Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

mi nina mdogo wangu kamaliza degree UDOM yupo tu home hajishughulishi hata ku-apply kazi na magazeti namletea kila siku yeye kutwa kushinda instagram na magroup ya whatsapp. Kila weekend lazima akupige mzinga wa laki 1 eti nataka kutoka outing bro!!
Maji hufuata mkondo, haujioni hata wewe kutwa unashinda JF unachangia huu uzi?
 
Ndio atupe facts sasa ili tujue yeye huo utafiti wake sio pumba,,, kama hana facts bas huo utafit wake pumba
Unajua maana ya facts Mkuu?

Alicho kitoa ni facts tosha tena sana tu.

Labda ungeomba aweke ushahidi ili kusapoti facts alizozitoa.
 
Vijana wengi wamejipumbaza wenyewe kwa sababu ya kutojituma kiakili. Hakuna anayefikiria positively, Ni Kufikiri tu kwa fasheni..na kufuata mkumbo. .ulimbukeni, akitokea mmoja akafikiri tofauti huonekana kituko.

Wanasiasa hasa wapinzani ndio wamewajazia upumbavu mwingi kichwani,na wala hawaoni kama ni tatizo. Wamewaaminisha vijana hawa adui yao ni Chama fulani, Ni mtu au watu fulani, Ni kiongozi fulani, na vijana wanaishi na itikadi hizo, hakuna anayefikiria nje ya hapo.

Kibaya zaidi walioathirika zaidi sio hata wasiosoma tu, mpaka waliosoma hadi vyuoni, upumbavu ni huohuo, kufikiri kwa fasheni. Kila siku kulalamika kusikoisha, kukashifu na kukejeli mitandaoni, kujifanya wajuaji hata wasichojua hujifanya wanajua. Kila siku kushabikia Wanasiasa ambao hawawafikishi popote.

Idadi yao ni kubwa mno. Kwa wale wanaojali wingi wa namba bila kujali ubora wa namba, wanaona kundo hili liko sahihi kiasi cha wao kushawishika kufuata mfumo huu wa kipumbavu,kufikiri kwa fasheni.
Kazi ipo kwa kweli!
 
wengi sasa wamejiingiza kwenye wizi wa vifaa vya magari maana hela ngumu na ana mademu kibao wote wanataka pesa, so lazima aibe kuwatosheleza.
 
Starehe za kila aina ndio maisha yao.Yaani hakuna substance kabisa katika maisha yao,ni kufukuza upepo mtindo mmoja.Wameshikwa pabaya kweli kweli.Inatia huruma sana kwa kweli.Ni watumwa 100%.
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida? (Mfano STRABAG, Nakumatt?)

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!
 
Ndio.misingi waliyowekewa.....kifikra...
Nini kifanyike sasa baada ya wewe kugundua hilo......???..neno lako muhimu sana humu,kama hili lilivyo ktk kubadilika vijana hao...
 
Mkuu umegusa penyewe .... Ukienda kwenye magroup ya whatsapp sasa, ndio utachoka hamana cha maana...
Mpenzi wangu kafanya hivi, nimeachwa, nimempenda fulani nifanyeje, kwa ujumla mambo ya ngono yanapewa muda zaidi!!
 
Mambo yaliyofanywa kwa vijana wetu na yanayyoendelea kufanywa kwa siri kubwa ni mazito kusimulia na yako kwenye nyanja nyingi,sio eneo moja.Niseme ukweli kwamba kwa jinsi mambo yalivyo kwa sasa,haiwezekani kufanya lolote sio kwa vijana tu,bali kwa wanadamu kwa ujumla.Humanity is so mind controlled kiasi kwamba kila utakalosema watakuambia wrongly kwamba ni conspiracy theory,not knowing that they have been taught to say that without themselves being aware.Humanity inatia huruma sana!
Ndio.misingi waliyowekewa.....kifikra...
Nini kifanyike sasa baada ya wewe kugundua hilo......???..neno lako muhimu sana humu,kama hili lilivyo ktk kubadilika vijana hao...
 
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida? (Mfano STRABAG, Nakumatt?)

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!
Baada ya kufanya utafiti (perpetuated follow up) vijijini muda kwa miaka mitano 2008-2012, niligundua kwamba watu wazima waliotumia akili muda wote walikufa chini ya umri wa miaka 78. walevi, wavivu, waganga wa kienyeji na wasema hovyo, waliishi muda mrefu zaidi kabla ya kufa pamoja na kwamba wanaishi maisha duni sana. Kwa hiyo huo upumbavu, matusi, vichekesho, nk, ni kwa ajili ya kupunguza stress na kuwawezesha kusogeza siku maana maisha wanayoishi hawajafikia kiwango wanachokiona kutoka kwa wengine hasa kutoka majuu, kupitia tv, internet, nk
 
vijana wengi ni mizigo kweli kweli! kwa familia na taifa kwa ujumla.
 
Baada ya miaka 10 dada zetu watakosa wanaume wa kuwaoa maana hao vijana sasa wamekalia kubana pua na kushinda instagram
 
Pumba Pumbani yaani kijana hawezi kuzungumza kitu cha maana mfululizo kwa dakika mbili. Huko vyuoni hata kujibu mtihani wanachora MAZOMBI kwenye karatasi za kujibia mitihani. ikifika 2020 tutakuwa na vijana wasiojielewa zaidi ya kubishania mipira ya ULAYA. Wahindi na Wachina ndo watajazana mpaka huko kwenye Biashara ya KU-BET
Kijana wa kitanzania ni mtu wa umri gani...naomba tu define age kwanza tuongee lugha moja....
 
Back
Top Bottom