Askofu Shoo alizwa na Ulevi wa Vijana Kilimanjaro

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) anayemaliza muda wake, Askofu Fredrick Shoo, amesema tatizo la ulevi kwa vijana limekuwa kubwa mkoani Kilimanjaro, akiitaka jamii kushirikiana na Serikali na kanisa kukemea tatizo hilo kunusuru nguvu kazi ya Taifa.

Dk Shoo, ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, ametoa rai hiyo leo Desemba 27, 2023, wakati akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wana Dayosisi hiyo waishio safarini.

Mkutano huo umefanyika uhuru Hoteli mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ukishirikisha zaidi ya wajumbe 444.

Hizi hapa sababu wakazi wa Dar kuongoza kukopa

Serikali yajipanga kuilipa Indiana mabilioni ikishindwa kesi

"Ukosefu wa ajira kwa vijana wetu bado ni tatizo kubwa sana kwa Mkoa wetu wa Kilimanjaro. Sehemu kubwa ya vijana wetu wamejiingiza katika ulevi na hata kuvuta bangi na dawa nyingine za kulevya.

"Tusipojitahidi kuondoa tatizo hili, hata sisi tulio wazima tutaathirika kwa namna mbalimbali ikiwemo usalama wa familia zetu na mali tulizonazo huku nyumbani,” amesema.

Akizungumza suala hilo katika mkutano huo, Mkuu wa mkoa mstaafu, Agrey Mwanri amesema zinahitajika jitihada za pamoja za Kanisa, serikali na jamii katika kumaliza tatizo hilo la ulevi.

"Ukiona mtu anapiga maji, maana yake anadhoofisha uwezo wake wa kufikiri na vitu hivyo vinafanywa na watu ambao hawana kazi ya kufanya. “Kanisa lina kazi ya kulea na kutunza, kanisa lina kazi ya kulinda imani na jambo hili ni letu sote, tushirikiane na viongozi wa serikali na kanisa ili kulitokomeza, kwani linatishia nguvu kazi ambayo ni vijana,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hizi hapa sababu wakazi wa Dar kuongoza kukopa.

Serikali yajipanga kuilipa Indiana mabilioni ikishindwa kesi.

"Ukosefu wa ajira kwa vijana wetu bado ni tatizo kubwa sana kwa Mkoa wetu wa Kilimanjaro. Sehemu kubwa ya vijana wetu wamejiingiza katika ulevi na hata kuvuta bangi na dawa nyingine za kulevya.

"Tusipojitahidi kuondoa tatizo hili, hata sisi tulio wazima tutaathirika kwa namna mbalimbali ikiwemo usalama wa familia zetu na mali tulizonazo huku nyumbani,” amesema.

Akizungumza suala hilo katika mkutano huo, Mkuu wa mkoa mstaafu, Agrey Mwanri amesema zinahitajika jitihada za pamoja za Kanisa, serikali na jamii katika kumaliza tatizo hilo la ulevi.

"Ukiona mtu anapiga maji, maana yake anadhoofisha uwezo wake wa kufikiri na vitu hivyo vinafanywa na watu ambao hawana kazi ya kufanya. “Kanisa lina kazi ya kulea na kutunza, kanisa lina kazi ya kulinda imani na jambo hili ni letu sote, tushirikiane na viongozi wa serikali na kanisa ili kulitokomeza, kwani linatishia nguvu kazi ambayo ni vijana,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Vijana wa huko hovyo kabisa , ukiachana na mali za urithi hamna kitu ....Hao jamaa wakifika mikoani ndio wanachangamka ila wakiwa kwao ni hovyo.

Tulienda kuzika Rombo vijana kama wazee unaambia huyu ana miaka 22 ila kachakaa ,nguo za mtumba chafu jua kali mtu kavaa makoti hawa jamaa hovyo kabisa....Pombe na usafi ni tofauti mtu mzima ananuka mikojo yaani balaaa.
 
Yeremia 25:27~28
27 Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu.
28 Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.****

tusinywe kwa nini ?
 
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) anayemaliza muda wake, Askofu Fredrick Shoo, amesema tatizo la ulevi kwa vijana limekuwa kubwa mkoani Kilimanjaro, akiitaka jamii kushirikiana na Serikali na kanisa kukemea tatizo hilo kunusuru nguvu kazi ya Taifa.

Dk Shoo, ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, ametoa rai hiyo leo Desemba 27, 2023, wakati akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wana Dayosisi hiyo waishio safarini.

Mkutano huo umefanyika uhuru Hoteli mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, ukishirikisha zaidi ya wajumbe 444.

Hizi hapa sababu wakazi wa Dar kuongoza kukopa

Serikali yajipanga kuilipa Indiana mabilioni ikishindwa kesi

"Ukosefu wa ajira kwa vijana wetu bado ni tatizo kubwa sana kwa Mkoa wetu wa Kilimanjaro. Sehemu kubwa ya vijana wetu wamejiingiza katika ulevi na hata kuvuta bangi na dawa nyingine za kulevya.

"Tusipojitahidi kuondoa tatizo hili, hata sisi tulio wazima tutaathirika kwa namna mbalimbali ikiwemo usalama wa familia zetu na mali tulizonazo huku nyumbani,” amesema.

Akizungumza suala hilo katika mkutano huo, Mkuu wa mkoa mstaafu, Agrey Mwanri amesema zinahitajika jitihada za pamoja za Kanisa, serikali na jamii katika kumaliza tatizo hilo la ulevi.

"Ukiona mtu anapiga maji, maana yake anadhoofisha uwezo wake wa kufikiri na vitu hivyo vinafanywa na watu ambao hawana kazi ya kufanya. “Kanisa lina kazi ya kulea na kutunza, kanisa lina kazi ya kulinda imani na jambo hili ni letu sote, tushirikiane na viongozi wa serikali na kanisa ili kulitokomeza, kwani linatishia nguvu kazi ambayo ni vijana,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

Halafu wanatumia plombe fake nyingi

Kilimanjaro ndio inaongoza kuwa na mapombe ya mchongo na mengi ni fake kutoka viwanda bubu

Matokeo yake ni vijana kupotea na
Magonjwa makubwa in the future
 
Back
Top Bottom