutafuta ajira we unawaajiri kwenye kampuni yako tena kwa mshahara wa diploma.......
 
Back
Top Bottom